MAAJABU YA AKIBA

HIKI NDICHO HUJUI KUHUSU KULALAMIKA.
Ndugu msomaji nakusalimu! Bila shaka u mzima na kama sivyo Ikawe heri kwako. Karibu tena ndani ya addvaluenetwork tujifunza kwa pamoja ili kuongeza maarifa yatakayoongeza thamani ya kila mmoja.
Kupitia mtanadano huu utajifunza mengi kuhusu uchumi, saikolojia, maendeleo binafsi, na maisha kwa ujumla.
Kwani, wengi wameripoti kujifunza na kuponywa katika changamoto zao. Hivyo nikukaribishe sana na wewe upate kujifunza pamoja nasi. Uhakika wangu ni kwamba, hutabaki kama ulivyo mara tu baada ya kusoma hapa.
Na kama utaweza mwalike na rafiki yako, na rafiki yako amwalike rafiki yake na yeye amwalike rafiki yake pia ili sote tujifunze.
Sasa leo nataka tujifunza kitu kimoja muhimu sana ambacho utapata kitu cha kusonga nacho. Kitu hiki ni kulalamika.
Watu wengi wamekuwa na kasumba ya kulaumu watu wengine, hasa wanapokutana na ugumu wowote katika maisha yao au pengine mambo yao kutokwenda kama walivyo panga.
Hapo ndipo watatafuta watu wa kuwalaumu mwanzo mwisho, huku wakidai kuwa wao ni chanzo cha kushindwa kwao.
Atalaumu wazazi wake, pengine kwa kutokumsomesha, kumlea au kufariki kwao, atalaumu serikali kwa kutokumwajiri, atalaumu ndugu zake, atalaumu mke/mme wake, atalaumu, watoto wake, atalaumu viongozi, atalaumu rafiki zake na wengine huenda mbali sana kwa kumlaumu hadi Mungu kwa kuzaliwa Nchi aliyozaliwa, kwa kuzaliwa na wazazi aliozaliwa nao, kwa kuwa na hali aliyo nayo kwa sasa. Yaani, atalaumu kila kitu.
Kitu hiki siyo sawa, ndiyo maana leo addvaluenetwork imeamua kukusogezea karibu mada hii ili uongeze maarifa yatakayo ongeza thamani yako.
Nyuma ya kulalamika kuna mambo mengi ambayo pengine unayafahamu au huyafahamu, kuhusu kulalamika ambayo leo ningependa ujifunze kwayo.
Hivyo twende pamoja;
Jambo la kwanza;
Unalaumu mtu ambaye unaamini ana uwezo na mamlaka kuliko wewe.
Kwa kawaida unapolaumu mtu yeyote katika kila gumu unalokutana nalo, maana yake unachukua mamlaka na uwezo wako wa kupambana na gumu hilo unauhamisha na kumpa unayemlalamikia.
By the way huwezi kulaumu huku ukasonga mbele. Hata katika maisha kiujumla, kitu usicho kijua ni kwamba unamamlaka, nguvu na uwezo mkubwa wa kukabiliana na changamoto yako.
Kama utaamua kuwalaumu wengine juu ya tatizo lako, ni sawa na kuuambia ubongo wako kuwa uwezo, nguvu na mamlaka hiyo husitahili kuwa nayo hivyo unachukua na kuhamisha kwa mtu mwingine. Ambaye unamlaumu.
Hebu jiulize kupitia kulaumu changamoto hiyo utaitatua kweli? Kama ni ndiyo endelea kulaumu, vinginevyo acha siasa mara moja tafuta suluhisho ya changamoto yako asee.
Jambo la pili;
Unapolaumu wengine hata fursa ndogo ambazo ungeweza kuzifanya hutaweza kuzifanya kabisa.
Unauwezo mkubwa wa kushughulika na changamoto zako mwenyewe. Na pindi utakapouhamishia uwezo huo kwa mtu mwingine ambaye unamlaumu, ubongo na akili yako itabaki kwenye freezing state ile hali ya kuganda na kushindwa kuchaji ili kufikiria njia mbadala ya kutatua shida yako.
Kwa maana kulalamika hakufanyi usonge mbele isipokuwa utabaki katika hali hiyo hiyo miaka nenda miaka rudi ukilaumu watu.
