MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

MAMBO YA KUJIFUNZA KUTOKA KWENYE PICHA HII.

 MAMBO YA KUJIFUNZA KUTOKA KWENYE PICHA HII.

Tunaishi kwenye karne ya 21. Katika dunia hii kwa kweli pesa yaani, hela ni muhimu sana. Kwani, ukitaka kusafiri utahitaji pesa, ukitaka kula utahitaji pesa, ukitaka kusoma utahitaji pesa, ukitaka kutibiwa utahitaji pesa, ukitaka huduma nzuri  za viwango utahitaji pesa n.k. Watu wengine wameenda mbali sana na kusema, pesa ni kila kitu katika ulimwengu tulionao.

 Kwa mkutadha huu ni shauku ya kila mtu  kuwa na pesa za kutosha angalau kutawala kila eneo. Si unajua pesa inanguvu ya kutawala eeh! Utakubaliana na hili pale utakapoona hata katika vikao vya familia mtu mwenye pesa anapewa umuhimu na kuungwa mkono kwa kila jambo hata kama anaongea utumbo, lakini kinyume kabisa, kwa wenye pointi ambao hawana pesa, utasikia ananini na yeye huyu? Full kupuuzwa. Kumbe pesa inatusaidia kujikimu, kupata mahitaji yetu ya msingi, inatoa kibali, inarahisisha mambo, ina ongeza umaarufu, inaongeza marafiki, na mengine ya kufanana na hayo.

Pamoja na hayo yote, naomba tuelewane kuwa pesa siyo kila kitu katika dunia hii. Hii ni kwasababu, kuna vitu vingi  pesa bado haijaweza kuvinunua, au kuvitatua. Vitu kama; usingizi, furaha, uhai, huruma, utu, uzazi, faraja ya kudumu na vitu vingine kama hivyo pesa haijafanikiwa kuvinunua bado. Hivyo basi, baada ya maisha pesa ni ya pili kwa umuhimu katika ulimwengu huu. Kumbe pesa ni muhimu sana lakini siyo kila kitu.

Kwa utangulizi mfupi turudi sasa kwenye picha yetu hapo juu. waweza rudi kuaiangalia tena ili tuende sawasawa.

Kama utaitazama vizuri hii picha utagundua kwamba kuna vitu kama vitatu vinaonekana wazi hapo, kwanza kuna mwanamke ambaye yupo katika uso wa simanzi na anatafuta namna ya kujiondoa katika simanzi hiyo, pia kuna pesa yenyewe na kitu kingine kuna mikono ambayo imeshika fedha hii na haijulikani kama ni mikono ya mwanaume au mwana mke lakini, ukiangalia vizuri hii mikono inatofautiana ule wa mwanamke. Kwa maana hiyo, inawezakuwa ni mikono ya mwanaume.

Bila shaka, umeeanza kupata kitu sasa eeh!

Mambo niliyo jifunza katika picha hii ni kama yafuatayo;

1. Fedha ikitumiwa vibaya huleta unyanyasaji wa kijinsia. 

Pamoja na kwamba pesa imehusika hapa lakini, mwanamke huyu anaonekana kuwa hana furaha kabisa na kitu hichi  ndiyo maana ukiangalia vizuri ni kama vile analia. Kwasababu ya umhimu wa pesa watu huwa lazimu kufanya chochote ili kupata mahitaji yao ya msingi kitu hiki kimeleta manyanyaso mengi kwa jinsia zote na kupelekea, kuishi maisha ambayo hawakuchagua.

2. Fedha siyo kila kitu katika maisha lakini, ni muhimu sana. 

Kama tulivyoona hapo juu kuna baadhi ya vitu pesa haiweze kuvifanya. Kama tunavyoona pia katika picha hii kuwa, fedha haijaweza kuleta furaha na amani ya mwanamke huyu. Lakini, itampatia mahitaji ya msingi kama chakula, malazi, nguo n.k. Hivyo pesa ni muhimu lakini siyo kila kitu.

