MAAJABU YA AKIBA

MAMBO MATATU (03) YA KUEPUKA KWENYE MAISHA YAKO.
U hali gani ndugu msomaji wa addvaluenetwork!
Nikukaribishe tena upate kujiongezea thamani yako kwenye maisha yako.
Leo tunaenda kuangali vitu vitatu ambavyo hupaswi kuvidekeza kabisa kwenye maisha yako.
Kwani vitu hivi vimekuwa ni kikwazo katika mafanikio ya watu wengi sana.
Si unajua wengi wanatamani kusonga mbele na kufanikiwa lakini kwa kujua au kutokujua wamekuwa na tabia fulani ambazo badala ya kuwapeleka mbele zina wabakiza palepale na kuwavuta nyumaa.
Hii ni changamoto kwa wengi. Ndiyo maana nimeamua kuzungumza hili na unapaswa kujitenganayo kabisa.
Wacha nikupongeze kwa kuwa umepata nafasi hii ya kusoma hapa, kwani hutabaki kama ulivyo.
Nami nikuahidi kuwa hujapoteza, hutajutia na utajishukuru kwa kusoma hadi mwisho leo.
Wacha tuyaangalie Sasa........
JAMBO LA KWANZA: TABIA YA KUMLAUMU (BLAMING HABIT).
Tabia hii si nzuri hata kidogo.
Kuna watu ni wazuri sana wa kulaumu, yaani kosa kidogo atalaumu kweli. Atakumbuka na kukusanya makosa yote ya nyuma.
Tatizo linapotokea hukimbilia kujua nani kasababisha ili aanze KUMLAUMU. Badala ya kutafuta suluhu. Hili ni tatizo.
Hapa atalaumu, serikali, atalaumu wazazi, atalaumu, marafiki, ndugu, atalaumu mazingila, atalaumu Mke/mme. Na wengine huenda mbali sana hadi kumlaumu Mungu.
Rafiki yangu ngoja ni kwambie, kama na wewe ni fundi wa kulaumu, bora uache mara moja kwani, kulaumu hakutakupeleka popote .
Kulaumu ni sumu ya kupalalaizi speed yako, shauku na UBUNIFU wako.
Kulaumu kutakupotezea muda na kukuchelewesha.
Hebu shika kichwa chako Kisha tafakari ni nani umekuwa ukimlaumu? Ana nini nawe hadi umlaumu?
Je ni wazazi wako kwa kutokukusomesha?, Ni serikali kwa kutokukuajiri? Ni mvua kuwa kunyesha au kutokunyesha? Hapa mifano ni mingi nadhani umeanza kupata picha.
Mimi kama mwalimu wako na sema hivi. Kulaumu ni kosa kubwa sana tena ingekuwa Korea ungepigwa risasi na ingekuwa uarabuni ungetupwa kwenye acid.
Natania bana 😁 lakini point kubwa hapa ni kosa sana kulaumu....
Kama hutaki kawaulize Wana wa Israel kilichowapata..
Wacha tuangalie Jambo la pili..
JAMBO LA PILI: TABIA YA KUHALALISHA (JUSTIFYING HABIT).
Hivi ulisha wahi kukuta mtu amepambana kutafuta pesa hadi akachoka bila mafanikio...?
Watu wa namna hii utasikia wanaishia KUHALALISHA kuwa unajua kwanza pesa sio muhimu sana, au utasikia unajua pesa ni mapepo, au pesa ni chanzo cha maovu yote. Haya ni ya kweli jamani?
Yaani anaamua tu KUHALALISHA kisa kwake imekuwa mtihani.
Niliwahi kukutana na mtu ambaye alikuwa anaogopa sana kuzungumza mbele ya watu. Katika kuzungumza naye nikasikia anahalalisha kuwa si unajua watu wote hatuwezi kuwa wazungumzaji kila mtu anaeneo lake. Ni kweli hatukatai lakin.....🤔
Akaendelea kusema kwanza kiasili wanaume sio wazungumzaji kama wanawake.
We kama umeshindwa umeshindwa tu bhana usianze KUHALALISHA na kufanya kamasherea.
Ukiona unajitetea sana nakutafuta visababu vingivingi jua upo karibu kuchemsha, tafuta suluhisho bhana.
Katika hili pia watu hupenda kujiweka katika makundi, ambocho si kitu kizuri ani.
