KABLA HUJAITA MTU MJINGA, SOMA HIZI TABIA 10 MOJAWAPO INAKUELEZEA WEWE MWENYEWE.
KABLA HUJAITA MTU MJINGA, SOMA HIZI TABIA 10 MOJAWAPO INAKUELEZEA WEWE MWENYEWE.
Hapa boss naenda kuelezea tabia, ishara au vitu vinavyoonyesha mtu huyu ni mjinga, hana busara, hekima wala ujuzi. yaani hajastarabika. Soma hadi mwisho ujikague mwenyewe.
1. ANAZUNGUMZA ZAIDI KULIKO ANAVYOSIKILIZA.
Mdomo wake daima uko wazi, masikio yake daima yamefungwa, muhimu kwake ni kuongea tu wala hata kama hajui anachoongea pia hatoi nafasi ya wengine kuzungumza, yaani ukitaka tuuongee tayari ashadakia . Mtu mwenye busara, hekima au ujuzi wa kweli anajua kwamba ukimya wake una thamani zaidi ya maneno yake mengi. Husikiliza kwanza, hufikiria pili, kisha huongea na pale anapoongea, kila neno lina uzito na maana. Pia ni watu wanaoskiliza sana wengine bila kuwa katiza.
2. ANAPINGA KILA KITU BILA USHAHIDI/HOJA YEYOTE.
Unajua boss, Kubishana ni rahisi. Kutoa hoja ya nguvu hiyo ndiyo ngumu kwa watu wengi. Mtu asiye na hekima, busara au ujuzi hupinga kwa nguvu lakini hana kitu cha maana cha kusema. Anabishana kwa sababu ego yake haikubali kushindwa, si kwa sababu ana ukweli mkononi.
Utakuta mtu hata kitu akijui, wnapinga tu ajabu sana.
Sikiliza boss, siku zote hatulipingi wazo kwa nguvu au kwa kumpelekq jela mtoa wazo, bali tunapinga wazo kwa kutoa wazo bora zaidi boss.
3. ANAAMINI ANAJUA KILA KITU.
Hii ndiyo hatari kubwa zaidi. Mtu anayefikiri amefika mwisho wa kujifunza amefika mwisho wa kukua. Wenye hekima wa kweli wanaishi katika hali ya kushangaa wanajua kadri unavyojua zaidi, ndivyo unavyogundua kuna mengi zaidi ya kujua.
Hawa ni watu ambao hawataki kabisa kujishusha, yaani anataka aonekane anajua kila kitu. Hawa watu wanasifa sana. Hata hivyo wanakwepa ukweli muhimu sana, kwamba hakuna anayejua kila kitu boss.
4. ANAONA KOSA KILA MAHALI ISIPOKUWA KWAKE MWENYEWE.
Kidole chake daima kinaelekea wengine. Matatizo yote yana lawama moja kuwaelekea watu wengine. Lakini mtu mwenye ukomavu wa fikra anajua: tatizo linalojirudia maishani mwake, yeye mwenyewe ndiye sehemu ya tatizo hilo.
Siku zote nimejifunza kuwa, katika ushirika wowote partnership tatizo linapotokea kila mshirika anakuwa amechangia asilimia kadhaa katika hilo. Sijui unanipata boss.
5. ANACHUKIA KUREKEBISHWA.
Marekebisho kwake ni shambulio. Ushauri kwake ni udhalilishaji, kuna watu boss ukiwakosoa, ukiwashauri inaonekana unamwonea wivu, anadhuka hasira na vita ya kimya kimya. Lakini ukweli ni huu mtu anayekataa kurekebishwa amechagua kukaa mahali alipo milele. Ujuzi hukua kupitia makosa yanayokubaliwa, si kupitia kiburi kinachojificha boss.
6. ANAZUNGUMZIA WATU BADALA YA KUTATUA MATATIZO.
Muda wake mwingi unatumika kuchambua watu na udhaifu wa wengine. Lakini swali ni hili: Matatizo yanayomzunguka yanatatuliwa na nani? Mtu mwenye ujuzi hana muda wa umbea ana kazi ya kufanya. Mara nyingi watu wa chini kabisa huzungumza kuhusu watu, watu wa kati huzungumza kuhusu matukio na watu wa juu sana huzungumza kuhusu mawazo Idea that always bring changes boss.
7. MANENO YAKE NA MATENDO YAKE NI MAMBO MAWILI TOFAUTI.
Anasema vizuri anaandika vizuri anawasilisha vizuri. Lakini matokeo? Hapo ndipo ukweli unajificha. Dunia haijalipwi kwa ahadi nzuri. Inalipwa kwa matokeo ya kweli. Maneno bila vitendo ni muziki bila sauti. Hqwa ni watu wa ahadi kibao, maneno lukuki lakini matendo ni zero kabisa. Si waaminifu, kuvunja ahadi, uongo yaani maneno na vitendo ni tofauti kabisa.
8. HESHIMA YAO KWA MUDA NI YA MANENO TU
Anachelewa bila aibu. Anavunja ahadi bila maelezo. Anafika tayari amekwisha pata udhuru mzuri. Lakini muda ni rasilimali ambayo haiwezi kurejeshwa na mtu anayeichukua yako bure anaonyesha wazi jinsi anavyokuona wa hovyo.
9. ANAKOPI BILA KUELEWA KIINI
Anaona mtu amefanikiwa anaiga mavazi yake, maneno yake, hata mwendo wake wa maisha. Lakini hakopi msingi, mchakato, taamuli, nidhamu, na miaka ya kazi iliyofichwa. Ndio maana anaonekana kama nakala dhaifu ya asili boss.
10. HASIRA NDIYO JIBU LAKE LA KWANZA
Anapoulizwa swali gumu hasira. Anapopingwa hasira. Anapokosea hasira anaposhauriwa hasira. Kila kitu ni kukasirika tu yeye yaani ni mtu wa kuona baya kila sehemu. Mtu mwenye ujuzi anajua kwamba hasira ni ishara kwamba akili imeshindwa kupata jibu. Udhibiti wa hisia si udhaifu ni nguvu ya hali ya juu kabisa kama tulivyo jifunzq boss.
"Hekima, busara na Ujuzi wa kweli haupigi kelele unasimama kimya, unatenda, na matokeo yenyewe yanaongea." Au siyo boss.
Hebu jiulize leo: Ninaonekana mjinga, hana busara, hekima wala ujuzi. au NIKO upande gani?
#SeeYouNextLevel
Share na mimi kupitia comment ulichojifunza. Ikiwezekana share na wengine ujumbe huu ili wajifunze pia.
Kujifunza tembelea,
https://addvaluetz.blogspot.com/2026/05/p5-sababu-ya-maisha-yako-kubadilika-au.html
#SelfAwareness (#Kujitambua). #Investment (#Uwekezaji). #PersonalDevelopment (#Maendeleobinafsi). #MigongoElias. #AddValueNetwork.
+255767653697.
