LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA TANO.

 


LEVEL ZA MAFANIKIO SEHEMU YA TANO.


Baada ya kufika Investor Level, ambapo pesa zinaanza kufanya kazi kwa ajili yako kama tulivyoona somo lilopita boss.
Sasa kuna hatua ya mwisho ya juu zaidi ambayo watu wachache sana duniani wanaifikia kwa ufahamu na nidhamu kali sana, hii si nyingine bali ni:
FREEDOM LEVEL ( HATUA YA UHURU WA KWELI) HII SIYO TENA LEVEL YA PESA TU, KAMA ZILE LEVEL ZINGINE.
Boss hapa siyo swali la: una pesa kiasi gani
una biashara ngapi, una assets kiasi gani?

๐Ÿ‘‰ Hapa swali ni moja tu:
UNAISHI MAISHA UNAYOYATAKA? Unajua kila mtu qnamatamanio yake, namna ya lifestyle yake, kuna vitu anapendelea kuvimiliki, lakini sasa ni wacahche wanaosatify wengi wanaishia kutamani tu boss.

MAANA HALISI YA UHURU HUU
Freedom level ni pale ambapo:
---- Hufanyi kitu kwa sababu unalazimika kufanya.
๐Ÿ‘‰ Yaani, Unafanya kwa sababu unachagua kufanya. Sijui kama unanipata?

AINA 4 ZA UHURU KATIKA LEVEL HII
1. UHURU WA MUDA
Unaamua: uamke saa ngapi, ufanye nini,
uishi wapi, uende wapi bila kisumbuliwa na boss au kazi yako. Huu ni uhuru wa muda, hapa muda unaamua kuutumia vile unapenda na vile unataka boss.

2. UHURU WA FEDHA
Boss hapa Pesa: siyo tatizo, siyo kizuizi
siyo chanzo cha stress. Unajua boss moja kati ya vitu vingi vinavyoongoza kwa stress na vifo ni pesa na mapenzi na chanzo cha stress kuu 75% ni pesa. Hapa ni short unaweza fanya chochote unachotaka kwenye maisha yako kinachohusu pesa na pesa isiwe tatizo ya kukukwamisha boss.

3. UHURU WA MAAMUZI
Ndugu hapa unaishi kulingana na: maono yako,
thamani zako, malengo yako na mawazo yako
Sio presha za family, marafiki wala jamii. Unaongozwa na maamuzi yako boss.

4. UHURU WA AKILI (MENTAL FREEDOM).

Hapa ndipo wengi hushindwa kufika hata kama wana pesa.
Hapa unakuwa huna: hofu ya kesho, msongo wa pesa, presha ya kuthibitisha  validate kitu kwa watu. Hauishi na pressure ya watu , unaishi maishq yako halisi boss.

5. UHURU NA FURAHA YA NDANI (THE INNER PEACE AND JOY FREEDOM).

Unajua ndugu yangu nimekuja gundua kwamba, kumbe kuwa na pesa mingi haimanishi kwqmba ndo umefanikiwa.  Na nimeona watu wengi sana wanakila aina ya pesa lakini hawana amani wala furaha na pesa zao.

Kumbe ndugu mafanikio ni zaidi ya kuwa na  Pesa mingi boss
Ni kuishi maisha mazuri, kuridhika satisfying, kufurahia maisha enjoying, kutimiza na kufanya vitu unavyovipenda, kuwa na amani ya ndani, na kuwasaidia wengine. Nje na hapo ni michosho tu boss.

BILA SHAKA BOSS UNATAKA KUULIZA SASA
NITAJUWJE KWAMBA NIPO AU NAKARIBIA LEVEL HII ?
Simple sana;
Pesa zako zinakutosha bila kufanya kazi ya lazima,
Una muda wa kufanya vitu unavyopenda
Una amani ya ndani the inner peace.
Una control ya maisha yako, wewe ndo decision maker boss.

UKWELI NIMEGUNDUA KWAMBA;
๐Ÿ‘‰ Watu wengi wanatafuta pesa,
lakini wanachotafuta kwa kweli si pesa bali ni
UHURU a real freedom. Sijui naeleweka boss?


HATA HIVYO NIMEKUJABAINI KUNA MAKOSA MAKUBWA AMBAYO WATU HUFANYA.

1. KUFIKIRIA PESA NDIO UHURU.
kama hujui watu wengi sana wana pesa lakini:
hawana muda, hawana amani, furaha, utosherevu na  bado wamefungwa na kazi zao.

2. KUKOSA DIRECTION.
Wengine wakipata pesa: wanapotea
๐Ÿ‘‰ hawajui waishi kwa kusudi gani. Afu ujue kuna watu wakipatq pesa wanabadilika ghafla inakuwa kama si wao, akili zao hurudi baada ya kumaliza pesa. Wengine hadi pesa hiita kuwa ni majini, shetani n.k. kumbe wala tatizo ni wao na tatizo lao ni lack of direction boss.

3. KUTOKUJITAMBUA.
Kitu hiki nimeimba sana, boss bila kujua wewe ni nani dunia haiwezi kukufahamu.
๐Ÿ‘‰ hata ukifika hapa, hutajua uishi vipi.
SIRI KUBWA YA LEVEL HII
UHURU WA KWELI HUANZIA NDANI — SIYO NJE.
Yaani,  Ni mchanganyiko wa: pesa, akili, utulivu, kusudi furaha na kuwafanya wengine kuwa bora zaidi.

Sasa unawezakuwa kwenye hiii level hata kama hujafika bado kuna,
NAMNA YA KUISHI LEVEL HII KWA USAHIHI BOSS.

1. ISHI KWA KUSUDI
Usiishi tu , jua kwanini unaishi. Hii ni muhimu sana the reason of being in the planet boss.

2. RUDISHA KWA JAMII (GIVE BACK)
Hapa ndipo impact inaanza kuwa muhimu kuliko pesa. Maisha yenye alama na urithi hapa ndo oale unasaidia watu kwa pesa zako n.k kumbuka if your wealth can't help others, then it means nothing.

3. ENDELEA KUKUA
Hata ukiwa huru, ukuaji hauishi. Kunywa madini jifunze jiboreshe kila siku. No prison can hold a continuous learning mind boss.

4. LINDA AMANI YAKO
Hii ndiyo asset kubwa kuliko zote. Kama tulivyoona hapo juu boss.

TAJIRI NAWEZA ONGEA SANA LAKINI INSHORT

Hatua za mafanikio ni kama safari:
Mwanzo → unapigania kuishi Survival
Kati → unajenga mfumo wako boss
Mwisho → unaishi maisha unayotaka wewe mwenyewe boss.

Boss,
Hii ndiyo hatua ambayo:
hauishi kwa hofu, hauishi kwa presha,
Hauishi kwa kulazimika, unaishi kwa uchaguzi.
Lakini pia,
“Lengo la mafanikio siyo pesa pekee tu, ni uhuru wa kuishi maisha yako kwa namna unayotaka huku ukiishi kusudi lako na kuwasaidia wengine .” ndiyo maana nikaamua kuiandikia mada hiii.

Boss kama kweli umesoma ujumbe huu hadi mwisho hebu jibu swali hili.

“Kama ungekuwa na pesa zote unazohitaji leo ungeishi maisha gani?”


Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.

Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/05/kama-unataka-uhuru-wa-kifedha-anza.html

#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork. #SeeYouNextLevel
+255767653697. 

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29