MAAJABU YA AKIBA

Ilipoishia....
Katikati ya ule moshi walionekana watu wawili wanatembea
kuingia ndani ambao walikuwa mwanaume na mwanamke, wenye sura za tabasamu
zilizojaa chuki, mateso pasipo huruma na furaha Kwa wengine. Lakini ni ajabu
maana walipoingia walikuwa watu
wanaofahamika sana na ni ajabu kuwafahamu....
kusoma sehemu ya 18 bonyeza hapa
Inaendelea....
Alionekana binti mmoja mrembo kapendeza mno kwa mavazi yake
mekundu kwanzia juu mpaka chini. Yaani, gauni refu jekundu lililokuwa
likitambaa mpaka chini renye maua ya kuvutia sana, viatu vyake virefu vyekundu
ambavyo kama hujawahi vaa viatu virefu basi viatu vile huwezi kuvitumia kwa
majaribio kabisa, kichwani alibana nywele zake ndefu kwa kibanio chekundu na
mikononi alivaa bangili mbili za rangi nyekundu pia, ni wazi kusema kwamba
alipendeza mno na hakuvaa kimaskini hata kidogo maana mavazi yake kwa makadirio
ya haraka labda yalikadriwa laki tano au sita ili mtu kuyamiliki.
Alikuwa kashikwa mkono na kijana mmoja ambaye ni wazi
alikuwa kamzidi kiumri yule binti. Sura ya Binti yule ilikuwa inang'aa sana na
kadri aliposogea jukwaani ndipo alipozidi kung'aa zaidi.
Walipanda jukwaani ndipo hali ya pale ndani iliporudi kama ilivyokuwa awali. Yaani, watu wakaacha kukohoa na moshi
ukatoweka. Mtu mmoja ambaye ndiyo alikuwa kama muendesha hafla ile yaani MC
akasimama mbele ya jukwaa na kuwakaribisha wageni hao ambao ndio walionekana ni
muhimu sana katika tukio hilo, Kisha akawaamuru watu wakae na kuachia jukwaa
chini ya uongozi wa wageni walioingia.
Yule kijana wa kiume alisimama na kutabasamu na kuanza kutoa
hotuba yake.
" Ni muda mrefu sana sijatoka kuona Dunia inavyoenda
lakini sasa nadhani ni nafasi yangu ya kuisumbua Dunia na Elvine lazima
nimnyooshe kidogo japo ni mpendwa wangu. Leo ninafuraha sana maana binti yangu
kaanza kuonesha ujuzi alioupata masomoni unafanya kazi kwakweli makofi kwake!
(Wote wakapiga makofi).
Akaendelea; "Mimi kama baba wa Erijini nataka kufanya
mambo kama navyoagizwa na makao makuu bila makosa kabisa. Mimi kukabidhiwa nyie
niwaongoze ni kwaajili ya hatima ya huyu binti maana bila yeye kuzaliwa mimi
nisingeaminiwa kuongoza kundi hili. Nataka mjue kitu kimoja Kwa sasa kikundi
cha powers kinaenda kupata nguvu zaidi maana binti yangu kakamilisha masomo na
yupo tayari kwa kazi na hakuna wa kumzuia. Erijini njoo binti yangu useme neno.
Binti alisogea pale alipo baba yake, kwa kuwatazama kwa
haraka ni vigumu kuamini kama ni mtu na baba yake maana nyuso zao hazikuonesha
kutofautiana sana. Erijini alitembea kwa madaha sana na akabadilisha macho yake
kuwa mekundu kama damu kisha akaanza kucheka bila sababu tena Kwa sauti kubwa.
Alipofika mahali baba yake kasimama akamkumbatia na kumwambia "Bado muda
kidogo tu namalizia kazi ulionipa baba" alipomaliza kusema alipaa hewani
bila mabawa na kusimama juu kabisa mahali pasipo na chakusimamia na yote
aliyafanya kuwaonyesha wale watu namna gani anauwezo mkubwa sana.
Alisimama Kwa muda kisha akabadilisha mazingira ya pale
ndani na kupafanya paonekane tofauti kabisa na mwanzo yaani kila kitu
kilibadili rangi yake na kuwa nyeupe sanaa. Mara hii pale mbele hapa kuwa na
jukwaa ila madhabahu iliyofunikwa na shuka jekundu. Yaani, kila kitu kilikuwa
cheupe isipokuwa hiyo madhabahu pekee. Viti havikuwepo tena kama mwanzo. Wote
walishangaa na kuanza kumpigia makofi yule binti.
