HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23. Ilipoishia...... Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana.  "Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira.... Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto? Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa   Sasa inaendelea...... Elvine alikuwa anatetemeka  kwa hofu ya yale anayoyaona lakini alistaajabu kuona ni kama mkewe hajali sana kuhusu yeye. Alimtazama kwa makini sana mkewe akiwa anajaribu kutafakari kwanini anaonekana kuwa na hasira juu yake. Elimina akajishitukia "Hey, wewe! Nini sasa unanitazama hivyo?" "Nakutafakari sipati majibu!' "Nimefanyaje kwani?" "Hamna ila sijajua kama umenihofia mimi au hilo swali lako linamaana gani? "Elvine baba sina maana hiyo uliyoelewa wewe kabisa. Shida yangu mimi umefanya nini mpaka unataka kuhatarisha maisha Yako namna hii. Hujui namna ga

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA 16.

 

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.  

SEHEMU YA 16. 

Ilipoishia.....

     Sherehe zilianza na watu wengi sana walikuja tena wachungaji walikuwa wengi sana. Elvine alifurahi baada ya kumuona baba yake na mama yake wamekuja tena wakiwa wazima wa afya. Elvine pamoja na kufurahi lakini bado alikuwa na wasiwasi

 kusoma sehemu iliyopita bonyeza hapa.

Sasa inaendelea....

Alitazama Elimina namna alivyopenda akasema kimoyomoyo 'hakika malkia wangu usife mapema bado natamani kuona ulipendeza hivihivi daima'. Wakaingia kanisani ambapo aliyesimamia ibada ya send-off alikuwa ni mchungaji wa kanisa jilani. Lakini Elvine alikuwa na wasiwasi sana na yule mchungaji maana tangu alipofika alikuwa hawatazami watu usoni bali mda mwingi alitazama chini kama anayetunza sheria za familia. 

Elvine hakutaka kujaji saana lakini kuna namna alimkazia macho sana yule mchungaji maana kwa mauzauza tu yanayomuwinda aliona ni lazima amchunguze kila mtu anayemsogelea. Ghafla alitazama pembeni akaona kundi kubwa la malaika limezunguka eneo lile. "Haaa!  Waoh kumbe na mimi napenda sana na Mungu kiasi hiki?" alijisemea maana alijua Mungu kamfunulia yeye tu jambo hilo. 

Akiwa anawatazama malaika wale ambao walikuwa wanang'aa sana sura zao aliguswa begani na baba yake Mr. Edwin, "my son for the first day after a lot of years to see an angel, all its just for you" (mwanangu kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi kuona malaika, yote ni kwaajili yako). 

"Unawaona pia? "

"Ndio"

"Waoh! Sijui kwanini wamekuja wengi hivi?"

"Ndio ujue kuwa Mungu anampango mkubwa juu yako"

"Sasa baba unadhani ni kwaajili ya mimi tu kuwa mchungaji ndio haya yote yanatokea?"

"Siwezi sema neno, lakini Mungu pekee ndiye ajuaye"

Ibada iliendelea sana na yule mchungaji mgeni aliisimamia vizuri ibada lakini wakati yupo anasoma neno aliacha ghafla na anasema anaumwa. Kila mtu alishangaa kwanini mchungaji kaumwa madhabahuni. Wakati anashuka pale madhabahuni alidondoka na kupoteza maisha. Taharuki zikaanza "mchungaji kafa madhabahuni... Mchungaji kafa madhabahuni..." kila mtu alitoka na lake, labda ni Mungu kamchukua.. Au labda alitenda dhambi... Kila mtu alisema cha kwake. 

Elvine mwenyewe hakujua nini kimetokea. Alitazamana na baba yake wakastaajabu. Yule mchungaji akapelekwa hospitali ikabidi mchungaji Moses mwenyewe asimamie ibada ile ya sendoff ya binti yake. Ibada ikisha watu wakatakiwa kwenda ukumbini alafu kuhusu yule mchungaji aliyekufa walipoteza kwanza maana alikuwa anatokea kijiji jirani sio pale. Usiku watu walikwenda ukumbini na sherehe zilipamba moto sana. Elvine kila alipotazama kushoto na kulia alizidi kuona wale malaika. 

Akafumba macho kwa hisia sana alafu akajisemea kimoyomoyo "Elvina natamani kukuona nijue kunanini hapa" alipofumbua macho alimuona Elvina(malaika wake) kaka karibu yake. Neema ya Bwana iwe nawe!" yule malaika alimsalimu

" Amina" Elvine alijibu

"Kuna vita kubwa huko nje, unataka kuona?"

"Vita tena? Nani anapingana na kwanini?"

"Mimi nisingeweza kukutetea peke yangu maana wewe unagombaniwa na falme mbili. Alafu maajabu sana haya... Mungu ndio kakuumba, lakini shetani anakung'ang'ania kweli yaani"

"Mbona mimi sioni hiyo vita!? Au inapiganiwa mawinguni huko? Elvine aliongea kwa kutabasamu kama utani vile"

"Elvine huu sio utani, unazungumzia mawinguni wakati kuna mtu kafa unaona?"

"Unamaana gani?"

