MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

MISINGI MITATU YA MAFANIKIO

 

MISINGI MITATU YA MAFANIKIO

Hakuna mtu asiye penda mafanikio, lakini ni wachache tu hufanikiwa.

Leo tutaangalia Jambo hili kwa mapana zaidi.

Hili ni somo muhimu kuwahi kutokea..

Na mara baada ya kusoma hapa, utabadili fikira zako juu ya mafanikio.

Utajua kwanini wengine huwa ni ngumu sana kufanikiwa hata kama ni wapambanaji.

Utafahamu njia na kanuni sahihi za kufanikiwa kwako.

Na mengine mengi.......

Siku za nyuma kidogo, nilimtembelea rafiki yangu. Ambaye ilipita miaka mingi hatujaonana, kwa namna yake amepiga hatua katika mafanikio haya ya mwili.

Tulijikumbusha mambo ya nyuma, kwa namna ambavyotuliishi, kwa kweli tulifurahi sana. Kwani kila mmoja alikuwa connected aseee.

Ilikuwa special day ukilinganisha na kwamba ni miaka mingi hatukutiana machoni ingawa tulikuwa tunawasiliana.

Bwana tuliongea vitu vingi na tulifurahia sana asee.

To cut the story short, ilibidi tuanze kuulizana mambo ya point, kujitathimini na kujenga...

Kama kawaida yangu nilikuwa na maswali mengi ya kudadsi......

Moja ya swali nililomuuliza lilikuwa ni kwamba; NDUGU YANGU NI MUDA SASA HATUJAONANA, NA SASA UMEPIGA HATUA SANA, NINI SIRI YA MAFANIKIO YAKO?.

Alivuta kiti na kusogea huku akisema rafiki yangu, naona bado niko nyuma sana, lakini kwa hapa nilipofika kuna vitu vimenisaidia na kunifanya niwe hivi leo...

Aliendelea kusema.........

Katika mafanikio nimejifunza vitu vingi sana, na moja ya kitu ambacho kinanisaidia mimi ni. Kanuni za mafanikio ambazo sasa ninaziishi.....

Nilimuuliza kanuni zipi hizo!??

Aliendelea kuzitaja na kuelezea kwa namna ambavyo zimemsaidia..

Lakini pia, kutokana na kufanya utafiti, kwa kuuliza watu waliofanikiwa, kwa kusoma vitabu na njia zingine.

Nimekuja kugundua mafanikio yana vitu vitatu muhimu kwa mtu yeyote kufanikiwa katika kada aliyopo... Na hizi nina ziita  kanuni muhimu za mafanikio...

Lakini leo nataka tuzungumze kitu kimoja ambacho ni muhimu sana katika mafanikio....

Kitu hiki nakiita NGUVU NA CHANZO CHA MAFANIKIO ( POWER AND SOURCE OF SUCCESS).

Kama ulikuwa hujui ni kwamba, MTU ni roho yenye nafsi na inakaa ndani ya mwili.

Mara zote roho haionekani lakini inatumia mwili kufanya kazi hapa dunia.

Na kama haionekani basi inaongozwa na Nguvu isiyoonekana pia. Yaani, INVISIBLE POWER.

Kwa taarifa yako huruhusiwi kutawala hata DUNIANI kama hauna Nguvu, POWER.

Na Nguvu Ninayo izungumzia hapa siyo ya misuli na nyama za gym, au Nguvu za kiume,  noo!.

Ni Nguvu isiyoonekana yaani, SPIRITUAL POWER.

kadiri utakavyo kuwa imara rohoni ndivyo utakavyo tawala kwa wepesi kwenye ulimwengu wa kawaida.

Kanuni hii inasema chanzo cha mafanikio makubwa hapa dunianii ni SPIRITUAL POWER, Nguvu ya kiroho.

Hii ni Nguvu inayokupa, ulinzi na kukuongezea Nguvu pale akili zako zinapofika mwisho au kukata tamaa.........

