USISAHAU KILICHOKULETA HAPO.
USISAHAU KILICHOKULETA HAPO. Kuna makosa mawili makubwa ambayo watu wengi hufanya wanapoanza kuyaona mafanikio yao: wanasahau walikotoka, na wanasahau kilichowafikisha hapo. Haya ni makosa makubwa mawili, ni kesi ya kutokujitambua. Hapo ndipo safari yao huanza kushuka bila wao kujua yaani, kimya kimya. UKWELI AMBAO NIWACHACHE WANAUJUA, Mafanikio hayakuji kwako kwa bahati mbaya. Yalikuja kwa sababu ya vitu fulani ulivyofanya. Yamkini huenda; Ulijituma sana, Ulijinyima, Ulijifunza, Uliomba sana, ulisave sana, Ulijitoa zaidi kuliko wengine, Ulivumilia wakati mgumu. 👉 Hiyo ndiyo “formula” yako ya mafanikio. Lakini shida inaanza pale unapopata mafanikio walau kidogo, halafu ghafula unaanza kubadilika. UNAPOSAHAU KILICHOKULIPA, UNAPOTEZA MWELEKEO WAKO. Watu wengi wakianza kuona matokeo: Wanaacha nidhamu, Wanaacha kujifunza, Wanaanza kujiamini kupita kiasi, Wanasahau kujituma, Wanaanza maisha ya anasa mapema sana. Kisa wameona matokeo kidogo tu. Namatokeo yake,...