HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31
.jpeg)
PESA HAITAFUTWI TUMIA NJIA HII
KUPATA PESA KWA URAHISI ZAIDI
Mtu mmoja alikuwa na mpango
wa kufuga nyuki pamoja na vipepeo. Aliamua kutengeneza sehemu ya kuwahifadhi,yaani mabanda hivyo, aliweka mkakakati wa kuwakamata nyuki na vipepeo.Alitumia njia ya kuwafukuza
na kukamata mmoja baada ya mwingine.Alijua zoezi litakuwa jepesi sana lakini
kiuhalisia mambo yalimwendea kinyume kabisa na matarajio yake.Kwasababu ilikuwa
vigumu kuliko kawaida hasa pale ilipokuja suala zima la kukamata nyuki
aliambulia kukamata wachache sana na wengi wao waliishia kumuuma na kusepa zao kabisa.Kwasababu
usalama ulikuwa ni sifuri yaani oo.
Bwana mmoja akiwa anapita
njiani alimwona huyo mtu mzima akifukuzia wadudu wadogo kama hao
alishangaa sana.lakini uzalendo ulimshinda akaamua kumhoji kwanini anafanya
hivyo kitu gani kimemusukuma kuwafukuzia hao wadudu alijibu akasema nina kamata
vipepeo kwaajili ya kuchavusha mimea yangu
nitakayo ipanda mana hawa ni wazuri sana wa kupandikiza mimea na hivyo kuzuia mimea kuzaa mapooza au
kutokuzaa kabisa hapo baadae, hivyo nawakusanya mapema mapema na kwa wingi ili nijekuvuna
mazao mengi na yakutosha . Aliendele kwa kusema lakini pia nakamata hawa nyuki
kwasababu nyuki wanazalisha asali tamu
sana ambayo naweza kutumia kama dawa,chakula na kujipatia pesa kutokana na
kuuza asali kama biashara nyingine, aliendelea kuseama lakini pia hawa nyuki
watasaidiana na hawa vipepeo kuchavusha
mimea ninayo kwenda kulima kwa wingi sana ili niweze kujipatia mazao mengi naya kutosha .
Mpita njia huyu alimwambia na
kusema ndugu hakika unampango mzuri sana hasa huu wa kujiongezea kipato chako
kupitia kilimo na ufugaji wa nyuki ndiyo
maana umeamua kupanua na kuongeza mashamba hata kuamua kuweka mkakati mzuri wa
kuhakikisha unakamata wadudu wengi wa kuwezesha uchavushaji na uzalishaji wa
mazao mengi ya kutosha hata nyuki kwa asali, ni uamuzi wa kupongezwa kabisa
yaani niseme hongera sana ndugu yangu.lakini kwa hii njia unayoitumia ya
kuwakamata wadudu hawa ilikukamilisha mkakati wako huu umeyakanyaga yaani
unasukuma kupandisha maji kwenye mlima mkali
wakati wahenga walisema maji hayapandi mlima na hewa haijazi kibubu
,jamaa aliduaa na kuvuta umakini wa kusikia kutoka kwa huyu mpita njia labda akawa na njia mpya na nyepesi ya
kukamilisha zoezi lake hivyo aliiuliza na kusema njia gani iliyo sahihi ya
kuwakamata vipepeo na nyuki maana kwa hii njia kweli nimeuona moto!.
Alijibu na kusema rafiki huna
haja ya kuhangaika kuwakamata na kufukuzana na wadudu wadogo wadogo namna hii
hali u mkubwa kiasi hiki ,sasa sikia
ukitaka kumkamata kuku huna haja ya kufukuzana naye unaweza ukavunjika mguu bure na zama hizi
tulizo nazo unaweza kugongwa na gari barabarani kabisa kwa kumfukuza kuku.basi
ili umkamate kuku yakupasa kumwaga mahindi au mchele kidogo tu karibu nawe ili
aje ale kisha umkamate kiulainiiii kabisa.Jamaa akadakia na kusema ndiyo maana
jilani yangu huwa akitaka kukamata kuku kwaajili ya kuchinja huwa anawarushia
mchele na kuwakamata.Hali hii ni toufauti na sisi huwa tunafukuza mguu kwa mguu
hadi kuku anakamatika mpita njia akasema
Ujanja ni kuchgua hakika!.
Jamaa akauliza kwa hiyo hata
hawa nyuki na vipepeo niwarushie mahindi na mchele vipi watakuja kweli ingali
hawali mchele na mahindi?.Mpita njia akasema wawezatumia njia hiyohiyo lakini
usifanye hivyo.
Yaani badala ya kukimbizana
na kufukuzana na vipepeo pamoja na nyuki hawa unaweza kutengeneza bustani ya
maua mazuri na kuitunza vizuri vipepeo na nyuki wakaja kwa wingi tena wakaja
wao wenyewe .pia unaweza kupanda msitu wa miti na kuweka mizinga ndani na pembeni
yake na hao nyuki watakuja kwa wingi kwenye bustani kutumia maua na kisha
kwenda kupumzika kwenye mstu na mizinga iliyo jilani na bustani tayari kwa
kutengeneza asali. kufanya hivyo utakuwa umepiga ndege wawili kwa jiwe moja tu
yaani unakuwa umefanikisha zoezi lako la kufuga vipepeo na nyuki pia utakua
umejipatia bustani ya bure kabisa hapo
ndipo utapata wadudu wa kuchavusha mimea ya shambani kwako na kupata nyuki wa
kuzalisha na kutengeneza asali kwa wingi ya chakula ,dawa na biashara n.k kwa
kulima bustani peke yake.
Kilahisi kabisa unakuwa umemkamata kuku kwa kumpa mchele na mahindi tu. Jamaa alishukuru kwa ushauri ule na alienda kuufanyia kazi mara moja alikuja kushangaa lengo lake la kupata mazao mengi na kujipatia asali kwa wingi analifikia kwa urahisi sana.
UJUMBE.
Watu wengi wamekuwa
wakifakamia na kutafuta pesa na mali kwa njia ambazo siyo sahihi na hatarishi
sana badala la kutengeneza vitega uchumi vya kuuvutia utajiri na pesa .zingatia kuwa pesa haitafutwi rafiki yangu
ila inavutwa na vivutio vyake kama ilivyo katika watalii kuvutwa na vivutio vya
utalii,hivyo acha kutafuta pesa tengeneza njia za kuitega na kuivutia pesa
itakuja tu yenyewe .mitego na vivutio vyenyewe ni kama biashara
sahihi,kilimo,uvuvi,maarifa,uandishi n.k.
Mungu akubariki sana.
rafiki! ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine unatamani ujue zaidi kuhusu Uchumi wako wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia,Uchumi na Maisha.Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz.Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe