HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

NJIA 5 ZA KUACHA ALAMA DUNIANI.

      

NJIA 5 ZA KUACHA ALAMA  DUNIANI.

Kutokana na kamusi sanifu  ya kiswahili alama ni mchoro unaoonyesha ishara fulani. Yaani, kwa ufupi alama ni ishara ya kitu fulani. Lakini mimi nitaeleza alama kuwa ni utambulisho wa kitu au mtu wakati na baada ya uhai au kuwepo wake. 

Kwa maana fupi ni kwamba alama ni vile ambavyo unaweza kugusa maisha ya watu wa sasa na hata baada ya kuondoka kwako duniani. Kwa mfano tukimuangalia mtu kama Stive Jobs mwanzilishi wa simu janja ya kwanza, huyu mtu pamoja na kwamba amekufa lakini bado tunatambua thamani ya kuishi kwake hapa duniani.

Robin Sharma kwenye kitabu chake cha nani atalia utakapokufa, ameandika vitu vitatu vitakavyo kufanya uache alama  duniani hata baada ya uhai wako. Vitu hivi, hata wewe utakapo vifanya utakuwa na uwanja mzuri wa kuacha alama, vitu hivi ni;

1. KUANDIKA KITABU.

Vitabu ni vyanzo vizuri na muhimu sana linapokuja suala zima la maarifa ambavyo hudumu karne kwa karne. Sharma ameandika kuwa, kutokana na vitabu kudumu kwa muda mrefu, hata baada ya mtu kuondoka kwa dunia. Hivyo kutokana na kuhifadhi maarifa mbalimbali na watu watakapo hitaji maarifa hayo ndipo mwandishi atahusika moja kwa moja kwa mchango wake.

Kumbe mtu anaweza kuishi miaka mingi sana hata kama ukifa. Hebu chukulia vitabu kama vya kina William James, Nelson Mandela, Adolf Hitra, Shark spare na wengine kibao, watu hawa walishakufa lakini bado tunajifunza mengi sana kutoka kwenye vitabu vyao. 

Kitu hiki kimebaki kuwa ni alama na zawadi kwetu na vinaendelea kutumika siku kwa siku ingawaje wenye navyo walishafariki. Hivyo hata wewe unaweza kuishi na kuacha alama kupitia kuandika vitabu, ambavyo vitakuwakilisha na kukusemea sehemu ambazo usingeweza kufika kabisa na uzuri ni kwamba kitabu chako kitaendelea kuishi hata kama wewe utakufa.

2. KUPANDA MITI.

Kutokana na faida nyingi kuonekana za kuwepo kwa miti katika mazingira yetu. Miti inatumika kwa kuni, mbao, hewa safi ya oksijeni, kivuri, utarii, masikani ya viumbe hai wengine, dawa, chakula na mengine kama hayo. 

Nakumbuka nyumbani nilipanda miti ya matunda sikujua kama itakuja kuwa na matokeo makubwa kiasi hicho. Lakini, kutokana na faida wanazopata kwenye miti hiyo, kwa kweli wananishukuru na kunikumbuka sana kwa kuipanda miti  hiyo. 

Nakumbuka pia, kuna mzee mmoja alipanda miti mingi ya matunda (maembe) lakini ilipofika kimo fulani hivi akaing’oa hiyo miembe. Alipoulizwa kwanini, akasema ukipanda miche ya miembe ikikua na kuanza kutoa matunda mpandaji unakufa hapohapo hahahahaha! Ajabu kweli. Hakutaka kabisa kufa mapema kiasi hicho kwahiyo, aliamua kuikata na kuing’oa palepale. 

Hii ni imani ambayo inaweza isiwe na maana kabisa. Ajabu ni kuwa miembe iliyopandwa kipindi kile yule mzee anaing’oa miembe yake bado ipo inatoa matunda ya kutosha na mpandaji wake bado anadunda tu mtaani. Sasahivi yule mzee anajilaumu sana kwa kuing’oa miti ile, lakini sasa amebadilika amekuwa ni mpandaji mzuri wa miti. 

Hata wewe nikushauri  uwe mpandaji mzuri wa miti. Pamoja na kwamba utapata faida nyingi za kupanda miti lakini pia, utakumbukwa kwayo. Na wachina husema muda mazuri wa kupanda miti ulikuwa ni miaka 20 iliyopita na muda mzuri zaidi ni sasa, yapende mazingira yako kwa kupanda miti ambayo tutakukumbuka kwayo.


3. KUZAA MTOTO.

Ukweli ni kwamba kila mtu ana ndoto na malengo yake. Pia ni lazima tukumbuke kuwa hakuna mtoto asiye na mzazi, kila mtu anapofanikisha na kutimiza malengo yake huwa hatuachi kuwataja na kuwakumbuka wazazi wao. Kwa kuwazaa na kuwalea watu hao.

