HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 23. Ilipoishia...... Alipofika nje, alimkuta Elimina katahamaki sana tena anahasira sana.  "Umefanya nini Elvine? Elimina aliuliza kwa ukali sana tena hadi macho yalikuwa mekundu kama damu kwaajili ya kujaa hasira.... Swali; kwanini Elimina anahasira? Na Elimina huyu anasiri gani na nyumba iliyoungua moto? Kusoma sehemu ya 22 bonyeza hapa   Sasa inaendelea...... Elvine alikuwa anatetemeka  kwa hofu ya yale anayoyaona lakini alistaajabu kuona ni kama mkewe hajali sana kuhusu yeye. Alimtazama kwa makini sana mkewe akiwa anajaribu kutafakari kwanini anaonekana kuwa na hasira juu yake. Elimina akajishitukia "Hey, wewe! Nini sasa unanitazama hivyo?" "Nakutafakari sipati majibu!' "Nimefanyaje kwani?" "Hamna ila sijajua kama umenihofia mimi au hilo swali lako linamaana gani? "Elvine baba sina maana hiyo uliyoelewa wewe kabisa. Shida yangu mimi umefanya nini mpaka unataka kuhatarisha maisha Yako namna hii. Hujui namna ga

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI NA TANO.

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.  

SEHEMU YA KUMI NA TANO. 

Ilipoishia...

Usisogee maana hapo unaposogea ndipo nataka kudondokea kwahiyo pishaaa!!" Kabla hajayatafakari yale maneno yule mtu alijiachia makusudi kabisa na kujitupa chini. Elvine alishangaa zaidi. Alitaka kusogea ili akatoe msaada lakini yule mtu ghafla alipotea. 

       Elvine alipata hofu zaidi. Akakimbia mpaka chumbani kwake na akajihisi kabisa hadi ile kiu imekata. Lakini alipofika chumbani kwake alipigwa na butwaa kwa kile alichokuwa anakiona mbele yake na wala hakuamini kwa haraka....

Kusoma sehemu ya 14 bonyeza hapa

Inaendelea...

    Alipotazama kitandani kwake alimuona kijana yule aliyekuwa kaanguka mchana na ndiye aliyemuona kajiangusha muda sio mrefu kutoka kwenye ngazi tena akiwa anacheka sana.

      "Kumbe ni wewe? Unajua nilikuwa najiuliza sana kuwa ni kijana yupi ambaye anakaa hapa na anauwezo wa kufanya mambo makubwa. Kwakweli nimekupenda, nadhni kazi nimeikamilisha. Kwasasa naenda lakini nitakurudia" aliongea maneno hayo yule kijana kisha akatoweka machoni pake.

      Elvine alikuwa kama mtu aliyekuwa kapigwa na butwaa maana hakuwa anaelewa chakufanya wakati huo. Alibaki kasimama pale kwa muda Kisha woga ulipoisha akajipa moyo kuwa ilikuwa ni ndoto tu. Akajikaza na akaamua kulala. Aliwa amelala aliota ndoto

     ""Kulikuwa na nyumba moja kubwa sana ambayo ilikuwa ni ya kisasa zaidi. Elvine alijiona akitoka ndani ya nyumba hiyo huku akiwa amepanda gari moja zuri sana. Alipofika nje alikuta watu wengi sana wakiwa na matatizo ya kila namna akamwambia dereva wake, "kwanini hawa wako hapa?" Dereva akasema "wamegoma kwenda kukusubiri kanisani kwahiyo wameamua kuja nyumbani kwako"

       Alishuka  kutoka kwenye gari na akaanza kuwagusa vichwani, mara wote wakawa wazima. Alitabasamu na kuingia kwenye gari lake. Alifika kanisani kwake ambako alipokelewa kama mfalme na alipolitazama kanisa alitabasamu maana lilikuwa kanisa la ghorofa na lilivutia hata kwa kulitazama, alifurahi sana""

       Elvine alishituka kutoka kwenye ndoto hiyo na kushangaa sana lakini aliamini kuwa hayo ni maono ya maisha yake ya badae. Alilala vizuri sana usiku huo.

      Zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya harusi yake Mr Edward alimwambia Elvine aondoke pale nyumbani akakae hotelini kwaajili ya maandalizi ya harusi. Alikwenda hotelini ambako alikuta wahudumu  kwenye chumba chake na huko alihudumiwa kila kitu na alikutana hadi na wataalamu wa kutengeneza ngozi kwa mafuta mbalimbali na perfume. Alimpigia simu babu na kumuuliza kwanini anamfanyia mambo makubwa hivyo lakini aliambiwa kuwa Mr Edward anafanya hivyo kwakuwa kwake yeye ni kama anafanya harusi mbili yaani anatumia gharama za harusi mbili yaani yakwake na ya mama yake Editrin. Alishangaa sana

       Siku iliyofuata asubuhi alitembelewa na wageni watatu ambao walionekana dhahiri kuwa ni watu wenye pesa. Hakushangaa maana alijua ni rafiki wa babu yake maana hakuna mtu mwingine ambaye alijua kuwa yeye yupo hotelini ila zaidi ya babu yake.

      Aliwakarimu na kuwakaribisha vizuri sana. Alikaa kwenye sofa safi zilizokuwepo kwenye chumba alichokuwa anakaa na kuanza mazungumzo.

       "Elvine u mzima wewe?"

       "Mimi mzima sijui nyie?"

       "As you see(Kama unavyoona)"

       "Tuna jambo kubwa sana na wewe."

       "Jambo gani hilo?

       "Wewe ni mtu ambaye unanyota Kali sana na tumejaribu sana kuichukua kwako lakini imekuwa ngumu sana kwetu Sasa tunaofa kwako"

       "Nyie ni akina nani?"

       "Sio muhimu kujua hilo Elvine. Cha msingi ni kuwa sisi tunamuhitaji wewe kwahiyo unatakiwa ukubaliane na tunachokitaka. Halafu sisi tumekufatilia muda mrefu sana maana tulisikia kuwa kunamtoto kuzaliwa mwenye uwezo wa kufanya mambo makubwa sana. Na pia yule kijana tulimtuma sisi yaani tulimvunja makusudi ili tukupime wewe na jambo ile hatukujua kama litaleta hasara maana kwaajili yako ulifanya watu wakaacha njia zetu na kuokoka, sasa wewe ni mtu wa muhimu sana kwetu"

      "Kwahiyo mnataka kusema kuwa yule kijana hakuwa mtu?"

      "Hapana ila tulimpandikiza roho fulani ya kufanya jambo asilolijua. Lakini cha msingi tunataka wewe uungane na sisi maana unatuharibia sana Elvine. Hata hivyo yule kijana bado tunae na tunamtumia sisi kwahiyo ili awe huru lazima uwe na sisi. Kumbuka kuwa kesho ni ndoa yako. Kwahiyo kuwa makini na hili"

     Elvine hakuwa anaogopa kabisa mwanzo lakini baada ya kugusiwa kuhusu suala la ndoa yake moyo wake ulipigwa ganzi ya baridi hadi akahisi baridi mwili mzima. Aliinama chini na ndipo alipoikumbuka ile ndoto

     ("Mimi ni Elimina Elvine nimekuja kukusalimia" yule skeleton aliongea

        "Hapana wewe sio Elimina"

        "Sikudanganyi mimi ni Elimina ila naomba unisaidie"

        "Hapana wewe sio Elimina nasema").

       Elvine aliogopa sana maana alijua kabisa akifanya mchezo kisasi kitarudi kwa mkewe mtarajiwa.

