MAAJABU YA AKIBA

SEHEMU YA KUMI NA TATU.
Ilipoishia..
Ghafla
mama aliingia na kushangaa kwa kile alichokiona
"Nyie
watoto ni upuuzi gani mnafanya hapo?....."
kusoma sehemu ya kumi na mbili bofya hapa
"Samahani mama sio kama unavyofikiria.
Ni kwamba Elimina hajisikii vizuri. Na alikuwa akilia na mimi sijui shida ni
nini na ndio maana nilitaka aniambie" Elvine alijaribu kujitetea
"Jiandaeni kwaajili ya kikao cha
familia akija baba yenu" mama aliongea kwa mkato kisha akaondoka na
kuelekea chumbani.
Elimina naye baada ya mama kupita
aliondoka na kwenda chumbani kwake kwahiyo Elvine akajikuta amebaki pekeyake
pale sebuleni.
Alikaa kwa muda akiwa hajui hata
anachowaza. Ilipofika saa 6:00 aliamua kuondoka na kwenda kulala.
Asubuhi aliamka na akawa anatamani sana
kuongea na mama ili amuelekeze vizuri asije akaendelea kumtazama vibaya maana
alishapata uwoga sana kuhusu mtazamo wa mama juu yake.
Alitoka sebuleni na akamuona mama
akienda jikoni. Alimfuata mpaka jikoni na akamkuta akiwa anawasha moto kwaajili
ya kuandaa chai ya asubuhi.
"Samahani mama naomba
tuzungumze"
"Kuhusu nini?"
"Mama naomba unielewe. Sikuwa na
maana mbaya kumzuia binti yako asilie maana kweli kabisa Elimina alikuwa akitia
huruma. Halafu Elimina ni rafiki yangu tu mama naomba usiniwazie vibaya"
"Kwani mimi nimesema nini? Mbona
maelezo mengi?"
"Mama Mimi naelewa wewe kama mzazi
hupendi mwanao aharibikiwe lakini Nina jambo. Naomba uniwasilishie kwa baba
pindi akirudi"
"Nikuwasilishie kuhusu
nini?"
. "Nahitaji kuoa kwenye hii
familia"
"Na nilijua tu."
"Naomba sana mama"
"Ni kweli lakini kwanza lazima
utambue kwanini Elimina anakuchukia na huwa anaumia sana pindi akikutazama
halafu ndiyo ujue kama atakubali kuolewa na wewe"
"Kwani kuna jambo ambalo lilitokea wakati mimi
sipo?"
"Sina jibu sahihi lakini
kamuulize yeye mwenyewe utapata jibu"
"Mbona unanitisha mama?"
. "Kwanini sasa?"
"Ok sawa! Nitalifanyika kazi
hilo"
"Elvine alitoka jikoni huku
akiwa anawaza, hivi ni nini kilichotokea? Ndio maana Elimina anaonekana hana
amani kabisa. Nahisi kuna jambo zito sana hapa. Ngoja nipeleleze, na lazima
nijue japo Elimina ni mgumu sana kueleza mambo yake kwangu"
Elvine wakati akiwa katika mawazo
hayo alijikuta akigongana na Elimina sebuleni.
"Ooh! Sorry Elimina... Eti
unausingizi?"
"Kwanini?"
"Naona unasinzia huku unatembea
"Mmh! Kwanini?"
"We unazani kwanini
tumegongana?"
"Basi hata wewe unasinzia ndio
maana huoni mbele" Elimina aliongea kwa masihala kidogo.
Elvine alicheka lakini Elimina
alitabasamu kidogo na kuondoka.
Ilopofika saa 7; mchana Elvine
alikwenda kwa mama na kumwambia kuwa anahitaji kutoka na Elimina japo anahisi
haitakuwa rahisi kwa Elimina kukubali kwahiyo anaomba mama amsaidie kumfanya
Elimina aweze kukubali.
Mama alimtazama sana Elvine kwa muda
kabla hajakubali ombi lake. Kisha akamwambia.
"Elvine, wewe ni nani
hasa?"
"Kwanini unauliza hivyo mama?
"Unatakiwa kuondoka hapa
nyumbani haraka maana watu wataanza kujaa hapa nyumbani hivi Karibuni"
"Unaongea kuhusu nini mama"
"Leo nilikuwa huko sokoni.
Nikakutana na wamama wawili pamoja na vijana Kama wanne hivi wakiwa
wanakuulizia. Sasa waliponisimamisha
sikuwa najua kama wataniuliza kuhusu wewe. Lakini nilishangaa waliponionyesha
picha yako na kuniambia unamjua huyu? Mwanzo nilihisi polisi lakini baadaye
nikajua tu kuwa wale sio polisi kwa namna walivyokuwa wanaonekana.
