MAAJABU YA AKIBA

SABABU ZA HOFU YA KUZUNGUMZA MBELE YA WATU (REASONS FOR FEAR OF PUBLIC SPEAKING).
Nakumbuka nilipokuwa sekondari kidato cha kwanza, mara
nyingi nilipokuwa nikipangwa kuzungumza hotuba ya asubuhi (Morning speech).
Nilikuwa nahisi kuchanganyikiwa, kuugua, kukosa utulivu, kutokwenda shule na wakati mwingine nilikuwa nawaza hadi
kuacha shule. Yaani, nilikuwa na hofu isiyokuwa ya kawaida lilipokuja suala la
kujieleza na kuzunguza mbele ya kadamnasi. Lakini Namshukuru Mungu kwakuwa alinikutanisha
na waalimu pamoja na watu sahihi wakanisaidia nikawa nafanya vyema katika eneo
hilo.
Katika mizunguko yangu hadi sasa nimekuja kugundua kuwa
siyo mimi tu niliyekuwa na tatizo hilo, kumbe ni watu wengi sana wakubwa kwa
wadogo, waume kwa wake tena karibia watu
wote duniani. Kwani hata tafiti zinaonyesha kuwa asilimia(75%) ya watu duniani
wanasumbuliwa na hofu hii . Hofu hii ni moja ya hofu zinazo ogopeka na kutesa
watu wengi sana duniani. Hapo ndipo utakuja kushangaa mtu alikuwa sawa kabisa
kabla ya kupita mbele ya watu lakini
baada tu ya kupita ili kuzungumza mbele
yao, utashangaa sauti inabadilika kabisa, mapigo ya moyo yanaanza kwenda mbio,
jasho linaanza kutililika, kuhisi kuumwa, kubanwa na haja ndogo na mengine
mengi. Kuna mtu alisikika akisema “Yaani
mimi bora uniue kuliko kunipitisha mbele ya watu eti nikajitambulishe au
kuzungumuza chochote wala siwezi”.
Ukweli ni kwamba hakuna mwanadamu asiye kuwa na hofu hasa
katika eneo hili sema ni vile tu watu wanavyitofautiana katika kukabiliana na
hofu zao mara zinapo wakabili. Pamoja na kwamba kila mtu anakumbana na hofu
lakini hofu hii ya kuzungumza mbele ya watu bado ni tishio na kipengele kwa
watu wengi duniani. Kitu hiki ndicho kimenifanya nitake kufahamu zaidi kuhusu
kisa hiki, hapa ndipo nimekuja na sababu lukuki
zinazowafanya watu wengi wahofie kuzungumza mbele ya watu. Fuatana na
mimi sasa;
Hizi ndizo sababu kwanini watu
wanahofia kuzungumza kwa mbele ya watu;
1. DHANA
YA KUWA KITOVU CHA USIKIVU (THE IDEA OF BEING THE CENTER OF ATTENTION).
Kitu hiki watu wengi huwafanya wahofie sana pale
lilnapokuja suala la kuzungumza mbele ya hadhara. Kwani, huogopa sana usikivu na umakini kutoka kwa
wasikilizaji ambao hutega masikio na kuvuta umakini wa kusikia kutoka kwa mzungumzaji. Kwasababu hiyo
mtu anaanza kujiona kama vile hana kitu cha kuzungumza na kuwaambia
wasikilizaji wake. Watu wengi hujiuliza na kufikiria sana kuwa watawaambia nini
wasikilizaji wao, hasa wakikumbuka macho ya
hadhira na umakini wao wa kutaka kujua kutoka kwa mzungumzaji wao.
Kitu kikubwa hapa ni kufanya maandalizi ya kutosha ,
kujiamini kuwa unaweza na kubwa kuliko ni kuamini kuwa unaweza kufanya hivyo
kuliko mtu yeyote hapo, ndiyo maana wanakusikiliza. Ubongo wako ukiuambia hivyo
utafanya hivyo kweli si unajua ubongo unafata amri ya mtu mwenyewe.
2. KIWANGO
CHA MAISHA YA WASIKILIZAJI/HADHIRA (STATUS OF AUDINCE).
Watu
wale na digrii zao nitawaambia nini mimi, watu
wale na pesa zao watanisikiliza kapuku mimi! Maneno kama hayo nikutana nayo kwa
baadhi ya watu nilipo wauliza kuhusu jambo hili. Na nimekuja kugundua kwamba
kiwango cha maisha ya wasikilizaji (Hadhira) ni moja ya sababu ambayo watu
inawapa kiwewe cha kuzungumza mbele ya hadhira. Kutokana na hadhira kuwa na
kiwango kikubwa pengine cha elimu, uchumi, akili, maarifa n.k kumzidi yeye,
hapa msemaji huzani kuwa wasikilizaji wake wanajua kila kitu na hivyo huhisi
kama vile hatoeleweka au pengine kufanya marudio tu na kuwapotezea muda. Hiki
kitu siyo kweli kwani hakuna binadamu yeyote ambaye anafahamu kila kitu hayupo
na hawezi kuwepo. Mawazo haya nilikuwa nayo pia siku za nyuma nilikuwa nafikiri
kuwa, watu wote walioko sekondari wanajua kingereza kumbe ni fikira tu. Hivyo
hata wewe ukifikiri kuwa hadhira wako wanafahamu kila kitu
tambua kuwa hizo ni fikira tu.Jiamini wewe na chukulia kuwa ujumbe
unaowapelekea hawaujui ndio kwanza unakwenda
kuwasomesha.
