MAAJABU YA AKIBA

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.
Ilikuwa tarehe 25052024 Nilipata nafasi ya kuhudhuria, tukio la mahafali ya kuwaaga wahitimu wa Casfeta tayomi Chuo kikuu Mzumbe.
Iliyofanyika katika ukumbi wa Professor Kuzilwa uliopo Mzumbe Morogoro Tanzania.
Shughuli ilifaana sana, tulikutana na jamaa, ndugu, rafiki na watu kibao. Pia tulifurahi, tulijifunza, tulikula n.k
Baada ya siku chache kupita, wadau na marafiki kadhaa nilipo kutana nao walisema; Mwl. nilikuona kwenye sherehe!.
Nami kujibu ndiyo nilikuwepo, Ilikuwa nzuri sana.
Wengi waliuliza kuwa, kwanini hadi sasa hujasema chochote mwl?
Ukwel mtupu, sikupanga kuandika chochote.
Lakini kwasababu ya maswali mengi nikaona kunahaja ya kuzungumza. Ukweli ni kwamba kuna mambo mengi sana nilijifunza kwenye shughuli hiyo.
Laikini pia kuna mambo mengine ambayo mtu yeyote anaweza kujifunza kwenye mahafali na matukio yafananayo na hilo:
Na hapa naenda kukushirikisha mambo 9 muhimu ambayo mtu yeyote anaweza kujifunza kutoka kwenye tukio kama hili.
Na hii si katika mahafali tu! Bali haka kwenye halaiki na mialiko mingine inayofanana na hii.
Mambo haya 9 ni muhimu sana lakini jambo la tisa ndiyo nalipendelea zaidi. Hivyo soma uelewe.
1. Umuhimu wa kuungana na kujamiiana na wengine.
Hapa unaweza kujifunza kuwa;
Mahafali yanaweza kuleta pamoja watu kutoka sehemu mbalimbali. Fursa hii inaweza kutumiwa kujifunza jinsi ya kuwasiliana, kuungana, na kujenga mitandao na watu wenye asili tofauti. Hii ndio tunaiita connection.
Mgeni rasimi alisistiza sana umuhimu wa kujenga mtandao watu kwenye matukio Kama hayo.
Jitahidi kadiri uwezavyo kuongeza mtandao wako hasa unapokuwa kwenye halaiki kama hizi. Si unajua kuwa "your network is your networthy" eeh.
2. Umuhimu wa Kuwapongeza Wengine.
Hii inanguvu sana kwani, watu huhisi hali upendeleo wa hali ya juu sana, pale wanapo pongezwa. yaani,
Kusherehekea mafanikio ya wengine ni muhimu. Inafundisha thamani ya kupongeza juhudi na mafanikio ya wenzako na kujenga utamaduni wa kusherehekea mafanikio ya pamoja.
kitendo hiki kilifanywa na kamati kuu ya tawi, ndugu jamaa na marafiki kwa kuwapa zawadi mabali mbali wahanga wa tukio.
Jenga utamaduni wa kiwaponheza wengine wanapo kamilisha mambo au kufanya mambo yao.
3. Kujenga tabia ya kujifunza kwa mwendelezo Maisha Yote.
Elewa kwamba kujifunza hakuishi baada ya kuhitimu. Dunia inabadilika kila wakati, na kuwa na uwezo wa kubadilika na kujitolea kwa kujifunza maisha yote kutakusaidia kubaki muhimu, kuhitajika na kufanikiwa.
Katika hili pia Mgeni rasmi alisisitiza kwa kuwataka wahitimu waweke nguvu kubwa katika kujifunza teknolojia na mabadiliko yake.
hata wewe katika sehemu yeyote uliyonayopo weka nguvu nyingi katika kujifunza. kwani " continuous learning is the minimum requirement for success in any field."
4. Kujifunza Kutoka kwa Wazungumzaji.
Hiki ni kitu muhimu sana kwenye sherehe yeyote. kwani,
Mahafali mara nyingi huwa na wazungumzaji mbalimbali wenye hekima na uzoefu tofauti. Kusikiliza wasemaji hawa kunaweza kutoa maarifa na motisha muhimu kwa wasikilizaji wote.
