MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

SHUKURU KWA KILA JAMBO


Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu...... 

Moja ya kitu muhimu na kinachohitajika sana angalau kwa Kila mtu ni Kushukuru.Nimekuja gundua kwamba asilimia kubwa ya waamini katika dini yeyote ile ulimwenguni, wamekuwa wanatumia muda mrefu sana kumuomba Mungu vitu ambavyo hawana, kuliko kushukuru kwa yale ametenda. Wengi wamekuwa wakilaumu na kulalama kwa vitu wanavyo tamani kuwanavyo lakini hawajavipata bado. Ndugu msomaji kunakitu natamani ukijue kwamba "kushukuru ni kuomba tena". Kumbe unaposhukuru unatengeneza mazingira ya kuomba tena. Waingereza wanasema "Is a polite expression used when acknowledging a gift, service, complement, accepting or refusing an offer" Yaani, Ni usemi wa heshima unaotumiwa wakati wa kukiri zawadi, huduma, inayosaidia, kukubali au kukataa ofa. Hii maana ina maana sana. Kwani, inaonyesha kushukuru kwa kila jambo iwe ni kibaya au ni kizuri kimetokea yakupasa kushukuru.

 Nakumbuka siku moja nilienda saluni nilipofika hapo nilikuta kunawatoto wawili nikaanza kuzungumza nao. watoto wale mmoja alikuwa darasa la pili na mwingine alikuwa darasa la tatu, nikaanza kuwauliza maswali kila mmoja kwa darasa lake. Kwa kweli watoto wale niliwapenda bure kwa namna ambavyo walikuwa na uwezo mkubwa sana na walijibu maswali mengi kwa ufasaha, walinifurahisha sana na bahati nzuri nilikuwa nimetembea na pipi, nikaamua kuwapa zawadi ya pipi kila mmoja walifurahi sana kwa zawadi ile, lakini kitu cha kipekee sana yule mtoto wa darasa la pili aliongea maneno ambayo yalinifurahisha na yalinifanya nijiulize sana, alishukuru na kusema "Ahsante nashukuru, Mungu akubariki" wakati yule wa darasa la tatu alifurahi na kuanza kuchekelea tu pipi. Kitendo kile kilinifanya nimpatie tena 200/= akashukuru tena. Nikagundua amefundishwa akafundishika, huku yule mwingine akaanza kuomba nimpe na yeye 200/= na hakujiuliza kwanini niliwapa pipi wote, lakini yule mwingine nilimpa tena 200/= aliendelea kuomba pasipo kutambua siri hiyo na sikumpa lakini nilimuelekeza nikamwambia akifanyia kazi wakati mwingine nitampa.

 Umeona hapo eeh! Kumbe ni kweli ukishukuru unakuwa umeomba tena bilashaka utapata tena zaidi ya mwanzo si umemuona yule kijana? Unaikumbuka wale wakoma kumi walioponywa ugonjwa huo na Bwana Yesu, pengine unaweza usiifahamu lakini Yesu aliwaponya wakoma 10 na kati yao mmoja tu alirudi kushukuru, kitu hiki kilimshangaza sana Yesu na akamuuliza  akisema, Hawakutakaswa wote kumi? Wale kenda wa wapi? Je! Hawakuonekana waliorudi kumpa Mungu utukufu ila mgeni huyu? Akamwambia, Inuka, enenda zako, imani yako imekuokoa. Kumbe kushukuru ni muhimu sana na tunaona huyu aliyerudi kushukuru alipata bonasi na wale wengine sijui kiliwapata nini.

Wakati mwingine Saikolojia imeripoti kuwa shukurani ni moja ya njia inayopunguza msongo wa mawazo. Hoja hii naungana nayo na mara nyingi nimekuwa nikiitumia na kunawakati nikihisi mambo hayaendi vyema, nashukuru kwa yale madogo ambayo nimeyapata hii inanipa kusonga mbele tena. Hata wewe leo hii unapohisi kukata tamaa, msongo wa mawazo, kushindwa kuendelea mbele, badala ya kulaumu na kulalamika pengine hata kukata tamaa amua kushukuru kwa vitu vidogovidogo  ambavyo umevipata, ukiona huna kabisa basi shukuru hata kwa uzima ulio nao, afya ulio nayo na mengine kibao. Ukifanya hivyo utaona mwenyewe kuwa huna msongo wa mawazo tena. 

Pamoja na hayo unaweza kupita katika nyakati tofauti tofauti kwenye maisha yawezakuwa ni nzuri au mbaya, kwa vyovyote vile jambo lolote kuja kwako linakuwa na sababu ambayo Mungu ameikusudia kwako, yaweza kuwa ni jambo zuri au baya Shukuru. Ndiyo maana nimeanza na mstari huu "Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu kristo".

kumbe hata kwa yale mabaya tusiyalalamikie na kulaumu sana kikubwa tukubali kujifunza kwa hayo, kwa sababu siku zote jambo lolote linapokukuta linakuwa na ujumbe maalumu kwaajili yako. Hivyo badala ya kulaumu na kulalamika tafuta kujua sababu ni nini Kisha pata ujumbe na uufanyie kazi naamini itakufaa sana.

Hebu angalia mstari huu pia "Siku ya kufanikiwa ufurahi, Na siku ya mabaya ufikiri. Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili, ili mwanadamu asipate kulijua neno lo lote litakalofuata baada yake". Haya ni maandiko matakatifu ya Mungu yanatuasa kuwa hata mabaya yanapo tukuta tujifunze kwayo badala ya kulaumu kila wakati. Jambo muhimu la kufahamu ni kwamba Kila changamoto unayokumbana nayo inaujumbe kwaajili yako na unahitajika kujifunza kutoka kwayo, ukishindwa kufanya hivyo utateseka na changamoto hiyo hiyo miaka nenda miaka rudi. Chukua hii itakusaidia na ninaamini itabidili mtazamo wako. 

Nimalize kwa kusema kwamba, ukipewa kitu shukuru, ukinyimwa shukuru, ukifaulu shukuru, ukishindwa shukuru, ukisaidiwa kitu pia shukuru. Hii ni muhimu sana ingawaje kunawatu hawajui umuhimu wake na bado wanachangamoto katika eneo hili. 

Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

LinkedIn>>Migongoe. 

Pinterest>>eliasmigongo.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe. 

Comments (12)

Loading... Logging you in...
  • Logged in as
Gwimevir Tesha's avatar

Gwimevir Tesha · 98 weeks ago

Hakika ni jambo jema kushukuru. Asante sana nimejifuza, Mungu Akubariki.
1 reply · active 98 weeks ago
Amen amen barikiwa pia Gwimevir Tesha.
Ubarikiwe mwalimu.
1 reply · active 95 weeks ago
Elias Migongo's avatar

Elias Migongo · 95 weeks ago

shukrani sana chyo
Joga heke's avatar

Joga heke · 55 weeks ago

Shukranii🙏🙏
1 reply · active 55 weeks ago
Thanks
Ubarikiwe mwl.
1 reply · active 55 weeks ago
Amen amen
MAIDA JAMES's avatar

MAIDA JAMES · 55 weeks ago

God bless you
1 reply · active 55 weeks ago
Amen amen and I hold the same to you
Ameni Barikiwa sana mtumishi
1 reply · active 55 weeks ago
Elias Migongo's avatar

Elias Migongo · 55 weeks ago

Amen amen rafiki

Post a new comment

Comments by

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.