HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI NA MOJA.

  

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.

SEHEMU YA KUMI NA MOJA. 

Ilipoishia....

         Wakiwa pale ghafla mlango ulifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Emiliano. Editrin hakutarajia kwasababu Emiliano siku hiyo hakuja na gari kama siku zote hivyo walijisahau. Na pia walinzi hawakumzuia Emiliano kuingia kwakuwa walikuwa wakijua kuwa Emiliano ni mkwe wa ile familia na hawakuambiwa chochote kuhusu kutoroka kwa Editrin kwa mume wake.

         "Editrin mke wangu" Emiliano aliita na wakati Editrin kashangaa pale. Emiliano akimkimbilia na kumkumbatia. Huku alionesha kufurahi sana kumuona

Kupata sehemu ya kumi bofya hapa

       Inaendelea......

      "Editrin nisamehe kwa kila kitu lakini kumbuka kuwa mimi bado ni mumeo huwezi kunitelekeza kama hivi nakuomba sana nipo chini ya miguu yako rudi nyumbani" Emiliano aliongea huku akipiga magoti na kukumbatia miguu ya  Editrin

      "Weeee!!! Naomba niache tena wewe unastahili kufa kabisa. Huwezi kuiangamiza familia yangu kiasi hiki. Na labda tu nikuambie, unamuona huyo hapo nyuma yako? Ni mume wangu halisi na hakufa kama ulivyodhani na sasa familia yangu imekamilika na sitoweza tena kuiacha lazima niungane nayo" Editrin aliongea kwa ukali huku akimpiga mateke Emiliano, kwa lengo la kumtoa miguuni pake.

        Emiliano alishituka sana baada ya kumuona Edwin na hakuamini. Akamsogelea Edwin na kumkazia macho.

      "Unawezaje kuishi wakati ulitakiwa kufa? Kwanini siku zote wewe ni kikwazo katika maisha yangu?"

       Wana wa kifalme hawafi kirahisi hivyo. Na siku zote kifo cha watu waliookoka ni Mungu ndio anayepanga na sio watu kama wewe. Lakini acha nikushukuru tu kwakunitunzia mke wangu maana bado anaonekana mrembo sana licha ya kuwa umri umeenda kidogo. Japo umempotea muda. Na pia tarajia mengi mazito yanafuata kwako" Edwin aliongea huku akiwa anaonesha kujawa na hasira sana.

       Emiliano alichukia sana na akamshika Edwin na kisha akampiga mtama ulimfanya Edwin kuanguka kama gogo hadi chini. Emiliano alipomwangusha tu Edwin alimkalia tumboni na kuanza kumkaba. Editrin na Elvine walianza kupambana kumtoa pale lakini alikuwa na nguvu sana. Edward baba yake Editrin ghafla aliingia pale ndani kukuta tukio linaendelea. Alisogea kwa kasi na kumpiga ngumi moja nzito ya shavu Emiliano ambayo ilimfanya aanguke chini na kumwachia Edwin. Mr. Edward alienda na kumuinua Edwin huku akimpukuta pukuta vumbi wakati hakukuwa na vumbi mule ndani.

      "Pole kijana wangu nimepata habari zako. Maana mke wangu kanipigia simu nikiwa kazini na kaniambia kila kitu kilichotokea na aliniambia kuwa upo hapa. Nisamehe kwa kila kitu maana hata mimi sikuwa baba bora kwa binti yangu. Lakini....." Wakati mr. Edward anaongea hayo alikatishwa na mlio wa risasi ambao ulisikika kwa nguvu sana.

      Wote walishituka na kutazamana ili wajue ni nani kapiga na nani kapigwa. Walishangaa kuona Eliana mama wa Editrin akitokwa na damu tumboni. Kumbe Emiliano alikuwa na bastola na alitaka kumpiga Edwin lakini baada ya Eliana kuona kuwa mkwe wake anataka kupigwa aliamua kukinga yeye hivyo akapigwa risasi ya tumbo.

       Wote walishituka, na hofu ikawatanda. Emiliano alionesha sura yake halisi wakati huo, maana alivaa sura ya tofauti kabisa na aliyozoeleka. Alikuwa amekaza sura na hakutishwa na kitendo cha kumpiga mama mkwe wake badala ya Edwin. Alimnyooshea Edwin tena silaha yake.

