MAAJABU YA AKIBA

KWANINI UNAHITAJI PESA?
Tunaishi kwenye dunia ambayo karibia kila kitu kina hitaji pesa. Chakula, maradhi, nguo na mengine kibao.
Kama utaniazima dakika mbili za kusoma hadi mwisho ujumbe huu? Zitakuwa ni dakika 2 za matumizi bora kabisa ya muda kwenye maisha yako.
Huta jutia bundle, muda wala nguza zako.
Mara nyingi watu wakija kupata ushauri kwangu, kuhusu kupata pesa huwa siwajibu Kama walivyouliza.
Wengi wao huuliza hivi, Mwl. nifanyaje ili nipate fedha zangu mwenyewe? Kama nilivyosema swali hili huwa silijibu kama lilivyo kusudiwa na waulizaji.
Nami huwajibu kwa kuwauliza swali; KWANINI UNATAKA PESA? Kwa bahati mbaya sana wengi huwa hawana majibu ya kueleweka ya swali hili.
Wengine huseme ili nitumie tu, ili niinjoy maisha n.k.
Nafahamu kabisa kuwa hata wewe unataka pesa. Ndiyo maana umeajiriwa, unafanya kazi, unakaba roba, unaomba, unalima n.k
moja ya sababu kubwa ya kufanya hivyo ni ili upate pesa. Si ndiyo rafiki!?
Kama ndiyo napenda kukuuliza na wewe leo kuwa; KWANINI UNAHITAJI PESA??
Kama utanijibu itapendeza sana kunijibu kupitia mawasiliano hapo chini, tutajua ni namna gani tunaweza kusaidiana.
Ndugu, kama utakuwa na sababu kubwa ambayo inaeleweka kulijibu swali hili. Hakika itakuwa ni rahisi sana kwako kutafuta, kupata na kutunza pesa utakayo ipata. Kinyume chake ni kweli!
Tafadhali rudi usome tena hapo!
Binadamu wanahitaji pesa kwa sababu kadhaa muhimu, lakini ni muhimu kukumbuka kuwa pesa yenyewe sio lengo kuu.
Hapo ndipo sababu inahitajika kufahamika🎤
Nimefuatilia na kugundua, kwanini watu wengi wanatafuta pesa, na hapa naenda kukueleza sababu hizo si unajua, kwa kila kwanini kina sababu eeh!
Na mwishoni kabisa nitaweka sababu za kwangu ambazo nazitumia.
Soma hadi mwisho utajifunza asee.✍🏽
Sababu ya kwanza.
Kutimiza Mahitaji ya Msingi : Pesa huturuhusu kununua vitu muhimu kama vile chakula, makazi, na nguo. Bila vitu hivi, ni vigumu kuishi na kustawi katika maisha..
Angalia sababu pili Sasa.
Sababu ya pili.
Usalama na Utulivu; kuwa na pesa za kutosha kugharimia matumizi na kuweka akiba kwa dharura hutoa warantii ya usalama. Hupunguza msongo wa mawazo na kukuruhusu kuzingatia mambo mengine ya msingi maishani mwako.
Sababu ya tatu;
Fursa na Uhuru: Pesa hufungua milango ya elimu, huduma za afya, na usafiri. Hukupa udhibiti zaidi juu ya muda wako na uchaguzi, hukuruhusu kufuatia ndoto na mambo unayoyapenda.
Sababu ya nne;
Kujenga Maisha Bora: Pesa inaweza kutumika kuwekeza katika maisha yako ya baadaye, kuanzisha biashara, au kuitunza familia yako. Inakupa uwezo wa kujenga maisha yanayoendana na maadili yako.
Sababu ya tano.
Shiriki katika Jamii:
Unakumbaka michango ya harusi, misiba, hafla na matukio mengine kwenye jamii?🤔
Katika jamii nyingi, pesa zinahitajika ili kushiriki katika shughuli na matukio ya kijamii. Inaweza pia kuwa sababu ya hadhi ya kijamii na kukubalika. Ingawaje uwepo wako pia ni muhimu lakini pesa ina mata ujue.
Hizi ni baadhi ya sababu nilizo zipata kwanini watu wengi wanahitaji pesa?.
lakini ngoja nikushirikishe baadhi ya sababu zangu kama nilivyo kuahidi hapo kabla.
Mimi binafsi nahitaji pesa kwasababu;
1. Sipendi kuomba pesa . Kitu kigumu kinachoniwiaga ugumu kwa watu ni kuomba fedha. Naionaga kitu siyo nzuri.
Hata hivyo nimeshapata njia bora ya kupata pesa kutoka kwao. Kueleza yote ni ngumu, lakini waweza kuwasiliana nami ukajifunza, ikusaidie na wewe.
2. Nahitaji pesa ili kutimiza mipango, ndoto na malengo yangu.
kwenye hili pesa ina nafasi yake.
3. Ili Kujenga makanisa na kusambaza injili.
sasa hizi sababu zangu bhana usihoji sana.
4. Ili kuwasidia wengine.
Hii inanipa nguvu kutoka na ule usemi ninao tembea nao wa kuwa.
"When you get to the peak of your success, don't forget to raise men."
Hizi ni baadhi ya sababu zangu, unaweza kunishirikisha na sababu zako pia.
kwamafundisho Kama haya na mengine zaidi unaweza kubonyeza linki hapo chini ili kujifunza zaidi.
Kunishirikisha na kujifunza zaidi bonyeza hapa.
Lakini pesa sio kila kitu. Kuna mambo mengi ya kuridhisha maishani yenye thamani, kama vile mahusiano mazuri, afya njema, na hisia ya kusudi, kuna baadhi ya vitu pesa haiwezi kuvitatua au kuzuia.
Siri iko katika kupata usawa na kutumia pesa kama zana ya kufikia malengo yako, usiache iwe ndio kitu pekee cha kuzingatia. Rudia kusoma tena.
MIGONGO ELIAS.
Add Value Network.
GeT tO tHe NeXt LeVeL💪
255767653697
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Joga heke · 45 weeks ago
Migongo · 44 weeks ago