"Mchungaji kafa bila hatia yule. Wala hakuwa mtu mbaya kama unavyozani wewe. Yule mchungaji alikuwa na wasiwasi maana pekee alipata neema ya kuona vita ilivyokuwa inaendelea. Alikuwa akiomba sana hili jambo lifanikiwe, maadui walipambana zaidi na madhabahu na mwisho yeye alikuwa tayari kufa maana alijua thamani ya wewe kuishi ndio maana alijitoa kuja kusimamia harusi. Yeye alijua fika kuwa madhabahu itakuwa na vita na akataka kuzuia ubaya usifanyike lakini wakati tuko bize kukusaidia wewe yeye tulimpoteza. Ila hakika nakwambia nafsi yake imepumzika salama mikononi mwa malaika wa Bwana.* Kuna mambo yanatokea ili wewe ujifunze lishike hili*"

"Sasa kwanini nyie mnanithamini sana mimi?"

"Malaika ni mtumishi wa mwanadamu kwahiyo wewe lazima uwe salama maana umekusudiwa kupambana na ushetani hapa duniani. Na haupo pekeako. Ila kila mmoja yupo mahali fulani mahususi"

"Mmh! Naogopa"

"Usiogope!"

Elvine alitazama nje na ndipo alipoona vita kali ikipigwa kati ya malaika wa giza na malaika wa nuru. Elvine alishangaa sana na ndipo alipoanza kujua namna gani yeye ni wathamani mbele za Bwana. Sherehe zilienda vizuri kabisa na baada ya sherehe Elvine na Elimina pamoja na wazazi wao walipanda gari usiku huo kurudi Dar es Salaam kwaajili ya kujiandaa na harusi siku iliyofuata. 

Walifika salama na maandalizi yakawa mazuri sana. Mda wa harusi ulifika na hakuna jambo baya lililo jitokeza. Walienda kanisani na harusi ikafungwa vizuri tu. Wakatoka kanisani mapaka ukumbini ambako walikula na kuinjoi sana huko. Baada ya sherehe kuisha Elvine na mkewe walikabidhiwa nyumba moja kubwa na Edwin ambayo ilijengwa dodoma. Pia babu wa Elvine (Edward) aliwakabidhi gari la gharama sana. 

Elvine aliondoka na mkewe usiku huo na kwenda kwenye hoteli moja kubwa sana ambayo walilipiwa kukaa hapo kwa wiki moja ndipo waondoke kwenda kwenye nyumba yao. Waliishi vizuri wiki hiyo hapo hotelini tena kwa furaha sana. Walipomaliza fungate yao walipanda gari lao na kwenda zao Dodoma walikojengewa nyumba yao. 

Walikuta nyumba imepambwa kwa mauwa ya kila namna. Wiki zile za mwanzo walizima simu na hawakutaka usumbufu kutoka kwa mtu. Baada ya mwezi waliwasha simu zao na kuanza mawasiliano na watu tofautitofauti. 

Elvine na Elimina walikuwa wakiishi wenyewe bila hata ya mfanyakazi japo nyumba yao ilikuwa kubwa sana. Kwakuwa Elvine hakuwa anafanya kazi yoyote kwa wakati huo basi walikuwa wakifanya kila kitu pamoja pale ndani na wala hawakuchoka. 

Baada ya miezi miwili Elvine alifungua duka la jumla ambalo alimkabidhi mkewe wakati yeye akifikilia cha kufanya kikubwa zaidi. Kila siku alimpeleka mkewe dukani na kurudi nyumbani. Mchana alikwenda kumuona na jioni alikwenda kumfuata. 

Siku moja kuna binti mmoja alivutiwa sana na maisha yao, akawa mteja maarufu wa Elimina na kutokana na yale maisha aliyokuwa anaona wakiishi alimuomba Elimina ampe siri ya mafanikio yao. 

"mdogo wangu, najua wewe bado huja olewa, ila siri ya upendo wa kweli ni ule uliojengwa katika misingi ya Kristo"

"natamani kuja kuishi kama nyie dada" 

" yawezekana mbona! Cha msingi okoka kwanza. Mungu atakupa mume bora" 

"ni kweli eeh?" 

"Yes"

Elimina baada ya kutoka dukani siku hiyo alikuja kumsimilia mumewe juu ya binti aitwae Elika ambaye kavutiwa na maisha yao na kaokoa kwaajili hiyo. Walifurahia sana yale maisha. Elvine alisahau hata kazi iliyomleta duniani. Alikuwa bize sana kutafuta kazi kubwa ya kufanya. 

Siku moja akiwa amelala aliota moto mkubwa inawaka ndani ya maji lakini ule moto ni kama unaofifia kwa kuzidiwa na yale maji. Alipoamka akakimbuka kuwa hatakiwi kuzima namna hiyo na akajikuta kakumbuka sana vile viusumbufu vya kivita na maadui. Lakini hakujua kumbe kuna bomu kubwa kaandaliwa..... 

Kusoma mwendelezo wake bofya hapa!.

Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mtunzi wa Hadithi (simulizi) .

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            &, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kuboresha na kujifunza zaidi.




Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.