MAAJABU YA AKIBA

FANYA MAMBO HAYA KUEPUKA KUJILINGANISHA NA WATU WENGINE.
Tunaishi kwenye dunia ambayo kuona au kufahamu hatua, maendeleo na mafanikio ya watu wengine ni rahisi sana. Hali hii imefanywa kuwa rahisi kutokana na kuwepo kwa mitandao na intanet.
Kupitia mitandao unaweza kujua, mtu fulani anawaza nini, anapenda nini, yupo katika kipindi gani na mengine mengi sana.
Ulisha wahi kuona mtu anaamka asubuhi tu anapost mtandaoni, hivi ndivyo naamka sasa, akipiga mswaki anapost, akianza kutumia chai anapost, akila chakula cha mchana anapost, akienda kutembea sehemu anapost, akitumiwa ujumbe wa kupongezwa au kusifiwa anapost, akutumiwa hela anapost, akisaidia watu anapost, akiachwa anapost, akikorofishana na mtu anapost, akitumia chajio anapost, akiwa anaangalia muvi anapost, akienda kulala anapost na hapo anaweza kupost hadi alichoota kwenye ndoto akiwa amelala.
Huko status utakuta imejaa yaani, ni full kupost. Naomba tuelewane vizuri hapo si kwamba nakataa kupost noo! Tena nasema noo! Nachotaka uone kuwa wakati mwingine unaweza kufuatilia maisha ya mtu na kumfahamu kupitia mitandao ya kijamii peke yake.
Hapa kuna kitu cha kijifunza kwamba huwa unapost nini kwenye mitandao yako? Kumbuka unaweza kuharibu au kutengeneza maisha ya watu kutokana na kile unapost, lakini pia watu watakujua wewe ni wa namna gani, hata kama wewe hukumaanisha hivyo.
Kumbe hapo post zako zinapaswa kuwa vile ambavyo unataka watu wakuelewe. Okey ngoja tusonge mbele kidogo, sasa kama hii ya kuona na kufahamu maisha ya watu wakipost kwenye mtandao na wengine kukutana nao ana kwa ana imewafanya watu wengi sana kujilinganisha na kila mtu anaye muona mitandaoni au kukutana naye.
Tambua kuwa kwenye mitandao utaona watu wanapost
wakila bata, wako beach, wana magari ya kifahari, wanazungumza vizuri, wanaimba
vizuri, wanafundisha vizuri n.k, utaona karibia kila kitu wana kuzidi an. Na unaweza
kufikiria kuwa huna kitu chochote wala wewe si lolote mbele ya watu wengine, yaani kama vile umechelewa maisha haswa.
Ndugu yangu kuna vitu unapaswa kuvitambua kabla ya
kujilinganisha na watu wengine, ambavyo ni;
1. Wewe una ndoto na malengo tofauti kabisa na wengine.
Hili ni kosa kubwa sana ambalo watu wengi hulifanya hasa wanapoona watu walio
wazidi wanafanya vitu vikubwa kuliko wao na wanaanza kujilinganisha moja kwa moja,
bila kujua kuwa kila mtu ana kipaji, ndoto na malengo tofauti kabisa na watu
wengine. Kwa vyovyote vile watu hatuwezi kufanana na hatutafanana kabisa.
Kwa maana hiyo, kila mtu ana njia yake katika kuyaendea mafanikio yake. Hivyo usitake kujilinganisha na watu wengine kwasababu hujui kunasiri gani nyuma ya mafanikio yao walipofikia.Pia, tambua kuwa kuwa kila mtu anaukurasa wake katika kuanza hadi kuyafikia mafanikio yake. Ukurasa wa 100 wa mtu mwingine kwako unaweza ukawa ni ukurasa wa tano au wa kwanza kwa mtu mwingine.
Hivyo kabla ya
kujilinganisha na watu wengine jiulize kuwa, hivi tunafanana? Je tuna ndoto
sawa? Je tuna vipaji vinavyofanana? Je tuna malengo sawa sawa? Kama ni ndiyo ma swali hayo hapo juu basi ni halali yako kujilinganisha asee.
Rafiki si kwamba nasema kila mtu anaishi maisha ya maigizo pasipo uhalisia wowote wa maisha yake hapana ! Lakini ninachotaka ujue kuwa, kuwepo kwa mitandao hii imefanya watu wengi kuonekana wamefanikiwa sana kuliko wewe, wanapesa nyingi sana kuliko wewe na wanaonekana wako na sura na maumbile mazuri sana kama vile walishushwa kutoka mbinguni.
Lakini % kubwa siyo uhalisia na wengi wao wanaigiza katika hilo, kwani siku hizi kuna vitu kama Adobe filter n.k vinaweza kumbadilisha kabisa mtu na kuwa na sura kama malaika hata kama anachunusi kama zote. Na kuwekewa urembo na mapambo kama yote. Hapo ndipo utakuja kuona mtu anakuwa na taharuki baada ya kuona picha za watu wengine mtandaoni na kuona yeye hafai au ana umbo baya, kumbe ni teknolojia tu!
Kwani kamera na vifaa vya kidigitali mfano, iphone camera, canoon camera, infinix na mengine kibao vinabadili uhalisia wao. Hivyo usihangaike kujilinganisha na watu wengine kwani hujui mengi kuhusu wewe, pambana na hali yako upunguze stress.
