HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

HATUA 4 ZA KUSEMA HAPANA KWA HESHIMA.

 

HATUA 4 ZA KUSEMA HAPANA KWA HESHIMA.

Asilimia kubwa ya watu duniani, wanakumbwa na changamoto hii ya kushindwa kusema hapana kwa ombi walilo ombwa kufanya. Hii inatokea mara nyingi wakati mwingine wanapohitajika kuwafanyia hivyo wapendwa wao, rafiki zao, majirani zao, wazazi, ndugu na jamaa wa karibu. Pia inatokea pale unapohitajika kufanya hivyo huku huna uwezo kabisa wa kufanya au kutoa msaada huo. Lakini kwa kuogopa kuwaumiza, kuwavunja moyo na kupoteza heshima watu wengi hujikuta wakisema ndiyo hata sehemu walipotamani kusema hapana. Hii husababisha mtu kuishi maisha ya watu wengine na yenye maumivu makali sana. Kama unachangamoto hii usiogope, kwani hauko pekee yako ni watu wengi sana duniani wanapitia changamoto hii. Lakini habari njema ni kwamba hapa nimekuandalia hatua nne za kusema hapana bila kuogopa, bila kuvunja heshima yako au kuharibu mahusiano yako na watu wengine, soma hadi mwisho naimani utasaidika;

HATUA YA KWANZA:  ONYESHA KUTHAMINI (SHOW APPRICIATION).

Kama unataka kukataa ombi la watu ambalo lipo nje ya uwezo wako, bila kuvunja mahusiano yako na watu wengine. Basi ni muhimu kufuata hatua hii ya kwanza ya  kushukuru na kuthamini nafasi hiyo ya kuombwa msaada kwani si kila mtu atapata nafasi hiyo. Lakini ukweli ni kwamba hadi mtu anapokuja kukuomba msaada anakuwa amekuthamini na kukuamini  sana hadi kukutafuta, umsaidie kutatua changamoto hiyo. Hivyo ni muhimu kulitambua hilo na kumshukuru sana kwa kukuamini. Hapo ni muhimu kusikilkiza kwa makini, kuuvaa uhusika, ikiwezekana uliza maswali na onyesha kuguswa na changamoto hiyo. Mfano mtu anaweza akaja anataka umkopeshe  100,000/= akaongezee mtaji, wakati huo na wewe huna hela ya kutosha. Unaweza kumwambie hivi,  Hongera sana kwa namna ambavyo unapambana kukuza na kuendesha biashara yako. Lakini pia, nashukuru sana kwa kutambua kuwa ninaweza kukusaidia katika hili... wacha tuende hatua ya pili sasa.

HATUA YA PILI: SEMA HAPANA YA KUELEWEKA NA SABABU YAKE.

Kutoka sehemu ya kwanza ambapo umesikiliza na umefahamu shida ya mtu huyo kwa undani lakini pia umeonyesha kuthamini na kushukuru kwa nafasi hiyo ya kuaminiwa. Sasa hii ni hatua ya muhimu sana ambayo inawashinda wengi, nayo ni kusema hapana lakini siyo hapana tu, bali eleza za sababu yake. Ukirejea kwenye mfano wetu hapo juu wa mkopo wa 100,000/= ambayo huna. Mwambie mtu ukweli mapema kabla hamjafika mbali na ukweli wenye ni hapana, sema hapana ni ngumu kidogo kuisema sasa goja tuiseme hapana kwa heshima kutokana na mfano huo. Unaweza kusema hivi, nashukuru sana kwa kutambua kuwa nina weza kukusaidia katika hili. Lakini nasikitika kwamba sitaweza kukusaidia katika hili. Kwa kingereza ndo nzuri zaidi (am sorry that i wont be abble to do so). Na usiishie kusema hivyo tu hatakuelewa na utamvunja moyo kweli lakini, lazima utoe na sababu kwanini huwezi kumsaidia. Sababu ya hapo juu unaweza kusema staweza kukusaidia katika hili kwasababu jana nimefanya mahemezi lakini pia nimelipia ada ya watoto shuleni, nimetumia pesa nyingi sana (usidanganye weka sababu yako hapa), na hii kupelekea mfuko wangu kuyumba, hivyo itakuwa ngumu kidogo.... hallo sijui kama unanielewa? Okey twende hatua ya tatu tukaone sote.

HATAUA YA TATU: TOA OFA YA KUKANUSHA OMBI HILO.

Mama mmoja ambaye ni mama mlezi kwangu aliwahi kuniambia, wakati mwingine msaada siyo hadi upewe pesa  kama watu wengi walivyo kariri. Sasa na hatua hii ya tatu isiishie kusema hapana na sababu yako tu, watu wengine wana roho ndogo wanaweza kukuelewa vibaya na wakavunjika moyo. Hivyo basi, badala yake unaweza kuwepatia ofa ya kitu unacho kiweza. Yaani, nazungumzia unaweza kutoa msaada mbadala ya pesa, hii inawezakuwa ushauri, muda, kiasi cha fedha ambacho unaona utakimudu na mengine kibao. Hebu turudi kwenye mfano wetu, hapa unaweza kumpa ofa ya kumshauri, au wakati mwingine kumwonyesha sehemu wanayo toa mkopo wa riba nafuu au una weza kumwelekeza sehemu wanako chukua bidhaa kwa bei nafuu sana ambapo anaweza kukujibana kwa mtaji huo huo alio nao na kudunduliza kidogo kidogo hatimae atakuwa na kiasi cha kutosha kama anavyotaka yeye si unajua hata mbuyu ulianza kama mchicha ee!

HATUA YA NNE: PATA MREJESHO NA MJULIE HALI.

Daada ya kupitia hatua hizo zote tatu za kusema hapana sasa, ili kuimarisha mahusiano na urafiki wenu usiishi hapo tu, endelea kuwasiliana nae na kuuliza hali na mwenendo wa biashara yake. Hapo anaweza kukupa changamoto anazokumbana nazo, endelea kumshauri na kumpa mwelekeo zaidi ili kukuza na kuendeleza biashara na maendeleo yake binafisi. Hii, itaonyesha kuwa kweli uliguswa na ombi lake, hii itaongeza heshima na kukuamini zaidi. 

Niseme tu kuwa, watu wengi wameingia kwenye migogoro, madeni, kesi, kuvunja heshima na hata kuvunja uhusiano wao na watu wengine  kwasababu ya kushindwa kusema hapana. Kama utatumia njia hizo hapo juu tatizo hili litabaki historia kwako. Nb: usiseme ndiyo au hapana ili kumridhizisha mtu, sema hivyo kwasababu unaweza na ipo ndani ya uwezo wako. Kushindwa kufanya hivyo utaishi maisha ya watu wengine na ya kitumwa kabisa . kuna msemo mmoja naupenda sama lakini ni wa kingereza ila usijali tutautafisiri nao ni kwamba “If you have nothing to say say nothing”  yaani, kama huna cha kusema sema sina.

Lakini pia ni muhimu kutambua kuwa kunasehemu za kusema hapana na sehemu za kusema ndiyo tusichanganye mambo hapo. Na mambo huwa yanajichanganyia wakati wa kusema hapana mtu anasema ndiyo  na penye ndiyo mtu anasema hapana, huu nao sijui ni ukosefu wa nini!

Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

LinkedIn>>Migongoe. 

Pinterest>>eliasmigongo.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe. 

  


 

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.