Erijini baada ya kufanya hayo alishtuka kutoka juu alipokuwa
kaganda hewani kisha akatua juu ya Ile madhabahu ambayo baada ya yeye
kuisimamia tu ilianza kuwaka moto na ndipo ukumbi mzima ukasema "MOTO KWA
MOTO, DAMU KWA DAMU" Kisha watu wote wakapiga magoti na kumsujudia yule
binti kuonyesha wamekubali na wapo tayari kutawaliwa. Yule kijana wa kiume
ambaye ni baba wa Binti yule alitabasamu na kutikisa kichwa ishara ya
kufurahishwa na uwezo wa mwanae.
Binti aligeuka na kumtazama baba yake Kisha akasema
"baba I shall win the battle before the battle wins me" yaani
atashinda vita kabla vita havijamshinda. Baba alitabasamu tu.
Binti alianza kuongea na kuwaambia wale watu " Mimi ni
Erijini lakini mtaani naitwa Erika na nimefanikiwa kuzizuia nguvu zangu
kuonekana mbele ya Elvine na kwa sasa nipo kwenye hatua nzuri maana nakaribia
kushinda moyo wake na nikifanikiwa hilo basi hatuna kikwazo kingine kwenye
mambo yetu. Kuzaliwa kwangu kupitia Efraim ambaye Dunia inamtambua kama mfu
kutaleta mabadiliko katika ufalme wa kishetani yaani, lazima lengo la baba
yangu kuletwa huku nilikamilishe ili awe huru pia maana kafungwa muda mrefu
kwaajili ya Elvine na amefungwa mpaka mimi nimekuwa sasa na leo yupo nusu huru.
Uhuru wa baba yangu Efraim mimi ntaukamilisha kwa kulifanya kazi hii kwa ujuzi
wangu wote.
Watu wote
wakashangilia kana kwamba kuna mashindano ya Simba na yanga mule ndani. Baada
ya muda waliruhusiwa kila mmoja kuondoka, hivyo wakaanza kuondoka pale ndani na
baada ya muda pakawa patupu bali Erika tu na Efraim ndio walibakia pale ndani.
Efraim akamwambia binti yake kuwa yeye hawezi kukaa na binti yake mpaka pale
atakavyotimiza kazi aliyopewa. Wakati wanaendelea kuongea Efraim alifungwa na
kamba ambazo hazikujulikana zilipotokea na kisha akatoweka.
Efraim alijikuta sehemu iliyokuwa inatisha zaidi maana huko
kulikuwa ni kama chini ya mlima wenye volcano maana moto ulikuwa kila mahali na
hapo alikuta kiti ambacho alikuwa akikalia miaka mingi sana kama kifungo na
hakutakiwa kutoka hapo na ndipo alipokumbuka namna alivyochukulia.
Alikumbuka kuwa akiwa mdogo alikuwa rafiki wa Elvine na
walipendana sana na kipindi hicho alianza kuota ndoto za ajabu ajabu sana mara
yupo polini na watu asiowajua mara yupo barabarani anashuhudia ajali n.k.
lakini hakujali pengine kutokana na utoto alionao alihisi ni ndoto tu za
kawaida. Akakumbuka siku ambayo aligongwa na gari kwa makusudi na watu ambao
lengo lao ilikuwa ni kumuuwa Elvine lakini hawakuwa wanamfahamu Elvine hivyo
wakamuuwa yeye, lakini ukweli ni kuwa hawakumuuwa hata na ulikuwa mpango kamili
wa mashetani kutaka kumtumia yeye hivyo Ile siku aligongwa lakini alijikuta
sehemu nyingine kabisa na hakujua kafikaje. Akiwa huko alioneshwa namna watu
wanavyolia kwenye msiba wake na akaambiwa hatoruhusiwa kuwa huru kutoka kwenda
kuzurura Duniani mpaka atakapofanikiwa kupata mtoto ambaye atapewa nguvu za
kishetani na kumuangusha Elvine. Mtoto alipatikana baada ya yeye kupewa mke
ambaye ni jini na baada tu ya mtoto kuzaliwa yule jini aliteketezwa. Efraim
aliishi ile sehemu ya kutisha pasipo ndugu wala rafiki bali mtoto wake tu ndio
aliyekuwa anakuja kumuona na wala hakuishi naye pia maana Erijini alikuwa
anakaa kwenye chuo cha mafunzo maana alitarajiwa kuja kufanya kazi moja tu ya
kumuangamiza Elvine na wote ambao ni watumishi wa Mungu wenye uwezo mkubwa wa
kuwasumbua.
