MAAJABU YA AKIBA

SEHEMU
YA KUMI NA MBILI.
"Mmh!
Mbona amekata tena simu huyu au anabip? Ngoja nimpigie" Elvine alianza
kutabasamu huku maneno yaliyokuwa yameandikwa kwenye ile barua ya baba yake
yakijirudia kichwani mwake.
"ila kama ningekuwa mimi basi
ningekushauri kuwa yule binti Elimina anaweza kuwa mke mzuri sana kwako, maana
anaonekana kuwa na heshima sana na mwanzo nilipokuona naye nilizani unamalengo
naye. "
kama hujasoma sehemu ya kumi na moja bonyeza hapa
Alipiga simu lakini haikupokelewa. Akajaribu mara kadhaa lakini haikupokelewa. Aliamua kutuma meseji lakini nazo hazikujibiwa. Baadaye alipopiga tena simu haikuwa inapatikana. Aliumia sana amani ikapotea tena.
"Huyu binti anashida gani? Si amepiga
hapa jamani? Mbona hapokei simu yangu?"
Alijiuliza maswali mengi lakini hakupata
majibu. Aliamua kulala pale hotelini mpaka jioni. Alipoamka alipata wazo la
kumpigia mchungaji Moses baba yake Elimina.
"Hallo baba! Shikamoo"
"Marahaba Elvine kijana wangu. Upo?
Bwana yesu asifiwe"
"Amina. za nyumbani?"
"Ni njema tu. Mbona
umetususa?"
"Nitakuja baba"
"Lini?"
"Muda wowote tu"
"Sawa karibu sana"
"Samahani, hivi
Elimina yupo?"
"Haaa!
kumbe huwa hamuongei bado mpaka leo mnaugomvi?"
"Hapana, ni kwamba simu yake
haipatikani"
"Anhaaa labda imeisha chaji ila
alikuwa nayo sio mda anaichezeachezea hapa, badae aliondoka sasa sijui labda
yupo anaichajia huko chumbani kwake."
"Anhaaa
Asante baba, basi nitamtafuta baadaye"
"Sawa.
Uje bwana, mama yako kakumisi huku"
"Nakuja
wiki ijayo"
"Waoh!
Ngoja tukuandalie jogoo"
"Asante
baba"
"Karibu
sana"
"Asante
ubarikiwe baba"
"Amina"
Baada ya mazungumzo hayo Elvine alishusha
pumzi na akachukua kadi ya pesa aliyoachiwa na baba yake kisha akaenda kwa babu
yake Mr. Edward ambako alikuta bibi yake amekwisha kuzikwa masaa machache kabla
ya yeye kwenda.
Baadaye wakati akiwa katika mazungumzo
na babu yake aliweza kutambulishwa ndugu wa mama yake na aliambiwa kuwa
angewahi basi angeweza kumuona mama yake maana Mama yake na baba yake
walikuwepo pale msibani toka asubuhi.
Elvine alijilaumu sana kwanini
hakwenda mapema nyumbani maana alihisi kuwa kama angeenda mapema pengine
angekuwa na uwezo wa kuwazuia.
Aliamua kuanza maisha mapya sasa
pasipo kuiwaza familia yake maana aliona hakuna haja kwasababu wakati huu
alikuwa na uhakika kuwa familia yake ipo salama.
Siku iliyofuata mapema saa 12:00
aliamka cha kwanza alishika simu yake kwa lengo la kumtafuta Elimina. Simu
iliita tu lakini haikupokelewa. Alianza kuhisi vibaya, na akahisi kuwa Elimina
anamfanyia makusudi.
Aliamua kuachana na simu kwa wakati
huo maana aliona inamfanya akereke tu hivyo akaenda sebuleni. Alipotoka nje
sebuleni aliwakuta watu wenye fedha zao wamekaa sebuleni na babu yake wakiwa
wanakikao naye kifupi kwaajili ya kumpa mkono wa pole.
"Aisee najua tu hawa watu hapa mkono
wao wa pole sio wakitoto. Mmh! Kweli haya magepu maana izo pesa bora wangetoa
tu kwawahitaji maana sioni umuhimu wa kumpa babu hela nyingi wakati yeye tu anahela
hadi anaumwa" Elvine alijisemea kimoyo moyo huku akiwa anapita pale
sebuleni na kutoka nje.
