HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23. Ilipoishia...... Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana.  "Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira.... Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto? Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa   Sasa inaendelea...... Elvine alikuwa anatetemeka  kwa hofu ya yale anayoyaona lakini alistaajabu kuona ni kama mkewe hajali sana kuhusu yeye. Alimtazama kwa makini sana mkewe akiwa anajaribu kutafakari kwanini anaonekana kuwa na hasira juu yake. Elimina akajishitukia "Hey, wewe! Nini sasa unanitazama hivyo?" "Nakutafakari sipati majibu!' "Nimefanyaje kwani?" "Hamna ila sijajua kama umenihofia mimi au hilo swali lako linamaana gani? "Elvine baba sina maana hiyo uliyoelewa wewe kabisa. Shida yangu mimi umefanya nini mpaka unataka kuhatarisha maisha Yako namna hii. Hujui namna ga

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA 17.

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA KUMI NA SABA

Ilipoishia....

Siku moja akiwa amelala aliota moto mkubwa unawaka ndani ya maji lakini ule moto ni kama unaofifia kwa kuzidiwa na yale maji. Alipoamka akaikumbuka ndoto aliyowahi kuota utotoni ikamkumbusha kuwa hatakiwi kuzima namna hiyo na akajikuta kakumbuka sana vile viusumbufu vya kivita na maadui. Lakini hakujua kumbe kuna bomu kubwa kaandaliwa..... 

Kusoma sehemu ya 16 bonyeza hapa.

*.   *.    *.   *.    *.    *.   *. 

Elvine alikuwa ameketi juu ya mti katikati ya poli fulani akiwa na amani sana. Akiwa pale aliweza kuona umbali mrefu sana. Alishangaa baada ya kumuona mtoto wa kiume mwenye umri kama wa miaka 7 hivi anazunguka zunguka mule polini. Akacheka sana halafu akasema "Kuna vitoto vya ajabu Duniani jamani. Sasa angalia huyu mtoto anataka nini huku polini muda huu?" Akatabasamu akachuma embe lililoiva kwenye ule mti na kuanza kulila.

Yule  mtoto alikuwa akijiimbia "ukutiukuti" mwenyewe. Elvine akamtazama kwa makini yule mtoto na akahisi kama anamfahamu. Kwakuwa alikuwa mbali hakuweza kumtambua vizuri. Aliacha kumtazama yule mtoto huku akaendelea kula maembe matamu yaliyokuwepo kwenye mti  mkubwa aliokuwa ameketi.

     Moyoni ni kama aliambiwa amlinde yule mtoto lakini hakujali maana maembe yalimpendeza zaidi. Na kwakuwa hakuona hatari yoyote mahali pale hakumzingatia sana yule mtoto. Baada ya mda alipomtazama tena yule mtoto hakumuona. Akajiuliza kaemda wapi lakini hakupata majibu na wala hakuweza kumuona.  

Kidogo alipatwa na wasiwasi akahofia yamkini kaliwa na wanyama au kuna jambo baya limemkuta. Aliamua kushuka mtini na kuanza kumtafuta. Paaap! Alimuona yule mtoto yupo mbele yake. Alishtuka kidogo lakini akaona kawaida. Lakini sura ya yule mtoto alihisi anaifahamu kabisa.

       Alimsogelea mtoto yule huku anatabasamu Ili amuulize maswali. Alipopiga hatuna kusogea na yule mtoto alisogea kwake. 

"Unaitwa nani mtoto?"

"Wewe" yule mtoto alijibu akiwa siliazi sana.

"Sijaelewa, namaanisha jina lako nani!" Elvine aliuliza.

"Elvine" yule mtoto alijibu, ila mara hii alitabasamu kidogo. Elvine alipoendelea kumkazia macho ndio ufahamu wake ulipofunguka na akajikumbuka yeye alipokuwa mdogo alifanana sana na sura ya mtoto yule. Hapo sasa ndipo alipohisi nywele zinasimama na tabasamu la mtoto yule ndio lilimtisha zaidi. 

Wakati anashangaa yule mtoto alimkimbilia na kumkumbatia miguuni. Halafu akawa analia " Elvine naogopa,,, naogopa,,, Kuna giza sana kwenye huu msitu.... Nataka kwenda nyumbani. Unaweza kunilinda mimi?"...

"We...we...we kijana ... Niachie nasema niachie .... Unanijua mim?.... Nasema toka kwangu...." Elvine alilalamika Kwa uwoga sana.

      Yule mtoto alimuachia Elvine na kuanza kuondoka. Nyuma yake yule mtoto alikuwa kavaa shati iliyokuwa imeandika Kwa maandishi mekundu yaliyorembwa vizuri sana * YOU MUST WIN THE BUTTLE BEFORE THE BUTTLE WINS YOU". 

Alistaajabu sana na wakati anashangaa alishtuka kutoka katika wimbi zito la usingizi. Na alipoangalia saa ilikuwa saa kumi jioni. 

*.    *.     *.     *

Alimkumbuka mkewe hivyo aliamua kujiandaa na kuelekea dukani kwa Elimina mke wake. Alitembea akiwa na mawazo sana juu ya ndoto aliyoiota. Maana alikuwa kapata utata. 

      Alifika dukani na Kwa furaha alimkuta mkewe ameketi dukani akiwa na yule binti anayewapenda sana aitwaye Erika. Aliwasalimu... Elimina alipomuoana Elvine alisimama na kwenda kumkumbatia kisha akamkaribisha kiti. Elvine aliketi jirani binti yule ambaye alikuwa mcheshi sana na muongeaji japo alikuwa na sura ya kipole sana. 