Niliwajibu ndio. Baada ya jibu langu
wale watu walifurahi sana. Na wakanishukuru sana. Waliomba niwaambie
unapopatikana na mimi nikawaambia kuwa wewe ni kijana wangu. Mmoja wao alisema
kuwa nnabahati sana kuishi na kijana kama wewe. Nilipouliza kwanini waliniambia
wanahitaji kupafahamu kwangu. Nilikuja nao mpaka hapo nje. Lakini hawakuingia
ndani. Tukiwa hapo nje ndipo walipoanza kunieleza kuhusu mambo uliyoyafanya
wakati umefika Iringa. Nilistaajabu sana maana hata mimi nilisikiaga kwenye
taarifa ya habari lakini sikujua kama ni wewe"
"I am sorry mama kwakuwa sikuwahi
kuwaeleza kuhusu suala hili. Lakini ni kweli mama. Mimi ninabaraka fulani za
kipekee kutoka kwa Mungu na mara nyingi nimefanya mambo mengi sana ambayo hata
mimi sikujua nimewezaje ila ni kwa nguvu za Mungu tu"
"Sawa lakini najua wale watu
watarudi. Na pindi wakirudi hawatakuja peke yao bali watakuja wengi sana na
mwisho tunaweza jenga hospitali hapa"
"Ni kweli lakini pasipo Elimina
mimi hapa kuondoka itakuwa ngumu"
Lile neno lilimpa kigugumizi mama na
asijue cha kueleza. Wakati huo Elvine aliongea akiwa kamkazia macho mama.
"Lakini katika taratibu zetu za
kuoa binti wa kihehe lazima wazazi wako ndiyo wahusike"
"Mimi hapa nipo mimi tu. Na kila
kitu ni nyie na mimi ndiyo tutakao shughulikia. Maana hapa Tanzania mama wala
baba hawapo. Labda mambo yakiwa sawa basi babu yangu atashughulikia kila
kitu"
"Sawa basi, lakini lazima ujue
kwanza Elimina anawaza nini"
"Naomba msaada wako basi mama
eeh?"
"Mmmmmh! we mtoto mbona unanitia
majaribuni? Aya sawa basi"
Mama na Elvine walitazamana kisha
wakatabasamu na mwisho waliangua vicheko.
Mama alitoka jikoni na kumuita Elimina
kumueleza kuwa yeye anatoka kidogo kwahiyo anahitaji watoke wote pamoja na
Elvine maana kuna mahali anataka awapeleke.
Elimina akakubali kwahiyo akaenda
kujiandaa. Wakati huo Elvine alikuwa kajificha jikoni anachungulia sebuleni.
Mama alimpa ishara kuwa ajiandae haraka kutoka. Elvine alitoka mbio mpaka
chumbani. Alipofika chumbani alichukua begi lake na kumwaga nguo zake zote
kitandani.
Alitazama suti zake na kila
aliyoishika aliona kama haifai. Alianza hadi kuchanganyikiwa maana alijihisi
kama hana nguo licha ya kuwa na nguo nyingi sana.
"Sasa hapa nitavaa nini mimi
jamani? Leo nataka niwe tofauti sana lakini naona kama ni ngumu kwangu.
Daah!" Baadaye alipata wazo. Akachagua suti moja ya bluu ya kawaida tu
Kisha akaipasi vizuri na akaanza kujiandaa kwaajili ya mtoko huo.
Ilipofika saa 9:30 kila mmoja alikuwa
tayari amejiandaa. Elimina ndiye aliyependeza kuliko wote siku hiyo hadi Elvine
akajiona hajapendeza. Walipofika mlangoni kwaajili ya kutoka walikuja wageni
wanne wakiwa wamebebe wagonjwa wawili.
Wale watu walikuja kwa Elvine ili
wamueleza kuwa wanahitaji msaada wale. Kwakweli Elvine alitamani kulia na
kuwafukuza maana aliona mipango yake inaharibika.
Alimtazama mama ambaye kwa wakati huo
hakujibu neno bali alionekana wazi kabanwa na kicheko ila anajizuia tu. Elimina
yeye hakuwa anaelewa chochote kwahiyo aliona ni sawa tu hivyo akafungua mlango
na wageni wakaingia ndani.
Elvine alikaa na wageni sebuleni na
kuanza kuongea nao huku akiwa na maumivu moyoni.
Wale watu waliianza kumueleza namna
wagonjwa wao walivyoanza kuumwa. Elvine alijikuta kapata moyo wa huruma
baada ya wale watu kumueleza kuwa wale
wagonjwa ni wazazi wao na walianza kuumwa baada ya mjomba wao kutamani mali zao
na kuanza kulazimisha kuzichukua kwa nguvu. Lakini baada ya kunyimwa alisema tu
lazima atazipata zile mali, na haikuchukuwa muda toka mjomba wao aseme hivyo
wazazi wao walianza kuumwa. Na baada ya kuumwa walipolwa mali zote na mjomba
wao maana hawakuwa na wakili wa kuwatetea na isitoshe hawakuwa wamesoma,
kwahiyo hawakujua ni wapi wanaweza kudai haki zao.