Akiwa katika hayo mawazo yake
aligongana na mtu mlangoni.
"Ooh! Sorry sister (ooh, samahani
dada), sijui hata nilikuwa natazama wapi?"
"It's ok don't worry (ni sawa
usijali). Najua utakuwa ni mshituko tu wa msiba ndiyo unaokusumbua"
alijibu yule binti kwa tabasamu
(Mmmh! Ungejua hata sio kwaajili ya
msiba maana hata sijakaa sana na hawa watu na sikuwazoea) Elvine alimjibu yule
binti kimoyo moyo pasipo kutoa neno.
"Ooh! Eeh! Itakuwa labda ni
msiba ndiyo. Samahani sana" Elvine alimjibu yule binti huku akijichekesha
chekesha.
"Hivi wewe na Mr. Antony undugu
wenu upoje?"
"Ni babu yangu"
"Anhaaa! Unaitwa nani?"
(Mmmh huyu binti vipi mbona ana
maswali mengi inakuwa kama kituoni bwana? Halafu wafiwa hawasumbuliwagi, huyu
binti sijui wawapi?) Elvine alilalamika kimoyo moyo
"Naitwa
Elvine"
"Jina zuri sana, nashukuru
kukufahamu. Mimi naitwa Eriviela ni mtoto wa mfanyabiashara pia"
"Anhaaa Asante, nashukuru
kukufahamu pia, kwaheri"
"Mbona unaharaka Elvine unakwenda
wapi?"
(Hiiii, huyu binti pepo nini
mbonaa anajipendekeza sana asee) "anhaa
eeh! Kuna mahali nawahi". Elvine alijibu huku alilalamika moyoni.
"Vipi naweza ku......"
Kabla hajamaliza kuongea Elvine aliamua kuondoka na kwenda zake. Alipofika nje
alikutana na baba yake mjomba wake akiwa na mkewe aliwasalimia na wakaanza
kupiga stori za hapa na pale.
"Elvine hivi hujaoa eeeh?"
Mjomba wa Elvine aliuliza ghafla wakiwa katika mazungumzo.
"Hiii? Uncle bwana. Mbona
ghafla umeuliza hivyo?"
"Hapana, nataka kujua tu, ila unajua
mama yako na baba yako bwana. Walioanaga ndoa ya ofisini"
"Kwanini sasa?"
"Huyo mzee kipindi hicho
alikuwa anazingua sana bwana"
"Nani? Babu Mr Edward?"
"Eeh! Nani mwingine sasa?.
Alitaka kumlazimisha mama yako aolewe na jamaa fulani wa kijinga sana".
"Kwahiyo ikawaje sasa?"
"Nitakusimulia siku nyingine,
sahizi ngoja niende mahali fulani mara moja"
Elvine alihisi kakatishwa simulizi
moja tamu sana yenye maajabu ndani yake. Mjomba wake aliondoka na yeye akaagana
na shemeji yake na kuamua kurudi chumbani kwake.
Baada ya wiki moja watu walikuwa
wamesha tawanyika na sasa kukawa kimya sana pale ndani. Wafanyakazi tu ndiyo
waliokuwa wakionekana kupitapita napo ni kwautulivu na heshima kubwa. Babu yake
alikuwa mnyonge sana muda mwingi.
Siku moja Mr. Antony alimuita Elvine
na kumwambia kuwa angependa sana kama Elvine angeoa na kumleta mkewe pale
nyumbani maana kama akiwaona wajukuu zake huko mbeleni pengine atapata furaha.
Elvine hakuwa na jibu sahihi lakumpa
babu yake maana akilini mwake hakujua kama ni kweli anachokiwaza akilini mwake
kinaweza kutimia.
Alikwenda chumbani kwake na akawaza
sana. Alikumbuka mambo mengi sana kuhusu Elimina, toka wakiwa China mpaka
wanarudi Tanzania. Alitamani kumuona Elimina lakini bado moyoni mwake alikuwa
akihisi hatia sana kwa yale aliyomfanyia binti yule. Alianza kutazama meseji
mbalimbali ambazo walikuwa wakitumiana toka wakiwa China ambazo nyingine
zilimchekesha sana. Lakini alikuja kushituka baada ya kukutana na meseji moja
ambayo hakuwahi kuiona.
