HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23. Ilipoishia...... Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana.  "Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira.... Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto? Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa   Sasa inaendelea...... Elvine alikuwa anatetemeka  kwa hofu ya yale anayoyaona lakini alistaajabu kuona ni kama mkewe hajali sana kuhusu yeye. Alimtazama kwa makini sana mkewe akiwa anajaribu kutafakari kwanini anaonekana kuwa na hasira juu yake. Elimina akajishitukia "Hey, wewe! Nini sasa unanitazama hivyo?" "Nakutafakari sipati majibu!' "Nimefanyaje kwani?" "Hamna ila sijajua kama umenihofia mimi au hilo swali lako linamaana gani? "Elvine baba sina maana hiyo uliyoelewa wewe kabisa. Shida yangu mimi umefanya nini mpaka unataka kuhatarisha maisha Yako namna hii. Hujui namna ga

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA 18.


HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA KUMI NA NANE.

Ilipoishia....... 

Siku moja wakiwa nyumbani Elvine alihisi nafsi yake kama ipo kwenye shida sana. Yaani inahangaika, na akakosa amani kabisa. Hakuweza kumweleza pertnar wake maana hakuwepo. Kwani alikuwa  dukani. Aliona bora akalale, ili atulize akili. Akiwa  mbioni kuusaka usingizi pale kitandani aliona popo kaingia chumbani na kuanza kurukaruka huku na huko. Alipata hasira maana aliona kapoteza usingizi wote. Aliamka na kutafuta mbao moja pana ambayo alitaka kuitumia kumchapa yule popo. 

"Yaani wewe kamnyama umenikosea sana maana mimi nimechoka halafu wewe unataka kunisumbua, Sasa subiri uone kazi.... 

Kusoma sehemu ya 17 bofya hapa.

Sasa inaendelea .......

Alimuongelesha popo kana kwamba anamsikia. Alipotaka kumpiga popo yule alikwepa. Wakaanza kufukuzana pale chumbani maana popo alikuwa mjanja sana. Elvine alijitahidi sana kumpiga lakini alishindwa mpaka akachoka. Alipochoka yule popo aliondoka kwa kupita dilishani kana kwamba alikuwa anampotezea muda Elvine kwahiyo alijua kuwa Elvine kachoka kucheza nae. Elvine alichukia sana maana yule popo alisababisha baadhi ya vitu kuharibika mle chumbani. 

Siku kadhaa zikapita na hatimaye mwezi wa tisa ukaingia. Mapema Edgar mjomba wake Elvine alikuja. Walikaa na kuweka mipango vizuri juu ya kampuni ya "A quality" Itakavyo funguliwa na Elvine aliwekwa kuwa meneja pale kwenye kampuni. Elvine aliona kama ni mwezi wa furaha sana kwake. Baada tu ya mjomba wake kuondoka baba yake na mama yake nao walitia timu Dodoma. 

Editrin alimwambia Elvine kuwa watakaa pale kwa muda kidogo maana wamekuja kuona namna kijana wao anavyoishi na binti wa watu. Elvine kwake kila jambo aliliona ni heri. Walikaa mpaka mwezi wa kumi na mbili ndipo wakaondoka lakini kabla hawajaondoka Edwin alimwambia Elvine kuwa aanze kujiandaa kwa ajili ya kutimiza kusudi lake yaani kufungua kanisa. 

Kwakweli Elvine hizo ndoto alishaanza kuzisahau  na wala hakuwa hata anakumbuka kuwa anatakiwa kufungua kanisa siku moja. Aliitikia tu sawa lakini moyoni hakuwa radhi maana alihofia kuwa akiwa mchungaji angeshindwa kuutawala vizuri uongozi wake akiwa kama meneja wa "A quality" Tawi la Dodoma. 

Mbele ya baba yake alikubali na akaonesha kufurahia sana. Baaya ya baba yake kuondoka alijisemea "kwa kweli baba yangu nisamehe, mimi nitakuja kuwa pastor lakini mpaka labda nifike hata miaka hamsini na tano hivi ila kwa sasa jamani acha nile maisha, kwanza hata yale mauzauza hayapo tena sio ajabu hata Mungu mwenyewe kajua siwezi kuwa mchungaji na ndio maana kaniacha kidogo nile maisha".

