HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31 Ilipoishia………. Elvine alipoteza amani kuliko hata mkewe maana kila alipomtazama mkewe basi moyo wake ni kama ulikuwa unachomwa na mwiba uliojishikiza huko kwenye mishipa ya moyo. Nafsi yake ilitaabika na ndipo alipoamua kutafuta muda mzuri, baada ya chakula cha jioni, azungumze na mkewe, maana ule ukimya wa siku mbili ulikuwa adhabu kubwa sana kwake. Kusoma sehemu ya 30 bonyeza hapa Sasa inaendelea………. Elimina mamy naomba kujua kwanini hutaki kuniuliza kuhusu sababu ya haya yote? Maana najua unajua kuwa kuna mahali mimi nilikosea, sasa unapokaa kimya hivyo… kiukweli unazidi kunichanganya maana ni kama hutaki kujua, sasa unadhani mimi roho yangu itatulia kweli?. Hata kama ungekuwa wewe lazima usingepata amani, ungekuwa hata unawaza hivi nakuwaziaje, nakuonaje na ninajisikiaje ninapokuona, sasa kwanini wewe umekaa kimya, sema neno tafadhali? (Elvine alikuwa akiongea bila kumtazama mkewe usoni maana moyo wake haukuwa katika hali ya utulivu). Pamoja na ...

SIFA MUHIMU ZA MAAMUZI UNAYOPASWA KUWA NAYO.

 

SIFA MUHIMU ZA MAAMUZI UNAYOPASWA KUWA NAYO.

Moja ya kitu muhimu sana kwenye maisha ya kila mtu ni kufanya maamuzi. Hii ni sehemu muhimu sana katika kila eneo la maisha ya mtu kama anataka kufika mbali.

 kama unataka kuwa na afya njema lazima ufanye maamuzi, kama unataka kuwa na familia bora itakuhitaji ufanye maamuzi, kama unatamani kuwa tajiri lazima ufanye maamuzi, kama unatamani kuwa mtu fulani lazima ufanye maamuzi. 

Maamuzi, mamuzi, maamuzi! Kitu hiki kinahitajika sana kwa kila mtu anayetaka kufika mbali na kuwa mtu wa kugusa maisha ya watu duniani. Ndiyo maana maandiko matakatifu yana sema “ Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza  na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? ” soma luka14:28. 

Hili ni swali biblia inauliza ya kuwa nani kati yetu ambaye akitaka kujenga mnara asipigie gharama yake ili kufahamu kuwa anavyo vya kuumaliza au laah?  Na, mwandishi bila shaka akijua kuwa hayupo mtu wa aina hiyo, na kama yupo awe na uhakika kuwa hatatoboa wala kufika mbali. Haya nayo ni maamuzi.

Kwa ufupi maamuzi ni uchaguzi wa mwisho anaochukua mtu katika kutatua changamoto zilizojitokeza. 

Hapa ni sawa na kusema katika kila tatizo linapotokea kwa mtu yeyote huwa kuna chaguzi nyingi sana mtu anaweza kufanya ili kulikabili tatizo hilo na uamuzi huo unaweza kuwa ni mzuri au ni mbaya. Mfano mtu anaweza kuwa na changamoto ya fedha ya mavazi. 

Chaguzi ambazo mtu anaweza kuchukua ni, kwenda kukopa, kwenda kuiba, kwenda kuomba, kwenda kuiba  au kwenda kufanya kazi ili apate fedha. Mtu mmoja anaweza kuamua kwenda kuiba. 

Hapa, bila shaka atakuwa amechagua chaguo baya. Mwingine anaweza kuamua kwenda kufanya kazi iliapate fedha ya kununulia mavazi, huyu atakuwa amechagua fungu jema. Kumbe, maamuzi yanaweza kuwa mazuri au mabaya. 

Ndugu yangu maamuzi ni daraja kati ya kushindwa na kufanikiwa ingekuwa naongea kingereza ningesema “Decision making is the bridge between failure and success”

Huu, ni mwanzo na msingi wa mafanikio yeyote katika maisha ya kila mtu. Ninachotaka uelewe ni kwamba maamuzi yako, ni matokeo yako ya kesho. 

Ukiamua vyema utapata mema, ukiamua vibaya utapata mabaya. Kwanini usiamue vyema upate mema?

Kwa kuwa tumeona jinsi ilivyo vyema katika kufanya maamuzi kwenye maisha ya mtu husika. 

Vinginevyo mtu atakuwa na matarajio makubwa sana lakini, katika uhalisia anakuwa amebaki vile vile. 

