HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31 Ilipoishia………. Elvine alipoteza amani kuliko hata mkewe maana kila alipomtazama mkewe basi moyo wake ni kama ulikuwa unachomwa na mwiba uliojishikiza huko kwenye mishipa ya moyo. Nafsi yake ilitaabika na ndipo alipoamua kutafuta muda mzuri, baada ya chakula cha jioni, azungumze na mkewe, maana ule ukimya wa siku mbili ulikuwa adhabu kubwa sana kwake. Kusoma sehemu ya 30 bonyeza hapa Sasa inaendelea………. Elimina mamy naomba kujua kwanini hutaki kuniuliza kuhusu sababu ya haya yote? Maana najua unajua kuwa kuna mahali mimi nilikosea, sasa unapokaa kimya hivyo… kiukweli unazidi kunichanganya maana ni kama hutaki kujua, sasa unadhani mimi roho yangu itatulia kweli?. Hata kama ungekuwa wewe lazima usingepata amani, ungekuwa hata unawaza hivi nakuwaziaje, nakuonaje na ninajisikiaje ninapokuona, sasa kwanini wewe umekaa kimya, sema neno tafadhali? (Elvine alikuwa akiongea bila kumtazama mkewe usoni maana moyo wake haukuwa katika hali ya utulivu). Pamoja na ...

FAIDA ZA KUSIKILIZA KWA MAKINI.

HIZI NDIZO, FAIDA ZA KUSIKILIZA KWA MAKINI.

Moja ya ujuzi muhimu sana ambao kila mtu ningependa awe nao katika nyakati hizi ni commmunication skill. Huu ni uwezo wa kuwasilisha ujumbe na mawazo yako mbele ya watu, na watu wakakuelewa. Na, hii inaweza kufanyika kwa kutumia maandishi (writing skill), kuzungumza (speaking skill), kusikiliza kwa makini (listening skill) n.k.

Juzi kama hizi ni muhimu sana kwa kila mtu. Kwani, zitaongeza thamani na uhusiano wako na watu wengine. Leo tunaenda kuutazama ujuzi mmoja utakao ongeza thamani na mahusiano yako na watu wanao kuzunguka. Na ujuzi huu ni ujuzi wa kusikiliza kwa makini yaani, active listening skill. Ukweli ni kwamba, kumekuwepo na wimbi kubwa sana la watu  kutaka kuongea tu na kusilizwa  muda wote. Pasipo wao kuwasiliza watu wengine .

Kuna namna saikolojia inaeleza kuwa mtu anaposikilizwa kwa makini hasa anapojielezea na kueleza mambo yake ya moyoni, huwa anajisikia vizuri sana kupata burudiko la moyo. Hali hii, humfanya ajione mwenye kuthaminiwa na kupendwa kweli kwel. 

Katika hili, changamoto bado ni kubwa sana. Kwani, watu wengi bado hawajajua kusikiliza ingawaje wapo vizuri kwenye kuongea. Kitu hiki ni kidogo sana. Lakini,  usipojifunza kusikiliza kwa makini na kuepuka kuwaingilia wengine katika mazungumzo  utashusha brand yako rafiki. Na, hapa nikafikiria na kuona kuwa watu wengi wanafanya hivyo pengine, ilikuwafurahisha wasikilizaji, ilikuonekana kuwa wanajua vitu vingi sana pamoja na hayo pengingine hawajajua umuhimu na faida ya kusikiliza kwa makini. Nipo hapa, naenda kukupa faida kabambe za kuwa msikilizaji mzuri, ambazo ni;

Faida ya kwanza:

Utaokoa muda na kuelewa haraka.

 Usipokuwa msikilizaji mzuri uwe na uhakika wa kupoteza muda mwingi sana katika mazungumzo yako na watu wengine na kushindwa kuelewa haraka kile kilicho kusudiwa.  Kitu hiki hutokea sana pale munapokuwa watu  wengi kidogo mada ikiwekwa mezani utashangaa kuona kila mtu akizungumza bila utaratibu wowote yaani, inakuwa kelele badala ya maongezi. Na, mbaya zaidi si kwamba anaongea vitu vya kueleweka no, ni vile tu anataka kuonekana kuwa anazungumza. Kitu hiki utajikuta mmepoteza muda mwingi sana. Je unataka kusikilizwa? Basi wasikilize wengine kwanza. Hapa si kwamba tu mtaokoa muda bali mtaelewana mapema pia.  

Faida ya pili.

Utajenga heshima na uaminifu. 

