HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”. SEHEMU YA KUMI.

 

SIMULIZI YA KUFURAHISHA, “KUHUSU HATIMA YA KIMUNGU”.

SEHEMU YA KUMI. 


Ilipoishia.... 

Ile nyumba haikuwa mbali na barabara hivyo akafika barabarani lakini kwa yale maumivu aliyokuwa nayo hakuweza kukimbia zaidi, alidondoka katikati ya barabara, akiwa pale alisikia sauti ya mama mmoja kwambali sana ikimwambia

      "Kijana wangu nini shida amka! Nini kimekukuta? Haa! Mungu wangu. Mwanasheria!! hebu tumbebe huyu tumuwahishe hospitali kwanza, maana nahisi kavamiwa na vibaka wa mji wetu huu...."        

kusoma sehemu ya tisa bonyeza hapa

Sasa inaendelea....

    Elvine alipoteza fahamu kwa muda, alipoamka alijikuta yupo hospitali na pembeni yake alimuona mama yake Editrin. Hakuamini kwa haraka kuwa yule ni mama yake maana alihisi anaota ndoto ya mchana. Alitulia kwa muda kidogo akiwa anamtazama mama yake pasipo kuongea chochote bali ni machozi tu ndiyo yaliyokuwa yakiongea kwa kutiririka kwa uchungu.

       Editrin hakujua kwanini kijana yule alikuwa akilia, hivyo akahisi labda ni kwasababu ya maumivu aliyokuwa nayo.

       "Vipi kijana, unaendeaje? Na nini kimekukuta" aliuliza Editrin kwa huonyesha kuhuzunika sana kwa kile kilichotokea kwa Elvine

        "Mama!!!" Elvine aliita akiwa bado anahisi yupo ndotoni.

         "Usijali kijana wangu, utakuwa salama tu", nitakuchukua hapa baada ya matibabu halafu twende kwangu ukaniambie kilichokukuta."

          Elvine hakuwa anaongea chochote zaidi ya kulia kwa sababu ya uchungu aliokuwa nao. Editrin aliendelea kumuongelesha lakini hakujibiwa. Daktari alikuja na kukamilisha matibabu. Baadaye Editrin alimchukua Elvine mpaka kwao ambako alikuwa akiishi na wazazi wake.

        Elvine Alishangaa sana baada ya kuiona nyumba ambayo mama yake alikuwa akiishi na hapo ndipo akagundua kuwa haoti bali ni uhalisia kabisa kuwa yule ni mama yake.

        Alikaribishwa vizuri na bibi yake Eliana. Alikupofika mule ndani alikuwa akishangaa tu kama haelewi kinachoendelea.

        Walikaa sebuleni, baada ya dakika chache alikuja Mr. Edward naye akakaa sebuleni.

        "Baba! huyu ndiye kijana niliyemuokota jana njiani muda ule nilipokuwa nakuja na mwanasheria ofisini kwako." Aliongea Editrin kwa kufungua maongezi

        "Anhaaaa! Nini kimetokea kwako kijana wangu? Maana nasikia kuna majanga yalikukuta"

        "O..o.. ndi.. ndiyo"

        "Ni nini?"

        "Nilikuwa nimevamiwa"

         "Na nani?, Je, hao watu unawajua?"

         "Ndio"

         "Basi subiri kidogo mwanasheria wetu anakuja sio muda, ili tujue namna ya kukusaidia, maana hata uyo mama yako hapo anakesi anataka kuifungua, kwahiyo nazani mwanasheria akija tutakusaidia pia sawa eeh?" Aliongea Mr. Edward kwa tabasamu pana la ukarimu.

          Baada ya muda mfupi mwanasheria alikuja.

         "Karibu sana Mr. Ebrania" Mr. Edward alimkaribisha mwanasheria yule

          "Asante sana, za hapa?"

          Njema sana

          Vipi kijana wangu unaendeaje sasa maana jana ulikuwa hali mbaya sana, aliongea Mr. Ebrania kumwambia Elvine

         Naendea vizuri sasa.

         Basi vizuri

          Baada ya kukaa kutulia, Editrin alimwambia mwanasheria amsikilize kwanza Elvine

         Elvine alianza kueleza kuwa alitekwa na mtu mmoja ambaye anamfahamu lakini hakutaja jina. Baada ya kueleza kilichotokea aliamua kujitambulisha vizuri kwa mama yake.

        Editrin hakuamini baada ya Elvine kusema yeye ni kijana wake aliyepotea miaka mingi iliyopita. Kila mtu alishangaa. Editrin alisimama na kwenda kumkumbatia mwanaye lakini kwa furaha aliyokuwa nayo alilia sana mpaka akapoteza fahamu.

        Elvine alilala pale ndani tena akapokelewa vizuri sana na babu na bibi yake. Hakutaka kukaa mbali na mama yake tena kwahiyo, alilala kwenye kiti karibu na kitanda ambacho mama yake alikuwa amelazwa na alilala akiwa kashikilia mkono wa mama yake.

        Asubuhi Editrin alirudisha fahamu na alipoamka tu alitaja Elvine kwakuwa hakumuona pale chumbani; Elvine alikuwa kaamka mapema sana na akaenda kuandaa maziwa jikoni kwaajili ya mama yake.

        Editrin aliogopa sana maana alihisi Elvine kaondoka. Alitoka haraka sebuleni huku akiita Elvine. Sebuleni alikutana na mama yake Eliana.

        "Usijali Elvine yupo jiokoni kasema anataka akuchemshie maziwa"

         Editrin pasipo kujibu neno haraka alikwenda jikoni kuhakikisha.

