KUJILINGANISHA NI SUMU HATARI.
KUJILINGANISHA NI SUMU HATARI. Tatizo kubwa la kizazi hiki si kukosa UWEZO binafsi. Bali ni KUJILINGANISHA kupita kiasi. Hebu tazama kwa mfano, nafungua simu yako, unaona maisha ya wengine, yanaonekana yamepangwa. Wamefanikiwa. Wanasafiri. Wanaonekana kuwa na furaha sana. Wanavaa na kula vizuri. Halafu unaanza kujiuliza: “Mimi niko wapi?” mara unasema mimi si chochote. Mdogo mdogo, unajikuta unapima thamani yako kwa vipimo vya watu wengine. Hapo ndipo tatizo linapo anzia. Lakini ukweli ni huu; 👉 kila mtu ana safari yake, kila mtu anasababu yake. Ambayo yaweza kuwa nitofauti kabisa na wengine. Kuna anayekimbia haraka kwa sababu alianza mapema. Kuna anayepanda polepole kwa sababu anajenga msingi imara. Kuna anayeficha mapambano yake nyuma ya picha nzuri. Usilinganishe mwanzo wako na mwisho wa mtu mwingine. Si unajua maisha ni kama kitabu, ukurasa wako wa kwanza una weza kuwa ni wa mwisho kwa mwingine. Kila mtu anakitabu chake na kurasa zake. Maisha yako hayakuitwa KUIGA watu...