HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

KWANINI HUWEZI KUPENDWA AU KUCHUKIWA NA KILA MTU?

 

KWANINI HUWEZI KUPENDWA AU KUCHUKIWA NA KILA MTU?

Ni hulka ya kila binadamu kutaka kupendwa na watu wote popote anapokuwa. 

Ndiyo maana utakuta watu wanafanya kila namna ili tu kuwafurahisha watu wote popote waendako. 

Na kama mtu atakosa upendo huu kutoka kwa watu walio mzunguka, na utashangaa atakuwa na msongo wa mawazo (stress), hasira kupita kiasi, wivu kupita kiasi, kujichukia, kuwa mnyonge sana, kujidharau mwenyewe na mengine yanayofanana na hayo.

Watu wengi kwa kutaka kuwafurahisha watu wote na kulenga kupendwa na kila mtu kwa 100%, wamejikuta kwenye gubiko kubwa la kudharaulika na kuchukiwa zaidi.

Rafiki yangu mmoja alisikika akisema “kama ukitaka kuwafurahisha wote basi jiandae kuwaudhi wote”. Soma tena uelewe tafadhli

Sasa zipo sababu zinazosababisha watu wengine wasikupende hata kama utafanya mengi ya kuwafurahisha said. 

Hapa ndipo tunaenda kujibu swali letu la kwanini huwezi kupendwa au kuchukiwa na watu wote kwa 100%. 

Na baada ya hapo nitatoa ufumbuzi wake, wa nini ufanye.

SABABU YA KWANZA:

MWONEKANO WAKO (YOUR PHYSICAL APPEARANCE).

Mwonekano wa nje wa mtu, ni moja ya sababu kubwa ya kuchukiwa au kupendwa na watu wengine. 

Ukweli kuwa kila mtu yupo na mapungufu na dosari zake. 

Na watu wengine huwa na upendeleo wa mionekano fulani wanayo itaka wao wenyewe. 

Utakuta mtu anajichukia yeye mwenyewe au watu wengine kwasababu ya kuwa na umbo kubwa au dogo sana, kuwa mfupi au mrefu sana, kuwa mnene au mwembamba sana, kuwa mweusi sana au mweupe sana, kuwa na saizi ndogo au kubwa ya pua, mdomo, mikono, miguu, macho, kifua n.k.

Ndugu yangu, hakuna mtu ambaye ana mweonekano mzuri kwa 100%, hata watu wakubwa  mashuhuri duniani ukiwaangalia vizuri hata siyo wazuri wa kutisha sana ya wezekana hata wewe unawazidi. 

Hata hao warembo, mamisi wa dunia waulize wanatumia muda gani kwenye kioo. 

Yaani na sema hivi, kupitia mwonekano wako kuna watu wengi sana watakuchukia na hawatakupenda hata uwabebe mgongoni. 

Lakini ajabu ni kwamba kupitia huohuo mwonekano wako ambao wewe na watu wengine mnauchukia kuna watu kibao watakufurahia na kukupenda kwa mwonekano wako.

Ni sawa na kusema mwonekano wako ni sababu ya watu kukupenda au kukuchukia.  Tambua huwezi kupendwa au kuchukiwa  na watu wote kwa 100%.

SABABU YA PILI: 

KILA MTU ANAVIGEZO NA SIFA ZAKE ZA KUMPENDA MTU (EVERYONE HAS, HIS OWN STANDARDS TO LOVE OTHERS.).

Hapa utakuta mtu mwingine anapenda sana watu ambao ni smart muda wote. 

Na hapa haijalishi yupo na mwonekano gani ilimuradi ni msafi na yupo smart watu hawa huwaelewa sana, utakuta mwingine anapenda watu wenye bidii ya kuchapa kazi, mwingine anapenda wenye tabia nzuri, weusi, wafupi, warefu, wapole, waongeaji,wacha Mungu n.k. 

Je wewe unapenda watu gani?

Sasa ukikutana na mtu ambaye anakigezo cha kuwapenda wacha Mungu na wewe huna hiyo sifa hapo utachukiwa tu, na ukikutana na mtu mwenye kuwapenda wafupi na wewe ni mrefu hapo utachukiwa tu na mengine kama hayo. 

Kwasababu ya standards na mitazamo fulani fulani ya watu kwa watu wengine, kwa sababu tu hujakizi vigezo vyao watakuchukia. 

Hapo nikushauri tu kuwa, watu wa namna hiyo usibabaike nao na wala wasikusumbue kwani kuna mamilioni ya watu watakupenda hivyohivyo ulivyo.

Kitendo cha kila mtu kuwa na vigezo atakavyo yeye kitendo hiki kimechangaia kwa kiasi kikubwa kutokuwepo kwa mtu mzuri au mbaya kuliko watu wote duniani.

SABABU YA TATU: 

HISTORIA YAKO (YOUR HISTORICAL BACKGROUND).

Kila mtu yupo na historia fulani aidha ni ya kufurahisha au kuhuzunisha, mbaya au nzuri n.k.  mfano historia ya uchawi, ubakaji, ulevi kupindukia, umalaya, umasikini, uganga, kukataliwa na kutengwa, kuwa yatima na nyingine nyingi. 

kitu hiki tu kuna watu wakifahamu kuhusu wewe watakuchukia na wengine kukudharau kutokana na historia mbaya uliyo wahi kupitia. 

