MAAJABU YA AKIBA

MUDA WA KUINGIA NA KUTOKA (ENTRY AND EXIT TIME).
Kwa kila jambo kuna muda na majira yake.Nadhani kila mmoja
wetu angalau alisha wahi kusafiri kutoka sehemu moja kwenda sehemu
nyingine.Inawezakuwa ndani ya wilaya au nje ya wilaya,ndani ya mkoa au nje ya mkoa,ndani
ya nchi au nje ya nchi,kama ndiyo kweli utakubaliana na mimi kuwa,kuna wakati
ulianza safari yako na kuna wakati uliimaliza safari yako.Hapo ndipo kusema
kunawakati wa kuanza safari na wakati wa kuimaliza safari yako.Chukulia hata
katika kusoma aidha shule ya msingi,shule ya sekondari,shule ya upili,Chuo cha
kati au Chuo kikuu,utagundua kuwa kuna muda watu huingia kujiunga na masomo na
kuna muda watu huhitimu masomo yao.
Vivyo hivyo kwa wakulima kuna muda wa kupanda na kuna muda
wa kuvuna.Hii yote hutokea angalau kwa kila jambo kuwa na wakati wa kuanza na
wakati wa kumaliza ndiyo maana kuna wakati ulizaliwa na kuna wakati
utakufa.Sikutishii lakini ndivyo ilivyo na huo ndio uhalisia ya kuwa kila kitu
kina wakati wa kuanza kwake na wakati wa kumalizika.Na haiwezi kutokea kuwa
ukianza ndiyo umeanza hapana,lazima kuna wakati utafikia mwisho tu.Kwa mfano
ukichukulia mfano wetu hapo juu wa kusafiri,wakati umepanda gari haukusafiri
muda wote kuna wakati ulifika ukashuka kwasababu wakati wa kushuka ulikuwa
umefika.
Rafiki hivi unajua ya kuwa muda unazungumza? Mfano,ukilala
wakati wa kuamka ukifika,hata bila kuamshwa utaamka tu.Ukishindwa kufahamu
nyakati na majira katika Maisha yako utapata tabu sana. Kuna wakati mwingine
unaweza kupishana na gari la mshahara
kabisa .Hivyo wakati unaongea tena muda mwingine unakusemesha hata huna habari,
ndiyo maana Mungu anaweza kukuletea watu fulani watakao saidia kusukuma mbele
hatima ya maisha yako(destiny helper) lakini usiwatambue na wakati
mwingine waliletwa ili wakuvushe katika hatua moja au nyingine na watu hawa
usipo watambua kwa wakati sahihi unaweza kuja kuwagundua wakati ulishaenda na
isikufae tena.
Wakati mwingine inaweza kuwa ni fursa ambayo imekuja mbele
yako tena imekuja kwa wakati sahihi kabisa, inaweza ikawa ni kujifunza jambo fulani
na wewe usiielewe wala kuchukua hatua yeyote.Utashangaa ukija kuielewa fursa
hiyo wakati wake wa kutoka(exit time) ukawa umeshafika na usiifaidi
tena.Na,hii hutokana na kutokujua wakati wa kuingia na kutoka kwa kitu fulani
au wewe mwenyewe katika kitu fulani.
Nakumbua nilipokuwa nyumbani nilikutana na mama mmoja
aliyekuwa akiuza Mchicha nilimuuliza kuwa anamuda gani anauza mchicha? Alijibu
na kusema ana miaka kama nane hivi.Nikamwambia woow! muda mrefu sana kumbe utakuwa ushajenga na
nyumba tayari eeh? Akasema hapana,sababu alikuwa akikutana na changamoto nyingi
sana na ilifika wakati aliamua kujiingiza kwenye kilimo lakini hakufanikisha
chochote na matokeo yalikuwa yanafeli tu kila mara.Kwani kila alipo lima aidha
mvua haikunyesha kabisa mwaka huo au maji kuzidi na kubeba mazao yake yote,na wakati
huo anakuwa ametumia gharama kama zote.Nilimpa pole na kuuliza shida nini?
Akasema hata yeye hakuelewa sababu ilikuwa nini.Lakini ilifika kipindi akakata
tamaa kabisa na kuamua kuto kulima tena.Hivyo akaamua kufungua mgahawa kwaajili
ya kujikimu yeye na familia yake.Pamoja na hayo mgahawa haukuendelea na alishindwa kuuendesha kutoka
na mtaji kuwa finyu,huku pesa nyingine ikitumika nyumbani kwa matumizi ya
Nyumbani.Matokeo yake alijikatia tamaa na kurudi kwenye hiyo biashara yake ya
kutembeza mchicha,hakutaka tena kusikia habari za kilimo.Ilipokuwa mwaka 2021
Mchungaji wake akamwambia alime Mpunga kwamaana mashamba yenyewe yalikuwa
yanapatikana kwa bei ya chini sana,alikuwa amekata tamaa katika kilimo na hakutaka
kusikia habari hizo kabisa,huwezi amini wakati mwingine mchungaji wake alikuwa
akimkopesha hadi pesa na kumtafutia shamba ili tu alime,lakini hakutaka kusikia
habari hizo.Mavuno ya mwaka huo yalikuwa mengi kuliko kawaida huku bei yake ilipanda
mara tano zaidii.Mama huyo aliishia kujilaumu kwanini hakulima na alikataa hadi
msaada kutoka kwa mchungaji wake.Basi akasema siyo mbaya akafanya harakati za
kulima tena mwaka uliofuata lakini
mpunga wake ulipigwa na maji wote.
