MAAJABU YA AKIBA

Mtu mmoja alikuwa analalamika sana huku akidai kuwa, amejifunza vitu sana ikiwemo kulima, kushona nguo, amesoma sana kompyuta, kufanya biashara, kama ni vitabu amesoma sana. Kimsingi alidai kuwa anajua karibia kila kitu. Lakini alichokuwa analaumu kwamba haoni badiliko lolote kabisa katika maisha yake, licha ya kujifunza vitu na maarifa kama yote. Nilipo muuliza, kwenye kompyuta anajua kitu gani? Akasema anafahamu kompyuta yote na amejifunza miaka miwili iliyopita na notisi aliandika zote sema hakumbuki daftali alipoliweka, lakini akituliza akili atalipata mara moja. Nikamuuliza nikileta kompyuta hapa unipangie kazi yangu utaweza? Akasema, hivyo vyote nilisha visoma na niliviandika tena vipo kwenye lile daftali, sema kompyuta mi sijawahi kutumia lakini nikiangalia kwenye lile daftali naweza afu mbona ni simpo tu.
Nikagundua kuwa mtu huyo
alikuwa ametumia muda mwingi na gharama kubwa sana katika kujifunza vitu vingi sana.
Alikuwa ameandia notisi na hatua zote muhimu ili kuvifanikisha vitu hivyo.
Ajabu ni kwamba ingawa alikuwa amejifunza vitu vingi, lakini hakuwahi
kuvifanyia kazi na vingine hata hakuvifahamu kabisa. Mfano alikuwa amejifunza
kilimo cha nyanya mtandaoni, lakini hakuwahi kulima hata siku moja, pia alikuwa
amejifunza kutengeneza sabuni ya mche, unga na maji lakini hakuwahi kutengeneza
hata sabuni moja, alijifunza sheria za fedha na namna ya kuepukana na madeni
kwenye kitabu cha Tajiri mkubwa wa babeli, lakini hakuwahi kuzingatia na
kufanyia kazi hata kimojawapo japo alikuwa anazifahamu, pia alikuwa
amejifunza kompyuta na matumizi ya kompyuta lakini hakuwahi kutumia kompyuta, na
vitu vingine kedekede ambavyo alinitajia.
Ikumbukwe kwamba si kwamba vitu hivi alikuwa
amevisahau vyote hapana, vingi alikuwa anavikumbuka kabisa lakini pamoja na kuvikumbuka kwake bado alikuwa anaona maisha yake yako
vilevile hayabadiliki kabisa. Yaani, kama ni madeni yalizidi kuongezeka, kama
kudharaulika ndo usiseme, kukosa pesa ndo kabisa n.k.
Mtu huyo nilimuuliza kwamba unafahamu sababu
kwanini bado maisha yako hayabadailiki ingawaje unamaarifa na unafahamu vitu
vingi? Akasema bado hajafahamu shida ni nini? Nikamwambia usipolifahamu tatizo
huwezi kulitatua tatizo, vinginevyo itakuwa ni chanzo cha matatizo mengine. Akaomba
nimusaidie sana katika kulifahamu tatizo lake kwani nilikuwa namfahamu vizuri.
Hapo ndipo nilipoamua kumsaidia na kumwambia tatizo lake liko wapi, na tatizo
lake lilikuwa ni hili hapa.
Kutokufanyia mazoezi kitu alicho jifunza yaani nasema, kutokufanyia kazi au utekelezaji maarifa aliyokuwa amejifunza na kuyafahamu. Aidha, kwa kuambiawa, kujifunza au kwa kufundishwa. Kitu hiki hakikumwacha salama kabisa. Nasema hivi kutokufanyia kazi maarifa aliyo nayo hiki kitu hakikumwacha salama kabisa, kwani alibaki na matatizo yake hata kama alikuwa na maarifa kama yote. Nilimshauri na kumwambia maisha yake yatabadailika endepo ataamua kufanyia kazi , kutekeleza na kufanyia mazoezi ya mara kwa mara katika kila atakacho jifunza, ambacho kinalenga kuboresha maisha yake, fanyia kazi tena kwa bidii.
Namshukuru Mungu kwamba alikuwa mwelewa na aliamua kufanya mazoezi ya
mara kwa mara katika juzi zote alizokuwa amejifunza na atakaokuwa anajifunza,
na kuanzia hapo maisha yake yalianza kubadilika kabisa na Hadi Sasa amekuwa mtu mwenye
mchango mkubwa sana kwa watu waliomzunguka na jamii yake kwa ujumla, na hadi
sasa ni mtu ambaye anafanya vizuri na kuna mengi ya kujifunza kutoka kwake.
