HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA21

        

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 21.

Ilipoishia......

Elvine baada ya kula alihisi kizunguzungu sana lakini badae alirudi kwenye hali yake ya kawaida. Yeye alijihisi labda kuzungumza kuhusu maji yaani hanywi maji mengi. Wakati kakaa pale kwenye kile kigoda alianza kuhisi usingizi na mwisho alijiona kashachukuliwa yupo mahali pengine asipopajua.,....

Kusoma sehemu ya 20 bofya hapa.

 Sasa inaendelea....

Alijikuta yupo mtoni kwenye mtumbwi usiojulikana unaenda wapi ila unajiongoza wenyewe na maji ya mto yalikuwa machafu sana, pia hali ya hewa ni mbaya na baridi kali mno. Alitazama pande zote na asione mtu yoyote karibu yake, kulikuwa na ukungu na giza hafifu kama la jioni. Hakuweza kuona umbali mrefu kutoka alipokuwa na akawa anahisi kana kwamba macho ni mazito sana hayataki kuona yale yanayojiri pale. 

Alipata hofu kidogo na akawa na maswali moyoni mwake. Alitamani angaliuliza mtu kuwa yu wapi na anakwenda wapi lakini hakuweza. Wakati anajiuliza akatahamaki baada ya kuona mamba wengi ndani ya maji. Aliamua kukaa tuli ndani mtumbwini mpaka atakapofika mwisho maana mpaka wakati huo tayari jasho lilikuwa linamtoka. Alitazama saa ikaonesha ni saa 5:30 asubuhi, wakati anatazama saa ni kama kuna mtu alikuwa anatazama kila anachofanya, ghafla Ile saa ikamvulika na kutumbukia majini yaani kitu ambacho hata yeye hakuamini kama inawezekana.

Aliona hana msaada mwingine zaidi ya kuomba Mungu amsaidie lakini hata hilo halikufanikiwa maana hakuna aliemsikia hata mbingu kama zilifungwa, kwahiyo hakusikika. Aliona huo ndio mwisho wa maisha yake. Lakini akajiuliza sasa imekuaje yeye kufika pale? Na mara ya mwisho alikuwa kwa Erika vipi Erika pia yuko wapi?, alipokuwa pale alimkumbuka mkewe na upendo wake kwa mkewe ndipo alipouhisi tena yaani ulirudi kwa nguvu sana moyoni mwake ( ni kama aliyekuwa katenganishwa na kitu cha thamani sasa kakipata tena). 

Alijikuta ameanza kulia, majuto yakawa mengi sana na msiba wake ukawa mzito sana na asijue cha kufanya.

"Elimina mammy! Elimina my dearest natamani nikuone japo mara moja, natamani hata nipige magoti kwako niombe msamaha, kwakweli nimekosea na najuta, natamani uisikie sauti yangu popote ulipo. Elvine nakuita Elvine nakuita, nisamehe mammy, nisamehe sana, niombee msamaha kwa Mungu pia maana mimi sizani hata kama atanisikia tena maana nimekosea sana" Elvine alisikika akilia na kujutia makosa yake ya kujiungamanisha na watu asiowajua maana hakujua hata ilikuwaje akaacha ibada na kwenda kumuona Erika.

Wakati anawaza hayo yote ule mtumbwi ulikuwa unatembea tena kama kuna mtu anaepiga kasia maana ulikuwa katika uelekeo mmoja tena stahiki yaani ulijiongoza vyema kabisa. Baadae ule mtumbwi ukasimama na akasikia sauti ikimnon'oneza kwa chini sana. Elvine mpendwa wangu jiandae ndio kunakucha. Kabla hajakaa sawa kuitafakari Ile sauti vizuri chanzo chake ni nini! Alimuona mamba mmoja mwenye rangi nyekundu akiwa kainua kichwa  kisha akazama majini na akaondoka zake. Akajiuliza huyu mambaa...... Akiwa anamtafakari mamba alishangazwa kuona mamba wengi wameinua vichwa kutoka majini tena wameachama midomo yao kuonesha namna wanavyomtamani. 

Uwoga ukamwingia maana hakuwa na siraha yoyote. Akasikia sauti tena! Vipi unahitaji siraha pia? Basi kama unahitaji sema ndio. Elvine haraka alisema ndio! Hapohapo aliona kashika bunduki mbili. Alianza kuwashambulia mamba wale ambao walikuwa kama wanafurahia anachofanya maana hakuweza kumpiga hata mmoja. Mamba walikuwa wanakwepa kama binadamu mwenye kasi ya ajabu sana. 

