HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

ACHA KUJARIBU, ANZA KUFANYA.

 

ACHA KUJARIBU ANZA KUFANYA.

Hivi ulishawahi kuona mtu anauwezo wa kufanya au wa kukusaidia jambo lakini ukimwambia kufanya hivyo utashangaa anakwambia goja nijaribu. Wakati mwingine unakuta mtu anatamani kabisa kufanya au kufanikiwa jambo fulani, lakini utashangaa anakwambia ngoja nijaribu kama nitafanikiwa. Mwingine  akiwa darasani au kwenye kikao swali likiulizwa katika kulijibu utashangaa goja na mimi ni jaribu. Na maneno mengi tu ambayo hayaendi moja kwa moja katika kufanya badala yake watu hujificha katika kivuli cha  kujaribu huku wakijikuta wanashindwa kabisa kufanya.

Wapo watu wenye mipango na mawazo lukuki tena adimu kutokea ambayo kufanikiwa kwayo ni swala la muda tu. Sasa badala ya kuyafanyia kazi utakuta mtu anakwambia sijui kama nitaweza labda ngoja nijaribu. Wengine wanatamani sana kufanikiwa eneo fulani mfano utakuta mwingine anatamani sana kuajiriwa badala ya kutuma maombi anasema ngoja nijaribu kutuma maombi. Penmgine utakuta mtu ameitwa na kwenye usaili lakini utakuta anasema ngoja nikajaribu lakini sijui kama nitapita. Yaani, amejijengea notion fulani ya kujaribu jaribu tu ambayo uhalisia wake siyo nzuri.

Na hapa na kwenda kukuambia kwanini hupaswi kujaribu, kisha tutaona badala ya kujaribu tunapaswa kufanya nini;

1.   KUJARIBU NI SAWA NA KUSHINDWA.

Wazungu wanasema trying implies failure. Ukweli ni kwamba mtu anayejaribu na anayefanya kabisa huwa hawafanani hata katika usiliasi utakuta aliye zamilia kufanya yupo siliasi huku anayejaribu ataonekana kama yuko siliasi lakini mwisho wa siku ataishia tu kujaribu na hataumia kwa kushindwa kwake kwasababu alikuwa anajaribu. Kwahiyo mara nyingi mtu anaye jaribu huwa na uwezekano mkubwa sana wa kushindwa yaani kufeli kuliko yule anayefanya kwa kuzamilia kabisa. Pamoja na kwamba wapo wanaojaribu na kufanikiwa mazima kabisa huku wapo aliozamilia kufanya na wakashindwa pia. Lakini, bado takwimu na chunguzi zinaonyesha kuwa watu walio ingia kwenye biashara, kilimo, ugugaji, uandishi, michezo, utangazaji, ualimu na sehemu zingine kwa lengo la kujaribu wengi wao waliishia kushindwa huku wale waliojitoa kimasomaso kufanya  asilimia kubwa walifanikiwa katika kufanya kwao.

Usikubali kuingia katika biashara, kilimo, ushirika, aua kazi yeyote kwa lengo la kujaribu huku ukitegemea kufanya vizuri zaidi.

2.   TAARIFA HII HUINGIA NDANI YA UBONGO WAKO.

Uhalisia ni kwamba chechote unachokifanya kimetokana na fikra ulizokuwa nazo ndani mwako. Hivyo hata wewe ukiwa na fikra za kujaribu jaribu ubongo wako utapata taarifa hiyo na kupelekea msukumo wa kufanya kile unachokiwaza. Yaani nasema kuwa ukiingia na fikra za kujaribu kufanya kazi, biashara, kusoma, kuajiri/kuajiriwa. Kuoa/kuolewa akili yako itakusukuma na kukwambia kuwa upo katika hali ya kujaribu tu ko hata ukishindwa haina shida. Na kweli unaishia kujaribu tu na wakati mwingine kushindwa kabisa. Kuwa makini asee!

3.   UNAKUWA HUNA UHAKIKA WA KUFANIKIWA.

Kama tunavyofahamu kujaribu ni kama kubahatisha yaani, kupata au kukosa hivyo hata wewe unapojaribu maana yake unakuwa huna uhakika wa kile unafanya ya kwamba utafanikiwa au utafeli, ni kama vile unabeti vile si unajua unaweza kupata au mkeka ukachanika eeh! Hivyo kwa uhakika zaidi achana na kubahatisha badala yake amua kufanya kabisa vinginevyo usifanye tu nakushauri.

NINI CHA KUFANYA?

Marc Reklau  amewahi kusema “Try not. Do or do not. There is no try.” Yaani, usijaribu. Fanya au usifanye. Hakuna kujaribu. Ninachojua ni kwamba kujaribu hakutakupeleka kokote si unajua kwanza unakuwa huna uhakika na kile unafanya. Hivyo badala ya kuwa mtu wa kujaribu jaribu katika kazi zako amua kujitoa kimasomaso kufanya kile unatamani na siyo kujaribu.

Pia uondoe msamiati jaribu kwenye kazi na maneno yako. Ninachotaka ujue ni kwamba usipoteze muda wako kujaribu kwa kana kwamba huna uhakika na kile unafanya katika kazi zako. Kama unafanya fanya kweli kweli na kama hufanyi nalolifahamike kabisa. Vinginevyo kujaribu ni marufuku kama marufuku zingine.

Kabla ya kufanya kazi yeyote au kushirikishwa kitu chochote kaa chini kisha jiulize kuwa unafanya au  haufanyi. Maswala ya kujaribu waachie watu ambao hawana uhakia na maisha yao ambapo wewe siyo mmoja wao. Labda nikuulize rafiki kuwa unataka ufanye biashara? Basi usijaribu nenda kafanye, unataka ufanye kilimo? Nenda kafanye hakuna kujaribu, unataka kuwa dalali nenda kafanye usijaribu asee, unataka kufanya kazi gani? Amua kufanya usilete habari za kujaribu jaribu hapa hapa vinginevyo acha kufanya hiyo kazi. Harafu Kama hujui, wakati unajaribu wenzako wanafanya kabisa.

Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork. Karibu sana ujiongezee thamani yako.

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

LinkedIn>>Migongoe.

Instagram>>migongo_elias.

Pinterest>>eliasmigongo.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.

 

 

 

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.