       "Sikiliza kijana hatuna muda wakupoteza kabisa hapa cha msingi tunataka jibu lako lasivyo upo hatarini na sisi hatutakuumiza wewe ila tutahangaika na watu wako wa muhimu. Tunachotaka ni wewe kutumika na sisi. Unakumbuka ndoto uliyoiota mara ya mwisho? Nadhani unakumbuka. Tutakupa vile vitu vyote ulivyoviona na maisha yako yatakuwa ya tofauti na si hivyo tu, tutakupa upako zaidi ya hapo yaani hutatumia nguvu kubwa kuponya watu na utatuvunia watu wengi tukiwa na wewe. Lakini pia sisi tupo tayari kukupa uongozi kwenye himaye yetu moja ya hapa Dar es salaam. Sisi hatukubembelezi saaana lakini tunamaanisha kabisa"

       "Hapana.... hapana....nasema hapana mimi siko tayari kuiuza huduma yangu kwa mashetani Elvine alisema huku kasimama kwa gadhabu

       "Nani kasema sisi ni mashetani?"

       "Kila kitu kinaonesha hadi sura zenu zimejaa ushetani. Tokeni kwangu sitaki kusikia vitisho vyenu"

       "Waooh!! Upo vizuri kijana. Hivi unakumbuka mauzauza ya wiki iliyopita? Sasa yatakuwa zaidi maana ile siku tulikuja kuchukua nyota yako lakini tulishindwa na tunajua hatuwezi lakini subiri utajionea yatakayojiri kwenye maisha yako. Namba yetu ni hii 666000999. Utatutafuta yakikushinda" wale wababa walisimama na kuondoka zao.

       Elvine alichanganyikiwa sana. Hakujua atafanya nini. Alifikiria ndoa yake ambayo imeshawadia kasolo masaa tu. Aliogopa sana. Siku hiyo Elvine alipiga magoti akaomba pasipo kuchoka tena kwa uchungu sana huku akiwa anaihofia ndoa yake. Aliomba masaa 12 pasipo kuchoka mpaka alipojikuta kapoteza fahamu pasipo kujua. Alishituka saa 10 usiku baada yakuamshwa na wahudumu wa hoteli kwaajili ya kuanza maandalizi ya harusi yake. 

     "Haaaa inamaana nimeomba mpaka nikapoteza fahamu kweli? Hivi jana sikuenda kwenye send-off ya Elimina? Kwanini hawakuja kunichukua wakati babu alisema atakuja? Mungu wangu sasa Elimina atanielewaje katika hili?"

      Alikuwa kashangaa tu na asijue kilichotokea wakati alipokua kazimia. Alitazama simu yake na kukuta missed call kama 29 kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Elimina, babu yake, mama yake na pastor Moses. Alifungua upande wa meseji na akakuta message 66. Meseji ya mwisho ilikuwa imetumwa na babu yake.

     ""We Elvine mimi nimeshindwa kuja kukuchukua huko maana nimechelewa kutoka sasa wewe tangulia kwenye send-off alafu mimi nitakuja baadaye maana send-off itaanza saa 5. Najua unaweza ukawahi hata saa 6 maana dereva wangu yupo vizuri atakupeleka""

      Haaa, hapana haiwezekani kuwa hivi. Huyo dereva alikuja kweli? Kama alikuja lazima wangetambua kuwa nimezimia hapa ndani. Hapana....sio kweli.....kuna uongo hapa umefanyika haiwezekani.

      Alitoka nje na kukutana na dereva ambaye alimchukua na kumpeleka saloon. Wakiwa kwenye gari alimuuliza dereva kama jana alikuja hotelini. Lakini derava alisema yeye hakuwa na taarifa yoyote labda kama Mr. Edward alisahau kumwambia. Alishangaa sana maana kila kitu kilizidi kumchanganya.

      Alifikishwa saloon na akaandaliwa tayari kwaajili ya kupelekwa kanisani. Akiwa kwenye gari alichati na Elimina na akamuomba msamaha kwa kilichotokea na kwa kifupi akimueleza kilichotokea lakini hakueleza kila kitu. Elimina hakuwa na shida na alisema hakuna kilichoharibika. 

