HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

CHANGAMOTO KATIKA MAISHA

 

             CHANGAMOTO KATIKA MAISHA. 

Changamoto inaweza kuwa na maana nyingi, lakini wacha tukubaliane kuwa changamoto ni ugumu au vizuizi anavyokutana navyo mtu katika kuyaendea yale aliyoyakusudia. Yaani, malengo na ndoto zako. 

Wakati mwingine changamoto ni jaribu katika eneo fulani la maisha ya mtu husika. 

Katika hili nimegundua kuwa changamoto haiji kwa lengo la kukuharibu, kukukomoa, kukurudisha nyuma, au kukufanya ushindwe kabisa. 

Lakini, changamoto ipo kwa lengo la kukupima na kukuthibitisha kwamba umekizi vigezo vya kuwa au kuvuka katika hatua fulani ya maisha uliyopo na kwenda hatua nyingine.

Wakati mwingine ugumu au changamoto ni kipimo cha kuufikia ushindi. 

Ukweli ni kwamba, huwezi kuwa mshindi pasipo kushindana, kama ndivyo hivyo, sasa katika mashindano hayo utakutana na ugumu fulani ambao ndiyo changamoto zenyewe.

Kadiri unavyotatua na kushinda changamoto nyingi na kubwa ndivyo unavyokuwa bingwa na mshindi katika eneo hilo. 

Wakati mwingine, changamoto inalenga sana katika kutuimarisha. 

Changamoto ni kama moto kwa dhahabu, dhahabu huimarika na kuwa imara zaidi pindi inapopita katika moto. Hivyo, lengo la changamoto kwa mtu ni kumuimarisha mtu huyo. 

Ndiyo maana mtu anapokutana na jaribu au changamoto akapambana na kuishinda hatakuwa kama alivyoingia kwenye changamoto hii, hapo utakutana na mtu ameongeza ujasiri na kujiamini zaidi. 

Moja ya faida ya changamoto ni kwamba inatupa uzoefu katika maisha yetu na uzuri wa uzoefu ni kwamba unatupunguzia makosa. 

Hivyo kumbe changamoto na ugumu unaopitia ni sehemu ya maisha na ipo kwa mema na si kwa lengo la kukukomoa kama wewe unavyofikiri.

Hebu chukulia katika maisha kusingekuwa na ugumu wowote yaani, kila kitu ukikitaka unakipata wakati huo huo, kwa namna ileile kwa kiwango kilekile pasipo shida na ugumu wowote, unadhani maisha yangekuwaje?

 Pamoja na kwamba Maisha yangekuwa mepesi sana, sidhani kama tungekuwa wabunifu, watu wa bidii, wavumilivu n. k

Siku za nyuma nilikuwa na mtazamo ambao kiuhalisia siyo sahihi kabisa. 

Nilikuwa najua kuwa, kunawatu fulani fulani hivi hawapitii kabisa changamoto na ugumu katika maisha yao. Kumbe  ulikuwa ni mtazamo ambao hata sio sahihi. 

Ndugu, tambua kuwa hakuna mtu hata mmoja asiyekutana na ugumu katika eneo fulani la maisha yake

Pia ni muhimu kufahamu kuwa Kila mtu ana ugumu na matatizo yake ambayo yanaweza yasifanane kabisa na matatizo yako.

Ukiishi na mtazamo huo itakuwa ni mwanzo wa kukata tamaa (give up), msongo wa mawazo (stress), kujidharau na kuona hufai pengine huna akili kabisa.

Ukifahamu malengo na faida za changamoto huna haja ya kulalamika na kuwanung'unikia watu wengine wakati mwingine hadi kumlaumu Mungu mwenyewe. 

Niandike kukwambia kuwa, changamoto zipo kwa watu wote na zipo kila hatua ya maisha unayoifikia. 

Na kwa wale wanao mwamini Mungu tufahamu kuwa kumwamini Mungu haimaanishi kuwa hutakutana na ugumu katika maisha yako. Hii inamaana kuwa, pamoja na ugumu utakao kutana nao Mungu atatupa uwezo wa kukabilina nazo. 

Pia elewa kuwa matatizo yapo kwa watu wote na si kwa baadhi ya watu kama unavyo dhani. 

Kila ukimaliza kutatuza tatizo kwenye maisha yako, uwezo wa kukabilina na matatizo huongezeka hivyo unapewa matatizo makubwa zaidi ya mwanzo.

Hapa ndipo utagundua kuwa, kila ukivuka changamoto fulani unakutana na changamoto nyingine ambayo hukutegemea kabisa, tena wakati mwingine ni kubwa kuliko ile ya mwanzo. Na sababu yake ni kwamba, uwezo wako wa kutatua matatizo umepanda viwango na wewe unapewa changamoto za viwango.

 Ndiyo maana maandiko matakatifu yanasema

"Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili (1 Wakorintho 10:13)".

Hapa tunapata funzo ya kwamba Kila changamoto inayokuja mbele yako, tambua kabisa kuwa unaweza na ipo ndani ya uwezo wako, kwababu tumeona kuwa Kila mtu anapewa changamoto kulingana na uwezo wake. Hapa ndipo atakapo ikabili ataishinda na ikionekana ni ngumu Mungu anasema atafanya mlango wa kutokea.

Hivyo hata kama unaona ugumu unaopitia umekuwa mkubwa sana tambua kuwa upo na uwezo nao na kinachotakiwa ni kupambana mwanzo mwisho hata utakapo uona ukuu. 

Utakutana na changamoto katika biashara, katika ndoa, kwenye kilimo, kanisani, shuleni, kwenye siasa, kwenye uchumi, michezo na sehemu nyingine kibao. 

Tambua kuwa pamoja na changamoto hizo, unao uwezo wa kupambana nazo na kuzishinda kabisa. 

Watu waliofanikiwa si kwamba hawakutani na changamoto laah! utagundua wanapitia changamoto tena kubwa tu! Lakini wanapambana nazo kimaso maso hadi kuufikia  ukuu wao.

Na wewe nikuambie, kuna ukuu fulani hautaufikia hadi utakapo ivuka changamoto hiyo, pambana , usikate tamaa, vumilia hata utakapo ivuka na ukuu unaoutaka utaufikia.

Changamoto yako ni yako mwenyewe pambana nayo hadi uishinde, usidhani kuna mtu atakuja from no where aje akupambanie. 

KUNA MAHALI HAUTAFIKA HADI UTAKAPO IVUKA HIYO CHANGAMOTO YAKO.

Ndugu naweza kuzungumza mengi sana katika hili, lakini, wacha kwa leo nisema kwamba, changamoto ni mtaji, ni njia ya kuuendea ukuu wako. 

Na ugumu wa maisha ni kipimo cha akili.

 "Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali;(Yakobo 1:2)". 

Kama wewe ni mtu wa kutamani mafanikio makubwa huku ni mtu wa kuogopa changamoto hautafikia mafanikio hayo badala yake utaishia kuyatamani tu, kusingizia mikosi , laana, wachawi, na kujiita huna bahati. 

Hakuna namna ya kuufikia ukuu huo pasipo kupambana na kuzishinda changamoto zako. 

Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

Na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na changamoto yako, sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu wa Saikolojia, uchumi, maendeleo binafsi na Maisha

Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork

Karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

Fb page>>> add value network.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe. 

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.