MAAJABU YA AKIBA

Siku moja nilikuwa naongea na
mtu mmoja. Katika mazungumzo yetu, ambayo, yalitumia muda mrefu kidogo. Kimya
kilitawala muda kuashiria kuwa mada zimeisha na kusubiri mada yingine mezani. Baadaye, nilichomekea swali na kumuuliza kuhusu mipango yake ya maisha ndani ya mwaka
tuliokuwa tumeuanza maana ilikuwa ni mwanzoni kabisa mwa mwaka 2022. Naye
alijibu akanieleza mipango na mikakati yake ambayo alipanga kuitekeleza
ndani ya mwaka mmoja . Ukweli nilimpenda bure, kwa namna ambayo alikuwa ameandaa
mipango na mikakati ya kuukabili mwaka huo mpya. Kwa mipango ile mtu yeyote
angeweza kutoboa kama angeifanyia kazi. Kwa kufupisha sana nilimpongeza na
kumtakia utekelezaji mwema ndani ya huo mwaka. Niseme tu kuwa, saa zilienda,siku
zikaenda, wiki ndo usiseme na miezi ilikatika hadi mwaka ukaelekea ukingoni. Nilipo kutananaye nikamuuliza vipi rafiki umefikia wapi, akajibu akasema, we acha
tu! Mambo yaliingiliana na mipango ikavurugika kwa hiyo sijafanikisha lolote. Mipango na mikakati niliyojiwekea haijafanikiwa kabisa, kwahiyo, najipanga
nianze kwa kasi ya ajabu sana mwaka ujao.
Kisa hiki ndicho kimenisukuma
kuandika Makala hii leo kwamba, kwanini watu wengi wanakuwa na mipango mingi
sana na wanajiwekea ratiba ili kuitimiza lakini mwishoni inakuwa ngumu sana
kuitimiza. swali hili tunakwenda kulijibu hapa.
Martin
Meadows kwenye kitabu chake cha Daily self-Discipline ameelezea sababu tano ambazo zinasababisha
watu wengi kushindwa kuweka nidhamu ya utekelezaji wa mipango na mikakati yake
fuatana nami sasa;
1.
AINA
MBAYA YA HAMASA (THE WRONG KIND OF MOTIVATION).
Hivi ulisha wahi kusikiliza hamasa fulani hivi labda ya
uchumi na ukatoka unajiona kabisa kama vile unamagari, una nyumba, ndege na vitu
vingine vikubwa? Naomba tuelewane hapo kwamba sipingi hamasa apana! Lakini
nachotaka uelewe ni kuwa kuna aina mbili za hamasa au motisha mwandishi
ameelezea kwa kusema motisha ya ndani
(intrinsic motivation) hii, inatokea mtu anapotenda mambo bila malipo na
vishawishi kutoka nje.
Na aina ya pili ni hamasa ya nje(extrinsic motivation). Hii, hutokea mtu anapofanya mambo yake kutokana na vishawishi au malipo ya nje. Kwa hiyo siku zote mtu akifanya maamuzi kulingana na motisha ya nje ataanza vizuri kabisa lakini kwa sababu haikuwa ndani yake atakapo kosa tu hamasa na msukumo wa kufanya kitu hicho atashindwa kuendelea mbele.
Ndugu, tumia hamasa ya nje kama kichocheo cha hamasa ya ndani katika
kufanya maamuzi na mambo mengine. Hii itakusaidia sana usifanye kitu ili watu
wakuone, ili watu wakusifie, ili uwe maarufu au ili watu wakupende bali fanya
kulingana na hamasa na musukumo wa ndani ilikutimiza hatima na ndoto zako.
2.
MATARAJIO
MABAYA (WRONG EXPECTATIONS).
Ni kawaida ya watu wengi kutarajia makubwa na kutaka mambo
yaje kama walivyo panga wao. Watu wengi hutaka mambo waliyo jipangia yaje kwenye
uhalisia kama yalivyo na huku wanasahau kupigia gharama zote muhimu
zinazohitajika. Lakini, pamoja na hayo naomba nikuambie kuwa, kwa kweli mambo
huwa hayaji kama ulivyopanga bali, mambo hutokea kama yalivyopangwa. Siyo kama unavyo taka wewe. Sasa mtu akipata matokea tofauti na alivyotarajia macho yanakuwa juujuu hadi hukata tamaa na kushindwa kuendelea kabisa.