Alipambana nao sana lakini ilikuwa kazi ngumu. Mwishowe akachoka sana tena hana hata nguvu tena maana silaha kwake ilikuwa ni jambo jipya kuitumia. Ilifika wakati akawa Hana nguvu tena za kufanya jambo lolote zaidi ya kuamua aliwe tu. Alipochoka alikaa chini kwenye ule mtumbwi na kusubiri aliwe. Wakati kakata tamaa alishtushwa na fujo za wale mamba ambao walianza kuupigapiga mtumbwi lakini hakuna hata mamba mmoja aliejaribu kumdhuru ila waliupigapiga mtumbwi jambo lililomfanya apate hasira tena na kushika siraha. Mara hii alikemea lazima awaangamize wale Mamba.

Mapambano yakawa makali sana. Elvine alibahatisha kumpiga mamba mmoja mdomoni Kwa kumuuote tu. Alipomgipa yule mamba ni kama akawakasirisha mamba wote sasa. Yule mamba alizama majini na kutoweka. Akiwa anashangaa alipunduliwa kutoka kwenda mtumwi mpaka majini, alizama kwenye kina kirefu cha maji na akawa na hana pumzi ya kutosha mule. Akiwa anatapatapa majini alijikuta karudi kwenye mtumbwi. Alishangaa imekuaje tena, akiwa pale aliona ukingo wa maji. 

Alipofika ukingoni na ule mtumbwi alishuka nchi kavu. Hali ya hewa Bado ilikuwa mbaya sana. Akiwa pale aliona mtu anakuja. Alishangaa kumuona mkewe kwa mbali.

"Elimina? Kajaje huku? Yaani how?" Lakini kwa namna aliyokuwa anafuraha alimkimbilia mkewe na kumkumbatia kwa uchungu sana na machozi. Elimina nae alionekana kulia sana. "Hubby! Nimekuja huku kwaajili yako tu" Elimina alisemama huku akiwa katika kilio cha kwikwi.

"Imekuaje mammy!? Kwanini uko hapa?"

"Nitakueleza tu, hata usijali cha msingi tutoke eneo hili kwanza, alafu mengine utajua!"

Elvine alipata amani sana baada ya kuona yupo na Elimina maana alijua kuwa watapambana pamoja na itakuwa rahisi kutoka kule. Walianza kukimbia mpaka wakafika kwenye nyumba moja ambayo nje walikutana na Efraim ambaye aliwaita na kuwauliza wametoka wapi na wanakwenda wapi?

Elvine alianza kueleza kilichomkuta mpaka kufika kule lakini Elimina hakueleza kafikaje kule na wala Efraim hakutaka kujua sana yule binti kafikaje pale. Elvine alikuwa hakumbuki kuwa alishawahi kuonana na Efraim kabla japo alihisi kawahi kumuona mahali. Efraim aliwakaribisha ndani na kuwapa viti vya miguu mitatu. Elvine alihisi kama kawahi kuviona mahali viti vya namna Ile ila hakuwa anakumbuka vizuri aliviona wapi: yaani ni mtu ambaye alikuwa anasahausahau mambo kila baada ya muda fulani.

Walikaa pale ndani mpaka usiku ulipoingia kisha wakapewa chumba cha kwenda kulala. Walipoingia kulala Elvine alilala sana kutokana na uchovu wa misukosuko ya mchana lakini Elimina hakulala hata. Usiku wa manane Elimina aliona kivuli kinaingia chumbani akaanza kutetemeka kwa hofu sana akaamua kutoka pale kitandani na kusogea mlangoni ili achungulie nje aone kuna nini. Alipochungulia nje alitabasamu kisha akageuka kumtazama Elvine huku akiwa na sura ya tabasamu, alafu akafungua mlango na kutoka nje.

*.   .  *.      *.      *.      *.        *

Elimina alikwenda ibadani siku ya jumapili akiwa anawaza sana kuhusu Elvine maana alionekana kubadilika sana na wala sio kama aliyokuwa mwanzo. Elimina akiwa ibadani alijikuta anawaza sana kuhusu Elvine na moyo wake ukaingia baridi ambayo ilimfanya ahisi kuganda kwa namna fulani. Alijikuta anakosa amani kabisa kuhusu hiyo safari ya Elvine. Ilipofika saa 5:30 alijikuta anapigwa na butwaa muda maana moyo wake ulipigwa na kitu kisichojulikana. Ni muda ambao mchungaji alikuwa anahubiri, Elimina muda huo alijikuta anatokwa na machozi pasipo kujua chanzo, moyo ukauma kama kachomwa kisu, akahisi akili inaruka kama sio inapotea, Kwa muda wa sekunde kama kumi Elimina aliishiwa nguvu na kupoteza fahamu. 