        "Editrin wewe ni mke wangu halali kabisa siwezi kumruhusu huyu panya aondoke na wewe. Lazima afe leo"

        "Hapana.... Hapana..... Nisikilize Emiliano huwezi kuendelea kuwa mtu mbaya siku zote. Ni wakati wa wewe kujutia makosa yako" Editrin aliongea kwa kutetemeka sana.

      "Hahahahaha acha kunichekesha, chaguo ni moja kwako. Aidha uondoke na mimi na usahau kila nilichokifanya kwako au nimuue Edwin"

       "Bora uniue lakini sio kumchukua mke wangu" Edwin aliongea kwa hasira

       "Kaa kimya Edwin huwezi kufa kirahisi wakati mimi ndio sababu bora mimi ndio nife na sio wewe" Editrin aliongea kwa uchungu sana huku alitokwa na machozi ya huzuni sana.

        Elvine alimsogelea mama yake na kumkumbatia huku akimfuta machozi. Emiliano alifyatua lisasi nyingine ambayo ilelekezwa kwa Edwin lakini kabla ya ile lisasi kumkuta Elvine alimsukuma Editrin na kwenda kuikinga ile risasi ambayo ilipiga kifuani.

        Wote pale ndani walipigwa na butwaa halafu wakaganda kwa mshangao. Hakuna aliyeamini hata Emiliano mwenyewe hakutegemea kilichotokea. Aliitazama mikono yake kisha akakaa chini na kuiachia silaha yake chini.

        Edwin alimkumbatia mkewe ambaye alikuwa anatokwa na damu nyingi sana kifuani. Edward alikuwa kamkumbatia mkewe huku akilia sana lakini baada ya kuona na Editrin kapigwa risasi aliishiwa nguvu zaidi hivyo akapoteza fahamu kwasababu ya uchungu pamoja na mshtuko alioupata.

          Wakati yote yanaendelea Elvine alikuwa kashangaa tu wala hakuwa analia Bali alikuwa akimtazama baba yake ambaye alikuwa kamkumbatia mama yake Editrin. Emiliano na Edwin walikuwa wakilia sana.

           Alisimama kwa dakika kama kumi hivi Kisha akasogea mahali ambapo mama yake kalala na kumshika mahali ambapo damu ilikuwa ikitoka na ghafla ilikauka na kovu likafutika na hakuonekana kama mtu aliyepigwa risasi maana hata damu haikuwepo. Emiliano alishangaa sana na hata Edwin alishangaa sana. Lakini Editrin hakuamka Wala hakujitikisa.

           "Unangoja nini si umpeleke hospitali sasa au unalengo afie hapa we huoni Elvine kamsaidia kidogo" Emiliano aliongea kwa kumfokea Edwin ambaye alikuwa kaduwaa kwa kilichotokea.

            Sijajua huyo Mungu wenu ni wanamna gani. Lakini leo nimejua kuwa nyie kweli mna Mungu wa kweli kama hata hili limetokea basi nyie walokole sio wakuchezewa. Emiliano aliongea kwa kuonesha kutoamini kilichotokea pale ndani. Ghafla polisi walifika pale ndani maana kuna mfanyakazi ambaye alitoa taarifa polisi kuwa kuna ugomvi unaendelea kwenye ile nyumba.

          Polisi walipofika walimkuta Eliana kapoteza maisha na damu imetoka nyingi sana. Walimuona Editrin kapoteza fahamu na hawakujua kuwa alipigwa risasi. Walimkamata Emiliano maana mwanasheria wa Editrin alikwisha peleka taarifa za Emiliano polisi kwahiyo polisi walijua tu kuwa muhusika wa mauaji yale atakuwa ni Emiliano.

            Baada ya polisi kuondoka na Emiliano. Elvine na baba yake walimchukuwa Editrin pamoja Mr. Edward na kuenda nao hospital. Wakati huo walinzi walimchukua Eliana mke na kumpeleka mochwali.  Editrin alipofikishwa hospitali alionekana hana shida yoyote.

            Edwin alimchukua Elvine na kwenda naye kwenye hoteli moja kubwa sana aliyokuwa anakaa yeye wakati anamtafuta mkewe. Alikuwa na mazungumzo machache na kijana wake.

          Walipofika hotelini Edwin alikwenda kwenye kabati na kutoa sahani ya udongo pamoja na kisu kisha akakaa navyo kwenye sofa moja nzuri.

