MAAJABU YA AKIBA

KUWA KIELELEZO (BE A REFERENCE).
Tunaishi kwenye dunia ambayo
kila mtu anataka kuwa maarufu,tajiri
na mtu muhimu sana katika Dunia hii.Na wengine wanajitahidi kufanya kila linalowezekana
ili tu kufikia lengo hilo la kuwa maarufu ulimwenguni,Kubwa Zaidi watu wanasahau
kuwa kuna gharama za kuufikia umaarufu
na kuwa mtu muhimu duniani.
Mwalimu wangu wa shule ya Msingi
aliwahi kunambia ukitaka kuwa maarufu na kujulikana sehemu yeyote ile basi inakupasa ufanye kitu kizuri au kibaya sana tena ufanye kwa bidii na utofauti .Nikamuuliza kivipi?
Akasema ukifanya kitu kizuri cha kujenga na kuisaidia jamii watu watakufahamu
tu tena watakufahamu kwa mazuri mfano, kutengeneza labda ndege,kuelimisha
jamii,kuwa kiongozi bora n.k,mchango wako katika jamii utafahamika.Lakini pia
ukifanya jambo baya la aibu katika jamii mfano, kama kuiba,kujiingiza kwenye
makundi ya ugaidi,umalaya n.k watu watakufahamu tu tena watakufahamu kwa mabaya
hayo.
Hapa ndipo nikaja kugundua
kuwa kumbe hata ufanye jambo zuri au baya watu watafahamu tu kuhusu wewe hata
kama ufanye kwa siri.Nakumbuka mama mmoja alikuwa rafiki yangu sana mwaka 2020
siku moja nilikua napiga naye stori ,mama huyu alikuwa na watoto wanne ambao
hawa kuwa wakubwa bado.Alinambia na kusema kuwa natamani sana watoto wangu waje
wawe kama watoto wa Fulani au hata wote
wakiwa kama familia ya mtu Fulani nitafurahi sana.Nikauliza kwanini?, akasema
kwa namna ambavyo familia hiyo wanajiheshimu ,wanafanya kazi kwa bidii,wanautii
lakini pia ni watu ambao karibia kila mtu katika jamii anawafahamu kwa wema
wao.Mama huyu alichomekea na kusema tena kijana wa kiume akitaka kuoa namshauri
akaoe katika familia hiyo hahaha.Kwa uelewa wangu mdogo kwa kipindi kile
nilimjibu na kusema mtoto umleavyo
ndivyo akuavyo kwa hiyo kama unataka
wawe kama hiyo familia nenda kajifunze kwamba familia hiyo inafanya vipi na
imewezaje kuwa mfano wa kuigwa ,kisha amua kufanyia kazi njia hizo.
Lakini ukijiuliza tena kwa
upande mwingine utakuja kuona kuna watu au familia ambazo ni pasua kichwa
mtaani kila mmoja anaelewa kasheshe lake .Na wakati mwingine utakuja kuta watu
hawa wanalifahamu hilo au hawalitambui kabisa kuwa wao ni pasua kichwa mtaani.
Rafiki ninachotaka uone ni
kwamba ukiamua kufanya mema au mabaya
hayohayo ndiyo yatakutambulisha na watu watakujua kwayo,yaani ukiwa
mlevi wa kupindukia watu watakujua kwa
ulevi huo huo,ukiwa Malaya au tapeli watu watakujua kwa namna hiyo hiyo,ukiwa
mwema watakujua kwa wema huo huo,ukiwa mwalimu na mshauri mzuri watu watakujua
kwa namna hiyohiyo,hali kadharika kwa uongo,umbea,wizi, n.k
Tambua kwamba mtu kuwa kielelezo chema au kibaya ni suala la yeye kuchagua awe kielelezo
kwa mambo mazuri au kielelzo kwa mambo mabaya,na haya yote yanaonekana
katika jamii hata kama utaamua kuyafanya kwa siri watu watafahamu tu.hapa kuna
msemo mmoja unasema “Even if no one is
watching you, you have to be sure that everyone is watching you”.kwa
tafsiri isiyo rasmi ni kwamba “hata kama
hakuna anayekuona uwe na uhakika kuwa kila mtu anakuona”.kwa lolote unalolifanya
tambua kuwa watu wanakutazama na amua kuwa kielelezo chema katika hilo.
Hivi ulisha wahi kuona kila
mtu katika eneo lake mfano kwa wachezaji wa mpira wanatamani kuwa kama messi na
lonaldo,kwa waandishi wanatamani kuwa kama kiyosaki,Robin shama,Robert
Green,Brian Tracy n.k, wanamziki, wakulima, waalimu, washauri kadharika katika
maeneo yao.Hii ni kwa namna ambavyo watu hawa walichagua kuwa kielelezo chema
na mfano wa kuigwa katika jamii pengine hata wao hawakujua kuwa itakuwa
kieleleza kwa kuchagua kufanya mema.Sina hakika kama na waliokuwa kielelezo kwa
mambo mabaya kama walijua kuwa siku moja watakuwa mfano wa tabia na watenda
mabaya.
