HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26.

Image
  HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 26. Ilipoishia.......... Alipomgeuza tu alishangaa kuona sura ya yule binti ni ya mbuzi. Aliogopa na kudondoka chini kwa kelele kuu alilia 'maaamaaaaaaa!!!!" Alijiokotaokota huku akiangukaanguka mpaka kwenye gari yake. Alipanda ndani ya gari na kuwasha gari. Alikimbiza gari mpaka akafika karibu na geti la nyumba ya Elvine, lakini kabla hajafika getini alishangaa kuona anaguswa mabegani ndani ya gari lake. Alitoa macho kwa uoga na mshtuko mkubwa mpaka akakosea njia na kwenda kugonga mti... Kusoma sehemu ya 25 bonyeza hapa. Sasa inaendelea......, Aligonga mti kwa nguvu mpaka naye akajipigiza kichwa kwenye usukani wa gari na gari ikaharibika sana upande wa mbele, alipona kwa neema tu kwa namna gari ilivyokuwa mwendo kasi angeweza hata kupoteza maisha lakini haikuwa hivyo. Alijikaza na kushuka kwenye gari akakimbia kuelekea kwenye nyumba ya Elvine,  njiani alikumbwa na kimbunga cha ajabu sana. Baada ya kile kimbunga kumpitia na kumzingazinga kwa muda

TIBA YA KUKATA TAMAA.

 

  TIBA YA KUKATA TAMAA.

Uhali gani ndugu msomaji! Bila shaka hujambo  na kama si hivyo basi Mungu akusaidie sana . 

Karibu katika mtandao wa addvaluenetwork tujifunze kwa pamoja, ambapo leo tunakwenda kuangali moja kati ya njia muhimu na makini katika kuondosha hali ya kukata tamaa. 

Kipindi cha nyuma nimewahi kuandika makala nzuri sana juu ya KUKATA TAMAA   na makala hiyo umesomwa na watu wengi sana, na huko nilieleza sababu kadhaa zinazowafanya watu wakate tamaa mapema   katika maisha yao. 

Unaweza kuisoma sasa hapahapa addvaluenetwork ili kujifunza mengi.

Lakini pamoja na hayo ngoja  nikwambie maana ya kukata tamaa ambayo ni ile hali ya kukosa tumaini la kuendelea mbele na kuona uwezo wako wa kupambana na changamoto hiyo ni mdogo kuliko tatizo lenyewe. 

Ukweli ni kwamba kila mtu anachangamoto zake ambazo hukutana nazo katika maisha ya kila siku. 

Zipo changamoto za fedha, changamoto za afya, changamoto za mahusiano au ndoa, changamoto binafsi, changamoto za kiroho na nyinginea kibao. 

Kwa vyovyote vile magumu hayo ilimradi unakaa ndani ya dunia ni lazima tu utakutana na changamoto za aina yako. 

Na uzuri wa changamoto hizo haziui watu badala yake huimarisha na kumweka imara mtu mwenyewe

Kumbe ni muhimu kutambua kuwa changamoto zipo kwa lengo la kumjenga, kuimarisha na kumpatia uzoefu mtu husika. 

Kwa maana hiyo usihesabu kuwa ni matatizo, shida na mizigo unayopitia badala yake hesabu kama ni mtaji na faida ya kukuimarisha na kukujenga wewe kwenda viwango na sehemu nyingine ambayo ni bora kuliko ile ya kwanza.

Ingawa magumu na changamoto ni faida na muhimu katika kutuimarisha na kutujenga, lakini kunawatu zimewabomoa na kuwaharibu kabisa. 

Hivyo ni muhimu kufahamu ni kwanini changamoto hizo huwaharibu na  kuwabomoa moja kwa moja. Ambapo wameharibu maana ya changamoto kuja kwake kwao. 

Ukweli ni kwamba kunamagumu mengine huja na mazito, simanzi na misiba pengine hata makubwa kuliko hayo. 

Hayo yote yamewafanya kukosa tumaini na kuona hawawezi kabisa kusonga mbele wala kuendelea tena, hichi kitu ndicho tunakiita KUKATA TAMAA

Na hapa naandika kukupa njia moja makini katika ya njia nyingi ambazo unaweza kuitumia kuachana na kukata tamaa katika kazi ufanyazo. 

Ambapo nimatumaini yangu kwamba utasaidika  kwa namna moja au nyingine.

TIBA MOJA  ITAKAYO KUSAIDIA USIKATE TAMAA.

tambua kwamba hata hili litapita. Tunaishi kwenye dunia ambayo kila kitu kinapita isipokuwa maneno ya Mungu pekee. 

Kwani watu huzaliwa hukua na kisha kufa, majengo mazuri hujengwa na mwisho hubomoka, warembo wazuri nao huzeeka na kupoteza uzuri wao, walikuwepo watu maarufu na mashuhuri duniani kote lakini walipita, walikuwepo waigizaji wazuri sana lakini walipita, walikuwepo wanasiasa bomba lakini baadae walipita, walikuwepo wakulima bomba na makini lakini, sasa hawapo, yalikuweo magonjwa makali na hatari lakini, yalipita, vilikuwepo vimbuga  hatari lakini  vilipita, walikuwepo viongozi makini lakini waliondoka, walikuwepo waandishi wazuri lakini walipita.

 walikuwepo watu wenye shida kubwa na kubwa na hatari kuliko hata yako lakini walishinda.

Ninachotaka nikuambia ni kwamba haijarishi ni ukubwa gani unapitia tambua kuwa hata hilo linapita yaani, changamoto yeyote unayokutana nayo tambua kuwa imetumwa kukuimarisha napo haitakaa milele yaani, ipo kwa kitambo tu. 

Labda nikuulize  swali ndugu yangu ya kuwa je kunachangamoto gani unapitia? Fanya kitu kimoja elewa kwamba hata hilo litapita tu, je unachangamoto ya fedha?  Elewa kwamba hata hilo litapita tu. Je unachangamoto ya ndo? Hilo ni swala  la muda tu. 

Nataka nikuhakikishie kuwa hata kama changamoto hiyo unaiona ni kubwa kwako tambua kwamba siyo kweli changamoto hiyo ni size yako kabisa  pambana nayo.

Ukweli ni kwamba uwapo hapa duniani, utakumbana na dhoruba, changamoto, magumu, kushindwa, na wakati mwingine vinatukatisha tamaa, na kutufanya tuone kutokuendelea mbele tena. 

Na unaweza kushindwa na kukata  tamaa, wakati mwingine tumefundishwa njia nyingi sana za kutokukata tamaa, na nyingine zimetusaidia kwa kiasi na nyingine hazijafanya kabisa. 

Nataka pia utumie njia hii ya kwamba popote utakapo hisi kukata tamaa jiambie kuwa hata hili litapita na pambana huku ukilipa muda tu. 

Changamoto na magumu unayo pitia yanapita tu, hata Bill lucas aliwahi kusema “when you feel that adversary is too much to handle remind youself, that this too shall pass”  yaani, ukihisi kwamba tatizo ni ngumu sana kulikabili jikumbushe kwamba hata hili litapita.

Hivyo hayo yote yatapita lakini pia ni muhimu kufahamu yatapitaje?  Pambana asee na usikubali kukata tamaa kizembe namna hiyo. 

Nimatumaini yangu kuwa umepata kitu na umetiwa nguvu tena na nimaombi yangu Mungu akusaidie upate kuvumilia na kuivuka hivyo changamoto. Yaani changamoto hiyo ipe muda tu.

Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.

na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS.

 Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi, maendeleo binafsi, na Maisha. 

Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork

Karibu sana ujiongezee thamani yako.

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe.

 

 

Popular posts from this blog

GHARAMA 5 ZA KUUFIKIA UKUU UNAOUTAKA.

USIKUBALI KUAJIRIWA KABLA HUJASOMA HAPA.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.