MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

JE NI NANI UMWAMBIE MIPANGO NA NDOTO ZAKO ZA MAISHA?

 


JE NI  NANI UMWAMBIE MIPANGO NA NDOTO ZAKO ZA MAISHA?

Kijana mmoja mdadsi, ambaye Ilikuwa ni kawaida yake kujiuliza na kudadsi vitu katika uhalisia wake.

Na hufanya hivi kwa kujiuliza yeye au kuwauliza watu wengine...

Ngoja kwanza nimwambie, dakika tano za kusom ujumbe huu hadi mwisho zinaenda kuchukua sura mpya ya maisha yako.

Sasa wacha tuendelee,

Siku moja kijina huyo alimuuliza baba yake ambaye alikuwa mvuvi.

Baba hivi ni sawa mimi kuwaambia watu malengo, na ndoto zangu kubwa?

Yule mvuvi akanyamaza kwa muda kisha akauliza.
"Kwa nini unataka kujua hivyo?"

Bila shaka huyu mvuvi alikuwa Mtanzania  nahisi😁

Kijana akajibu,
"Sawa, baba, nina ndoto nyingi kubwa, tena kubwa sana! Nataka kuwa mtu mwenye mgoso na athari chanya katika kizazi changu na nyanja zote za maisha.

Lakini, sijui niseme au nisiseme kwa watu kuhusu ndoto hizi nilizo nazo."

Mvuvi akatabasamu kisha akasema,
"Unajua nini... twende tukavue samaki mtoni. Kisha, tutaendelea na mazungumzo haya, huko sawa?"

Wakati huo, mvuvi na mtoto wake walichukua vifaa vyao vya uvuvi na kwenda kuvua mtoni.

Kama kawaida waliweka kipande cha chambo  kwenye ndoano na kutupa ndoano mtoni ili kukamata samaki.

Saa chache baadaye, tayari walikuwa wamevua samaki wengi na kapu lao lilikuwa karibu kujaa sasa.

Mvuvi akasimama, akamnyooshea kikapu na kumwambia mwanawe.

"Angalia samaki hawa wote kwenye kikapu. Wamenaswa na ndoana, na hatima yao sasa ni tofauti na ile waliyokuwa nayo mtoni.

Samaki hawa wamepoteza kila kitu katika maisha yao, familia zao, marafiki, jamaa na nyumba zao.

Inasikitisha kwamba watalazimika kuteseka na kuuawa kwa njia ya kutisha sana.  Wengine watakaangwa, wengine wataokwa, wengine watachomwa moto, wengine vitachomwa kwa mvuke, n.k.

Yule mvuvi aliendelea kuhoji...

Je, unajua ni kwa nini inawabidi kupitia maafa mengi namna hii?"

Kijana alifikiria kwa dakika moja, kisha akatikisa kichwa na kusema,
"Sijui, baba. Niambie."

Mvuvi akashusha pumzi ndefu kisha akapiga mluzi na kusema,
"Sawa, ni kwa sababu hawakuweza kufunga midomo yao.

Imeelezwa kuwa samaki aliyefunga mdomo kamwe hawezi kunaswa na ndoano. Yaani ni ngumu mno  kuathirika na majanga haya."

Baada ya kusema hivyo, mvuvi huyo alimpiga bega mwanae, akatabasamu kisha akaendelea.
"Mwanangu, hivi ndivyo inavyotokea katika maisha halisi.

Watu wengi wameshindwa kufanikiwa na wengine kupoteza kila walichopata katika maisha kwa sababu walifungua midomo yao sana na kuwaambia watu wengine juu ya ndoto na mipango yao.

Sababu nzuri ya kulinda hisia zako ni kufunga mdomo wako.

Yes kufunga mdomo wako kuhusu miradi yako , biashara  yako, mahusiano yako, kazi yako n.k,

Yaani ni kwamba watu wengi hawataki kukuona ukifanikiwa, kusonga mbele na kuwazidi hawataki kabisa.

Hivyo utakapo waambia mipango na ndoto zako wengi wataonyesha kufurahia na kukuunga mkono kwa nje. Lakini ndani yao 🤭,  aty kumbe ukigeuka tu wanakung'ong'a.... Kuwa makini nao.

Huu ni ushauri wa kuokoa mipango yako dhidi ya kuhujumiwa na watu wanaokuhusudu. Haupaswi kamwe kutangaza ndoto zako kwa kila mtu hadi zitakapokaribia/ kamilika.

Elewa hapo hupaswi kutangaza kwa kila mtu.

Kama italazimika jua ni taarifa gani utoe na zipi usitoe kwa wakati huo..

Kwani, watu wengi watafanya kila wawezalo kutuma mishale na daga kifuani mwako ili tu kuhakikisha haufanikiwi.
Jihadhari nao.

Kinywa kilichofungwa kamwe hakipati shida.