Nimekuja
kugundua kuwa asilimia
kubwa ya watu wengi hawapendi kabisa kukosolewa, hasa kukosolewa mbele
ya hadhira. Wengi wanapenda kusifiwa, kupongezwa, kutambuliwa n.k, lakini siyo kukosolewa na kuambiwa ukweli.
Hivyo watu wa aina hii wakifahamu kabisa kuna watu fulani ni maarufu ka kukosoa
na wapo mbele yao, watajitahidi wasizungumze kabisa, kama itawabidi kuzungumza
hapo ndipo huwa mwanzo wa hofu na kujawa na wasi wasi mwingi.
Pia ni muhimu kutambua kuwa ukosoaji ni muhimu sana katika maisha yetu kwani huu ndiyo huibua makosa ili kurekebisha na kuimalisha katika kila jambo, ndiyo maana kuna msemo unasema criticisim may not be agreeable but its very neccessary it calls attention to unhealthful state of thing. Tafisiri yake ni kwamba “Ukosoaji unaweza usikubalike, lakini ni muhimu sana kwani huleta umakini kwa mambo ambayo hayaendi sawa”. Usipende kuwachukia wanao kukosoa jifunze kutoka kwao. Japokuwa wengine wanaboa kweli kweli.
4. HOFU
YA KUSHINDWA (FEAR OF FAILURE).
Hiki
ni kitu kingine ambacho watu wengine huweka akili na mitazamo yao mikubwa kuwa
wakishindwa kufanya vizuri kama watu fulani itakuwaje? Na wengine huwaza kuwa
mama yupo, baba yupo, mke, mchumba, mme, rafiki, na watu wengine muhimu kwamba
nikishindwa kufanya vizuri kama nilivyo waaminisha itakuwaje? Au wataniona je?
Kwa kuwaza hivi watu wengi hujikuta wapo katika hofu ya kupoteza uaminifu, sifa
na jina ambalo watu hao wamelijenga.
Kama
ulikuwa hujui ni kwamba “poor preparation prepare poor performance” yaani, “Maandalizi
duni huandaa matokeo mabaya”. Huo ni ukweli usio pingika kwamba kadiri
unavyofanya maandalizi ya kutosaha na kufanyia mazoezi mengi ndivyo
unavyoongeza ujasiri na kupunguza hofu au uoga.
Saikolojia
inaonyesha kuwa malezi na makuzi ya mtu hasa kipindi cha utotoni yana mchango
mkubwa sana katika kuathiri akili yake hata anapokuwa mtu mzima. Hii ni sawa na
kusema kama umelelewa kwenye familia ya wazazi wakali, wenye kukufokea,
walevi,wenye sifa mbaya mtaani, mzazi mmoja,kulelewa na ndugu mfano kaka,
shangazi, mjomba,kukukosoa sana, kubaguliwa,kufanyiwa manyanyaso na mateso
mengi. Hii husababisha mtu atakapokuwa mtu mzima kujichukia, kutokujiamini,
kuwa na aibu sana pia anakuwa mtu wa kujikatia tamaa mapema sana.
Kuna
watu automatic tu hawajiamini wao wenyewe. Sasa mtu kama huyu akiwa hajiamini
yeye mwenyewe hata linapokuja suala la kuzungumza mbele ya watu wengine huogopa sana akihofia atawalisha
matango poli watu wengine. Ndugu yangu kama hujiamini hili ni tatizo ambalo
inatakiwa ulishughilikie mapema sana kabla halijakughalimu.
Kujiamini ni muhimu sana kwa kila mtu aliyepanga kufika
mbali vinginevyo itakughalimu na kukurudisha nyuma katika kuyaendea malengo na
ndoto zako na utaishia kuwa mtu wa kawaida tu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha
hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo
chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa
na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia,
Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz.
Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja
nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Lilian clinton · 99 weeks ago
Migongo · 99 weeks ago
Scholastica Ernest · 97 weeks ago
Elias Migongo · 97 weeks ago
Cheyo · 97 weeks ago
Timotheo · 53 weeks ago
Elias Migongo · 53 weeks ago
Helana · 53 weeks ago
Elias Migongo · 53 weeks ago
Eric january · 53 weeks ago
Elias Migongo · 53 weeks ago
Gcheyo · 53 weeks ago
Elias Migongo · 53 weeks ago