Akiwa kapoteza fahamu alijikuta yupo mahali fulani ambapo alikutana na binti mmoja mdoga wa kike. Yule binti alimsalimu Elimina na kumwambia kuwa Elvine hayupo tena mahali salama. Yaani Elvine kajipoteza mwenyewe, kwahiyo Elimina anahitajika kusimama kwenye nafasi yake maana tayari Elimina alikuwa na ujauzito wa Elvine wa wiki mbili na wala yeye hakujua. Yule Binti mdogo alimwambia Elimina maneno yaliuumiza sana moyo wa Elimina.

" Sikia wewe mwanadamu uliepata neema ya kukutana na malaika wa Bwana. Mimi naitwa Elvila ni malaika wa habari wa mumeo. Nimehitaji kuonana na wewe kwakuwa mumeo kamkosea sana Mungu. Elvine alijifanya anamchukulia Erika kama mdogo wake lakini Mimi nilikutumia wewe kumuonya mara kadhaa kwa kupitia usemi wako. Elvine sio kwamba hakuelewa kuwa ni mimi nasema nae alijua vizuri kabisa ila tayari Elvine alitekwa na upendo wa yule binti. Alijikaza kwa kutaka kumfanya kama mdogo wake lakini alikuwa anaongopa, na kujidanganya mwenyewe maana ukaribu wake na yule binti ulimuathili.

        Mwanadamu, wewe ndie ulikuwa wakwanza kutumiwa na Erika ili kumpata Elvine. Erika alianza urafiki na wewe akapata uaminifu kwa Elvine na ndivyo ilivyokuwa. Erika alimpata Elvine kirahisi mno maana kila walipokuwa pamoja alimpandikiza roho chafu pasipo Elvine kujua. Na wakati kama huu, kumsaidia Elvine ni kazi kubwa mno maana wale wanahaki ya kumumiliki kwakuwa ni mtenda dhambi pia kosa kubwa ni kudanganya na kukosa ibada. 

       Mwanadamu, naumia mno kumpoteza Elvine ambaye alimzoea sana Mungu na wala hakujali kujua kusudi lake la yeye kuumbwa japo alilijua. Kama angalijikita kwenye kusudi lake tangu mwanzo, hakika asimgalikuwa hapa leo na malaika wengi wangekuwa upande wake. Lakini hakuna malaika wakutumwa kumsimamia mtu ambaye anafanya mambo yake na wala hajali kusudi la Mungu kumuumba. 

Kwasasa Elvine yupo kwenye shida japo bado tunamuhitaji maana hajatimiza kusudi, baba yake anamuombea kwa Mungu kila siku kwa kudhani Elvine anahudumia watu lakini sivyo kabisa. Sasa kwakuwa Elvine kakamatwa kwa sasa wewe unapaswa kulindwa maana unaujauzito wa wiki mbili, mtoto wako atawindwa sana na hawa watu pindi wakijua kuwa unaujauzito wa Elvine lakini omba sana pia kwakuwa umeujua ukweli huu. Mwanadamu, mwanadamu afanyiwe nini ili aridhike na aseme Mungu anampenda? Ooh! Mwanadamu!!" Elvila alikuwa anaongea huku analia tena kwa kuugua.

"Kwahiyo, Elvine mume wangu hatorudi tena? Au unamaana kuwa naweze kumsaidia Kwa kufunga na kuomba? Niambie nifanye chochote nipo tayari ili Mungu amsamehe Elvine na amsaidie. Niambie basi!!" Elimina aliongea akiwa analia sana

"Kulia sio suluhu ila nenda kamlilie Mungu wako, usipende kutoa machozi kama hivi mwanadamu mbele ya asiyeweza kukusaidia(malaika), tuungane kumsaidia japo ni mtihani ila wewe kama mwanamke kaushinde....

Swali; unadhani Elimina ataweza kumsaidia mumewe, na je kule kwenye ardhi ya maajabu Elimina kafikaje?

Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa.


Simulizi  hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

Tu follow kwenye.

Facebook page>>> Add Value Network.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.


Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.