Wakati wale wageni wanaongea hayo.
Elimina alikuwepo pembeni anasikiliza. Elimina alipata huruma sana na machozi
yakamtoka. Elvine alipomtazama Elimina na kumuona analia alijikuta anatabasamu
kimoyo moyo.
Elimina alisogea pale na kuketi
karibu na wagonjwa lakini alikuwa hajui
kabisa kuwa Elvine anauwezo gani kwahiyo alihisi wageni wale hasa walikuwa
wanamuhitaji baba yake.
"Poleni sana. Lakini yupo Mungu
anayeweza kuponya na kuondoa huzuni zetu. Sisi tutawaombea japo mchungaji
hayupo. Lakini imani zenu ndizo zitakazo waponya wazazi wenu maana sisi
hatuwezi chochote bali ni Mungu tu" Elimina aliongea hivyo kwa kuonesha
hisia na huruma.
Elvine alikuwa akizidi kufurahia
maneno ya kitumishi na hapo ndipo akaona kumbe yeye anaweza kuwa mchungaji.
Maana Elimina alizungumza kama mama mtumishi.
Elvine alijikuta kapata nguvu hata ya
kuomba. Alisimama na kuanza kuomba. Na alipomaliza kuomba ndipo alipowagusa
wagonjwa wale nao wakawa wazima.
Elimina alishangaa kidogo maana
hakuelewa namna wale wagonjwa walivyopona. Alimtazama sana Elvine ambaye bado
alikuwa uweponi. Baada ya uponyaji wa watu wale basi waliondoka zao. Elvine
alikwenda chumbani kwa mama kugonga wakati Elimina akiwasindikiza wageni kidogo
na kuwatia moyo.
"Mamaaa!! Sahizi bado mapema
naomba tusiahirishe jamani"
"Saa ngapi kwani"
"Ni kumi na moja kasolo chache.
Please mama"
"Mmmh!! Tutaenda kesho, hapana
mama haiwezekani. Basi nitakununulia zawadi nzuuuuri ila we nisaidie tu"
"Aya nakuja" Elvine
alifurahi sana baada ya jibu la mama.
Baada ya dakika Kama tano mama
alitoka na Elimina alikuwa karudi.
"Aya twendeni wanangu"
"Nikajua tumeahirisha maana
muda umeend pia"
"Kuna umuhimu wa kwenda leo
hiyo sehemu. Kwahiyo twendeni"
Basi walitoka pale nyumbani na
kuondoka mpaka hotelini. Ambako aliagiza juice tu na wakaanza kupiga stori za
hapa na pale. Elimina aliuliza. Kwanini wako pale. Mama alisema kuwa kuna mtu
wanamsubiri.
Elvine
aliondoka na kusema kuwa atarudi sio muda mrefu. Elimina na mama yake walikaa
pale na kuendelea na stori mbalimbali za kupoteza muda.
Ilipofika saa moja kamili simu ya mama iliingia sms, aliitazama na kisha
akatabasamu tu.
"Sasa Elimina, mgeni wangu yupo mahali nazani hatokuja hapa,
kwahiyo msubiri Elvine aje halafu mrudi nyumbani mimi nitawakuta"
"Elvine toka aondoke mpaka sahizj hajarudi mimi nitajuaje kama
anarudi? Pengine kashaenda hata nyumbani maana yule naye"
"Hapana mimi aliniambia anakoenda kwahiyo najua atarudi. Usimuache
maana si unajua yule bado ni mgeni hapa?"
"Aya, sawa mama"
Elimina
alisubiri pale wakati mama anaondoka. Alikua kachukia maana kitendo cha kufika
pale halafu Elvine kuondoka kilimkera sana.
"Elimina nimerudi..." Sauti ya Elvine ilisikika nyuma ya
Elimina.
Elimina
alipogeuka alishangaa sana namna ambavyo Elvine alivyokuwa anaonekana....
Sehemu ya kumi na nne >>>>>Itaendelea jumatano. Usikose kufuatilia
Kupata mwendelezo wake bonyeza hapa
Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.
Mwimbaji
na mtunzi wa nyimbo, mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
Na,
Imehaririwa
na MIGONGO ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
Kama
umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kujifunza na
kuboresha zaidi.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Cheyo · 82 weeks ago
Elias · 82 weeks ago
scholastica · 82 weeks ago
Migongo · 82 weeks ago
Abel Banene · 82 weeks ago