Hii pengine si kwamba hakuchukua maamuzi lakini, alifanya maamuzi bila kuzingatia sifa na vigezo vya maamuzi. Hapa nimekuandalia sifa kuu tano za maamuzi yatakayo leta matokeo chanya kwenye maisha yetu nazo ni;

Sifa namba moja.

Maamuzi yawe yanaeleweka (Specific).

Kama tulivyoona maamzi ni daraja kati ya pande mbili, yaani, ni uchaguzi na mtu inampasa achague kitu kimoja tu kati ya chaguzi nyingi. Hivyo, maamuzi pia lazima yawe yanaeleweka kama ni ndiyo iwe ndiyo kweli kama ni hapana iwe ni hapana kweli kweli. Hapa maamuzi yanapaswa kuambatana na malengo au ndoto yako  yaani, uwe na lengo linaloeleweka moja kwa moja.

Sifa namba mbili.

Maamuzi yawe yanapimika (measurable).

 Maamuzi yanayomfikisha mtu mbali ni lazima yawe yanapimika, kwa maana ya kiasi, kiwango, urefu, au ukubwa fulani.

 Mfano mtu anaweza kuamua kuwa kiwango cha ubilionea katika maisha yake kwa baada ya muda fulani, hapa ilituyapime  ni kuangalia kiwango chake cha pesa kilichopo. Hivyo hata wewe unapofanya maamuzi ni lazima ujiulize nitayapima vipi haya maamuzi.

Sifa namba tatu.

Maamuzi yawe yanafikika. (archiavable).

Watu wengi kutokana na kuwa na matamanio makubwa sana katika kufanikiwa kwao. Mfano unaweza ukakuta mtu ameshauriwa kufanya mazoezi ya viungo labda kamuona mtu anapiga push up. 

500 kwa siku, aua kukimbia 10 km kwa siku. Na akaanza kweli. Kufanikiwa na kwa lengo hili ni ngumu sana kwasababu halifikiki kirahisi. Na, mtu kama huyu utakuta anaishia kupanga na kuweka mikakati tu bila kulifikia lengo hilo.

Sifa namba nne.

Maamuzi yawe halisi (realistic). 

Pamoja na kwamba maamuzi yanatakiwa kufikika lakini pia, yanatakiwa kuwa na uhalisia, mfano mtu anaweza kuwa atafanya kazi kila siku mchana na usiku pengine akaweka muda wa kulala labda saa1 kwa siku muda wote uliobaki ni kazi kazi. Kitu hiki ni kizuri lakini kipo nje na uhalisia hivyo yaweza kuwa akafanikiwa mwanzoni lakini hatafika mbali.

 Au mwingine anaweza amua kuwa bilionea wakati huo hana kitu chochote, lakini akaamua ndani ya wiki moja awetayari ameshakuwa bilionea. Kuwa bilionea ni lengo zuri sana lakini kulifikia kwa wiki moja ni nje na uhalisia. 

Hivyo amua ndani ya uhalisia ili usiwe mtu wa kuamua na kurudi tena katika hali ile ile.

Sifa namba tano.

Maamuzi yawe na muda (time framed).

Likifika suala la kufanya maamuzi muda ni muhimu sana kuhusika. Mfano mtu anaweza kuamua kuoa au kuolewa lakini bila kuweka muda, kulima bila kuweka muda, kufanya biashara bila kuweka muda, kusoma bila kuweka muda kufanya hivi, itaonyesha kuwa kabisa hupo serious. 

Hata kuyafatilia maamuzi ya namna hiyo huwa ni ngumu sana kwani, yanakuwa kama vile una muda wa kutosha. Hivyo, usijichanganye kufanya maamuzi bila kukumbuka kipengele hiki cha muda.

Ukweli ni kwamba unahitaji kufanya maamuzi na kuya fanyia kazi maamuzi hayo ili kufika mahali unapotaka. 

Na kufanya maamuzi siyo kazi kazi ni kutembea katika maamuzi yako. Na hii hutokana na watu kuvunja kanuni na sifa za maamuzi kama tulivyoona hapo juu. Yaani maamuzi ni muhimu yawe ni halisi, kueleweka, muda, fikika na kupimika. Usifanye maamuzi kwa kukurupuka tuliza akili utafanikiwa sana. 

lakini, pia tambua kuwa ni wakati wa kufanya maamuzi hatima ya mtu hutengenezwa.

Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork

Karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

LinkedIn>>Migongoe. 

Pinterest>>eliasmigongo.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe

 


Popular posts from this blog

MAAJABU YA AKIBA

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.