      Alifika kanisani lakini wakati anaingia aliona mule ndani kama kuna moshi lakini cha ajabu ni kuwa watu walikuwa bize sana na hakuna aliyeona tukio hilo. Alianza kuogopa lakini alijikaza huku akiomba kimoyo moyo ili usalama uwepo na harusi yake ifanyike salama. Alipofika mbele ya kanisa aliwaona wale wababa waliomjia jana asubuhi wapo pale, tena wanatabasamu sana aliogopa maana alijua tu kuwa wale 'vigagula'(wachawi) watakuwa wamepanga jambo. Alijikaza huku akiongeza maombi moyoni.

      Alishuhudi kuona mchungaji anakabwa na tai aliyokuwa ameivaa mpaka akaishiwa pumzi na kudondoka chini lakini watu hawakuwa wanaona tukio hilo maana hawakushituka kabisa na aliona namna ambavyo mchungaji mwingine akija na kuchukua nafasi ya yule mchungaji wa mwanzo lakini cha ajabu huyu wa pili alifanana sana na yule wa mwanzo yaani kama mapacha vile.

      Alipata wasiwasi lakini huyu wa pili hakutumia biblia iyokuwepo pale madhabahuni bali alikuja na biblia yake na ile ya pale madhabahuni alisema itolewe na wahudumu wa pale ndani. Cha ajabu zaidi ni kuwa yule mchungaji aliyedondoka hakuguswa na mtu bali aliachwa palepale chini. Elvine akajua kuwa tayari utawala wa mapepo umevamia kanisa. 

      Wakati hajui afanye nini yule mchungaji alianza kufungisha ndoa. Na ndoa ikakamilika vizuri tena kwa amani. Wakati wanatoka pale kanisani yule mchungaji alisema

      "kwaherini muende mkaishie. Elvine utajuta" halafu akaondoka pale madhabahuni

      Elvine aligeuka na kumtazama sana yule mchungaji, na kisha akatazama watu ambao walikuwa wakicheka kana kwamba yale maneno yamewachekesha maana walijua kuwa mchungaji anamtishia Elvine maana ndoa sio kitu chepesi.

      Elvine alisikitika sana lakini hakuwa na namna. Alitoka na mkewe kisha wakarudi saloon ili kujiandaa na safari ya ukumbini. Wakati huu walikwenda saloon moja yeye na mkewe tena wakiwa nafuraha sana. 

       Baada ya maandalizi walitoka ili wakapande gari waanze safari ya ukumbini. Elvine alitoka kwanza kisha Elimina akafuata. Elvine akiwa kwenye gari na dereva wakiwa wanamsubiri  Elimina walikuwa wanatabasamu tu na kupiga stori mbili tatu pamoja na msimamizi wake. Ghafla dereva aliwasha gari na kuanza kuliendesha jambo ambalo liliwashangaza Elvine na msimamizi wake.

     "We nini shida mbona umewasha gari ghafla"

     "Mimi sijaliwasha na wala hata sielewi kwanini linatembea wakati mimi siliendeshi na hata kulisimamisha siwezi" dereva alijibu kwa woga sana. Ghafla mlio mkubwa ulisikika 

     paaaaaaah!!!!! Na ndipo gari liliposimama. Hakuna aliyeamini kilichotokea maana Elimina na msimamizi wake walikuwa chini na hakuna aliyekuwa na fahamu kati yao. Elvine alishuka haraka na kumfuata mkewe pale chini lakini aligundua kuwa kapasuka vibaya kichwani kuliko hata yule msimamizi ambaye alionekana kabisa kaumia kidogo sana.

      Elvine alihisi kuchanganyikiwa alipiga kelele kama chizi kwa kilio. Na mbele ya macho yake alishuhudi kuona mkewe akipoteza maisha mikononi mwake. 