3. Kama ikitumiwa vibaya, pesa inaharibu utu na maisha ya mtu. 

Kutokana na umuhimu wa fedha katika dunia hii, watu wengi wamekandamiza haki za watu wengine, wamewanyayasa kwa namna yeyote ile kwasababu ya pesa. Wengine wamekuwa wakinyanyaswa kingono kwa mkono wa pesa, wameingia kwenye biashara haramu kama, ukahaba, madawa ya kulewa, ushoga n.k. ili kupata pesa. Kitu hiki kimeharibu na kuvua kabisa utu wa waetu.

Hayo ni machache tu niliyo tamani tujifunze pamoja kupitia picha hii.

Kutokana na  matumizi,  pamoja na  faida  zake, pesa ni muhimu sana. Na kuandika hivyo, sikukukatisha tamaa kutafuta pesa hapana bali, pambana na tafuta fedha zako kwa jasho lako mwenyewe na fanya hivyo kwa kutumia njia halali tu, kakuna vya bure.

Tambua kwamba pesa ikitafutwa kwa njia zisizo halali huharibu kabisa maana na dhana ya kutengenezwa kwake kubwa kuliko inaharibu utu wa watu. Na wakati mwingine maovu mengi yanatokea kwasababu ya utafutaji haramu wa pesa. Tunaona watu wakiingia katika ushoga, wizi, ukahaba, ujangiri, ujambazi na maovu mengine mengi kwasababu ya matumizi na utafutaji mbovu wa pesa.

Achana na njia hizo mbovu zitakupeleka kubaya. Utakosa amani kwasababu ya pesa, utakosa furaha kwasababu ya pesa. Yanini yote hayo? Hebu tumia njia halali kupata pesa zako na utaishi maisha ya furaha. Vinginevyo utakuwa mtumwa wa fedha eti.

Mtu mmoja alinikuta naiangalia sana picha hii ili, kujifunza kitu.  Akaniuliza inamaana gani picha hiyo? Nikamuuliza wewe umejifunza nini kutoka kwayo? Akasema mara nyingi wanawake wananyamazishwa kwa pesa. Nimeipenda hiyo lakini sijajua kama kuna ukweli hapo hahahahah.

Pointi yangu ni kwamba wewe umejifunza nini kutoka kwenye picha hii? Naomba comment yako hapo chini.

Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

LinkedIn>>Migongoe. 

Pinterest>>eliasmigongo.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe. 


 

Comments (11)

Loading... Logging you in...
  • Logged in as
Umenena vyema kabisa
1 reply · active 97 weeks ago
Ahsante nashukuru Mary
Ngimba tito's avatar

Ngimba tito · 97 weeks ago

Boss kwa kweli somo lako na masomo yakoo yananipa kitu chenye mchango Mkubwa maishani mwangu mungu akupiganie mr memy
1 reply · active 97 weeks ago
Ahsante nashukuru Ngimba Tito.
CONT.... LIFE IS NOT LIKE MONEY WHILE maisha ni jinsi unavyoishi hata kama huna hela uwezi itwa ni hela maisha ni lstaili ya kutafuta Ila binadamu husema maisha ni kutafuta Wala si kutafutana hivyo binadamu na walimwengu wanatafuta pesa kwa Njia mbali mbali ndiyo maana wanakuja na sababu ya kusema money is each and everything which is impossible so uhai. Upo chini ya hela hivyo ahsante sana kijana kwa kunikumbusha snanerio hii.
2 replies · active 97 weeks ago
Migongo Elias's avatar

Migongo Elias · 97 weeks ago

Ahsante nashukuru Daniel nimejifunza kutoka kwako
Migongo Elias's avatar

Migongo Elias · 97 weeks ago

Ahsante nashukuru Daniel nimejifunza kutoka kwako
Scholastics Ernest's avatar

Scholastics Ernest · 97 weeks ago

M nmejifunza kwamba mtu anaweza akafanyiwa kitu kibaya na akashindwa kutetea haki yake kwasababu ya nguvu ya pesa ambayo itatumika kama rushwa kwaajili ya kunyamazisha kitu hicho.
1 reply · active 97 weeks ago
Migongo Elias's avatar

Migongo Elias · 97 weeks ago

Point nzuri sana hii, barikiwa Scholastica Ernest
Thanks
Elias Migongo's avatar

Elias Migongo · 97 weeks ago

Nice Mage

Post a new comment

Comments by

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.