HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 20.


HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 20.

Ilipoishia.....

 Lakini Elvine alikuwa anaipenda kazi yake, anapenda kuitwa meneja, anapenda kuonekana bosi, sasa akiwaza kuhusu kuwa mchungaji anaona kama hailipi kabisa japo zamani alikuwa anapenda sana kuwa mchungaji. Alijiwazia mwenyewe kisha akaamua kuondoka pale sebuleni maana aliona anazidi kuchanganywa na maneno ya mkewe. Aliingia chumbani kwake ambako alishangazwa baada ya kumkuta mtoto mchanga analia kitandani kwake......

Kusoma sehemu ya 18 bonyeza hapa.

Sasa inaendelea....

"Mmmh!" Elvine alisikika akiguna kwa umakini sana alianza kumsogelea yule mtoto aliyemkuta kalazwa kitandani. Alikuwa ni mtoto mchanga sana ambaye anakadiliwa kuwa na miezi kama mitatu au minne hivi. Alikuwa na wasiwasi maana alitamani kujua mtoto kafikaje fikaje pale ndani wakati anamsogelea akiwa katika hali ya umakini sana alishtuka sana baada ya kuguswa bega Kwa nyumba na mtu. 

"Yesu kristo! Kwa jina la Yesu toka pepo!!!" Elvine alikemea kwa kulalamika kuashiria woga alionao. 

"Nini shida?"

"Ooh! Kumbe ni wewe Elimina, umenitisha ety!"

"Kwani kuna nini unanyata chumbani kwako mwenyewe utafikiri umeona mwizi au wewe ndio mwizi sasa"

"Mtoto!!...." Elvine alipotaka kuzungumza suala la mtoto aliepo kitandani kwao alistaajabu baada ya kutazama kitandani hakumuona mtoto yule tena.

"Mmmh! Kumekucha nadhani!" Elvine alisema na kumtazama mkewe

"Kivipi? Kwani nini kimetokea?"

" Unajua kuna mtoto alikuwepo hapa kitandani kabla hujaja"

"Na ndio maana umeogopa?"

"Kwahiyo unataka kusemaje? Kwani mimi ni malaika kwamba nisiogope?" Elvine alijibu kama mtu alikwisha pandwa na hasira tayari.

"Hivi Elvine kwanini sikuhizi unahasira za ajabu ajabu, umekutwa na nini?" Elimina alihoji huku akimkazia macho Elvine

"Hamna shida, mimi sijachukia, ila nili..." Kabla hajamaliza simu ya Elvine iliita. Alipoitazama akajua kuwa ni Erika ndiye anaepiga. Akaacha kuongea na mkewe kisha akaenda zake nje kabisa ya nyumba.

"Erika mdogo wangu"

"Kaka jamani! Nimekukumbuka sana yaani natamani kukuona"

"Ooh kweli? Sasa si uje nyumbani? Elimina pia yupo anatamani kukuona"

"Hapana mimi huko siji maana wewe hujawahi kuja hata kwetu"

"Hujanikaribisha tu mimi naachaje kutokuja kwenu sasa kama ukitaka nije?"

"Basi uje kesho jumapili" 

" Erika kesho ni jumapili sasa ndio tatizo. Yaani, huwa tuna ratiba nyingi sana kanisani kwetu" Elvine aliongea kama anaejitetea kwa Erika

"Unaonaa sasa!. Kwani ukiacha ibada moja tu ya kesho ukaja kwetu. Utapungukiwa nini kaka Elvine. Kweli hunipendi" Erika aliongea kwa unyonge kama mtu anaedeka Kwa Elvine. 

"Sawa basi ntakuja mchana baada ya ibada"

"Saa ngapi?"

"Saa saba hivi"

"Mimi huo muda sitakuwepo maana mama kasema natakiwa kuanza kujiandaa na kurudi shule. Likizo ndio inaishia hivi"

"Hapana basi na wewe!. Usilie sasa, kesho ntakuja ila sitamwambia Elimina na wala wewe usimwambie maana hatakubali"

"Hapo sawa! Sasa nimefurahi" Erika aliongea kwa uchangamfu sana. Wakati huo Erika alikuwa anamuona Elvine kupitia kioo chake fulani cha kichawi. Kiufupi nguvu za Elvine zilikuwa zimeanza kupungua.

Elvine aliagana na Erika kwa makubaliano ya kukutana kesho yake asubuhi saa mbili. Elvine akaanza kutunga uongo wa kumwambia mkewe. Kwake hakuwa ana maana mbaya sana. Alikuwa anaona kama Erika ni mdogo wake maana alikuwa hana ndugu wa kike aliezaliwa nae zaidi ya Elvila mtoto wa Ezhu yang baba yake mlezi wa china, ambaye kwa sasa mawasiliano hayakuwa vizuri sana. Kwahiyo alimpenda Erika sana kama mdogo wake wa kujitolea.

Aliporudi ndani alimkuta Elimina kalala. naye akalala. Lakini usiku wa manane alishtuka baada ya kuamshwa na mkewe kwa pupa sana. 

