MAAJABU YA AKIBA
MAAJABU YA AKIBA
Akiba (saving) ni kiasi cha fedha
au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza
kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake
ya sasa.
Hata katika biblia ``Mwanzo
41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na
kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili
kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili.
Farao aliona kabisa kuwa
nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia
kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea
akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia
yenyewe,
Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa
mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye.
Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli
alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula.
Ni muhimu kujiwekea akiba ya
kile kidogo unachokipata kwa sasa kwani kitakuwa na faida nyingi sana sasa na
hapo baadaye.
Zipo aina kadhaa za akiba
ambazo inampasa mtu kuwa nazo, kama ifuatavyo;
AINA
YA KWANZA: AKIBA YA ROHO NA NAFSI YAKO;
Kwakuwa mafanikio na ukuaji muhimu huanzia ndani ya mtu,
hivyo ni muhimu sana kwa kila mtu kuwekeza vilivyo katika nafsi na roho yake,
ili akijiwekea akiba ya kutosha basi atapata matokeo yake. Unawezakufanya hivyo kwa maombi, kusoma na
kujifunza neno; kuwasaidia na kujitoa kwa wahitaji na kazi zote kwaajili ya
utukufu wa Mungu.
Akiba muhimu pia katika eneo hili kwa watu wote ni
kumwamini Yesu kuwa bwana na mwokozi wa Maisha yako. mwanadamu yafaa ujiwekee
akiba kwa kumpokea Yesu na kufanya yote yampendezayo ili kujifaidia mwenyewe na
kizai chako.
AINA
YA PILI: AKIBA YA MALI AU FEDHA;
Ni muhimu kukumbuka kujiwekea sehemu ya fedha au mali
unayoipata kila siku kwa ajili ya baadaye ili kupambana na changamoto mpya
zitakazoibuka mfano utasikia; utasikia bei ya hiki imepanda au ada imeongezeka
au kodi imeongezeka au namna yoyote ya mabadiliko hayo yanakuwa yanahitaji
fedha zaidi.
Ajabu ni kwamba utakuta pamoja na hayo kutokea lakini
uchumi wako hauongezeki na wakati fulani ni kama unashuka usipo kuwa makini
unaweza kujikuta umekuwa mtu wa kuomba misaada kila wakati sababu haukufikiria kuhusu
kesho.
Hebu tazama viumbe hawa wa ajabu chungu ni watu wasio na
nguvu lakini hujiwekea chakula wakati wa hari (mithali 30:25) ni muhimu sana
kutambua majira na nyakati za Maisha.
Chungu analijua hilo ndio maana hujiwekea akiba, mara
nyingi tunapata sana fedha au mali kwa wingi hadi unaweza kujiulliza ulikuwa
wapi siku zote huko nyuma kufanikiwa?
Huu ni wakati wako wa kufurahia na kuwa makini sana.
Kuna kanuni moja inaitwa ``bread and seed`` hujaribu kutueleza wakati unafikiri umepewa
chakula pekee toka kwa Mungu yeye huona amekupa chakula na mbegu hivyo
hautakiwi kula mbegu kwani utashindwa kuleta matokeo pindi chakula kitakapoisha
utahitaji kuvuna kilichopatikana kwa mbegu kama hukujiwekea akiba huu ndo
wakati ambao utaona ni kama kitu hakiendi na hauna pesa ``usisahau akiba ni mfano wa
mbegu hivyo haiwezi kukuletea matunda isipo pandwa kwa upande wa pili akiba
isipo wekezwa haiwezi kukusaidia
wakati wa shida fulani``
Na
muhimu ni kuwa hatuishii kuiweka tu hii akiba bali tunaenda hatua ya Zaida
mbele kwa kuiwekeza ili ilete matokeo makubwa tarajiwa.
AINA
YA TATU: AKIBA YA MUDA;
Wataalamu wa mikakati ya maisha au life
strategists husema muda ni mali kama ni mali tumeangalia hapo juu lazima tuweke
akiba ya mali tulizo nazo. Namna ya kuweka akiba ya muda ni kuto kupoteza muda
kwa vitu visivyo na umuhimu kwa maisha yako mfano kuangalia tu TV bila ratiba
maalumu, kushinda unalala bila sababu yoyote, Kukesha ukiwa una chart au
unaperuzi mitandaoni billa ya sababu maalumu.
Ikumbukwe rasilimali muhimu ambayo tumepewa kwa usawa ni muda. Hapa kila
mmoja ana 24 na utofauti unakuja kwa namna kila mtu anavyoutumia muda wake.
Unaweza kufanya vitu kama; kusoma vitabu ili
kujipatia maarifa fulani lakini pia kujiunza
ujuzi mpya au new skills zitakazo kusaidia katika maisha yako, kama
namna nzuri ya kuukomboa wakati wako’
AINA
YA NNE: AKIBA YA MAHUSIANO;
Mahusiano mazuri na watu yanaweza kutumika
kama bidhaa ya kupata mahitaji ya mtu husika.
Mara nyingi mtu akijikusanyia watu muhimu wengi basi atakuwa na akiba
njema iliyomzu nguka.
Kila mtu hutamani kuona anathaminiwa, anapendwa na
anajaliwa na watu wake wa karibu akiba ya mahusiano ambayo wewe binafsi unaijenga
kwa ajili ya kukusaidia wewe mwenyewe. Njia rahisi ya kujiwekea akiba kwa watu
ni kwa kuongeza thamani kwao kwa kuwatafuta na kuwajulia hali au kuwasaidia
katika yale matatizo au shida wanazozipitia na wakati fulani kujaribu kuomba
ushauri wao kwa mambo sumbufu kwako.
Mwandishi>> Erick Mgaya.+255 764 032 905
Mhariri >>> Migongo Elias. +255767653697
Ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu... Kama ndiyo waweza fanya yafuatayo.
1. Washirikishe wengine ujumbe huu wajifunze pia.
2. Unawezaa kutembelea ukurasa wetu wa Facebook Add Value Network. Au wasilina nami kwa masomo mengine ili kujifunza zaidi.
Let us sign out🖐️
Add Value Network
SeE yOu NeXt LeVeL 💪
Michael · 27 weeks ago