Miaka ilipita mingi sana na sasa mtoto wake kakua na kaanza
kazi aliyopewa maana aliambiwa kuwa mtoto huyo akimuangusha tu Elvine basi yeye
atakuwa huru. Efraim alikuwa tayari kapandikizwa roho mbaya ndani yake kwahiyo
aliona ni sawa apotezwe na alikuwa akimfundisha binti yake mbinu za kumfanya
Elvine afurahi maana yeye alikuwa anajua vitu ambavyo Elvine anapenda toka utotoni
mwake. Kwahiyo kazi kubwa aliyokuwa nayo yeye na Erijini yaani Erika ni
kumuangusha Elvine.
Ilikuwa ni vigumu Elvine kuona ushetani ndani ya Erika maana
Erika alipokuwa anaenda Kwa Elvine alikuwa anajua nguvu zote alizonazo kwahiyo
hakuwa hata na chembe ya nguvu za kishetani ndani yake ila hurudi kuubeba uwezo
wake pindi akitoka kuonana na Elvine.
*. *. *. *. *
Elvine alikuwa akimpenda sana Erika na kwake alimfanya kama
mdogo wake. Elimina hakuwa anajua sana urafiki mkubwa uliojengwa kati ya mumewe
na Erika. Siku moja Elimina aliota ndoto ambayo bila shaka ilikuwa ni kama onyo
kwa Elvine maana aliota kuwa shati la Elvine linaungua. Alipojaribu kumsimulia
Elvine, Elvine hakujali maana alikuwa anajiamini sana kuwa ananguvu za Mungu
sanana Mungu hawezi kumuacha.
Siku moja Erika alikwenda nyumbani kwa Elvine na alipofika
aliwakuta Elvine na mkewe sebuleni wamekaa wanakula. Alipofika alikaa pembeni
yao na stori zikaanza ambapo. Wakati wanaongea Erika akauliza "hivi hii
nyumba mbona sijaona vitoto vinacheza shida nini?" Kwa namna alivyo mropokaji
hakuna aliejaji sana lakini neno lile likaingia moyoni mwa wanandoa wale.
Erika alipoondoka Elvine akamuuliza Elimina "hivi ni
lini na mimi nitaitwa baba?" Aliuliza hivyo akiwa katika namna isiyo ya
utani kabisa. Elimina alitabasamu na kusema "wakati wa Bwana"
"Hiii!! Elimina hivi unautani eeh? Mimi natamani niitwe
baba sasa khaa!"
"We si unaimani kubwa! Kwanini usimuombe Mungu wako
afanye jambo"
"Ety eeh!? Ndio unaniambia mimi hivyo?"
"Ni kosa?." Wakati mabishano yasiyo rasmi sana
yanaendelea kati yao. Elimina aliingiwa na malaika wa Bwana palepale na Elvine
hakujua. Elimina akaanza kuongea maneno ambayo ki uhalisia sio yeye alikuwa
alisema ila ni aliye ndani yake.
"Masikini Elvine! Umetulia! Wala huoni mbele! Umekunja
mikono wala hutaki kufanya kazi uliyoitiwa. Unatamani ufanyiwe na Mungu mambo
mengi lakini je wewe umefanya nini? Kamwe Mungu hawezi kukupa mwana kama huwezi
badilika. Ataharibu uzao wote tumboni mwa Elimina kamwe huwezi pata uzao"
"Unaongea nini wewe?"
Sijui na wala sifahamu naongea nini lakini jitahidi
kumtafuta Mungu tena. Rudi kwenye njia, kafanye kile Mungu anataka, acha kazi
unayofanya maana sio yako. Fanya maamuzi haraka maadui zako wako mbioni
kukuangamiza. NI ONYO!" Elimina alikuwa anaongea hayo maneno Kwa upole
sana jambo ambalo lilimfanya Elvine kutambua kuwa yele sio Elimina ila kuna
anaeongea ndani yake. Lakini Elvine alikuwa anaipenda kazi yake, anapenda
kuitwa meneja, anapenda kuonekana bosi, sasa akiwaza kuhusu kuwa mchungaji
anaona kama hailipi kabisa japo alikuwa anapenda sana kuwa mchungaji zamani.
Alijiwazia mwenyewe kisha akaamua kuondoka pale sebuleni maana aliona anazidi
kuchanganywa na maneno ya mkewe. Aliingia chumbani kwake ambako alishangazwa
baada ya kumkuta mtoto mchanga analia kitandani kwake......
"Huyo mtoto ni nani na katoka wapi? Fatilia sehemu
inayofuata..."
Kusoma sehemu ya 19 bonyeza hapa.
Simulizi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.
Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .
Mawasiliano:
Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
&,
Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Meshaki Katala · 51 weeks ago
Nimejifunza kitu.
Migongo Elias · 51 weeks ago
Cheyo · 51 weeks ago
Elias Migongo · 51 weeks ago