Elvine alianza kujikita zaidi katika ufunguzi wa tawi la mabasi ya "A quality" Na ilipofika mwezi wa tatu mwaka uliofuata Elvine aliletewa magari hamsini mapya yaliyoagizwa kutoka china. Kwake alijiona kama mtu mwenye bahati sana duniani. Furaha ikaongezeka nyumbani. 

Siku moja Elvine akiwa ofisini baada ya kuanza kazi rasmi alipigiwa simu na katibu wake akaambiwa kuwa kuna mtu anahitaji kumuona na jina lake anaitwa Erika. 

"Erika?"

"Ndio bosi kasema mnafahamiana"

"Ok! Sawa mwambie aingie"

Wakati huo Elvine alikua kaketi kwenye kiti chake anazunguka maana hana presha na haya maisha. Pamoja na kuwa meneja baba yake na mama hawakuwa wanajua na hakutaka wajue hivyo alimwambia mjomba wake Edgar asimwambie mama yake. Alipoulizwa kwanini alisema kuna mambo anaweka sawa kwanza kwahiyo anaomba wazazi wasijue kwanza. 

"Erika alipoingia pale ofisini alikuwa anachekecheka tu! "

"Waooh! Jamani kaka! Wewe ndio unafanya kazi hapa?"

"Ndio mdogo wangu. Vipi lakini kwani chuo kimefunga Erika? Mbona umerudi nyumbani mwezi huu?"

"Mimi nipo likizo ya wiki mbili maana tumetoka kufanya mtihani wa chuo wiki iliyopita tu"

"Ooh waoh. Unahakika matokeo yapo vizuri lakini?" 

"Sanaaaa. Maana najuwa kaka Elvine ananiombea  na hata nikifeli mimi ntakuja kufanya hapa kazi na wewe! "

"Hahahahhahha. Yaani, wewe binti mdogo hauishiwi vituko. Sawa nitafurahi ukija pia"

"Kweli?"

Hapana. We soma kwanza sawa mdogo wangu? Vipi umepita kwa Elimina kumuona? 

"Haa dada tena? Mimi nimeshinda kwake jana na sahivi hapa nimetoka kwake maana yeye ndio kanielekeza hapa"

"Ooh! Ni mzima mrembo wangu lakini?"

"Jamani kaka Elvine kila muda Elimina, Elimina khaa! Utamuuliza mwenyewe mkionana kama ni mzima au la. sahivi hapa Elimina hayupo bhana"

"Sasa nisipomuulizia Elimina muda wote ntamuulizia nani mwingine wakati hata wazazi wangu hawapo hapa?"

"Utaniulizia hata mimi hahahahh" Erika aliongea na wote walicheka. Waliongea kwa muda mrefu sana mpaka jioni. Elvine akamwambia Erika kuwa muda umeenda angepaswa kurudi nyumbani sasa. 

"Jamani kaka Elvine mbona wewe ni mkatili sana yaani, nirudi mwenyewe halafu mpaka nyumbani nauli buku. Si bora unipeleke tu" Erika aliongea kama anadeka vile akiwa mbele ya mtu wake wa karibu mno. 

Elvine alicheka tu na akatoka na Erika mpaka kwenye gari lake ambalo lilikuwa kwenya bustani nzuri ya maua ambayo ilikuwa ni maalumu kwaajili ya magari ya watu maalumu yaani, VIP pekee. Binti yule licha ya kuwa alikuwa akiishi Dodoma mjini lakini alionekana kama mshamba kidogo kuona vitu vizuri kama vile. Elvine aligundua hilo baada ya kuona yule binti anashangaa kila kitu pale ofisini. 

Walipanda gari mpaka sehemu iliyoitwa sabasaba ambapo binti yule aliomba kushuka na akasema amefika.

