MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

AKILI NNE (04) ZA KUKUFAN

 


AKILI NNE (04) ZA KUKUFANIKISHA KATIKA MAISHA YAKO.

Kuwa na akili, hekima na maarifa  ni jambo ambalo kila mtu hulitamani sana.

Kitu hiki ni kizuri sana lakini ni wachache tu hufanikiwa kuwa nalo.
Akili na hekima mara nyingi zimekuwa nyenzo mhimu sana katika kuyaendea mafanikio ya mtu.

Kwa kuwa vitu hivi ni muhimu sana kuwa navyo, hivyo ni muhimu tukajifunze akili nne zitakazo tusaidia kufanikiwa katika maisha yetu.

Goja tujifunze kupitia maandiko haya kwanza;

MITHALI 30:24-28

[24]Kuna viumbe vinne duniani vilivyo vidogo;
Lakini vina akili nyingi sana.

[25]Chungu ni watu wasio na nguvu;
Lakini hujiwekea chakula wakati wa hari.

[26]Wibari ni watu dhaifu;
Lakini hujifanyia nyumba katika miamba.

[27]Nzige hawana mfalme;
Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.

[28]Mjusi hushika kwa mikono yake;
Lakini yumo majumbani mwa wafalme.

Naam, kuna jambo kubwa sana nataka ulifahamu, kwani linaweza kuleta sura mpya katika maisha yako

Soma uelewe.........

Kama umesoma kwa makini hapo juu, utagundua kuwa mwandishi ametaja;

"........Vidogo, lakini vina hekima nyingi:"

Licha ya viumbe hawa, kuwa wadogo wanaonyesha hekima na akili kubwa sana.

Kumbe hapa tunaona  size, umbo sijui ukubwa hauhusiki kabisaa....

Hebu twende tuzame ndani tuwatazame viumbe hawa;

Kiumbe wa kwanza; Mchwa.

Mchwa ni wadogo na hawana nguvu kubwa kila mmoja, lakini wanatajwa kuwa wenye Bidii, Akili na Hekima ya Kujitayarisha kwaajili ya siku zijazo:

Mchwa hukusanya na kuhifadhi chakula wakati wa kiangazi ambapo chakula kinapatikana kwa wingi, kuhakikisha wanacho cha kutosha wakati chakula ni haba. Tabia hii inaonyesha busara, mipango, na bidii.

Hata na wewe nataka ujifunze kwa MCHWA. Upatapo Leo usitumie vyote ikumbuke na kesho .

Fanya maandalizi kwaajili ya kesho yako na hii ni pamoja na kujiimalisha wewe mwenyew kwa kujiongezea maarifa kila mara, kuweka akiba, mipango na utekelezaji. Naamini itakusaidia.

Kama hujanielewa soma tena.✍🏽

Sasa twende tutazame Kiumbe wa pili mwenye akili sana.

KIUMBE WA PILI: PIMBI.

Mwandishi anasema,

"Pimbi ni viumbe wenye nguvu kidogo, lakini wanajenga makao yao kwenye miamba;"

Pimbi, pia hujulikana kama panya wa miamba, sio viumbe wenye nguvu kwakweli.

Lakini huchagua kuishi kati ya miamba, ambayo hutoa ulinzi wa asili dhidi ya wanyama wanaowawinda.

Hii inaonyesha Akili, mikakati na umuhimu wa kuchagua mazingira salama na yenye ulinzi, kutumia rasilimali zilizopo kufidia ukosefu wa nguvu za kimwili.

Goja nimwambie kitu, hebu jifunze kwa huyu pimbi itakusaidia.

KIUMBE WA TATU: NZIGE.

"Nzige hawana mfalme, lakini wanapiga hatua pamoja kwa vikundi;"

Nadhani ulishaona au sikia nzige wanavyo tembeaga makundi makundi...

Nzige ni wadudu binafsi wasio na kiongozi au mfalme wa kuwaongoza.

Licha ya ukosefu wa uongozi kati yao, nzige husafiri kwa makundi yaliyopangwa. Nguvu yao iko katika uwezo wao wa kufanya kazi pamoja kwa maelewano, wakionyesha nguvu ya ushirikiano na hatua za pamoja.

Hii inafundisha thamani ya ushirikiano, mshikamano na kufanya kazi kwa timu.

Yaani namaanisha kuwa kuna mahali hautafika pekee yako utahitaji watu wa kushirikiana nao, kutiana joto, kutiana moyo n.k hata kufikia mipango na ndoto zako kubwa.

KIUMBE WA NNE: MJUSI.

"...... kukamatwa kwa mkono, lakini yupo katika majumba ya wafalme."

Mijusi inaweza kukamatwa kwa urahisi, ikionyesha udhaifu wao.

Licha ya udhaifu huu, mijusi huweza kuishi hata katika sehemu zenye ulinzi mkali, kama vile majumba ya wafalme.

Hii inaonyesha kuwa ustadi wao na uwezo wao wa kubadilika huwafanya waishi vizuri katika mazingira mbalimbali na wakati mwingine magumu.

Inafundisha umuhimu wa kubadilika na uwezo wa kuvumilia hali mbalimbali.

Ndiyo hali mbalimbali,,,,,

Kwa ujumla viumbe  vidogo vinavyoweza kutufundisha masomo muhimu kuhusu akili na  hekima na maisha kwa ujumla.

Kila kiumbe, ingawa kidogo, kinaonyesha aina ya hekima na akili ambayo inaweza kutumika kwa tabia na maamuzi ya binadamu.

Nimalize kwa kusema  kwamba hekima haitegemei ukubwa, udogo au nguvu, bali matumizi ya akili, busara, hekima na ufanisi katika kufanya vitu....kwenye maisha.

Kwa masomo kama haya bonyeza linki hapo juu kujifunza zaidi.

Au waweza wasiliana na Mimi kwa mawasiliano hapo chini.

MIGONGO ELIAS....
Add Value Network...
GeT tO tHe NeXt LeVeL!
eliasmigongo120@gmail.com
+255767653697.

Comments (2)

Loading... Logging you in...
  • Logged in as
Joga heke's avatar

Joga heke · 43 weeks ago

Thanks 👍.ili ufikie malengo lazima uwe na team
Itasaidia sana

Post a new comment

Comments by

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.