Utasikia mwaka huu tutakufa na njaa, siku hizi hatuna hela, Sisi waaafrika ni masikini sana, elimu haitusaidii kabisa, ajira zimekuwa ngumu, unajua sisi masikini n.k
Hii nayo ninajabu kweli.
Sasa sikiliza, watu hatufanani. Matatizo yako usiwagawie na kuwahalalishia na watu wengine..... Tafuta suluhisho.
Ndugu, watu wanahela, watu wanatatua shida zao watu hawalaumu,, Usijifariji acha kugroup vitu tafuta suruhisho.
Wacha tuangalie Jambo la mwisho kwa leo....
JAMBO LA TATU: TABIA YA KULALAMIKA (COMPLAINING HABIT).
Goja nikwambie kitu.
Usikubali kukaa karibu na walalamikaji, kwani na wewe utaanza ulalamishi.
Si unajua there's no neutral interaction with people eeh!
Na ikitokea wamekaa karibu na wewe waambie, wafunge midomo yao.
Na kama ni wewe acha mara moja.
Kulalamika nitofauti na kulaumu, kulalamika kumefunga milango na fursa ya kujifunza na kusonga mbele kwa watu.
Yaani, nasema kulalamika hakuleti suruhisho, kulaumu, kunapoteza muda kulaumu hakufaiiii. Elewa hilo.
Kwa taarifa yako, unapolalamika inamaanisha unachukua wajibu wako, akili yako, uwezo wako, na mamlaka yako katika kukabiliana na changamoto za maisha yako na kuuhamishia kwa mtu unaye mlalalmikia.
Kama hutaki basi, lakini kama utaacha kulalamika na kuchukua hatua kimaso maso utashangaa, maarifa, akili na UBUNIFU wa ajabu uliokuwa ndani yako.....
Nipo na malizia lakini moja ya sababu ambazo huwafanya watu kulalamika, kulaumu, na hata kuhalalisha vitu. Ni kwamba Wana vuta usikivu (attention) kwa watu ambao wanaamini ni wanauwezo mkubwa kuliko wao, ili waweze kuwaonea huruma na kuwasidia.
Unaweza kulalamika kwa sauti loud au kimya kimya kwenye akili yako.
Acha vyote
Stop, stop, stop blaming, complaining and justifying.
POINTS TO KEEP..
1. Maisha yako ni wajibu wako wewe mwenyewe kwa 100% ukiamua kuwapa watu wajibu wako. Yatakukuta.
Usizani kunamtu atatoka kusiko julikana aje akupambanie, pambana mwenyewe.
2. Tabia za kulaumi, kuhalalisha, na kulalamika ni tabia za kimasini, sijawahi kuona tajiri anafanya hayo mambo.
Kama umewahi kuona share na mimi WhatsApp.
3. Watu wana shida na matatizo yao, usitake kuwaongezea matatizo kwa kuwalaumu, kuwalalamikia n.k
4. Kulaumu, kulalamika ni kuhamisha wajibu, uwezo, nguvu na UBUNIFU wako na kumkabidhi unaye mlalalmikia.
Wewe kuweza?🤔
5. Kulaumu kunakupotezea muda na kukuchelewesha tu.
Ndugu naweza kuongea na kuongea mengi sana lakini nadhani umepata point eeh!!!
Kama ni mtu wa kubadilika badilika,, Kama hutaki sawa maana huo nao ni uamzi pia.
Sikiliza, baada ya kusoma hapa kuna mambo mawili tu ya kufanya
Cha kwanza ni kuachana na tabia hizi mara moja. Na kujenga tabia zingine tofauti...
Na cha pili ni kuendelea nazo kama mwanzo.
Uamzi ni wako.
Na njia pekee ya kuacha tabia hizo ni kuacha tabia hizo.
Ndiyo kuachana nazo
Hongera kwa kusoma.
Kama umejifunza na umeelewa kitu basi unaweza fanya haya;
1. Nishirikishe ulichojifunza inbox, na kama unapoint nyingine unaweza ukaongeza nijifunze pia.
2. Share ujumbe huu kwa uwapendao. Ili wajifunze pia.
3. Kama hujasave namba yangu save Kama Mwl. Migongo Elias Kisha nitumie jina lako WhatsApp nikusave ili kujifunza kila marakupitia WhatsApp status.
4. Bonyeza linki hapo juu kujifunza masomo mengine.
Ni hayo tu kwa leo
MIGONGO ELIAS.
Add Value Network!
GeT tO tHe NeXt LeVeL 💪.
+255767653697
eliasmigongo120@gmail.com
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.