"Vipi wewe mbona unanishtua kiasi hiki? Kuna nini?"

"Elvine naomba tuombe mume wangu! Nimeota ndoto mbaya sana!"

"Ipi hiyo mpaka unaniogopesha hivi?"

"Niliona umebebwa juu ya kiti chekundu.  Yaani, wewe umekarishwa kwenye kitu chekundu ambacho kuna watu wamekibeba juu.  Kama vile unaenda kutolewa sadaka kwenye miungu fulani. Nikasikia kama mtu ananiambia "hii sio hatima ya kweli ya mumeo, msaidie kama kweli unampenda. Wakati nashangaa tukio hilo 

nisijue sauti ilikotoka nikaona madhabahu fulani ambayo ilikuwa imefunikwa na shuka jekundu na humo ndani Kila kitu kilikuwa cheupe isipokuwa hiyo madhabahu pekee. Wakati nazidi kushangaa jambo hilo, nilimuona binti ambaye sura yake sio ngeni kwangu yaani Erika ana...."

"Hebu subiri kidogo!..." Kabla Elimina hajaendelea Elvine alimkatisha "Erika kaingiaje ingiaje humo ndani ya ndoto yako?"

"Sasa si usikilize nimalize?"

"Mmmh! Aya endelea nakusikiliza mama!" Elvine aliongea kwa namna fulani ambayo bila shaka iliashiria kutopendezwa na mwendelezo ya ndoto hiyo yaani ni kama kashaidharau baada ya kusikia jina Erika linataka kutaja kwenye ndoto mbaya kama hiyo"

Elimina akaendelea" kweli Elvine nimemuona Erika alishika kisu kikubwa akawa anataka kukuchoma wakati huo wewe ulikuwa tayari umelazwa kwenye ile madhabahu. Ila cha ajabu ni kama ulikuwa kipofu hivi, yaani huelewi kinachoendelea na kibaya zaidi ulikuwa unacheka tu maana hujui unachofanyiwa kutokana na upofu ulionao. Nilikuwa nakuita sana. Lakini Hukusikia. Na hapo ndipo nikashtuka

"Aiseee! Ndoto inatisha kweli yaani. Aya niombee sana mumeo sasa mimi naomba nilale maana bwana haya maisha yana mambo mengi.  Si unajua kuna muda sura ya Erika inaweza kutumia kuwasilisha mtu mwingine ila ambaye yupo jirani sana na mimi pia. Muombe akutafsilie sasa"

"Elvine wewe ndio mhusika mkuu hapa nahofia jambo baya juu yako"

"Kama lipi mama?"

"Mmh! aya lala baba yangu maana hujali hata!"

Elvine alilala kweli na wala hakujali. Kuna muda hata yeye alikuwa akijiona kabisa hayupo sawa maana hakuwa anaelewa kwanini kawa mkali kwa mkewe na kwanini hajali sana maneno ya mkewe. Alikuwa akitamani kuomba msamaha sana lakini kabla hajaomba msamaha linatokea jambo jingine anafanya makosa zaidi. Alikuwa anajutia sana akiwa mwenyewe mambo anayoyafanya lakini kujizuia asifanye kwake ilikuwa ni mtihani

Jumapili ilipofika Elvine aliaga kuwa kapata dhĂ rura ya kwenda mahali fulani kwa  mchungaji mwingine ambaye sio wa kanisa analosali. Mkewe alikubaliana nae tu ila hakuwa anamuamini sana.

Elvine alijiandaa na kuondoka kwenda kumuona Erika. Alipofika alipokelewa kwenye nyumba moja ya hali ya chini sana tena akakalishwa kwenye kigoda,(kakiti kadogo ka miguu mitatu). Alipokelewa na Erika na baba yake Erika yaani Efraim. Elvine alikuwa anamshangaa sana baba yake Erika, kwanza kijana kama yeye tu lakini anamtoto ambaye kashafika chuo, pili kijana yule ni kama anamfahamu japo hakujua ni nani hasa!

Elvine alipewa chakula na Erika na akafurahia sana namna chakula kilivyo kizuri. Ukweli ni kuwa Elvine alikuwa anazidi kilogwa kila siku na Erika kwakuwa alikuwa anapokea pokea sana vitu vyakula kutoka kwa Elimina na pasipo kuomba alivitumia maana alimuamini sana Erika kuliko chochote.

Elvine baada ya kula alihisi kuzungumza sana lakini badae alirudi kwenye hali ya kawaida. Yeye alijihusisha kuzungumzia  maji,  yaani hanywi maji mengi. Wakati kakaa pale kwenye kile kigoda alianza kuhisi usingizi na mwisho alijiona kashachukuliwa yupo mahali pengine asipajua.,....

Swali la kujiuliza; nani kamchukua Elvine ni ufalme wa kishetani au Mungu mwenyewe?

Kusoma sehemu ya 21 bonyeza hapa.


Simulizi  hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

Tu follow kwenye.

Facebook page>>> Add Value Network.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.