Mbaya zaidi utashangaa
kuona watu wengine wakikatiza wanafanya jambo kama lako na kufanikiwa huku wewe
umebaki kulaumu tu, vinginevyo labda wakuonee huruma.
Jambo la tatu;
Kulamu wengine hakusaidii kutatua tatizo lako.
Kuna namna watu tunategemeana katika kuendelea kwetu kwenye maisha yetu ya kila siku. Sasa hii sio pointi ya kuwalaumu wengine kuwa, hawajafanya katika kutatua changamoto yako.
Ni kweli lakini tambua kuwa hatutatui magumu yetu kwa kuwalaumu watu badala yake kwa kutafuta shuruhisho la nini kifanyike ili kuimarisha au kutatua changamoto hiyo.
Halafu ngoja nikwambie, katika patternaship yeyote mambo kama hayaendi vyema kabla ya kuwalaumu na kuwarushia mpira wengine hebu jiulize kuwa wewe umechangia kwa kiasi gani kutokea kwa tatizo hilo, kuvunjika kwa mahusiano haya au kuanguka kwa biashara yako.
Baada ya hapo jiulize pia, umejifunza nini? Na utabadilika kwa namna gani ili kuepuka kuteswa na changamoto moja miaka yote?.
Ukisha shughulika na wewe kwanza ndipo unaweza kuangalia na mwenzako yeye kachangia kwa kiasi gani katika hili. Hapo ndipo mtapata muda wa kuyajenga na kuimarisha biashara yenu, ndoa yenu, mahusiano yenu, kazi yenu n.k .
Mara nyingi nimekuja gundua kuwa si
watu tunao walaumu ndiyo chanzo cha kushuka kwetu kama wengi wanavyodhani, bali
tatizo lipo kwetu wenyewe na asilimia
kubwa ya watu tunao walaumu na kuwa lalamikia hatukupaswa kabisa kuwa laumu.
Na kama hujui ukipenda kulalamika kwa kila kitu kwenye maisha yako, utapoteza watu wengi sana kwa sababu watu hawapendi kulaumiwa na mara nyingi hujitahidi kujitenga na walalamikaji.
Ndugu yangu yapo mengi katika hili lakini nachotaka ufahamu ni kwamba maisha yako ni jumkumu lako mwenyewe kwa asilimia mia.
Kulaumu watu hakutasaidia wewe kusonga mbele badala yake utajichelewesha na kupoteza muda tu bure.
Katika hili usitegemee mtu kutoka nchi za mbali ili kujakukufanyia jambo lako, usitegemee mtu atakuja na kukufanyia hiyo biashara yako, hiyo elimu yako, wala hilo jambo ufanyalo badala yake watu watakuja kwako kama daraja tu la wewe kupita na kujifunza kwao jukumu la kuamua na kujifunza kwao kisha kufanya mwenyewe ni lako mwenyewe.
Wakati mwengine wao ni kutoa funzo na ushauri kwako ukiamua kuufuata ni wewe usipoamua ni wewe, si unajua maneno na ushauri mara nyingi huyolewa bure, lakini kuwa makini kuchagua unao faa tu.
ukibakikulaumu na kuwalalamikia watu utabaki kama ulivyo asee. Badilika pambana kwa nafasi yako, jifunze kwa watu, kisha usonge mbele.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya
kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia
mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS
Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi, maendeleo binafsi, na Maisha. Mwanzilishi na
Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork. Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
Facebook page>> Add Value Network
Kama umejifunza kitu, andika "KUNA MAHALI NAENDA".
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Victorine · 86 weeks ago
Elias · 86 weeks ago
Scholastica · 86 weeks ago
Migongo · 86 weeks ago
Ngwaaaa · 86 weeks ago
Migongo · 86 weeks ago
Chy · 86 weeks ago
Migongo · 86 weeks ago
Mhitaji · 86 weeks ago
Elias · 86 weeks ago
Joga heke · 50 weeks ago
Mwl. Kasunzu · 50 weeks ago
Elias Migongo · 49 weeks ago
deusmsafiri · 49 weeks ago
Migongo Elias · 49 weeks ago