Unaweza kusema huyu mama alikuwa amelogwa vile au alikuwa
na mkosi lah!,ni kwa namna tu hakujua wakati wake ni upi na pengine angelima
mwaka 2021 ndiyo ingekuwa wakati wake wa kutoka kwake lakini hakulitambua hilo
na aliamua kubaki kulaumu tu muda wote na kusema Maisha hayako fair kabisa.
Ngoja tumtazame jamaa mjoja anayejulikana kama Christopher
Michael Langan, mtu huyu alikuwa na IQ kubwa sana iliyokadiriwa kuwa
195-210 kuliko hata ile ya Albert
Einstein ambaye yeye ilikadiriwa kuwa 160 tu, yaani kwa ufupi alikuwa jiniazi.Mwaka
1999 alitajwa na waandishi wengi kuwa ni "the smartest man in
America" or "in the world".Mwaka 2008 Kuna siku alikuwa
anashiriki mashindano ya maswali na majibu ambayo yalikuwa yanafanyika kati ya
watu 100 wenye akili sana kushindana na mtu mmoja yaani (1 VS 100).Hapa
swali lilikuwa linaulizwa kisha pande mbili hizi zinashindana kujibu au kutoa
jibu sahihi kwa haraka na upande wowote utakao jibu swali utalipwa
pesa.Ikumbukwe upande mmoja ulikuwa na watu mia moja ambao wako vizuri kichwani
na upande mwingine ulikuwa na mtu mmoja tu,ambaye siku hiyo ndiyo alikuwepo
Langani ziidi ya hao wengine 100.Ningekupa historia ya Christopher Langan au
basi goja tufanye wakati mwingine,ilikuwa ni kawaida nchini marekani kutokea
kwa mashindano kama haya. Ajabu ni kuwa kila swali likiulizwa Langan alikuwa
analifahamu na alijibu kwa haraka na kuwaacha wapinzani wake wakinong’ona
kujadili jibu.Langan alivuna pesa nyingi sana kiasi cha dola za kimarekani 250,000
ambzo ni sawa na Tsh 587,500,000.Watu walimshangilia sana Langan lakini alipofikisha
kiasi cha shilingi 587,500,000 aliamua kuinuka na kuondoka katika mashindano
hayo.Watu walishangaa sana kuona akiondoka wakati alikuwa na uwezo wa kujibu
maswali yote yaliyofuata na kupata pesa nyingi zaidi.Alipoulizwa akajibu na
kusema “I know my entry and exit time”,yaani nafahamu muda wa kuingia na
muda wa kutoka sasa yanipasa kuondoka
kwani huu ndiyo wakati wangu wa kuondoka hapa.
Kuna mengi ya kujifunza kutoka kwa Christopher Langan
lakini yatupasa kutafakari na kuyafanyia kazi.
Hivi unafahamu kunawakati wa kuingia na kutoka katika kila
unachokifanya? Hivi unafahumu kuwa kunawakati wa kuingia na kutoka kwenye
mitandao ya kijamii? Kuna wakati wa kuingia na kutoka kwenye ajira? Hivi unajua
kuwa kuna muda wa kuingia na kutoka kwenye hiyo fursa? Tambua sasa na ondoka
ilikupata fursa kubwa zaidi.
Kuna msemo mmoja unasema A good dancer knows when to
leave the stage.Yaani mchezaji mzuri anajua ni muda gani wa kuondoka jukwaani.Hapa
niseme tu kwamba kuna watu hawana kiasi katika mambo,utashangaa mtu anakalia
kuchati kwenye mitandao ya kijamii kuanzia asubuhi hadi jioni tena bila ukomo
na hakuna anachopata zaidi ya umbea na kupoteza muda.Ifahamike kuwa kutumia
mitandao ya kijamii siyo vibaya kikubwa ni kuwa na kiasi katika kutumia na
itumike kwa manufaa na si vinginevyo,pia kuwa na kiasi katika kuzungumza.
Kuwa na kiasi na zaidi fanyia kazi ndoto yako wakati huu
kabla exit time yako haijafika,pambana kila kitu kinawezekana.Acha
kufuata mikumbo ya watu wengine,kuwa wewe jifunze kwa watu lakini usiwaige.Kila
kitu hakuna kisichowezekana tambua majira na nyakati katika maisha yako
itakusaidia sana kujua nini ufanye na wakati gani. Hakika itakuwa ni hatua
kubwa sana katika kuifanyia kazi ndoto yako.
rafiki! ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya
kuondokana na adha hii wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo
chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa
na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia,Uchumi na
Maisha.Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz.Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu,niachie maoni yako nitafurahi
kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Vivian Gwimevir · 102 weeks ago
Migongo · 102 weeks ago
January · 102 weeks ago
Migongo · 102 weeks ago