Utakosa uwezo wa kujiamini, kama tulivyoona hapa kuwa kuna vitu vingi ambavyo utaona watu wanakuzidi hivyo kuna uwezekano mkubwa sana wa kupunguza uwezo wako wa kujiamini ukiwa nao au ukiwa mbele yao.
Kitu kingine utakuwa ni mtu wa kukata tamaa mapema, na hapa utaona kama vile hakuna hatua yeyote uliyoifanya katika kutimiza malengo yako na kuona watu wengine wamepiga hatua sana hivyo utakuwa ni mtu wa kujikatia tamaa mwenyewe tu. Lakini pia utajiona hauna thamani kabisa.
UFANYE NINI BADALA YA KUJILINGANISHA NA WATU WENGINE?
Swali
hili wameniuliza watu wengi sana na wengine baada ya kukutana na madhara ya
kujilinganisha na watu wengine, wakaamua kutafuta ufumbuzi wake ndipo
walipokutana na mimi, nami sikuwa na hiana. Hivyo huwa nawaambia jawabu la maswali yao na huonekana kuponyeka kabisa. Na wewe hapa
naenda kukupa dozi nzima ya changamoto hii.Twende pamoja sasa;
Kujilinganisha
na watu wengine ni silaha inayo angamiza, kuzima na kuua ndoto za watu wengi sana,
wewe usiwe mmoja wao watakao angamizwa na silaha hii.
Pamoja
na hayo yote ukifika hatu ya kujilinganisha na watu wengine fanya yafuatayo;
1. Jifanyie tathimini yako mwenyewe (self-evaluation).
Kwa kuwa kila mtu anamalengo na ndoto tofauti na watu wengine, hivyo hupaswi kujilinganisha na wengine badala yake jifanyie tathimini kati yako na wewe wa jana yako. Kutokana na malengo uliyojiwekea. Mfano mwaka jana labda ulijiwekea kuwa baada ya mwaka mmoja utakuwa umefungua biashara fulani au utakuwa umeongeza ujuzi fulani na mwaka utakapofika badala ya kujilinganisha na wengine yakupasa uwe ni mtu wa kujikagua kuwa nilikwama wapi na nimefanikiwa wapi?
Ulipofanikiwa shukuru na ulipokwama tafuta sababu ni nini kisha jifunze na fanyia kazi hapo utafikia ukuu unao utaka mapema sana kuliko kubabaika na mafanikio ya watu wengine. Yaani, usihangaike na matokeo ya watu hangaika kutimiza ndoto zako.
2. Usiwaige Jifunze kutoka kwao. kumekuwepo na kasumba ya watu kuwaiga watu wengine hadi namna wanavyo tembea, wanavyoongea, wanavyo vaa n.k, kitu hiki si kizuri kabisa ukilinganisha na kwamba kila mmoja yupo na upekee wake. Sasa unapowaiga watu wengine unatuchanganya ujue.
Kitu kikubwa cha kufanya hapo si kwamba uache kabisa kuwafuatilia watu waliokuzidi katika eneo lako hapana! Wafuatilie tena waulize wametoka vipi katika eneo hilo kisha jifunze then nenda kafanye kitu bora kuliko wao na siyo kuwaiga asee.
Utatuchanganya sisi tunaokufatilia bhana. Kitu hiki ni sawa na kusema kwamba 1+2=1 hiki kitu hakiwezekani. Eti mtu anachukua ujuzi kwa mtu fulani akijumulisha na ujuzi wake bado tunapata ujuzi wa mtu yule yule wa mwanzo duuh! Hiki kitu ndicho wazungu wanakiita plagiarism. Hapo sisi tunategemea tuone 1+2=3 kitu tofauti kabisa.
Kuwa wewe “be you”, wasikutishe na mitandao yao, maisha yao, sauti zao na mafanikio yao bana, afu ujue wewe ni mtu mkubwa sana kuliko hata wao eeh! Ni vile tu umeendekeza kujilinganisha na kuwaiga wengine ambao kwanza ni watu wa kawaida tu. Ndiyo maana hatuoni maajabu yako sababu unajilinganisha na watu wengine.
Rafiki you have born an orginal don’t die a copy ” Umezaliwa halisi usife ukiwa nakala fulani”. Nikuhakikishia kuwa ukijifunza kutoka kwa watu waliokuzidi na kwenda kufanyia kazi na kufanya kitu cha kipekee utafanikiwa sana kuliko kuwaiga na kujilinganisha na wengine kwani hiki ndicho chanzo cha stress, kujidharau, kukata tamaa na hata kukosa thamani ya kuishi kwako.
Mungu
akupe ujasiri wa kuuishi uhalisia wako.
rafiki! ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya
kuondokana na adha hii wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo
chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi, maendeleo binafsi na maisha kwa ujumla.
Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork. Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa
mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi
kujifunza pamoja na wewe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Daniel · 101 weeks ago
Migongo · 101 weeks ago
Sarah · 101 weeks ago
Migongo · 101 weeks ago
Lilian clinton · 99 weeks ago
Migongo · 98 weeks ago
Cheyo · 54 weeks ago
Elias Migongo · 51 weeks ago
Edward · 51 weeks ago
Migongo · 50 weeks ago
Joga heke · 42 weeks ago