Kazi kubwa, inakupa ulinzi wa mafanikio yako, na kukutia Nguvu unapohisi kufika mwisho.

Mara nyingi Nguvu hii imegawanyika katika makundi makubwa mawili;

Moja ni Nguvu ya Mungu.  Hii ni SUPERNATURAL POWER.
Inatoka kwa Mungu mwenyewe. Siyo copy ni original......

Ya pili ni; Nguvu ya Shetani......Hiii wakati mwingine wanaiita DARK POWER.

Inatoka kwa Shetani mwenyewe....

Nguvu hizi zote zina misingi yake, zinafanya kazi na huwapatia matokeo waamini wake kama watafuata na kukizi kanuni na sheria zake.

Zote zinatoa matokeo.

Utofauti mkubwa ni kwamba, Nguvu hii ya Kwanza ya MUNGU, THE SUPERNATURAL POWER. Inadumu milele. Last longer...

Akati ile ya Shetani inadumu kwa muda tu!.

Mtu yeyote anaweza kuangukia katika kundi moja wapo hapo juu.

Na kama atafuata kanuni zake matokeo atayapata....

Chagua vyema unataka upande upiiii? Maamuzi ni yako.

Muda ungetosha ningechimba kila moja kinaga ubaga... Ili uone zinavyo fanya kazi.....

I wish nitafanya siku moja kama utaonyesha uhitaji zaidi....

Goja turudi kwenye mada.

Hapa ndipo unaweza kukuta mtu anapambana, anachapa kazi kama mtumwa anafuata kanuni zote anazopaswa kufuata lakini still mambo hayaendi.

Sababu yake ndo hii, hakuna backup nyuma yake,,, backup ya kumpa ulinzi na Nguvu ya kuendelea.

For your information!
Watu wote unaowaona wamefanikiwa na kufika mbali sana kwenye hii duniani, elewa kuwa nyuma yao Kuna Nguvu kubwa inawa backup....

Wewe elewa hivyo tu...

Watu hawa wanakuwa wamesha chagua upande mmoja na kujicommit kuwekeza na matokeo wakayapata..

N.b. Elewa utofauti nilio usema hapo juu kabla ya kuchagua upande wako.....

Mimi nimechagua upande wa THE SUPERNATURAL POWER. Nguvu ya Mungu. Matokeo nayaona na sababu nitaeleza wakati mwingine.

Kwa ku backup ujumbe huu na maandiko matakatifu ngoja tusome

.....( Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, MAANA NDIYE AKUPAYE NGUVU ZA KUPATA UTAJIRI; ILI ALIFANYE IMARA AGANO LAKE alilowapa baba zako, kama hivi leo.) Kumbukumbu la Torati 8:18
.............................

Umeona hapo? Anasema naye atakupa Nguvu za kupata UTAJIRI, haya ndiyo mafanikio yenyewe...

Zipo kanuni nyingine muhimu za UTAJIRI na mafanikio ambazo ni muhimu kuzifahamu.....

Ningali bado ninayo mengi ya kuzungumza, leo nachagua kuweka karamu kwanza......🖐️

kama kuna kitu umejifunza, nataka kujua kutoka kwako, usiwe mchoyo  share na mimi, nami nitafurahi....

Pia watumie uwapendao ujumbe huu.

COMMENT HERE..,.......................

Kama unataka kujifunza zaidi waweza save namba yangu kama MWL. MIGONGO ELIAS Kisha nitumie jina lako WhatsApp nami naahidi kusave ili uendelee kujifunza kila siku kupitia status......

Wako;

MIGONGO ELIAS
The Chief Value Officer
Add Value Network!
GeT tO tHe NeXt LeVeL 💪
+255767653697
eliasmigongo120@gmail.com

Comments (2)

Loading... Logging you in...
  • Logged in as
Joga haruna's avatar

Joga haruna · 41 weeks ago

Exactly
1 reply · active 40 weeks ago
Migongo Elias's avatar

Migongo Elias · 40 weeks ago

Nice

Post a new comment

Comments by

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.