Fanya hatua yako kubwa kuwa siri. Sogeza kwa ukimya. Chukua hatua, na ushtue watu kwa matokeo yako.

Hapo najua Kuna maswali bado unajiuliza... Kama vile,

Sasa kama hivyo ndivyo ilivyo je nisiwaambie kabisa watu ndoto zangu? Na kama nitawaambia je ni mwambie kila mtu au ni mwambie nani sasa?

Kama tulivyoona hapo namna ilivyo hatari kumwambia kila mtu mipango yako. Kwani inaweza kupelekea kukata tamaa, kupoteza Nguvu ya kuendelea na hata kuuwa ndoto zako..

Pamoja na hayo peke yako huwezi kukabilisha mwenyewe ndoto zako, vinginevyo utachelewa sana.

Hivyo, kuna watu tu inabidi uwashirikishe na kiwaambia mipango na ndoto zako.

Hii ni kwaaili ya kupata hamasa, Nguvu, ushauri, pesa na misaada mingine. Si unajua umoja ni Nguvu eeh.

Baadhi ya watu unaopaswa kuwashirikisha mipango yako ni;

1. Mungu wako.

Ndiyo Mungu wako.

mshirikishe yeye na mkabidhi mipango na ndoto zako nazo zitathibitika.

2. Wazazi au walezi wako.


Tafiti zinaonyesha 98% ya wazazi na walezi hupenda watoto wao kufanikiwa sana na kuwa na maisha bora. Ni wachache huenda kinyume.

Lakini unaweza kuwashirikisha wazazi wako kama wanaeleweka.

Nakumbuka niliwahi kumshirikisha mama yangu mpango fulani hivi aliniunga mkono kwa namna ambayo sikudhania kabisa.

3. Mentors, Role models, counselors.

Hawa ni watu ambao mara nyingi wanakuwa wako na uelewa wa juu kuliko wewe na mara nyingi unajifunza kwao na wengine wanakuwa wamesha pitia njia unayoipitia hasa mamentors.

So mbaya ukiwashirikisha watu hawa.

4 .Marafiki na watu wako wa karibu.

Mara nyingi marafiki na watu wako wa karibu wamekuwa wakifanyika msaada sana kwako.

Na hawa ni watu ambao unatumia muda mwingi upo nao. Share nao baadhi ya mipango yako.

5. Watu unao waamini,  wanathamini ulicho beba na wanapenda mafanikio yako .

Hawa ni watu mhimu sana kwani hawatakuwa na wivu, na hujuma za kukurudisha nyuma.

Ni unajua ni watu wachache sana watafurahia mafanikio yako wengi watataka washindane nawe. Na hawatataka kamwe uwazidi.

Lakini kwa hawa ni uhakika...

Watu nilio wapendekeza hapo ni muhimu sana.

Sijui unanipata
???

Hata hivyo watu usiwashangaze kwa ndoto na mipango mikubwa uliyo nayo.

Washangaze kwa matokeo.

tafadhali rudia tena kusoma hapo.

Hivi unajua kuwa dunia inataka matokeo, haitaki bra bra ee...?

Sasa ukigundua hili usihangaike kuwaelezea watu ndoto zako, waonyeshe matokeo.

Wakiona matokeo yako Kisha watasema wao wenyewe.

Af tena usiwaambie kwa maneno waonyeshe kwa vitendo wataelewa zaidi kuwa wewe ni nani.

Kama wewe ni mwalimu tuonyeshe, Kama wewe ni coach tuonyeshe, Kama wewe ni mfanya biashara tuonyeshe, Kama wewe na mwimbaji tuonyeshe n.k.

Usituambie tuonyeshe si unajua "Action speaks louder than words " eeh

Ninachojua ni kwamba unauwezo mkubwa Sana, unaweza, unaweza. Lakini utakutana na watu wengine watakuaminisha huwezi, watakuvunja moyo na wengine kuuwa ndoto zako kabisa, kuwa makini ni nani una mwambia.

Na kubwa kabisa Tambua kwanini unamwambia mtu. Sababu hapo ni muhimu.

Chunga mdomo wako usije ukakughalimu kama wale samaki wakaishia kukaangwa.😁.

Ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu... Kama ndiyo waweza fanya yafuatayo.

1. Kama hujasave namba yangu waweza kusave Kisha unitumie jina lako WhatsApp nami nikusave uendelee kujifunza kila siku kupitia status.

2. Washirikishe wengine ujumbe huu wajifunze pia.

3. Unawezaa kutembelea ukurasa wetu wa Facebook Add Value Network. Au wasilina nami kwa masomo mengine ili kujifunza zaidi.

Let me sign out🖐️

MIGONGO ELIAS
Add Value Network
GeT tO tHe NeXt LeVeL 💪
eliasmigongo120@gmail.com
+255767653697.

Comments

Loading... Logging you in...
  • Logged in as
There are no comments posted yet. Be the first one!

Post a new comment

Comments by

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.