Tambua kwamba, watu wana vitu vingi sana ndani ya mioyo yao. Sema hawana watu wa kuwaeleza watu wenyewe ndo hao wanataka kuongea muda wote. Kama ni kiongozi atataka aongee muda wote, kama ni baba atataka aongee muda wote, kama ni mfanya biashara atataka aongee muda wote, kama ni mke atataka aongee muda wote tena ana taka asikiliwe kwa makini hali na huku hataki kabisa kuwasikiliza wengine. Kitu hiki kitapunguza imani na heshima kwa anaye eleza haja zake. Watu hujisikia amani na kuhisi wapo sehemu salama pale wanapo pata watu wa kuwasikiliza. Hivyo chagua kuwa msikilizaji mzuri watu watakuheshimu na kukuamini pia.

Faida ya tatu.

Utapata nafasi ya kujifunza zaidi. 

Kuna msemo mmoja naupenda sana ambao unasema “when you talk you’re only repeating what you’re already know. But, when you listen you’re giving yourself a chance to learn something new” yaani, ukiwa unaongea unakuwa unarudia tu kile ambacho tayari unakifahamu. Lakini, ukisikiliza unajipa nafasi ya kujifunza kitu kipya.

Hivi ulishawahi kukutana na mtu unamweleza inshu yako lakini, huku anaitikia na kusema tupo sawasawa, hali huku unamuona kabisa anachati na kucheka cheka na status tu? Ukimaliza kuzungumza anakuuliza umesemaje kweli?  Binafsi nimeona wengi sana, ndipo nilipogundua kuwa kunashida mahali. Utakuta mtu amekuita na kukusubirisha huku akipigiwa simu  anapokea na kuanza kuongea na kucheka bila hata kutaka radhi. 

By the way utakuwa umebeba mambo mengi kwa wakati mmoja niseme tu kwamba kujifunza na kuelewa kwako kutakuwa ni kugumu sana. Na, matokeo yake utakuwa umetoka hola. Usiwe kama watu wengine wape watu masikio yako wanavitu vingi vya kukufundisha lakini kuwa makini kuchambua yakufaayo. Wakati wa kusikiliza sikiliza wakati wa kuchati chati kweli kweli na utajifunza mengi.

Faida ya nne:

Utaondoa mitazamo hasi juu ya wengine.

Kuna watu ni wazuri sana wa kuhukumu watu wengine. Hapo akiona au kuhisi kitu fulani tu kuhusu mtu fulani utasikia anahukumu hata kwa vitu ambavyo siyo kweli. Kuna watu kwa kuwatazama tu watu fulani fulani hivi, wamewaita wezi, wamewaita makahaba, wamewaita wachoyo, wamewaita masikini, wamevumisha kila uvumi, mtaani. Ndugu, kutokana na uwezo wa kusikiliza kwa makini  utakuja kushangaa kama ukikaa chini na kuwasikiliza watu utakuta wana mambo makubwa sana nyuma ya pazia. Hivyo jitahidi kuwasikiliza watu kwa makini na achana na habari za kuwahukuma na ukuwapa mitazamo hasi wengine wewe siyo Mungu.

Faida ya tano.

Kuboresha mahusiano yako na watu wengine.

Kama utakuwa msikilizaji mzuri utajikuta, watu wanakuamini, wanakuheshimu, wana kuthamini, utawaelewa haraka na hii italeta ushirikiano hasa katika kubeba changamoto zilizojitokeza kwa mzungumzaji. Kitu hiki peke yake tu kitaongeza sana uhusiano wako na watu wengine  hivyo jitahidi kuwa msikilizaji mzuri watu watakuamini, kukuheshimu na kukuthamini na hapo ndipo mahusiano yako na wengine yatakaa poa.

 

Mwisho kabisa tuelewe kuwa, kusiliza kwa makini ni ujuzi ambao angalau kila mtu na shauri ajifunze. Na hapa utafahamu sababu ya mtu kuwa na masikio mawili na mudomo mmoja ni kwamba anatakiwa kusikiliza mara mbili ya anavyoongea. Ingekuwa ni kwa kimombo ningesema the reason why we’ve two ears na one mouth is that we can listen twice as much as we can speak. Hapa ninasema wasikilize watu, acha kuchati wakati wa mazungumzo, usiingilie mazungumzo ya mtu subiri amalize kwanza kama unacha kuongezea au kuuliza, kupinga. Na wewe usikubali mtu akuingilie unapo zungumza. Lakini, sharti ni kwamba, lazima na wewe usiwaingilie kwanza wengine. Unataka watu wakusikilize? Wasikilize wewe kwanza. Unataka watu wasikuingilie kwenye mazungumzo usiwaingilie wewe kwanza. sikiliza kwa makini. Si unajua what goes arround comes around eeh?  

Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

Facebook page>>Add Value Network.

LinkedIn>>Migongoe. 

Pinterest>>eliasmigongo.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe. 


Popular posts from this blog

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31