HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31
.jpeg)
UMEPOTELEA WAPI?
Goja nikufikirishe na kukutakafakarisha kwanza nadhani utanielewa vizuri kile nataka nikueleweshe. Hivi, ulishawahi kuona mtu ambaye alikuwa amefanikiwa sana pengine alikuwa tajiri sana katika maeneo yenu? Lakini, saivi ni mtu wa kawaida sana, ulishawahi kuona mtu aliyekuwa mchezaji mkubwa na maarufu sana siku za nyuma, lakini siku hizi ni mtu wa kawaida sana? Vipi kuhusu wakulima wakubwa, wakubwa? Okey, utasema mara ooh! Mimi ni mtu wa mjini shambani tatizo, au basi! Vipi kuhusu wafanya biashara wakubwa? Viongozi wakubwa na wenye ushawishi mkubwa? Vipi wakufunzi na waalimu bomba? Kutaja yote ni ngumu sana.
Lakini, ukiangalia kwa namna ulivyokuwa
unawafahamu watu hawa, walikuwa ni watu wenye mafanikio walau makuwa kila mtu
katika eneo lake. Kitu cha kushangaza ni kwamba, maisha ya watu hawa kwa sasa
ni ya kawaida sana. Pengine wengine walisha geuka na kuwa machokoraa mtaani,
wengine wakabaji, wengine matapeli, wengine omba omba. Yaani, maisha yao
yamechuja kweli kweli. Si kwamba tuna wadadsi lakini, tunataka tuone watu wa
namna hii, pengine kunakitu cha kujifunza kutoka kwao. Swali la
kujiuliza watu hawa Walikwama wapi? na wamepotelea wapi?
Lakini, ukiangalia upande mwingine wa shilingi kuna watu
ambao mimi kama mimi toka nimewafahamu na kwa mafanikio yao wako nayo vilevile
na huku wanazidi kuchanja mbuga kwenda hatua ya mbali sana kwenye maendeleo na mafanikio yao binafsi. Watu wa
namna hii, kuna namna wako vizuri, wanaupiga mwingi na wanastahili pongezi zao. Kwani,
uhalisia jambo hili siyo jepesi kama unavyo dhani. Ingawaje ni rahisi sana kama
utazifahamu na kuzijua siri za kufanya hivyo. Na hapa ninao uhakika kuwa utakapomaliza tu kusoma hapa utafahamu vitu vingi sana na hautabaki kama ulivyo.
Twendelee kutafakari kwanza. Vipi ulisha
wahi kuona au kusikia watu wa aina hii? Wanakuwa na mipango mingi mingi sana na
wanakua wepesi sana wa kuifanyia kazi, na wanaanzisha vitu vingi vingi sana kwa pamoja. Utasikia amefungua mgahawa baada ya mwezi ashafunga, anafungua kibiashara ya duka baada ya wiki mbili ana funga, anaanza kusoma baada ya muda kidogo ashaacha shule,
anaanza kulima baada ya muda kidogo asha piga chini, anapata kazi fulani lakini
baada ya muda kidogo ashaacha, anaanza uandishi baada ya muda anapotea kwenye
ramani, anaanza kufundisha na kufanya uneni baada ya muda anatuacha solemba,
kutaja yote muda hautoshi ndugu yangu. Lakini, sasa nadhani umeanza kupata picha eeh! Lakikini swali la kujiula watu hawa wanapotelea wapi?
Kitu hiki ndicho kimenisukuma kuandika leo hapa ambapo ni uhakika kuwa kunakitu utapata. Kiujumla
hakuna mtu asiye penda kufanikiwa. Na watu karibia wote wanatamani sana
kufanikiwa, na kuwa watu wakubwa, maarufu, wenye heshima na mengine kama hayo.
Ajabu ni kuwa hawa watu hawawi kabisa kama wanavyotaka wao. Hii ni pamoja na
kwamba, watu wengi
wapo tayari kufanikiwa na kuwa watu maarufu, wenye ushawishi, wenye
kugusa maisha ya watu n.k. lakini, watu hao hao hawako tayari kabisa kuufuata
mchakato wa kuwa watu ambao wanataka wawe. Yaani, mtu anatamani tu
aamke asubuhi tayari ameshakuwa mtu heavy ndani ya usiku mmoja. Hivi kitu hiki kinawezakana kweli jamani? Kama ni sawa itakuwa tumerahisishiwa sana lakini kama siyo kweli ni
muhimu kufikiri tena yaani nasema, think again.