         Mwanangu jamani, umerudi kweli?. Alimkumbuka mwanaye kwa nguvu sana huku machozi yakimtoka. Elvine naye alipomtazama mama yake alitokwa na machozi; wakalia kwa muda mrefu sana.

         Editrin alikuwa na maswali mengi sana ya kumuuliza mwanaye lakini kabla hajauliza jambo, geti liligongwa, Editrin alikuwa bado anawasiwasi asije akawa Emiliano ndiye aliyekuja kumtafuta hivyo akamwambia mwanaye waende chumbani kwake ili wakajifiche huko. Elvine naye alipata maswali mengi sana ambayo alitamani mama yake akamjibu.

        Walikwenda chumbani na wakajifungia kwa ndani ili kama Emiliano atakuja Basi pale chumbani ashindwe kuingia.

       Walipofika chumbani, Editrin alimkumbatia mwanaye tena kama mtu ambaye katendewa muujiza wa ajabu.

       "Hivi ni kweli wewe ni Elvine? Ulikuwa wapi siku zote? Na kwanini uliniacha mwanangu?"

        "Nisamehe mama yangu mpendwa, nilipotea mama yangu" Elvine aliongea vile huku alilia sana. Ghafla meseji iliingia kwenye simu ya Elvine kutoka kwa Elimina mtoto wa mchungaji Moses

     "Elvine kwahiyo ndiyo umeamua hivyo eeh! Sawa bwana, kweli shukurani za punda mateke tena ya tumbo"

       Elvine alisikia mlio wa simu yake lakini hakujali wala kutazama kuwa ni nani aliyemtumia ujumbe.

        "Editrin!!!!" Editrin aliitwa na mama yake.

       "Mmh! Kuna nini huko?" Editrin alimuuliza Elvine kana kwamba Elvine anajua kinachoendelea sebuleni.

        "Sijui, lakini mama, kumbe hapa ni kwenu? Mbona haujawahi kuniambia kuwa tuna ndugu? Na Nini kimetokea mpaka umekimbia kwa Emiliano baba mdogo? Vipi kuhusu baba yangu pia? Natamani sana kujua kwanini ulinificha habari za baba na ndugu zako"

        Elvine alikuwa kamkazia macho sana mama yake kuonesha umakini wa kusikiliza.

          "Editrin!!!!!!! Njoo haraka mwanangu". Eliana alibisha hodi pale mlangoni.

          "Nadhani sio Emiliano, maana mama asinge niita hivyo. Twende kwanza sebuleni, halafu maswali yako yote nitayajibu badae." Editrin aliongea huku alisogea mlangoni kisha akafungua mlango.

           Walitoka pale chumbani na kuelekea sebuleni. Walipofika walimkuta baba mmoja ambaye alikuwa kavaa suti nzuri ya rangi nyeupe akiwa amepiga magoti tena akiwa kainamisha kichwa chini.

          "Kulikoni hapa tena? Editrin alimuuliza mama yake".

          "Unamjua huyo? Eliana naye alimuuliza binti yake"

          "Mmmh!! Ngoja nimtazame". Wakati Editrin anasogea kwa yule baba. Elvine alimtambua yule baba kuwa ni yule Mr. Edu ambaye ndiye alimwambia kuwa amuite pacha.

             "Haaa ni wewe baba yangu?" Yule baba alipoisikia sauti ya Elvine aliinua kichwa haraka na kusimama pale alipokuwa amepiga magoti. Na kuwasogelea Editrin na Elvine.

           "What? E... E.. edwi.... Edwin??" Editrin alishangaa na kumrukia Edwin mwilini kwa kumkumbatia.

           "Edwin ni nani tena?"

           "Elvine huyu ni baba yako"

           "What!? Baba yangu, hakufa? Ooh no! Kumbe wewe ni baba yangu?. Elvine naye alistaajabu sana uweza wa Mungu."

        "Nimewatafuta sana nyie watu, kumbe siku zote nilikuwa naonana na wewe halafu nikashindwa kukujua, nisamehe sana Elvine mwanangu, maana nilikupenda zaidi baada ya kuona jina lako linafanana na jina la mwanangu na kumbe ni wewe?" Edwin alimtazama Elvine na kumkumbatia pia. Wote wakakubaliana kwa furaha yenye machozi ndani yake.

        Wakiwa pale ghafla mlango ulifunguliwa na aliyeingia alikuwa ni Emiliano. Editrin hakutaraajia kwasababu Emiliano siku hiyo hakuja na gari Kama siku zote hivyo walijisahau. Na pia walinzi hawakumzuia Emiliano kuingia kwakuwa walikuwa wakijua kuwa Emiliano ni mkwe wa ile familia na hawakuambiwa chochote kuhusu kutoroka kwa Editrin kwa mume wake.

         "Editrin mke wangu" Emiliano aliita na wakati Editrin kashangaa pale. Emiliano akimkimbilia na kumkumbatia. Huku alionesha kufurahi sana kumuona.

       Kupata meendelezo bonyeza hapa

 

Hadithi hii imendaliwa na kuandikwa na JACQUELINE JOHN.

Mwimbaji na mtunzi wa nyimbo, mashairi, Hadithi (simulizi) na ngonjera.

 Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255789523850. Normal >>>>>+255747313148.

                            Na, 

Imehaririwa na MIGONGO ELIAS. Mhariri.

Mawasiliano:

Whatsapno. >>>>> +255767653697. Normal >>>>>+255783327456.

                        GeT tO tHe NeXt LeVeL!

Kama umejifunza kitu shiriki nasi katika comment hapo chini, ili kujifunza na kuboresha zaidi.

 

  

         

       

 

 

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.