"Habari yako binti mdogo?"

"Kwanini umeniita Binti mdogo?"

"Nimependa tu. Hivi unasoma eeh?" Elvine alimuhoji maana alionekana na umbo dogo la kiuanafunzi.

"Ndio tena nasomea kitu kikubwa sana"

"Ni nini?"

"Ualimu"

"Mmmh! Ndio kitu kikubwa. Upo mwaka wa ngapi chuo?"

"Wa kwanza. Ila Kwa sasa tupo likizo"

"Oh vizuri sana. Unayaonaje masomo lakini?"

"Masomo ni magumu kwakuwa nasoma kitu kikubwa mno kuliko unavyodhani. Ila naamini katika kushinda kwa kuwa najua *I must win the battle before the battle wins me". Yule Binti aliongea maneno hayo Kwa harakaharaka sana. Jambo hili lilimfanya Elvine kutabasamu. Lakini alihisi kama Kuna neno kati ya maneno ya Binti yule kawahi kuyasikia mahali lakini hakujua alisikia wapi kwahiyo alijikuta akicheke tu.

"Wewe ni mjanja sana aiseee, unanifanya nikumbuka miaka mingi sana iliyopita nilipokuwa mdogo sana"

"Aishii... Mimi sio mdogo lakini!"

Muda wote huo Elimina alikuwa akiwasikiliza tu na wala hakujibu neno zaidi ya kucheka tu. Kisha badae akataka kuzungumza "yaani darling huyu Binti na wewe ndio mmekutana maana ni mcheshi sana hapa naona muda umeenda hebu twende nyumba...." Kabla hajamaliza alikuja mteja hivyo Elimina alisimama na kwenda kuhudumia mteja huku aliwaacha Elvine na Erika wakiendelea kupiga stori mbili tatu za utani. 

      Elimina aliporudi alimuomba Elvine amsaidie kuingiza baadhi ya vitu vilivyokuwa nje ya duka ili wafunge duka na kurejea nyumbani. Elvine aliposimama na yule binti alisema anahitaji kuwasaidia. Elvine aliona itapendeza sana. Walifunga duka pamoja na Kisha Erika aliwaaga na kwenda zake. 

      Elvine na mkewe walipanda gari lao na kurudi nyumbani walipofika tu nyumbani Elvine alikumbuka neno * YOU MUST WIN THE BUTTLE BEFORE THE BUTTLE WINS YOU". Akajiuliza hili neno nimewahi sikia wapi? Lakini likawa linapiga kelele akilini kwake. Akakumbuka kuwa amelisikia neno hilo kwa Erika lakini akilini mwake alikuwa anahisi ni kama aliwahi lisikia kabla. Alijaribu kukumbuka ni wapi lakini ikawa ngumu kutambua ni wapi. 

"Hey we kijana mzuri nini shida? Unawaza nini?" Elvine alishtuliwa na Elimina Kwa kupigwa kidogo begani maana alizubaa sana.

"Ooh hamna. Lakini yule binti ni mcheshi sana aisee. Hivi siku zote Huwa anakuwa hivi?"

"Ndio. Yaani we acha tu. Huwa akija dukani kwangu akakaa basi ni atanipigisha mastory ya kila namba" Elimina na Elvine walitazamana na kucheka. 

          Siku iliyofuata Elvine alipigiwa simu na mjomba wake Edger ambaye alimueleza kuhusu kifunguliwa tawi jingine kubwa la mabasi ya Babu yake Mr. Edward yaani "A QUALITY" na akamueleza kuwa yeye Elvine ndie atakae simamia mabasi hayo ambayo yatafika Dodoma mwezi unaofuata ambao ulikuwa ni mwezi wa tisa. Elvine alikubaliana nae na akaambiwa ajiandae kwaajili ya kikao kati yake na baadhi ya watu walioweka ubia kwenye kampuni hiyo Ili kuweka mambo sawa, Elvine alikuwa radhi kwa kila kitu maana pia alikuwa na nguvu ya ushawishi na wala hakuwa muoga wa kuzungumza na kujenga hoja zenye mashiko mbele za watu.

         Wakati anajiandaa na kazi hiyo. Baba yake alimpigia simu kuwa atakuja Tanzania kumsalimia mwezi huohuo wa tisa. Kwake aliona mwezi wa tisa ni kama mwezi wa baraka sana, maana alikuwa kawakumbuka sana wazazi wake. Alimueleza mkewe juu ya taarifa hizo zote naye pia akafurahia na kumpongeza mumewe. 

     Siku moja wakiwa nyumbani Elvine aliona nafsi yake kama ipo kwenye shida sana. Yaani inahangaika na akakosa amani kabisa. Hakuweza kumueleza pertnar wake maana hakuwepo alikuwa kaemda dukani. Aliona bora akalale ili atulize akili. Akiwa yupo mbioni kuusaka usingizi pale kitandani aliona popo kaingia chumbani na kuanza kurukaruka huku na huko. Alipata hasira maana aliona kapoteza usingizi wote. Aliamka na kutafuta mbao moja pana ambayo alitaka kuitumia kumpiga yule popo. 

"Yaani wewe kamnyama umenikosea sana maana mimi nimechoka halafu wewe unataka kunisumbua, sasa subiri nikuonyeshe kazi..."

Kusoma sehemu ya 18 bonyeza hapa.

Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.





Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.