HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31
“Learning
makes a wise wiser and a fool more foolish”. Huu ni moja kati ya
semi ninazozipenda sana, sababu umebeba
uhalisia fulani hivi kwa namna ambavyo dunia ya sasa inaenenda. Hebu ngoja tuone
maana yake kwanza ambayo ni kwamba “kujifunza kunamfanya mtu mwenye hekima kuwa na hekima Zaidi na mjinga kuwa mjinga Zaidi”. Ukweli huu nauunga mkono kwa 100% kabisa nadhani hata wewe utakuja kuungana na mimi
katika hili hapo baadaye. Na Mara, utakapo maliza kusoma andiko hili hutabaki kama ulivyo.
Hivi ulishawahi kuona mtu wa
namna hii? Kwamba kabla ya kwenda shule tuseme labda sekondari au chuo alikuwa
na nidhamu, heshima, maadili, utii, kufanya kazi kwa bidii, uzalendao, tabia njema na
alikuwa mfano wa kuigwa katika jamii. Lakini mara baada tu! Ya kwenda shule au chuo
mambo yanabadilika kabisa na kuwa tofauti na vile alivyokuwa mwanzo, utashangaa
anaanza kuwa mkaidi, tabia mbaya kama vile uraibu wa pombe, umalaya , anapoteza
uaminifu n.k. yaani anabadilika nakuwa tofauti kabisa na vile jamii ilikuwa
ikimtarajia kuwa. Kwa maana hiyo, unakuja kujiuliza mtu kama huyo alikwenda shuleni
au chuoni kuongeza maarifa ili kujiboresha au alikwenda kujiharibu na
kujibomoa? Hebu twende pamoja kunakitu nataka nikuoneshe.
Hali hii imewafanya baadhi ya
wazazi huko kijijini na mijini kuwa na vigugumizi vingi kuwapeleka watoto wao
shuleni au Vyuoni wakijua ni wale wale tu kasoro mavazi. Juzi juzi tu hapa nilikuwa naongea
na mtu mmoja wa huko kijijini nikamuuliza kuhusu habari ya kusoma kwa watoto
wake. Ndugu huyo alikana wazi wazi na kusema kwamba hawezi kufanya ujinga kama
huo, huku akijua anafanya ujinga ingekuwa bora angekuwa hafahamu kama anafanya
ujinga. kama kawaida yangu nilitamani kujua sana juu ya msimamo wake aliokuwa
ameusimamia nilimdadsi kwa kina.
Na hoja yake kubwa ilikuwa ni
kwamba watoto wakienda shule wanakuwa na tabia mbaya, wanajiinua, wanakuwa wabishi, wavivu, wanaangukia kwenye, ushoga, umalaya na kupata magonjwa, wanaleta
mimba na kuzaa watoto kabla ya ndoa, wanaongeza idadi ya watoto ombaomba na machokoraa mitaa
wanaharibu maadili ya jamii na
wanashusha maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla. Sasa ukijiuliza tunapeleka
kusomesha au kuharibu watoto wetu ? Akaendelea kwa kutolea na mifano ya baadhi
ya watu pale kijijini ambao wamesoma lakini hao ndiyo wamekuwa wa kwanza
kukimbilia na kutetea maovu,sasa tunakwenda wapi na mimi sipo tayari kwenda
kuharibu watoto wangu bora nikapambana nao tu hapa hapa kijijini nitawafundisha
mwenyewe, afu mbona babu zetu walifanya hivyo na maisha yalikuwa safi
tu? Jamaa alihoji. Hallo! kwamifano mingi aliyonipa huyo mtu niliona kama kunauhalisia na ukweli
katika hoja yake.Niseme tu ukweli nilitumia nguvu kubwa na muda mwingi sana
kumwondosha katika mtazamo huo. Lakini Mungu ni mwema katika yote. huyo mtu alikubali
kusikiliza, akauliza maswali akaelewa, akawa mpole, akajifunza na akaahidi
kuufanyia kazi ushauri huo na kwamba amebadili mtazamo wake.
Pamoja na hayo ukija upande
mwingine utakutana na watu ambao pengine hapo kabla ya shule au chuo walikuwa
mbumbu, ziro, gesi, hawakuwa wanajiamini, waongo, tabia mbaya, waoga na mengine mengi ya
kufanana na hayo. Lakini baada ya kwenda shule walibadilika kabisa na kuwa watu
wa kutegemewa, kuaminika na kuwa mifano mizuri ya kuigwa katika jamii. Baada ya
shule walifanyika kuwa watu tofauti na zamani sasa ni watu wema na wenye msaada
katika jamii na taifa kwa ujumla.
Ndugu hapa ukubali au ukatae
kunawatu wanaenda shuleni na vyuoni wanapotelea hukohuko juu kwa juu huku
wengine wakibadilishwa na kuwa watu wema na muhimu sana katika jamii zetu na
taifa letu. Na hapa ndipo penye uhalisia wa ule usemi wetu hapo juu “Learning makes a wise wiser and a fool
more foolish”, Na hii, si katika shule na vyuo tu. Bali ni katika Nyanja zote za
maisha mfano katika biashara, jeshi, kanisa na sehemu nyingine lukuki.Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba, maarifa yanawaimarisha wenye heshima na
kuwaharibu kabisa wajinga, hapa ndio maana biblia ilisema mwenye nacho
ataongezewa na asiyenacho hata alichonacho atanyang'anywa. Hii ni Kali asee!
