MAAJABU YA AKIBA

PANDE ZA MAFANIKIO
Mara nyingi MAFANIKIO huwa ni hitaji la Kila mtu.
Na hii huwa imebeba sehemu mbili muhimu.
1. SEHEMU YA KWANZA NI UPANDE WA MBELE( FRONT PART).
Sehemu hii huonyesha
jambo hili kuwa ni zuri na ni jambo la kutamanika, kufurahiwa, na mengine kama hayo.
Huu unaonekana kwa macho ya nyama. Na watu hujua na kutoa sifa kemukemu.
Na huonekana huleta hamasa, furaha, umaarufu, uhuru, heshima n.k
Siku zote watu waliofanikiwa na mafanikio yenyewe huonekana ni easy sana.
Na watu hulielezea Kwa urahisi naMSINGI WA NPGUVU YA MAFANIKIO. wa hali ya juu sana.
Utasikia alienda secondary, akaenda chuo akawa bilionea, mara utasikia alianzisha biashara saivi ni mkurugenzi, alikuwa masikini akapewa mtaji saivi ni milionea.
Hapa mifano ni mingi sana.
2. SEHEMU YA PILI NI UPANDE WA NYUMA (BACK PART).
Upande huu mara nyingi hauonekani haraka.
Watu wengi husahau kabisa kuuangalia na kuusemea. Yaani chini ya kapeti namaanisha nyuma ya mafanikio...
Rafiki hii ni sehemu ya mchakato.
Ukiachana na raha na umuhimu wa mafanikio.
Huu ni upande wa kulipa gharama, upande wa kufeli, upande wa mashaka, upande wa kujitoa mhanga, upande wa kukosolewa, upande wa kukataliwa, upande wa hali ngumu, upande wa kujitoa, upande wa kujenga nidhamu.
Kuyataja ni mengi sana, lakini nadhani umepata picha.
Na hii itukumbushe kuwa tunapotaka kufika sehemu ya kufanikiwa kwetu, kuna gharama na changamoto ambazo tutazipitia na lengo lake Si kutukatisha tamaa wala kutukomoa, bali ni kutuandaa ili kupata, kushukilia na kuhimili mafanikio tutakayo yapata.
Maandalizi yakiwa mabaya hii ni kusema kutokupata mafanikio au kupata na kushindwa kuhimili.
Na hii ni katika nyaja zote za maisha, kama ni michezo, kilimo, uandishi uongozi na mengine kama hayo.
Kinyume chake ni ukweli mtupu.
Upande huu ni chanzo, jikoni kunakopikwa mafanikio. Hapa ndipo mchakato wa mafanikio huandaliwa.
Ukifata mchakato na kuufanyia kazi, matokeo tarajiwa yatakuja tu.
Najua kunakitu umeongeza.
Mungu akusaidie sana.
Mwandishi>> Migongo Elias.
Mhariri >>> Erick Mgaya.
Ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu... Kama ndiyo waweza fanya yafuatayo.
1. Kama hujasave namba yangu waweza kusave Kisha unitumie jina lako WhatsApp nami nikusave uendelee kujifunza kila siku kupitia status.
2. Washirikishe wengine ujumbe huu wajifunze pia.
3. Unawezaa kutembelea ukurasa wetu wa Facebook Add Value Network. Au wasilina nami kwa masomo mengine ili kujifunza zaidi.
Let me sign out🖐️
MIGONGO ELIAS
Add Value Network
GeT tO tHe NeXt LeVeL 💪
eliasmigongo120@gmail.com
+255767653697
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Cheyo · 35 weeks ago