Goja nikuibie siri hii
kidogo,pengine hauifahamu nayo ni “kwa
maisha hayo hayo unayoishi kunawatu wengi sana wanayatamani na ni ndoto yao
siku moja kuishi maisha kama unayoishi wewe saivi”.Lakini ajabu nikwamba
unayadharau sana na kuona hayana maana,unakuwa mtu wa kunung’unika,kulalamika
kila kukicha hali hii siyo nzuri kabisa
tafuta furaha ya maisha yako.
Ndugu tambua kuwa kuna watu
wanakufuatilia katika maisha yako, wanajifunza kwako wengine wanajivunia
kukufahamu na wengine wanakuita Role model wao cha ajabu ni kwamba mwenyewe
huwafahamu ,hivyo usikate tamaa wala kurudi nyuma kwani utawakatisha tamaa na
kuwarudisha nyuma watu wengi sana .Ndiyo
maana utakuta mtu anasema kama Fulani kafanya hivi mimi ni nani nisifanye?.Binafsi
watu wengi sana wamekuwa wakinipigia simu na wengine kunifuata ana kwa ana na
kunishukuru na wakisema “ninajifunza vitu vingi sana kutoka kwako nilikuwa sian
hili wala lile lakini umenifanya nimekuwa na 1,2,3… Mungu akubariki sana”.Cha ajabu wengine hata
siwafahamu kabisa.kusema haya si kwamba najisifia sana hapana nachotaka uone ni
namna gani watu wengi wanafuatiria maisha yako na kujifunza kwako.
Rafiki kuna vitu muhimu sana
viwili yakupasa kuvifahamu navyo ni REPUTATION
NA CHARACTER..Reputation hiki ni
kitu au sifa ambayo watu wengine wanasema kuhusu wewe wakati wewe haupo.Mfano hivi
nikitaja John pombe Magufuli unafahamu nini,nikitaja Joel Nanauka je,vip kuhusu
Osama,Diamond je?.Binafsi nimeshiriki sana kwenye vikao vya kuchagua kamati,sasa
kunakitu nilikuja kujifunza katika hili kwani kuna majina yalikuwa yakitajwa
kila mtu anaguna na kupinga kabisa.Lakini baadhi ya majina yakitajwa kila mtu
anakubali tena kwa kuongeza na maelezo juu yake.
Wakati Character kile kitu unacho kifanya kwa siri pale ambapo hakuna mtu
anakuona.Hiki kitu ndiyo wewe
sasa. Hata kama ukienda nje au ukiwa na watu wanakusifia sana lakini kama
unafanya mambo ya kijinga siri ambapo watu hawakuoni amini kuwa ipo siku watu
watakudharau na kukupuuza sana.Kwa sababu character
ndiyo imebeba tabia na sifa za mtu halisi na hizi watu wengi huzifanya kwa
siri sana,na zinaweza kuwa ni nzuri au mbaya lakini wakija nje wanaigiza maisha
na kuishi nje ya uhalisia wao huku nako wanajulikana kwa sifa nyingine tofauti
na character yao. Na watu watakapo jua character yake wataivunja reputation
haraka sana, hivyo character ina nguvu
kuliko reputation na inaweza kuivunja reputation aliyo ijenga mtu.
Ulishawahi kuona mtu mhimu
sana mtaani anayeaminika na anajina lake kalijenga mtaani chukulia labda ni
mchungaji ,mara inagundulika kafumaniwa na mke wa mtu reputation yake itavunjika mara moja
kwasababu ya character (uzinzi) aliyo kuwa anaifanya kwa siri sana.Hata katika
mwizi au tapeli aliyekuwa anaaminika sana katika jamii ni hivyo hivyo
akigundulika na character yake.
Ndugu nimalize kwa kusema
achana na maisha ya kuigiza ishi maisha yako halisi usije kuangukia pua watu
wakizijua siri zako.Iwe ndani au nje popote utakapo kuwa fanya vitu ambavyo
vitakutafsiri vyema kwasababu watu wanakuona hata kama huonekani,watu
wanajifunza kwako hata kama hujawafundisha.kuwa kielelezo chema na cha kuigwa
katika jamiii,ifananine ile familia ambayo yule mama rafiki yangu alikuwa
anaitamani.
Afu ukiwa kielelezo ni rahisi
sana kuacha alama katika jamii yako ujue.
rafiki! ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuwa kielelezo wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo
chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii
imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa
Saikolojia,Uchumi na Maisha.Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz.Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp &
Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>>
eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>>
MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama
umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Scholastica Ernest · 104 weeks ago
Migongo · 104 weeks ago
Ayusto · 103 weeks ago