MAAJABU YA AKIBA

JIFUNZE KUJIFUNZA (PART 1)
Siku moja nikawa nimetulia natafakari nikawaza na kuwazua kuhusu binadamu. Nikaona
kuwa ni kawaida kabisa kwa binadamu yeyote kuzaliwa, kulelewa, kwenda shule au
kutokwenda kabisa, kuoa/kuolewa wakati mwingine kutokuoa/kuolewa kabisa,
kufanya kazi, kuzeeka na hata kufa. Lakini unaweza kufa hata kabla ya wakati wa
kuzeeka kwako. Nikagundua kuwa katikati ya utoto na uzee/ kifo. Mwanadamu huyu
atajikuta amefahamu vitu vingi sana. Aidha kwa kujifunza mwenyewe kwa kuona
kusikia au kwa njia yeyote ile, au kwa kufundishwa na watu wengine nyumbani au
kwa kwenda shule.
Kwa kifupi tumejifunza
au tumefundishwa mambo kemkemu. Ukienda shule za St. Kayumba utafundishwa
habari ya 3K yaani, kusoma, kuandika, na
kuhesabu. Na, ukibahatika ukapanda magari ya njano utafundishwa kuhusu, 3Rs
yaani, Reading, wRiting, and aRithmetic. Hata kwa wale hawakukanyaga
kabisa umande wa asubuhi nao wamejikuta wamejifunza vitu vingi sana huko
nyumbani na mtaani pia.
Kwahiyo utaona tumefundishwa vitu vingi sana lakini,
utagundua kuwa kunakitu hatufundishwi kabisa
siyo st. Kayumba wala kule kwenye magari ya njano ama nyumbani kule
mtaani. Na kitu hiki ni kujifunza. Kitu
kufundishwa kujifunza ni ngumu sana kufundishwa hata mashule. Ndiyo maana, utakuta
watoto wanakunywa madude na kukariri kwa kwenda mbele bila kujua ni namna
gani njia nzuri na rahisi ya kujifunza
na kuelewa kwa haraka. Mtu mmoja alisema Learning how to learn, is the key
skill and the brain is the key organ. Ingekuwa nakalimani ningesema kujifunza
jinsi ya kujifunza ni ujuzi muhimu na
ubongo ni ogani yake muhimu. Huu ujuzi kwa kimombo ndiyo tunauita LEARNACY
. Ukiachana na Reading, wRiting, and aRithmetic LEARNACY bado inakosekana
na haipatikani kabisa kwa watu wengi
duniani.
Kwakuwa toka enzi na enzi tumekaririshwa kuhusu 3RS,
sasa hapa hapa tutajifunza kwa habari ya 5Rs zinazokosekana katika
maisha ya kujifunza kwa mwanadamu yeyote yule. Na katika hili, utashangaa utakavyo
jifunza namna na njia rahisi sana za
kujifunza kwa haraka na kufanya kazi kwa ubora yaani, unakuwa smarter. Na hapa
tutaungana na Mwandishi Bill Lucas huku tukirejerea katika kitabu chake kimoja
makini kinachoitwa Power up your mind learn faster work smarter. Mr Bill
ambaye pia ameelezea kuhusu 5Rs
ambazo ni, Resourcefulness, Remembering, Resilience, reflectiveness and
responsiveness. Katika hili tutajifunza kinaga ubaga mambo kedekede, tutajifunza namna sahihi ya kutumia akili na
ubongo wako katika kujifunza kitu chochote kwa haraka bila kutumia nguvu kubwa,
hapo ndipo utafahamu namna nzuri ya kucheza na kuuamru ubongo wako katika
kujifunza kitu chochote unachotaka.
Learnacy ni ujuzi muhimu sana ambao ningependekeza kila
mtu aweze kujifunza, kwani tunaishi kwenye dunia ambayo kujifunza ni hitaji la
msingi kwa kila mtu katika kupiga hatua yeyote ile ya mafanikio anayoyataka. Hata
hivyo kujifunza namna nzuri ya kujifunza kwa wepesi na muda mfupi bado ni
tatizo kwa walio wengi, badala yake watu wamebaki kukariri na kutumia nguvu, na
akili nyingi kuliko uhalisia wa namna ambavyo mabo yanatakiwa yawe. Najua unaweza
kuwa ulihangaika sana juu ya namna gani ya kujifunza na pengine ni kutokana na
mifumo ya elimu uliyo fundishwa nayo au namna ulivyo lelewa na mambo mengine
kibao. Sasa na wewe umefikiwa ni suala la muda tu!
Na hapa ni utangulizi tu,unao lenga kukuandaa na kukuweka
tayari kupokea mambo hayo mhimu utakayo kwenda kujifunza, ambapo utabadili
kabisa maisha yako ya kujifunza. Ili kupiga hatua kila utakapo hitaji
kujifunza. Kuwa tayari sasa na usikose kufuatilia mfululizo wa mafundisho haya
ili upate kujenga uwezo huu muhimu sana.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine
namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa
moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO
ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha.
Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu
sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697
/+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu,
niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Masaga mlekwa · 92 weeks ago
Nasubir next part
Migongo · 92 weeks ago