Kuna kanuni moja ambayo watu wengi huivunja pindi wanapo
taka kufanikiwa na kuwa watu maarufu
badala yake wanakuwa watu wa kawaida sana. kanuni hii ukiifahamu kwa
kweli ukichanganya na kanuni zingine za mafanikio ambazo umewahi kufundishwa
kutoboa ni swala la muda tu. Na kanuni
hii, itakupa kujulikana na kukutambulisha kwa haraka sana tofauti na
unavyofikiria. Nayo si nyingine bali inaitwa,
Kanuni ya mwendelezo(consistency). Wakati
mwingine inaitwa copound effect. Kanuni hii inamtaka mtu kufanya kitu kilekile
kwa mwendelezo yaani, mara kwa mara bila kuacha. Kitu hiki watu wengi wanakivunja
na kupelekea kuanzisha vitu kwa muda tu kisha kuachana navyo. Hali hii, hupelekea
wawe watu wa kuanzisha vitu vipya kila siku , huku wakiendelea kujitafuta kila siku, na
hawajajipata bado. Pamoja na kuwepo kwa sababu nyingine nyingi za kusababisha watu kutofikia malengo yao na kuanzisha
vitu vingine vipya bila kufanikiwa. Kukosa mwendelezo imekuwa ni moja ya sababu zinazo wakwamisha
watu wengi sana. wakati mwingine kanuni hii, inawataka
watu kufanya vitu kwa muda mrefu bila
kuacha kabla ya kuanza kuonekana.
Goja nikuambie kitu kimoja muhimu hapa nacho ni kwamba, kuanzisha kitu chochote kile, hilo ni jambo la kwanza lakini kukisimamia na kukiendeleza kitu hicho ni jambo lingine tofauti kabisa. Tena wakati mwingine kuanzisha kitu ni jambo jepesi sana lakini, kukiendeleza kitu hicho inahitaji nidhamu ya hali ya juu sana. Vinginevyo itabaki story tu. Utarudi kuwa mtu wa kawaida sana. Sijui kama unaelewa!?
Tafiti zinaonye kwamba, kila kunapo anzishwa vitu au
biashara 100 ndani ya mwaka mmoja biashara ambazo huendelea na kufanikiwa huwa
ni asilimia 5% tu. Huku 95% hufa na kupotea kabisa. Mfano watu 100
wakaanzisha makampuni ya sabuni ndani ya mwaka mmoja zitabaki kampuni 5
tu. Na kampuni 95 hubadilishwa, hufa na kubaki maghofu
tu. Swali kubwa la kujiuliza kwanini watu wengi hukosa mwendelezo na kufanya
vitu kwa muda tu? Au wanakwama wapi? Sasa hapa naenda kukupa sababu kadhaa kwahiyo twende pamoja..
SABABU ZINAZO WAFANYA WATU WENGI WAKOSE
MWENDELEZO NI;
1.
Tabia ya kutaka kufanikiwa ndani ya
usiku mmoja. Kitu hiki watu wengi kimewandanganya baada
ya kudhani kuwa mafanikio ni kitendo cha kufumba na kufumbua tu. Hasa wakiwaona
watu wengine walivyo na biashara kubwa, magari mengi, ushawishi mkubwa wanajua
kuwa hiki kitu walikipata kwa muda mfupi tu. Haili hii, huwapelekea wanakata
tamaa na wanashindwa kuendelea mbele. Wewe usiwe mmoja wao.
2.
Wanataka kuonekana na watu (attention
seekers). Hawa ni watu ambao wao huishi kwa kutegemea sana mawazo
ya wengine na utakuta mtu, anafanya vitu kwa kuangalia watu wengine wanasemaje.
Lengo lake ni kutaka kusifiwa na kuheshimiwa sana. Hivyo, watu kama hawa kuna vitu kama,
kampuni, biashara, na mambo mengine walianzisha ili kusifiwa na watu fulani
fulani hivi lakini, kwa bahati mbaya sana watu walipoacha kuwasifia waliacha
mara moja na kutafuta kitu kingine watakacho sifiwa nacho. Tabia hii,
haitakufikisha popote kwanza inaashiria tu kwamba mtu huyu hajitambui bado.
3.
Kushindwa mara kwa mara huko nyuma.