Mfano mtu anasoma na
kufundishwa biblia vizuri kabisa lakini baadaye utasikia mtu huyohuyo anaipinga
na kusema imekosewa ooh mara imepitwa na wakati, kisha anaasi na kuacha iman. Lakini wengine
wanaimarishwa na kufanywa upya kila siku kupitia biblia hiyo hiyo.
Mwingine anafundishwa mafunzo
ya jesha na kuwa mzalendo na raia mwema lakini kuna mwingine anakengeuka na
kuwa jangili tishio la usalama, kama hutaki kuamini kamuulize Iddy Amini mjukuu wa Dadaa.
Utakuta mwingine mitandao ya
kijamii imemuharibu kabisa, imempotezea muda na kupoteza malengo yake haswa yaani
anakuwa ni yeye na wassap na mitandao mingine ya kijamii anachati na kufuatilia
kila kitu asubuhi hadi jioni. Lakini wengine wanaitumia hiyo hiyo mitandao kujifunza
vitu vipya, kufanya biashara, kujifunza kwa wengine ili kujiimarisha, kuelimisha jamii na kuzalisha
kipato cha kuendesha maisha yao.
Nachotaka ujue ni kwamba, tunaishi kwenye kipindi cha ulimwengu wa
taarifa na maarifa ni tofauti kabisa na vipindi vingine vilivyo wahi kupita
huko nyuma. Kulikuwa na vipindi vya kutumia nguvu na mabavu ambapo mataifa na
watu wenye nguvu waliweza kuushinda ulimwengu huo na kuwa watawala,watu muhimu na maarufu sana kipindi
hicho.Vivyo hivyo katika kipindi hiki watu
wenye wingi wa maarifa na taarifa wanautawala ulimwengu wa sasa na kuishi kama wafalme.
Nasema hivi tupo katika
utandawazi, taarifa, habari na maarifa. Watu wengi wanapo haribikiwa wanaanza
kuulaumu utandawazi na wingi wa maarifa kuwa vinawachanganya. Ndugu tambua kuwa
pamoja na kwamba hivi vitu vina faida na hasara, hivi vipo vimesimama tu havina upande wowote.Yaani ukiamua
kuvitumia kwa faida vitakufaidisha sana tena zaidi ya unavyofikiria. Na ukiaamua
kuvichukua kama hasara kwa kweli vitakuharibu na kukufilisi kabisa. Hapo ndipo
utabaki kuulaumu utandawazi pamoja na sayansi na teknolojia.
Nimalize kwa kusema
utandawazi upo, maendeleo ya technolojia yapo kabisa na kama ilivyo katika
uhalisia kuwa hakuna kitu kisicho na faida na hasara, hivyo hata hivi vina
hasara na faida yake. Wale wote wanaoharibiwa kutokana na kujifunza teknolojia, taarifa na
utandawazi wanachukulia upande wa madhara ya hivi vitu, ndiyo maana
badala ya kuboreshwa wanabomorewa na kuharibiwa kabisa.
Na wale ambao wananufaika na kufaidika ni wale ambao
wameaamua kutumia kwa upande wa faida na wamenufaika na kufanikiwa sana
katika Mipango na Malengo yao. Kwa hiyo uamuzi na uchaguzi wa mtu hujulisha kuwa
ataharibiwa au atafanikiwa . Ndugu chagua na amua kutumia kwa faida huu
utandawazi na wingi wa maarifa tuliyo nayo katika ulimwengu wa sasa pia, amua
kupuuzia katika upande wa harasa. Maamuzi! maamuzi! Maamuzi! ni yako mwenyewe.
Les Brown mwanahamasa huko
marekani amewahi kusema, “Hatima inaanza
kujengwa katika kipindi cha kufanya maamuzi” hivyo jenga hatima yako kwa
kufanya maamuzi sahihi usiendeshwe na mihemuko na mikumbo ya watu wengine. Fanya
kitu kitakacho kunufaisha na kukusukuma kuitimiza ndoto yako katika kila
unacho taka kukifanya jiulize kwamba hiki kitu kitaniongezea hamasa ya kufanyia
kazi ndoto yangu au hapana ? Kama ni ndiyo basi kifanye tena kwa bidii na ubora
na kama sivyo kipuuzie mara moja.
Amua sasa inawezekana kupambania malengo na ndoto yako kuwa mtu wa kuigwa na wa faida kwa familia, jamii na taifa kwa ujumla. Pia chagua kufanya
mema kwani watu wengi wanakufatilia na kujifunza kwako kimya kimya pasipo hata
wewe kujua,hivyo usiwaangushe asee!
rafiki! ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine jinsi yakufanya
maamuzi ya kutumia kujifunza kwa faida yako wasiliana na mimi moja kwa moja
kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala
hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri &
Mwalimu Wa Saikolojia,Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji
wa mtandao wa addvaluetz karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa
mawasiliano;
Whatsapp
& Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>>
eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>>
MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi kujifunza
pamoja nawe