"Inamaana kumbe kuna siku Elimina
alinitafuta wakati nikiwa hapa Dar es salaam?. Mmh! Hi ni mbaya zaidi"
Elvine alijihoji na kujilaumu sana
Kesho yake alimwambia babu yake kuwa
anasafari kidogo. Babu yake hakuwa na shida kabisa alimruhusu aende anakotaka
kwenda.
Elvine alipanda gari la kwenda Iringa.
Lakini akiwa anapanda alimwambia dereva.
"Kaka naomba uendeshe gari vizuri
maana nahisi kama tusipokuwa makini tutapata ajali"
Konda alijibu "ajali nazo ni mpango
wa Mungu tu ili binadamu apumzike" konda na dereva walicheka kama utani
lakini Elvine alikuwa anamaanisha kuwa anaiona ajali mbele.
Walianza safari. Elvine alikaa nyuma kabisa ya
gari. Gari ilikwenda kasi sana hadi abilia wakawa wanalalamika. Lakini kwa wale
wanaopenda kuwahi kufika walikuwa wakichekelea tu na kufurahia mwendo ule.
Walifanikiwa kufika Iringa lakini
wakati wanaingia stendi Ghafla gari liliacha njia na kugongana na gari nyingine
wakati dereva alipokuwa akitaka kumpisha mwenzie kwa pembeni na kumbe mbele
kulikuwa na gari jingine.
Gari ilianguka vibaya sana na wote
waliokuwa ndani ya gari walipiga kelele lakini wakati huo Elvine alikuwa
amelala kwahiyo hakuona kilichotokea na hata baada ya gari kuanguka wala hakushituka. Waokozi walikuja na kuokoa watu
wachache ambao waliweza kuishi lakini watu watatu walipoteza maisha.
Dereva na konda waliumia sana lakini
hawakufa. Elvine hakuumia popote lakini hakuwa anajitambua maana alikuwa bado
katika usingizi mzito sana. Waokozi walihisi labda kaumia kwa ndani ndio maana
kapoteza fahamu hivyo naye akapelekwa hospital kwaajili ya uchunguzi zaidi.
Alikuja kushituka
saa 12:30 jioni. Alishangaa kujikuta kalazwa maana hakuwa anaelewa
kilichotokea. Alipoamka nesi mmoja alikuja na kumsalimu.
"Unajisikiaje?"
"Kwani
nini kimetokea?"
"Kwani
hukuona wakati ajali inatokea?"
"Ajali?"
"Ila
ni ajabu sana. Maana wewe peke yako hata mchubuko hukupata ila ulizimia tu"
"Hapana
bwana, Mimi. mbona nililala tu. Na hata ajali Sina taarifa nayo"
"Kivipi?"
"Lakini
dereva alipohojiwa alisema kuwa kuna mtu alitabili ajali kabla haijatokea, au
ni wewe"
"Hapana
mimi sikutabili ajari Bali nilimuasa tu aendeshe kwa uangalifu tusije kupata
ajali"
"Kwanini
ulisema hivyo?"
"Basi
tu"
"Basi
maneno yako yalitimia"
Elvine
alistaajabu sana akaomba kuwaona waathirika wa ajali ile ambao hawakufa.
Alipelekwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi. Alipofika aliwahurumia sana mpaka
machozi yakamtoka. Alitembea tembea mule ndani huku akiwatazama wale wangonjwa.
Wale wagonjwa waligeuka kumtazama japo kwa shida sana. Na kila aliyemtazama Elvine
alipona hapohapo. Nesi aliogopa sana akaamua kukimbia mule ndani na kwenda
kuita watu.
Baada ya
muda watu walijaa mule wodini na wakastaajabu maana wagonjwa wato wa siku hiyo
walikuwa wazima kabisa. Elvine mwenyewe alijiogopa kidogo. Alipokuwa anatoka
pale ndani kila mtu alikuwa anamshangaa. Aliamua kutimua mbio maana hakutaka
awe maarufu kwa kitu alichokifanya asije akatukuzwa yeye.
Alipotoka
pale hospitali alielekea nyumbani kwa kina Elimina. Akiwa njiani alimuona
Elimina kwa mbali, akiwa kashika simu. Akaona ampigie iwe kama 'surprise'
lakini alishangaa sana baada ya kuona Elimina akiitaza simu mpaka inakata
pasipo kuipokea.
Alishangaa
sana. Akapiga tena, lakini kadharika Elimina aliitazama simu pasipo kuipokea.
Elvine alichukia sana, kwakuwa Elimina alionekana kama anayekwenda mahali
fulani, aliamua kumuacha aende kwanza na yeye akaenda nyumbani ambako
alipokelewa na mama na kuambiwa kuwa baba kasafiri kidogo kihuduma.
Akiwa anapiga stori pale sebuleni na mama, Elimina alirudi. Alishangaa
sana kumuona Elvine pale sebuleni.
"Elvine?"
"Yes"
"Ooh, karibu sana"
"Asante sana"
Elimina aliondoka na kwenda zake chumbani kwake. Elvine alishangaa maana
aliona kama kuna namna Elimina anampuuzia.
Siku iliyofuata asubuhi Elvine aliamka mapema sana. Alimkuta Elimina
akiwa anadeki sebuleni. Akamsalimia, Elimina alijibu kwa sauti ya unyonge sana
jambo ambalo hakulipenda.
"Unaumwa?"
"Hapana"
"Hivi bado hujanisamehe tu mpaka leo Elimina?"
"Kwa kosa gani?"
"Lolote"
"Ninakazi naomba unipishe kidogo, tutaongea badae"
"Lakini...." Kabla Elvine hajaendelea mama yake Elimina
alikuja na kuwasalimu. Waliacha kuongea walichokuwa wanaongea na kumsalimu mama
yule. Elvine aliamua kutoka nje lakini alianza kukata tamaa kuhusu Elimina na
akawa na hasira sana lakini akajipa moyo.
Waliendelea kuishi pale ndani kibubububu maana kila muda Elimina
alionesha kuwa bize na wala meseji hakujibu.
Siku moja muda wa jioni Elvine alikuwa na njaa maana mchana hakula
kwasababu alikuwa kwenye mfungo. Alipomuona Elimina sebuleni alimuomba amsaidie
kupika uji.
Elimina pasipo kujibu neno alisimama na kwenda kuandaa uji na akamletea
na mikate lakini hakuwa anaongea wala kuonyesha tabasamu.
"Asante" Elvine alishukuru, Elimina alitabasamu kwa mbali sana
Kisha akaketi na kuendelea na kutazama tv.
Elvine aliunywa uji ule huku akiusifia kimoyo moyo kwa namna ulivyokuwa
mtamu.
"Elimina, unaonaje jumamosi tukatembee?" Elvine aliongea huku
akitabasamu
"Sina muda" Elimina alijibu huku akiwa bize na tv.
Jibu lile lilimuuma sana Elvine maana hakutegemea kujibiwa vile
Elvine kwa hasira alisimama na kwenda mahali alipokaa Elimina. Alimshika
mkono na kumsimamisha kwa nguvu.
Aya niambie sasa. Nimekukosea Nini? Niambie tatizo ni nini? Hivi unajua
unachokifanya wewe.
"Sijui na sitaki kujua. Kwani wewe unajali nini? Hasa kuhusu mimi,
nimeona uendelee na mambo yako. Na katu sitokusumbua" Elimina aliongea
akiwa amelengwa na machozi.
Elvine alishangaa na akajikuta kamuachia huku alimshangaa maana baada ya
sekunde chache Elimina alikua akilia.
Aligundua kuwa kumbe Elimina anamachungu sana moyoni mwake. Aliacha
kumfokea na kuanza kumwomba msamaha huku akitamani kujua tatizo ni nini hasa.
Wakati akiwa anambembeleza alikaa pembeni ya Elimina kwenye sofa huku akisema
samahani.
Ghafla mama aliingia na kushangaa kwa kile alichokiona
"Nyie watoto ni upuuzi gani mnafanya hapo?"
kupata mwendelezo wake bonyeza hapa
Sehemu ya kumi na tatu itaendelea ijumaa
>>>>>. Usikose kufuatilia.
Hadithi
hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.
Mwimbaji
na mtunzi wa nyimbo, mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.
Na,
Imehaririwa
na MIGONGO ELIAS. Mhariri.
Mawasiliano:
Whatsapno.
>>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
Kama
umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kujifunza na
kuboresha zaidi.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Cheyo · 89 weeks ago
Migongo · 89 weeks ago
Pearson Mzunde · 88 weeks ago
Upuuzi gani huo nataka kujua
Big up sana kwa waandaji wetu wa hadithi hii
Migongo · 88 weeks ago