          "Karibu sana kijana wangu. Nafurahi umekuwa vyema na tena umekuwa kwa namna ambayo hata mini nilikuwa nikiomba kwa Mungu ukue. Nimependa malezi ambayo mama yako alikulea hata kama kwa muda mfupi lakini  kweli njia ulizofunzwa utotoni naona haujaziacha"

         "Asante sana baba yangu" Elvine alitabasamu huku alikaa kitako pembeni ya baba yake.

         "Nimefurahi sana kwa kile ulichokifanya kwa mama yako leo"

          "Ni Mungu sio Mimi baba"

           "Najua sio wewe na wala huwezi kuwa wewe. Hivi msukumo au ni nini kilikujulisha kuwa ukimgusa mama yako pale kifuani damu itaacha kutoka?"

           "Nii... Sina uhakika, lakini nilijikuta tu nimefanya vile. Hata mimi sielewi, ila hata sijui kwanini lakini nimekuwa nafanya mambo yaajabu mara nyingi na hata wakati mwingine nimekutana na malaika baba"

            "Vipi kama nikikwambia unahuduma ambayo hata mimi niliwahi kuwa nayo?"

             "Haaa! Uliwahi kuwa nayo baba?"

           Ndio lakini mimi niliipoteza kwasababu sikuwa tayari kuitumikia. Nikiwa mdogo baba yangu mlezi alisema kuwa baba yangu kabla hajafa alisema kuwa mimi nitakuwa mtu watofauti sana. Na baada ya baba na mama kufa Mimi nikiwa na miaka mitano nilianza kufanya mambo yaajabu. Kuna wakati nilikuwa nikiwa karibu na mtu mbaya huyo mtu lazima ajiseme tu na kama mtu akiwa na mapepo yalikuwa yakitoka pindi tu uyo mtu akinikaribia. Nilifanya mengi sana wakati nikiwa mdogo. Nilipofika kidato cha tano sikutaka watu wajue mimi nipoje. Nilimpenda mama yako nikiwa kidato cha tano na sikutaka ajue chochote kuhusu mimi pia. Kuna wakati ambao mama yako alinikwaza sana tukiwa shule na kwanzia hapo ndipo nikajidharau sana licha ya kuwa nilikuwa na uwezo wa kitofauti. Kuna malaika fulani alikuwa akinionya sana ndotoni lakini sikumsikiliza ndipo nilipoipoteza huduma yangu. Niliumia sana siku mama yako anaondoka shuleni kwetu wakati mimi tayari nilikuwa nimepoteza huduma yangu kwaajili yake"

         "Kwahiyo haikurudi tena kwako na wala haukutubu kwa Mungu wako"

         "Hapana mimi sikufanya hivyo ila siku ulipozaliwa wewe nilikuombea kwa Mungu ile huduma uitumikie wewe. Natamani uje utimize ndoto zangu. Japo uwe mchungaji maana mimi nilitamani kuwa mchungaji lakini baadaye nikashindwa kulitimiza hilo. Huu ni wakati wako wa kufanya mambo ya Mungu tena ukiwa bado ni kijana. Hakikisha haupotezi huduma yako sawa!"

           "Sawa baba lakini nawezaje kuitumia?.

           Edwin alimchoma Elvine na kisu tumboni kwa gafla sana. Elvine alipiga kelele za "Yesuuuuu zuia mwanao nisizulike" kile kisu kilipofika tumboni tumbo la Elvine lilikuwa gumu kama jiwe hivyo kile kisu hakikutoboa tumbo la Elvine bali kilijikunja na kikamtoka Edwin mkononi na kuanguka chini.

           Elvine alishangaa sana na akasimama mbali na baba yake huku katoa macho kwa hofu. Lakini Edwin alikuwa akitabasamu tu. Elvine alikwenda mlangoni kufungua mlango ili atoke nje lakini aligundua kuwa baba yake alikuwa kafunga mlango kwa funguo.

          "Ni nini unataka kufanya? We ni baba yangu kweli?"

           "Elvine.. njoo ukae hapa na wala usiogope"

            "Siwezi kabisa niambia unataka kufanya nini?"

             Edwin alisimama kisha akamsogelea Elvine pale mlangoni. Alipomkaribia aliiachia ile sahani ya udongo aliyokuwa kaishika. Ile sahani ilipofika chini ilipasuka.