Hivyo ndugu kitendo cha wewe kutofanyia
mazoezi vitu ambavyo unajifunza kwaajili ya maandeleo na maisha yako kwa
ujumla, kitu hiki hakita kuacha salama.
Kutochukua hatua ya kufanyia kazi au
utekelezaji wa maarifa unayo jifunza
kila siku kwa manufaa yako mwenyewe hiki kitu hakitakuacha salama.
Katika hili ni muhimu kufahamu kuwa kusoma na kuyafahamu maarifa ni jambo moja, na kuchukua hatua,utekelezaji au kufanyia kazi maarifa hayo ni jambo lingine tena la tofauti kabisa. Yaani, kusoma vitabu pekee hakutoshi, kujifunza pekee hakutoshi na kufahamu vitu vingi pekee yake hakuwezi kukufanikisha wala kukufikisha unakotaka.
Kufanya hivyo ni vizuri sana
tena ni hatua ya kupongezwa, pengine hatakupewa zawadi kabisa lakini kunahatua
muhimu ya pili ambayo unahitaji kuipiga baada ya kuvifahamu vitu vyote hivyo,
nayo ni utekelezaji (kufanyia kazi). Hapo unahitaji kufanyia kazi kitu
utakachojifunza na kuona kuwa kina manufaa katika maisha yako vinginevyo
mabadiliko utayasikia tu.
Ulishawahi kujiuliza ingekuwaje wachezaji wa
mpira wangekuwa wanasomeshwa mpira darasani wanaacha hivyohivyo bila kufanyia
mazoezi ya kile walichojifunza? Vipi kuhusu wakulima wangekuwa wanasoma kilimo
darasani pekee yake bila kwenda kufanyia mazoezi mafunzo hayo? Au ulisha wahi kujiuliza
kwanini baadhi ya watu pamoja na kufundishwa uzalendo, maadili na dini kila
siku lakini bado dhambi na maasi vinazidi kuongezeka ?
Hapo ndipo utakuja kujua kumbe kujifunza pekee
yake hakujitoshelezi, kujua vitu vingi pekee yake hakujitoshelezi hapo unahitaji
hatua moja mbele zaidi, ambayo ni kufanyia kazi tena kwa bidii kile ambacho unakifahamu au umejifunza.
Umejifunza kulima vitunguu nenda kalime, umejifunza kutengeneza sabuni nenda
katengeneze, umejifunza biashara nenda kafanye, umejifunza uwekezaji nenda
kawekeze, umejifunza uandishi nenda kaandike. Yaani, nasema nenda kafanyie
mazoezi huo ujuzi wako, hiyo ndoto yako, hicho kipaji chako vinginevyo kitu
hiki hakitakuacha salama.
Usiwe kama wale wengine ambao wakifahamu kitu ndo imeenda hiyo na wengine hawataki hata kufanyia kazi na mazoezi ya kile walichojifunza huku wakitegemea maisha yao kuna siku tu yatabadilika yenyewe bila kufanyia kazi.
Mwingine utakuta anakipaji kizuri kweli lakini hataki kukinoa na kukifanyia
mazoezi akisema eti yeye anakipaji kikubwa, ndugu tambua kuwa kipaji chako hata
kiwe kikubwa kiasi gani kama hukinoi na kukifanyia kazi utabaki kuwa mtu wa
kawaida sana, hebu jifunze kwa watu wenye vipaji vyao kama akina Diamond
platinum, Messi, Ronaldo, Mbwana Samata na wengine kibao. Watu hawa pamoja na
kuwa na vipaji hawajaacha kufanyia kazi juzi zao na vipaji vyao katika kufanikisha
na kufikia ndoto zao. Na wewe kama unatabia ya kutafuta maarifa, kujifunza kwa bidii
lakini hufanyii kazi kile unachojifunza yaani, unalala tu huna muda wa kufanya
mazoezi maarifa hayo. Nikwambie tu ukweli kuwa jambo hili halitakuacha
salama.
Rafiki! ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine
namna gani ya kuondokana na adha hii wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia
mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii imeandaliwa
na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa
Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu sana ujiongezee
thamani yako.
Kwa
mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697
/+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako
nitafurahi kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Nuru · 101 weeks ago
Migongo · 101 weeks ago
Ayusto · 100 weeks ago
Migongo · 100 weeks ago
Agripina Mghamba · 79 weeks ago
Nimejifunza mengi.
Mungu AKUBARIKI MNOOOOO 🙌
Agripina Mghamba · 79 weeks ago
Sio kuishia tuu kujaza notebook
Elias · 79 weeks ago
Migongo · 79 weeks ago