HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 31
.jpeg)
VITU VINNE VINAVYOJENGA TABIA YA
MTU.
Kama utatembea na kuzunguka sehemu mbailimbali katika dunia hii. Upende usipende utakutana na watu.
Hapa nasema hivi, ukienda nyumba fulani utakutana na watu, ukihama mtaa utakutana na watu, ukihama wilaya, mkoa, nchi au bara bila shaka utakutana na watu.
Kwa bahati mbaya au nzuri watu hawa wanakuwa na tabia fulani fulani hivi, ambazo zinaweza kufanana na tabia zako au zikakushangaza kabisa.
Pasipo kuelewa unaweza kulazimisha watu wote wawe na tabia kama zako, na wakati mwingine unaweza kuwa mkali sana pengine hata kuwachukia watu ambao utaona wanatabia mbaya au tofauti na tabia zako.
Ukweli ni kwamba tabia yeyote ile, iwe nzuri au mbaya huwa inajengwa na wakati mwingine huwa inabomolewa.
Pamoja na kuwalaumu watu wengine kwa kuwa na tabia mbaya unapaswa kujua kuna namna tabia hiyo waliijenga.
Cha kushangaza ni kwamba wakati mwingine hata wao hawaelewi waliijengaje tabia hiyo mbaya au nzuri kwao. Lakini jambo la kufahamu ni kuwa tabia ya mtu ni matendo / vitu ambayo mtu amezoea kuyafanya mara kwa mara bila kutumia nguvu kubwa au kulazimishwa katika kuyafanya. wazungu wanasema automatic actions.
Mazoea, mwenendo na desturi hii ya mtu,
hutofautiana kati ya mtu na mtu, jamii na jamii wakati mwingine taifa na taifa.
Pamoja na hayo yote tabia ya mtu inajengwa, inapaliliwa, inakua, na hata kufa.
Leo nataka tuangalie vitu muhimu ambavyo vinahusika katika kujenga tabia ya mtu, yeyote yule.
Vitu hivi vimetajwa na wanasaikolojia, wandishi mabilambali duniani akiwemo mwandishi mtanzania Saidi Kasege.
Nami
sasa nakwenda kukujuza vitu hivyo naamini utapata kitu muhimu
cha kukusaidia hapo baadaye na kuwa daraja la mafanikio yako mwenyewe, familia
yako, jamii yako, taifa na hata dunia kwa ujumla. Vitu hivi ni pamoja na;
1.
MAZINGIRA .
Kuna namna tabia na mienendo ya watu hutofautia kutokana na utofauti wa mazingira ambayo watu hawa wamekulia.
Mfano mtu ambae amezaliwa na kukulia mjini hakika hatafanana na mtu ambaye amezaliwa na kukulia kijijini.
Hii ni kwasababu mazingira huwa yanakasumba ya kulazimisha kitu kuishi kwa kuyafuata mazingira yenyewe.
Ndio maana ukiwa ndani ya bahari mazingira hayo yatakulazimisha tu kuogelea vinginevyo
utazama na kufa. Hivyo kabla hujamhukumu mtu angalia kwanza kuwa ni mazingira
gani amezaliwa, amelelew, au amekulia.
2.
VINASABA (KURITHI).
Kwa asilimia kubwa mtoto hurithi na kuchukua baadhi ya homoni kutoka kwa wazazi wake ambazo hubeba na kuchukua tabia na mienendo yao.
Saikolojia inaonesha kuwa kunatabia na mienendo ambazo mama mjamzito akiwa anazionyesha mara kwa mara, huenda kuathiri mfumo wa mtoto wake moja kwa moja.
Hali hii, hufanya mtoto azaliwe na hizo tabia, mfano hasira kupita kiasi, wivu kupita kiasi, ulevi n.k. inatupasa kuangalia chanzo cha tabia ya mtu kwani kuna wengine huwa wanatabia ya familia, au ukoo ndiyo maana unaweza kukuta familia yote ni vibaka, wezi, wambeya n.k
3.
WATU WALIO MZUNGUKA.
Kwa kuwa tabia ni yale mambo unayoyafanya mara kwa mara bila hata kutumia nguvu kubwa basi hata wale watu ambao tumekuwa tukitumia muda mwingi sana nao wameathiri sana maisha yetu, aidha wameathiri kwa matokeo chanya au hasi.
Kwa vyovyote vile watu ambao unatumia sana muda ukiwa nao hao ndiyo wanaweza kukuathiri pakubwa sana. Ukijiunga na walevu bila shaka na wewe utakuwa mlevi, ukiambatana na wenye heshima na wewe utakuwa wenye heshima, kama umezungukwa na waongo jiandae kuwa muongo.
Katika hili kuna msemo mmoja naupenda nao unasema tabia yako inatokana na watu 5 walio kuzunguka.
Kama umezungukwa na matajiri watano basi wewe ni tajiri wa sita, kadiri unavyotumia muda mwingi na watu wenye tabia fulani, hao ndio watajulisha tabia zako.
Ndiyo maana waswahili
wanasema nionyeshe rafiki zako nikwambie tabia zako.
4.
MALEZI.
Kitu hiki kimeathiri tabia za watu wengi sana kwani, wazazi wamekuwa wakisema na kupandikiza vitu ndani ya watoto wao pasipo hata wao kujua, utakuta mzazi anamwambia mtoto mbwa wewe! Toka utoto hadi anakuwa mtoto anajua yeye ni mbwa matokeo yake anakuwa mdokozi na kufanya tabia kama za mbwa.
Na hapa, tukubali tukatae malezi ya mtoto ndiyo hubeba tabia. Ukweli ni kwamba mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
Ndiyo maana bibilia inasema “mlee mtoto katika njia impasayo Bwana naye hataiacha hata atakapokuwa mzee” soma mithali 22.6.
Malezi ya mtoto hutofautina kutokana na wazazi walio lelewa nao, familia,
waliolelewa, kulelewa na wazazi wote, au mmoja, kulelewa na mleze au wazazi na
kwa namna hiyo, ukitaka watoto wakao wawe na tabia fulani ni muhimu ukawajengea
tabia hizo mwenyewe ili iwe tabia yao.
Pamoja na kwamba tabia yako unaweza kuijenga au kuibomoa ijulikane tu kuwa ingawaje kunavichocheo vingi sana katika kujenga tabia ya mtu fulani, na hata kama ni mbaya hiyo tabia mtu anaweza kuamua kuivunja na kuachana nayo kabisa.
Na njia nzuri ya kuua au kuharibu tabia ni kuibadilisha kutoka chanya kwenda hasi, au kutoka hasi kwenda chanya.
Lakini pia, tukumbuke anayehusika katika kujenga tabia yake ni mtu mwenyewe hivi hapa tajwa hapo juu ni kama visaidizi tu lakini muhusika mkuu ni mtu mwenyewe.
Kwahiyo
maamuzi yapo juu yako wewe mwenyewe.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
Na kama unachangamoto katika hili pengine
namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa
moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS.
Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi, Maendeleo binafsi na Maisha.
Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork.
Karibu
sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697
/+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
Facebook page>> Add Value Network.
Kama umejifunza kitu sema "KUNA MAHALI NAENDA".