          "Elvine naomba uiunganishe hiyo sahani kwa imani yako"

           "Kivipi sasa? Hiyo haiwezekani hata Mungu hajaribiwi hivyo"

          "Saafi"

          "Safi nini?"

           Huduma ya kweli ni ile isiyokalilika Bali huja kwa wakati maalumu na kwasababu maalumu. Unakumbuka wakati nakuchoma kile kisu kuwa ulitamka neno likawa? Basi unatakiwa kujua kuwa huduma hiyo ni ya ndani kwahiyo huwezi kuiongoza ila Mungu ndiye anayeiongoza maana kama ungekuwa unaiongoza wewe basi hii sahani hapa chini ungeiunganisha. Nilikuwa nataka nikupe funzo la imani maana mimi niliamini kuwa pindi nikikuchoma kisu hautadhurika maana ilikuwa ni kwaajili ya funzo tu"

       "Kwahiyo vipi kama kisu kingeingia tumboni na kunidhuru?"

        "Kama malaika wako hayupo nawe basi sahihi kabisa kuwa ungedhurika lakini pia ningepata wasiwasi kama wewe ni kweli umekusudiwa na Mungu"

       Elvine alituliza presha Kisha akaketi pembeni ya baba yake. Ilipofika mida ya saa 7:50 Elvine alipata usingizini hivyo akalala.

       Alishituka asubuhi na akajikuta yupo pekeyake. Alishangaa sana baada ya kuangaza mule ndani na kugundua kuwa hata nguo za baba yake hazipo. Alipotazama pembeni alikutana na barua iliyomshitua zaidi.

 ~   ~   ~   ~   ~   ~   ~   ~   ~                  

      **My dear son**

   Nakupenda sana tena sana. Najua hutonielewa wala hutaamini kwa hiki nacho kifanya. Mimi na mama yako tunaondoka Tanzania. Sababu ipo na niyamuhimu sana hasa kwaajili yako. Nakutakia maisha marefu na yamatumaini. Wakati ukifika nitarudi mwanangu. Lakini kumbuka wewe ni moto ambao hautakiwi kuzimwa na maji ya namna yoyote. Wewe ni kama moto katikati ya maji tafadhari usizime tumika maana ulikuwa mtoto wa nadhiri kwahiyo itumikie nadhiri hiyo.

     Halafu.... Oa kijana wangu ushakuwa mkubwa natamani siku yakuonana ni ile siku ya harusi yako, sijawahi sikia lolote kuhusu kuoa, ila kama ningekuwa mimi basi ningekushauri kuwa yule binti Elimina anaweza kuwa mke mzuri sana kwako, maana anaonekana kuwa na heshima sana na mwanzo nilipokuona naye nilizani unamalengo naye.

Tutaonana tu na kuhusu mama yako yupo salama kabisa na aliamka toka usiku. Bye kijana wangu I love you so much. Nimekuwekea milioni 2000 kwanye hiyo card ya benk hapo mezani na namba ya siri ni 3333 maana sisi katika familia yetu tupo watatu hapa duniani..""

 ~  ~  ~  ~  ~  ~   ~   ~     ~    ~ 

"Waongo nyie tena waongo wakubwa. Siku zote mnanitelekeza najua ni kwakuwa hamnipendi hata kidogo. Nendeni basi... Ee nendeni kwani nini? Hata mimi sihitaji kukaa na nyie kwakuwa hamnipendi. Kila siku ni nadhiri nadhiri aaah!! Mi sitaki hata izo nguvu sihitaji na wala pesa zenu sitaki, mimi nawataka nyie tu aashii!!"

Elvine aliongea maneno mengi sana ya kulalamika tena kwa uchungu sana. Alilia sana huku akijitembeza mule chumbani.

 

Ghafla simu yake iliita alipoitazama ilikuwa ni namba ya Elimina. Alijikuta kaacha kulia

 "Hee huyu binti kanikumbuka leo. Mmh ajabu!" Alipopokea tu simu ilikatwa.....

  Sehemu ya kumi na mbili itaendelea jumatano >>>>>. Usikose kufuatilia. 

kupata mwendelezo wake bonyeza hapa     

 Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo, mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            Na, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kujifunza na kuboresha zaidi. 

 

         

    

 

      

 

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.