Mimi binafsi nilijifunza vitu vingi Sana kutoka kwa wazungumzaji, wahitimu na washereheshaji.
Usifanye kosa ambalo watu wengi hulifanya, wanaenda kwenye sherehe kwaajili ya nyama, picha na vinywaji pekee.
wewe kuwa wa tofauti beba karamu, Notebook kajifunze kule. Lakini pia usisahau.
5. Uvumilivu, na Kuwa na Nia
Wakati mwingine, sherehe za kuhitimu zinaweza kuchukua muda mrefu. Hii inafundisha uvumilivu na nia ya kusimama na kushiriki hadi mwisho, hata pale inapokuwa ngumu au kuchosha.
Hii pia niliiona kwa wahitimu kuvumilia kwa muda mrefu tena hadi mwisho, licha ya kuwa sherehe ilichelewa ukuanza kutokana na changamoto ya vyombo.
Hawakukata tamaa.🖐️
6. Nguvu ya Ndoto na Shauku ya kusonga mbele.
Kuhitimu ni njia ya kufuata ndoto na hamasa zako. Ni muhimu kuweka malengo, kuwa na shauku, na kuwa tayari kuchukua hatari ili kufikia matarajio yako.
Kwani, katika kipindi hiki utakutana na maneno ya pongezi, zawadi n.k ambavyo vitakuwa hamasa ya kusonga mbele.
7. Ubora wa Maandalizi
Mahafali huonyesha jinsi ya kuandaa na kuratibu matukio makubwa. Mtu yeyote anaweza kujifunza umuhimu wa mipango.
Mahafali ni wakati wa kutambua na kuheshimu mafanikio ya mtu binafsi na ya kijamii. Hii inasaidia kujifunza jinsi ya kutambua na kusherehekea hatua muhimu katika maisha.
Nami pia nichukue nafasi hii kuwapongeza waandaaji wa shughuli hii kwani, vitu vilikaa si katika msosi tu, bali ukumbi na vitu vingine.
Sema wakati mwingine waandae vyombo mapema.😎
8. SHUKRANI.
Jenga mtazamo wa shukrani kwa uzoefu, elimu, na fursa ulizopokea. Shukrani inaweza kuongeza hali yako ya ustawi na kukuza mtazamo chanya wa maisha.
hali hii pia ilionyeshwa na wahitimu wengi walipo pata nafasi ya kuzungumza kila mmoja alionyesha hali ya furaha, bashasha, tabasamu na kushukuru.
hata hivyo jijengee nidhamu ya kutoa na kushukuru kwa vitu utakavyo pata au kukosa.
9. KILA KITU KINA MWANZO NA MWISHO.
katika maisha kuna kupanda na kuna kuvuna, kuanza na kumaliza, kuingia na kutoka.
yaani na sema muda wa kuanza na kumaliza kuingia na kutoka.
Wahitimu waliingia 2021 na leo 2024 wanaondoka.
Hata wewe katika maisha Kuna muda wa kuanza kazi, biashara, ajira n.k na kuna muda utatakiwa kubadili au kuachana na kitu hicho ili ufanye kitu kingine.
Kwa ujumla, mahafali si tu kwa ajili ya wahitimu bali ni tukio lenye fursa nyingi za kujifunza kwa mtu yeyote anayeshiriki. Ni wakati mzuri wa kujifunza kuhusu maisha, jamii, na jinsi ya kusherehekea mafanikio na maendeleo.
Ni matumaini yangu kuwa, Kuna kitu umejifunza.
1. Kama wewe ni Mmliki wa kampuni, biashara, taasisi, biashara n.k. Na unataka kuiweka bishara au taasisi yako katika maandishi,,,,, Nina jibu lako.
2. Kama wewe ni mwandishi unatamani kukuza uwezo wako wa kuandika, au pengine huelewi uanzie wapi kwenye uandishi ,,,,,, Nina njia.
Unaweza kuwasiliana nami kupitia mawasliano hapo chini.
Au bonyeza link hapa.
Migongo Elias.
Add Value Network.
GeT tO tHe NeXt LeVeL.
eliasmigongo120@gmail.com
+255767653697.
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.