Mazoea kati ya Erika na Elvine yalianza kuongezeka sana. Kila siku Erika alienda kazini Kwa Elvine. Elvine alimchukulia kama mdogo wake na hali hiyo ikawafanya hata wafanyakazi wengine pale wafikilie kuwa Erika ni mdogo wa damu wa Elvine au pengine hata ni ndugu yake. Ilikuwa ni vigumu sana wao kumfikiria vibaya bosi wao Kwa namna alivyoonekana kuwa na misimamo na ni mtu wa Mungu kweli. 

*.    *.      *.      *.     *.    *

Ulikuwa ni usiku wa manane na ambapo walionekana watu wenye heshima zao wakiwa kwenye kikao maalumu. Sehemu waliyokuwepo ilionekana kutisha kidogo Kwa jinsi ilivyoandaliwa. Kulikuwa na jukwaa ambapo hapo palikuwa na kiti kilichokuwa tupu na wengine walikuwa wamekaa kwenye viti kwenye ukumbi ambao ulipambwa Kwa rangi nyekundu kwenye kila kitu. Yaani, vitu vyekundu, zuria jekundu kutoka mlangoni mpaka pale kwenye jukwaa, maua mekundu na wote mule ndani walivaa viatu vyekundu isipokuwa mavazi yao tu! Walivaa suti nyeusi na mabinti magauni meusi pia. 

Wote walionekena ni watu wenye pesa sana na kanakwamba wana jambo la msingi sana wanataka kulifanya pale ndani kama sio sherehe basi ni kikao. Walikuwa wananyuso za tabasamu japo walichoma kazi maana nguo walizovaa na viatu hata havikuendana maana vilikuwa vya aina moja kwa wanawake na wanaume yaani, wote walivaa viatu vya kike virefu vyekundu, ni wazi kuwa hawakupendeza kwenye suala la viatu lakini hakuna aliemshangaa mwenzie wala kumcheka mwenzie bali kila mmoja aliona ni hali ya kawaida tu, japo ni wazi kuwa wanaume waliteseka kuvaa vile viatu ila walijikaza na wengine walionekena tayari ni wazoefu. 

Pale ndani kulikuwa na wahudumu ambao wao walionekena tofauti kidogo maana ni wazi kuwa hawakuwa binadamu wa kawaida maana walikuwa na uwezo wa kutembea hewani ili kuwahudumia watu wao kwa haraka, na walikuwa wanawapatia vinywaji  ambavyo vilikuwa na rangi nyekundu sana. Mule ndani mlikuwa na ndege mfano wa bundi juu ya paa japo ule ukumbi haukufaa kuwa na ndege wa namna hiyo kwa jinsi ulivyokuwa wa kifahari sana. Watu walikuwa wakipiga stori zao za kawaida na kucheka pasi na wasiwasi na pia, walionekana kama walikuwa wanasubiri muda ufike jambo lao ndipo lianze.

Ghafla!!!!!

"Ndugu wanapower!! Mgeni wetu tuliemsubiri Kwa muda mrefu hatimaye sasa amewasili naomba sote tusimame maana haikuwa kazi rahisi kuwa na mtu kama huyu mwenye nguvu na mafunuo kuhusu wanapower."

Ukumbi mzima ukasimama na wote wakaanza kupiga makofi kwa shangwe na miluzi. Wakati wanashangiria Moshi ukaanza kuingia mule ndani kupitia mlangoni jambo ambalo liliwafanya wote kuishiwa nguvu na kuanza kukosa pumzi. Yaani, ki ufupi hali ya hewa ilichafuka pale ndani na vikohozi ndio vilitawala. Lakini hakuna hata mmoja aliethubutu kunyanyua mguu wake kutoka aliposimama bali wote wakiendelea kusimama na huku wanahangaika na pumzi zao. 

Katikati ya ule moshi walionekana watu wawili wanatembea kuingia ndani ambao walikuwa mwanaume na mwanamke, wenye sura za tabasamu zilizojaa chuki pasi huruma na furaha Kwa mateso ya wengine. Lakini ni ajabu maana walioingia walikuwa  watu wanaofahamika sana na ni ajabu kuwafahamu....,.

"" Je hao walioingia kwenye ukumbi wa watu wenye imani ya namna ile ni akina nani???" Itaendelea.....

kusoma sehemu ya 19 bofya hapa


Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.






Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.