Hisitoria ya kushindwa yaani, kufeli mara kwa mara huko nyuma watu wengi
huwafanya waweze kuwa na mtazamo hasi, woga kupita kiasi na kukosa ujasiri
wakufanya kitu husika kwa mwendelezo wakijua kuwa napo watafeli tu kama
wativyoshindwa mara kadhaa huko nyuma. Hata hivyo, kuna kitu watu wa aina hii
wanakuwa hawajakifahamu bado ambacho ni kwamba kushindwa wakati mwingine ni
fursa ya kujifunza na kupata uzoefu. Kwani makosa hutupa uzoefu na uzoefu
hutupunguzia makosa. Kuna msemo mmoja wa kingereza naupenda sana ambao unasema failure teachs us the
way by showing us wich isn’t
the way. Yaani, makosa hutufundisha njia sahihi kwa kutuonyesha
ipi siyo njia sahihi. Chukulia makosa kama fursa ya kujifunza na kusonga mbele
vinginevyo utateseka na changamoto hiyo hiyo miaka nenda miaka rudi.
4. Maneno waliyo wahi kuambiwa. Ndugu, moja ya kitu kina nguvu sana ni maneno hasa yanapo pandwa ndani ya moyo wako, haya yanaweza kuchukua mimba na kuzaa kitu kilicho pandwa kama ni chema watoto watakuwa ni wema sana na kama ni kibaya watoto watakuwa ni wabaya kulioko. Watu wengi wamekuwa wakitamkiwa maneno mengi hasi yaani, mabaya sana na watu wao wa karibu, watu kama , waalimu wao, wazazi wao, wenza wao, ndugu zao na majirani zao na maneno haya yamewavunja moyo kabisa kila wakitaka kusonga mbele ya kuendelea tena. Kitu hiki kimewafanya wawe ni watu wa kuanzisha vitu kwa muda na pindi wanapoyakumbuka maneno hayo mabaya waliyo wahi kuambiwa wanashindwa kabisa kuendelea mbele.
Ndugu
yangu kanuni ya mwendelezo ukiivunja, utachelewa sana.
watu utawachanganya na watakuona hueleweki maana kila muda unakuja na jambo hili na
kuliacha lile, kitu hiki pekee kimewacost wengi sana . Ninajua kuna namna
pengine ulikuwa ni mtu wa kughairisha mambo yako ya msingi. Na pengine umekuwa
na mipango mingi sana, ndoto kubwa sana kitu hiki ni kizuri sana lakini hebu
chagua kuanza na kitu kimoja kwanza kisha ukomae nacho hadi kieleweke, tafuta maarifa juu ya
kitu hicho, jifunze kila siku na kifanye mara kwa mara na ikiwezekana
ujitangaze utashangaa watu watakavyokua wanakupigia simu kwaajili ya kitu
hicho yaweza kuwa labda ni uandishi,
kutengeneza sabuni, kulima, utaalamu wa kompyuta, uneni na mengine kede kede. Fanya kwa mwendelezo bila kuacha hata kama hujisikiii wewe
fanya tu. Utashangaa watu tutakavyoaanza kukukuita professional ,
mtaalamu, professor, mkuu, boss, legend n.k. hapo ndipo utakapo kuwa umeanza
kuukaribia ukuu unaoutafuta. Hata kama una mipango na malengo mengi tafuta kitu
kimoja ambacho utaanza nacho kisha fanyia kazi, bila kuacha kisha anza kingine kama
unao huo uwezo.
Labda
nikuulize swali, je unataka kuwa mjasiriamali? Basi inakupasa
ufanye ujasiriamali kwa mwendelezo. Je, unataka kuwa mwandishi bora? Anza kuandika
kwa mwendelezo. Je unataka kuwa muhubiri maarufu? Anza kuhubiri kwa mwendelezo.
Unataka kuwa mwigizaji bora? Igiza kwa mwendelezo. Je unataka kuwa mkulima bora?
Lima kwa mwendelezo. Je unataka kuwa mfanyabiashara bora? Fanya biashara kwa
mwendelezo. Je unataka kuwa mwalimu bora fundisha kwa mwendelezo. Mwendelezo! Mwendelezo!
Mwendelezo! Nasema mwendelezo, hiki kitu
wazungu ndicho wanakiita consisitency. Hapa ndipo watu wengi hukwama na kupotea kabisa. Kama ulikuwa hujui hii,
ni njia nzuri ya kujulikana na maarufu, itumie sasa.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine
namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa
moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO
ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha.
Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu
sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697
/+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu,
niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe