MAAJABU YA AKIBA

TUMIA NJIA HII KUTATUA CHANGAMOTO YAKO.
Hello ndugu msomaji! Ni matumaini yangu kuwa upo salama,
vinginevyo Mungu akusaidie sana upate kuwa sawa. Nikukaribishe tena lkatika andiko
hili tupate kujifunza kwa pamoja ili tuongeze thamani kisha tusonge mbele. Ni wazi kuwa hakuna binadamu asiyepitia
changamoto yeyote katika dunia hii. Kwenye biashara kuna chanagamoto zake,
kwenye ndoa kuna changamoto zake, kwenye kilimo kuna changamoto zake, kwenye
ufugaji kuna changamoto zake, kwenye uvuvi vivyo hivyo, kwenye elimu zipo pia,
na sehemu zingine utakutana nazo sana. changamoto hizo zaweza kuwa; kufeli,
kukata tamaa, maneno hasi, changamoto za afya, mahusiano, kazi, n.k . Yote kwa yote aidha uwe mwema sana au katili
sana utakutana nazo, uwe upole au mkali, uwe mtu maarufu au wa kawaida tu
utakutana nazo, uwe unasali sana au husali utakutana nazo. Na katika hili tambua
kuwa unapomwamini Mungu haimanishi kuwa hautapitia
katika changamoto laahasha, bali hata utakapopitia katika magumu Mungu atakupa
uwezo wa kushinda changamoto hizo.
Na leo kupitia hapahapa kwenye mtandao wetu pendwa wa ADD VALUE NETWORK tumekuletea njia moja mathubuti
utakayo itumia katika kutatua matatizo na changamoto yeyote inayokusibu. Hivyo fuatana
nami mwanzo hadi mwisho ili kujifunza
zaidi;
Njia hiyo ni SELF-COUNSELING yaani, KUJISHAURI MWENYEWE. Hapa namaanisha
kuwa, kuna namna mtu unaweza kujishauri mwenyewe hata
ukafanikiwa kutatua tatizo yako ingawa inategemeana na aina na ukubwa wa tatizo
hilo. Lakini kama utajua nguvu ya mawazo ambayo upo nayo utaweza kutoboa katika
eneo hili. Kwani, kwa kawaida binadamu huwa yanakuja mamilioni ya mawazo ndani yake,
yakizunguka zunguka huku na kule na kama
ataamua kuyafanyia kazi ndani na kuyatekeleza
yanaweza kumvusha kwenda katika hatua anayo itaka. Sasa kupitia nguvu ya
mawazo hayo mtu anaweza kuyatumia vyema ili kutatua matatizo yake.
JINSI YA KUFANYA.
Kama utakutana na changamoto au
tatizo lolote ndani yako jiulize kuwa kama changamoto au tatizo hili lingempata
rafiki yangu na akaja kwangu ili kutaka ushauri je, ningemshauri nini ili
kuondokana na changamoto yake? Hapo ndipo utakapo shangaa
na kuona jinsi utakapo pata wazo lililo bora kupitia mamilioni ya mawazo yanayo
kuja ndani yako yakizunguka zunguka ili yafanyiwe kazi.
Labda nikuulize swali je, unachangamoto ya kujua ni
biashara gani ufanye? Jibu ni rahisi tu, nalo ni kujiuza kuwa je rafiki yangu
ninaye mwamini angekuja na changamoto kama hiii huku anataka mawazo yako
ungemshauri nini? Hilo ndilo jibu fanyia kazi. Je, unachangamoto kuhusu
mahusiano yako? Jibu ni rahisi tu, nalo ni kujiuza kuwa je rafiki yangu ninaye
mwamini angekuja na changamoto kama hiii huku anataka mawazo yako ungemshauri
nini? Hilo ndilo jibu fanyia kazi. Je, unachangamoto ya kukata tamaa mapema? Jibu
ni rahisi tu, nalo ni kujiuza kuwa je rafiki yangu ninaye mwamini angekuja na
changamoto kama hiii huku anataka mawazo yako ungemshauri nini? Hilo ndilo jibu
fanyia kazi. Je, unachangamoto ya kutokuwa na nidhamu
ya fedha na muda? Jibu ni rahisi tu, nalo ni kujiuza kuwa je rafiki yangu ninaye
mwamini angekuja na changamoto kama hiii huku anataka mawazo yako ungemshauri
nini? Hilo ndilo jibu fanyia kazi. Je, unachangamoto gani inakusumbua? Jibu ni rahisi tu, nalo ni kujiuza
kuwa je rafiki yangu ninaye mwamini angekuja na changamoto kama hiii huku anataka
mawazo yako ungemshauri nini? Hilo ndilo jibu fanyia kazi.
Kupitia njia hii ya kujishauri mwenyewe kama itatumika
vyema itakuwa msaada mkubwa sana katika kukabiliana na changamoto mbali mbali
zinazo tukabili katika maisha ya kila siku. Na hapo utakuwa umeanza kuyafaidi
mawazo yako. Usiyadharau mawazo yako hebu
jaribu njia hii itakusaidia sana, jiamini na yakubali mawazo yako na anza kuyafanyia kazi.
Onyo!
kabla ya kuanza kulifanyia kazi wazo lako
lipime kwanza kama ni wazo sahihi au siyo sahihi na kisha lithibitishe kwa
kulifanyia kazi, ukiona limefanya kazi endana nalo na ukiona halijafanya kazi jaribu
tena, likishindikana achana nalo kisha angalia wazo lingine si unajua yapo
mamilioni ya mawazo eeh! Wakati mwingine ukiona mambo yamefika
shingoni tafuta ushauri kwa wataalamu au ktafuta watu unao waamini watakusaidia
katika hilo.
Ni imani yangu kuwa makala hii itakusaidia sana kitu
kikubwa tu ni kwamba usiishie tu kusoma na kupongeza hapa bali soma na litakalo
kupendeza anza kufanyia kazi mara moja. Matokeo utayapata naamini utaipenda.
Rafiki, ni matumaini yangu kuwa umejifunza
kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya
kuondokana na adha hii sasa waweza kuwasiliana na mimi moja kwa moja kupitia
mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii, imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS
Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na Maisha. Mwanzilishi na
Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork. Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Instagram>>migongo_elias.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi
kujifunza pamoja nawe.
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Chg · 86 weeks ago
Elias · 86 weeks ago