 Hapa kuna kitu cha kujifunza, wewe mzazi wa leo, mzazi wa kesho unalojukumu la kumlea na kumtunza mtoto/ watoto wako hata kumsaidia kuifikia  hatima aliyo umbiwa, ukifanya hivyo tutakukumbuka sana kwa malezi bora, na kutuletea mtoto bora ambaye atafanya vitu vitakavyo gusa maisha ya watu na sisi tutamkumbuka daima na wewe tutakutana pia.

Njia nyingine ni pamoja na;

4.KUGUSA MAISHA YA WATU.

Hiki kitu, ni muhimu sana kukielewa pindi uwapo duniani. Watu wapende wasipende watakukumbuka tu kama kuishi kwako kulikuwa kunagusa maisha  yao. Na hapo unaweza kujiuliza nitagusaje maisha ya watu? 

Unaweza  kufanya vitu vingi sana vitakavyokuwezesha kugusa maisha ya watu. Vitu kama vile kuwasaidia watu kupata wanavyotaka, hii ni kwasababu, ukiwasaidia watu kupata wanachokitaka, utapata unachokitaka tena utapata zaidi.

 Pia, kwa kutatua matatizo ya watu, watu wana matatizo kibao sana wanahitaji majibu ya matatizo hayo na si vinginevyo. Sasa, ukiwasaidia kupata majawabu ya matatizo yao utagusa maisha yao na utaacha alama. 

Kufanya matendo mema, hii itasaidia watu kujifunza kutoka kwako na kutajwa kama mfano wa kuigwa, katika jamii. Gusa maisha ya watu nakuambia watu hawatatamani ufe hata ukifa watakukumbuka sana. Kuna habari moja kwenye biblia mtu mmoja alikuwa anaitwa Tabitha alikuwa akiwapa watu misaada, kuwashonea kanzu na nguo wazee kwa wajane bure kabisa, kiufupi mama huyu alikuwa anawafanyia matendo mema watu na alikuwa anapendwa sana, mtaani kwa misaada na wema wake. Lakini ulifika wakati akafa watu walilia sana wakaamua kumwendea mtumishi wa Mungu akaja kumfufua akaishi tena.  Kasome biblia Matendo ya mitume 9:36-40

5. KUTIMIZA NDOTO YAKO.

Hivi unamkumbuka Yesu ? Julius Kambarage Nyerere? Nelson Mandela?  Kanali Mwamary Ghadafi? Mahatima Ghand? Nkwame Nkuruma? Maladona? Na wengine watu hawa wanakumbukwa kwa namna ambavyo wametimiza ndoto na malengo yao. 

Goja nikwambie kitu hapa, wewe kutimiza ndoto yako tu, ni alama kubwa ambayo itakumbukwa sana hata ukiondoka hapa duniani. Kwani ukitimiza ndoto yako utawasaidia wengi sana kufikia mipango na malengo yao, utagusa maisha ya watu wengine na pia utakuwa ni mtu wa kuigwa katika jamii yako na dunia kwa ujumla.

 Hivyo acha kabisa habari za kuwa bize na maisha ya watu wengine badaa yake kuwa bize kupambania ndoto zako, utashangaa watu watakavyo kuwa bize na wewe. Timiza malengo yako utakumbukwa kwa hilo na Mungu akusaidie sana.

Rafiki ukivifanya vitu hivi ipasavyo na kikamilifu,utakuwa kwenye hatua nzuri sana ya kuacha alama katika maisha yako. Na hapo ndipo utakapo kumbukwa kwa hayo na Mungu wa mbingu na nchi akusaidie sana. 

Lakini pamoja na hayo yote ikumbukwe kuwa si kila mara unaweza kuacha alama njema katika maisha yako uwapo au baada ya kuondoka hapa duniani. Bali unaweza kuacha alama njema au mbaya. 

Tunao watu wengi ambao hadi leo wanakumbukwa kwa mabaya waliyo tenda ambayo yameathiri maisha ya watu wengine, hii ni kwa namna ambavyo waliamua kuchagua kukumbukwa kwa mabaya. Kumbe uchaguzi ni wako kwamba uamue kukumbukwa kwa mema au mabaya? Hizi zote ni alama  ambazo unaweza kuacha hapa duniani na watu wakakukumbuka kwazo. Nikushauri chagua kukumbukwa kwa mazuri ndugu yangu.

Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

Kwa mawasliano, na ushauri piga simu au kutuma ujumbe WhatsApp kwa namba hapo chini.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi, maendeleo binafsi, na Maisha

Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa ADD VALUE NETWORK. Karibu sana ujiongezee thamani yako. 

mawasiliano

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

LinkedIn>>Migongoe. 

Pinterest>>eliasmigongo.

Facebook page>> Add Value Network.

Kama umejifunza kitu, acha  maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja na wewe. 

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.