HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31
.jpeg)
NJIA TATU ZA KUKUSAIDIA KUISHI KWENYE
DUNIA YA WATU WA BAYA.
Siku moja nilikutana na mtu mmoja, nikawa naongea nae mawili matatu kuhusu maisha kwa ujumla. Katika mazungumzo yetu ambayo yalikuwa moto sana. Kwani, mada hiyo ilikuwa nzuri haswa.
Lakini katika mazungumzo yale, niligundua kuwa, jamaa alikuwa
anayalalamikia sana maisha. Akidai kuwa vyuma vimekaza, maisha magumu, maovu yamezidi,
watu, siyo waaminifu, watu ni wabaya sana na malalamiko mengine kibao. Siwezi kuandia
yote hapa lakini mazungumzo yaliendelea na yalikuwa mazuri sana.
Kuna baadhi ya mambo sikukubaliana kabisa na huyo mtu. Lakini,
mengine niliunga hoja mkono. Na moja wapo ni kwamba tunaishi kwenye dunia
ambayo ipo kasi sana, imejaa maovu
mengi, ina wetu wema na wabaya n.k. katika huuhuu ulimwengu wa maasi na maovu
mengi, ndimo humo humo watu wema wanapatikana, humo humo na wewe unaishi, hata
mimi halikadharika naishi humu duniani ambamo hata wewe unaishi.
Mara nyingi tumeambiwa
tujitenge na watu wabaya, watu hasi yaani ambao hawanafaida kwetu. Ni kweli sikatai,
lakini jambo hili ni gumu kidogo. Sababu tunaishi kwa dunia ambayo kila siku tunakutana
na watu ambao tunaweza kuwafahamu ama laah! Na hao wanawezakuwa wema au wabaya,
waaminifu au wasaliti, waongo au wakweli. Ni ngumu kuwatambua moja kwa moja
kwani, wengi wao huvaa ngozi za kondoo kumbe ni mbwa mwitu. Kiufupi tunaishi
kwenye dunia ambayo, watu wengi tulioambiwa ni wema, kwakweli wengi wao si wema
ni wabaya kabisa. Watu wengi tulioambiwa ni wabaya kwakweli wengi wao si wabaya
ni wema sana.
Kwa vyovyote vile hawa watu tunaishi nao hapahapa duniani, na
wakati mwingine watu hao hao Mungu huwatumia kutubarikia, na shetani harikadhalika huwatumia kuwatesa watu
wengine. Sasa tukisema tujitenge na watu hawa itakuwa ngumu, vinginevyo itabidi
kutengeneza katika kadunia kengine tofauti na hii dunia. Ndiyo maana biblia
inasema, mimi siombi kwamba uwatoe
katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu” (yohana17:15).
Sasa kama hatuwezi kuwakwepa hawa watu ni muhimu sana tukajifunza namna
gani tukaishi nao katika dunia hii. Soma njia hizi tatu zitakusaidia sana.
NJIA YA KWANZA: JAA MAARIFA SAHIHI.
Karne hii tunaishi kwenye ulimwengu wa taarifa yaani, information
age. Ambao ni tofauti kabisa na zama zilizo pita, zama kama za kutumia nguvu,
ambapo watu wenye nguvu ndiyo walichukua nafasi na kuwa watu wakubwa. Lakini sasa,
watu walio na wengi wa maarifa na taarifa katika eneo fulani ndio huwa watawala
na wakuu katika eneo hilo. Hivyo hata wewe ukitaka ushinde katika ulimwengu huu
yakupasa uwe mtu wa taarifa na maarifa . maarifa safi na sahihi hapo ndipo
utakapo jua kutofautisha x na +. Kiufupi ndugu unahiitaji maarifa sahihi kuhusu
roho yako, maarifa sahihi kuhusu afya yako, maarifa sahihi kuhusu akili yako, maarifa
sahihi kuhusu kuhusu uchumi wako, maarifa sahihi kuhusu maendeleo yako n.k vinginevyo
utakwenda na maji.
NJIA YA PILI: KUWA WEWE.
Kwasababu ya mfumko wa wingi wa maarifa katika karne hii, watu
wengi wamekuwa wakiishi maisha ya kuiga kutoka kwa watu wengine, pengine kwa
kuwaona mtandaoni au kukutana nao
pengine kutokana na umaarufu wao, watu wengi huacha uhalisia wao na kuishi
maisha ya waengine. Hapo ndipo utakuta ameona watu wanaiba na yeye anaanza
kuiba, anaona watu wana danganya anaanza kudanganya, ameona watu wanaishi
maisha fulani anataka na yeye aishi maisha yale. Ukiwa mtu wa namna hii ndugu
kwa dunia hii, ni kuambie tu kwamba utakwenda na maji.
NJIA YA TATU: WASIFIE KWA MAZURI YAO.
Pamoja na kwamba tunaishi na watu wabaya (Negative people),
utakuja gundua watu hawa si wabaya kwa 100%, kwa namna moja au nyingine kuna
mazuri mengi sana wanayo. Tena, tukiyafahamu yanaweza kuwa ni msaada na faida
kwa maisha yetu. Si unajua dunia ni duara! Utakuja shangaa uliye mkataa na
kumkimbia ndo huyo huyo ukakutana naye kwenye shida zako. Halafu kitu hii,
inashangaza usiombe kukutana nayo. Hapa nacho taka kukazia ni kwamba, usiwe
mwepesi wa hukumu watu kwa makosa yao ya zamani au ya sasa, usikariri watu hubadilika, na kuwa tufauti
kabisa na vile unawafahamu.
Badala ya kujitenga na kuwakimbia watu wabaya wakati mwingine
jifunze kuuona uzuri wao na kuufunua kwao na pengine wanafanya mabaya hayo kwa
kuwa hawajui kuwa wao ni watu muhimu sana kwenye familia, jamii, nchi na dunia
kwa ujumla. Wasifie kwa mazuri yao pengine watajitambua na kubadilika kabisa,
binafsi njia hii nimeitumia sana na wengi wamebadilishwa na njia hii, kwa kujua
nafasi yao, nini wamebeba na wanaweza kuleta matokeo gani kama watautumia uwezo
wao.
Ndugu, kwa namna yeyote ile yaani, utake usitake utakutana na
watu wazuri kwa wabaya, waongo kwa wakweli, waaminifu kwa wasaliti. Hivyo usipo
kuwa na maarifa sahihi, kujitambua na kuwa wewe wakati mwingine kutambua umuhimu
wa watu unao kutana nao itakuwa ni changamoto sana kuishi katika dunia hii. Lakini,
kama utatumia njia walau hata moja tu hapo juu utakuwa ni mtu wa tofauti sana.
Lakini ifahamike kuwa kwakuwa
tumeona kuwa kujitenga na watu wabaya ni ngumu. Hii isiwe ni tiketi ya kung’ang’a
nia watu ambao hawana tija katika maisha yako, hivyo ni muhimu kutambua wewe ni
nani umebeba nini, watu gani wa kuambatana nao na wapi siyo. Katika hili watu wabaya kujitenga nao ni ngumu
lakini sikushauri uambatane nao. Si unajua kuna kujitenga na kuambatana eeh.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.