3.
KUKOSA
MSAADA (LACK OF SUPPORT).
Ukweli ni kwamba, tunaishi duniani kwa kutegemeana. Ndiyo maana hakuna mtu aliye kamilika hivyo, utahitaji msaada wa mawazo, maarifa, nguvu, fedha n.k kutoka kwa watu
wengine. Shida inakuja pale mtu anapotaka kufanya au kuanzisha kitu huku anategemea watu
wengine katika kufanikisha jambo au ndoto yake. Sasa, anapokosa msaada huo na kutengwa na
watu huacha mara moja.
Ndugu, nipende kukushauri kuwa, pamoja na kwamba
tunategemeana ,jukumu la maisha yako ni lako mwenyewe kwa 100% hivyo, pambana.
4.
KUKOSA
MUDA (LACK OF TIME).
Point hii ilitakiwa iwe ya kwanza kabisa, sema ni vile tu
nimeamua kuiweka hapa lakini umuhimu wake ni mkubwa sana. watu wengi wamekuwa
wakilalamika kukosa muda wa kutosha katika kufanyia kazi mipango na mikakati
yao. Lakini, cha ajabu wana muda wa kutosha kuangalia mpira kushinda
vijiweni, kupiga umbea, kushinda mtandaoni. Kwa namna hii huwezi kupata muda wa
kutosha wa kufanyia kazi ndoto yako ni ngumu sana. Halafu pia, tambua kuwa hakuna
muda wa kutosha kufanya kila kitu ila, kuna muda wa kutosha kufanyia kazi ndoto
yako. Hivyo, ukisubiri muda utoshe ndiyo uanze utapata tabu sana. Ndugu, muda
haujawahi kutosha hivyo anza sasa kupambania
ndoto yako inawezekana.
5.
KUKOSA
RAHA/FURAHA (LACK OF ENJOYMENT).
Kwasababu ya hamasa ya nje watu wengi hutamani kuwa kama baadhi ya watu maarufu hapa duniani. Wanatarajia kuwa na furaha siku zote za maisha yao hasa, katika suala la kutimiza mipango na mikakati waliyojiwekea. kitu hiki ni kinyume na uhalisia na haiwezekani kabisa. Kwani, kwenye maisha kuna nyakati za furaha , huzuni, kukata tamaa, kushindwa, kukosa msaada na kutaka kuonewa huruma na mengine mengi. Hivyo, kama utategemea kupata raha na furaha wakati wote na usitake kuukubali uhalisia utashindwa kusonga mbele. Kunamsemo mmoja naupenda sana na mwandishi kauzungumzia ambao unasema “if you don’t enjoy your fitness plan change it” kwa tafsiri isiyo rasimi ni kwamba “kama haifurahii program yako ya kujiimarisha ibadilishe”. Hapa tunajifunza kuwa usifanye kitu ambacho hukipendi fanya kitu ambacho kinakupa raha, unakipenda na unakifurahia.
Rafiki natambua kuwa una ndoto kubwa sana, mipango na mikakati lukuki ya kuitimiza hiyo ndoto, hilo ni jambo la kwanza na zuri sana. Lakini, kama hautaamua kuchukua hatua ya kuanza na kusonga mbele utabaki nayo mwenyewe ndani yako hivyo, amua kuifanyia kazi ndoto yako bila kujali wengine wanasemaji, watakuonaje au kutaka kuwapendeza wengine. Ndugu tumia hamasa ya nje kuichochea hamasa ya nje matokeo utayapata naamini utanipenda.
Ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu rafiki!
na kama unachangamoto katika hili pengine njinsi ya
kuigundua ndoto yako wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo
chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala
hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri &
Mwalimu wa Saikolojia, uchumi na maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji
wa mtandao wa addvaluetz karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Sim na Whatsapp >>+255783327456 / +255767653697.
Email>>
eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>>
MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza
pamoja nawe