      "Hapana..... hapana sio kweli.... Huwezi kufa ....nasema huwezi.....amka please amka..... Nisikilize Elimina huwezi kupoteza ndoto zako kama hivi.... Wewe si ulisema unanipenda mimi sasa kwanini unanisaliti kama hivi? Amka amka amkaaaa" Elvine alilia sana

       Alipotazama pembeni alimuona baba mmoja kati ya wale watatu akiwa kasimama na mkewe lakini mkewe alikuwa kafumba macho ila kasimama wima pembeni ya yule baba. Aligundua kuwa mkewe yupo sehemu mbili yaani pale chini na kwa yule baba.

       "Elvine nakupa nafasi ya mwisho. Mke wako ninaye mimi. Bado unanafasi yakumsaidia kama hutajali" alisema yule baba kisha akapotea. Elvine aliacha kulia na kufuta machozi. Watu wengi walikuwa wameshajaa eneo la tukio, walipotaka kumchukua mkewe ili apelekwe hospital Elvine aliwaambia wamuache. Watu walijua dhahiri kuwa amechanganyikiwa kwahiyo wakawa wanalazimisha kumchukua Elimina.

      Baba yake Elvine na mama yake Elvine (Edwin na Editrin) walifika eneo husika na wakawazuia wale watu kumchukua Elimina. Edwin alimwambia mwanaye kuwa anamuamini kwahiyo anaweza kumsaidia mkewe na akawa mzima.

      Elvine alilia sana na akasema "baba Elimina hayupo hapa... Wamemchukua mke wangu"

      "Wakina nani?"

      "Wauwaji"

      "Nawewe mchukue kutoka kwao"

      "Kivipi baba....nawezaje?"

      "Kwani wao wamewezaje?"

      "Baba"

      "Nini? Kwani wewe, wao na Mungu nani ana nguvu? Kama kaibiwa basi na wewe muibe. Huna muda fanya haraka kabla hawajamuiba kiukweli maana najua bado hajafika mbali"

       "Hivi baba unaelewa nachomaanisha mimi? Yaani kifo cha mke wangu kimepangwa na watu."

       "Kwani wewe na Mungu hamuwezi kukipangua?"

        "Mimi siwezi baba"

        "Ila Mungu akiwa ndani yako si unaweza?"

         Acha kulia kama mtoto wakati unaweza kufanya jambo. Elvine alifuta machozi na kupiga magoti pembeni ya mkewe huku akisema "baba upo sahihi natakiwa kumuiba pia kutoka kwao"

           *    *   *

         Elvine alishituka kutoka kwenye ndoto hiyo akiwa anahema sana. Aligundua kuwa alikuwa analia kweli na alijikuta palepale chini hotelini alipokuwa amepiga magoti baada ya wale wababa kuondoka. Alipotazama saa ilikuwa ni saa 2:30 asubuhi yaani aliomba saa moja na akapoteza fahamu kwa nusu saa tu na kuota ndoto hiyo ya ajabu. Aliogopa sana na alianza kupata wasiwasi kuhusu ndoa yake ambayo itafanyika siku inayofuata. Alijiandaa na gari lilifika kwaajili ya kumchukua na safari ya kwenda Iringa ilianza ili akahudhurie send-off ya Elimina. Alimuomba dereva asimuongeleshe njia nzima maana yeye aliinama chini kuomba mpaka walipofika Iringa ambako alipokelewa vizuri kwaajili ya sherehe hiyo. 

     Sherehe zilianza na watu wengi sana walikuja tena wachungaji walikuwa wengi sana. Elvine alifurahi baada ya kumuona baba yake na mama yake wamekuja tena wakiwa wazima wa afya. Elvine pamoja na kufurahi lakini bado alikuwa na wasiwasi sana. 

     Ghafla paaaaaap!!!! Kuna jambo likatokea.....

  Kusoma sehemu ya kumi na sita bonyeza hapa.

Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo, mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            Na, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kujifunza na kuboresha zaidi.

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.