Ulishawahi kuona mtu wanaaminiana sana na rafiki yake lakini baada tu ya kufahamu kuwa alikuwa mwizi na mbakaji, baada ya rafiki yake kujua tu anaanza kuishi naye kwa hofu na kuogopa atabakwa au kuibiwa.

Na kinyume chake ni kweli kwa upande mwingine wa shilingi.

Kumbe kupitia historia yako kuna watu watakuchukia na kukudharau kabisa lakini kuna watu watakusifia na kukupenda kabisa kwa namna ambavyo umepambana na kufika hapo ulipo kutokana na historia yako.

SABABU NYINGINE NI KAMA: MASUALA YA KIFEDHA, KIAFYA, ELIMU, CHEO, MAFANIKIO N.K

Elewa kuwa pamoja nakuziunganisha hizi pointi, lakini hizi ni pointi ambazo zinaweza kusimama na kujitegemea kila moja kivyake. 

Sema tu ni kwa namna ya kuokoa muda, pia nachotaka ujue kuwa vitu hivyo hapo juu ukiwa navyo yawezakuwa ni afya nzuri, pesa nyingi, cheo kizuri, elimu nzuri kuna watu pengine kutokana na figisu zao na wivu usio na maana wamejikuta wakiwachukia au kuwapenda watu wengine. 

Kumbe wakati mwengine watu  watakuchukia au kukupenda kutokana na kufanikiwa kwako tu, au kuwa na afya nzuri, kufundisha vizuri, kuzungumza vizuri utakuta watu watakwambia unajifanya duuh! Ajabu kweli.

NINI CHA KUFANYA?

Tambua dosari na mapungufu ya mwonekano wako na uyapende

Watu wengi wamekuwa makini kuyafahamu mapungufu na dosari za watu wengine huku wakijiweka pembeni kabisa kwa habari ya dosari zao. 

Aidha watu wamekuwa hawajui kabisa dosari na mapungufu yao kitu hiki pekee wamejikuta wakiingia kwenye simanzi na migogoro na watu wengine mara tu mapungufu yao wakisikia yanatajwa.

Kikubwa hapo ni kutambua mapungufu yako na kuyakubali kisha weka mipaka watu wengine kutumia mapungufu na historia yako kukuumiza.

Kuna usemi mmoja unasema “if you accept yourself the way you are the world recognizes you” maana yake ni kwamba “kama ukijikubali mwenyewe jinsi ulivyo dunia itakutambua”.

Epuka kumfurahisha kila mtu.

kwani watu wengi hawana shukurani hata kama utawafanyia mema mengi na makubwa kiasi gani. 

Elewa kwamba watu hawaliziki ukifanya jema watasema, ukifanya baya watasema, ukiwasaidia watasema usipowasaidia watasema pia. 

Hivyo huwezi kuwafurahisha watu wote kwa kitendo kilekile kwa wakati mmoja. Kubwa jitahidi kufanya lililo jema na linalompendeza Mungu. Binadamu ni watu ambao hawaridhiki na kama ukitaka kuwafurahisha wote basi jiandae kuwaudhi wote

Kubwa jitahidi kufanya mema, yanayokupa furaha wewe na yanayompendeza Mungu.

Tambua kuwa wewe ni binadamu. 

Kuwa binadamu maana yake ni kutokuwa mkamilifu, kama binadamu mapungufu huwezi kukosa na watu wanamapungufu yao na wewe unamapungufu yako, hivyo usitake kuonekana umekamilika kwa kutaka kuwafurahisha watu wote. Kufanya hivyo utaishi maisha ya utumwa na yasiyo yako. Ishi maisha yako bhana.

Mwisho nitumie nafasi hii kusema, kama utatumia mapungufu na mionekano ya watu wengine, kuwakandamiza au kuwachukia elewa kuwa jambo hili si zuri. 

Kwani miili yetu hii tuliyo nayo ni nyumba ya utu wetu wa ndani. Mtu halisi yupo ndani ya mwili wake na siyo huo mwili unao uchukia, urefu wake, weupe wake, ufupi wake, Ngozi yake macho yake n.k. Kudhibitisha hilo kuna watu wengi sana waliodhaniwa kuwa na mionekano na sura mbaya lakini wamefanya makubwa na wamegusa maisha ya mamilioni ya watu.

Kama tukilifahamu hili hata katika kuolewa na kuoa mwonekano na sura ya mtu isiwe kigezo pekee cha kutafuta mwenza wa maisha. 

Badala yake angalila pia utu wake wa ndani, hapa ni pamoja na ndoto, malengo na maono yake, nadhani itakufaa sana. 

Au itakufaa nini kuoa au kuolewa na mme (mke) mwembamba/mrefu ambaye si wa ndoto zako?

au itakufaa nini kuoa au kuolewa na mme(mke) mweusi/mweusi ambaye si wa ndoto zako?

au itakufaa nini kuoa au kuolewa na mme(mke) mrefu/mfupi ambaye si wa ndoto zako? N.k

Rafiki badilika, kisha tambue kuwa hata, uwe mwema kiasi gani katika hii dunia huwezi kukubalika au kupendwa na watu wote kwa 100%, vile vile huwezi kuchukiwa au kutokukubalika na watu wote kwa 100%.

Rafiki! ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi, maendeleo binafsi, na Maisha

Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork

Karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >> +255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

Facebook page>> add value network.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe. 

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.