KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA.

Image
  KAMA UNASAHAU MARA KWA MARA, SOMA HAPA KWANZA. Boss! Siyo  kila mara, kusahau ni ishara ya Ubongo dhaifu, mara nyingi ni namna tunavyojifunza ndugu. Nimekutana na watu wengi wakisema: "Mimi sina akili kubwa." Wengine "Kumbukumbu yangu ni mbaya." Mara "Ubongo wangu hauhifadhi vitu." Lakini ukweli ni kwamba, mara nyingi tatizo si ukubwa wa akili yako wala uwezo wa ubongo wako. Tatizo ni kwamba watu wengi hawajawahi kufundishwa jinsi kumbukumbu (memory) inavyofanya kazi boss. Sikia ndugu; Ubongo wa binadamu umeumbwa kwa ustadi mkubwa. Kazi yake si kuhifadhi kila kitu unachokiona au kukisikia, bali ni kuchagua filtering taarifa muhimu na kuacha zisizo muhimu wala matumizi. Kwa hiyo, kusahau si kasoro ya ubongo ni sehemu ya kawaida ya jinsi unavyofanya kazi. Hebu tuangalie sababu kuu zinazowafanya watu kusahau mara kwa mara. 1. Kukariri Bila Kuelewa (memorising without understanding). Hili ndilo kosa kubwa zaidi ambalo wanafunzi na hata watu wazima...

KUJILINGANISHA NI SUMU HATARI.


 KUJILINGANISHA NI SUMU HATARI.

Tatizo kubwa la kizazi hiki si kukosa UWEZO binafsi.

Bali ni KUJILINGANISHA kupita kiasi.

Hebu tazama kwa mfano, nafungua simu yako, unaona maisha ya wengine, yanaonekana yamepangwa.

Wamefanikiwa.

Wanasafiri.

Wanaonekana kuwa na furaha sana.

Wanavaa na kula vizuri.

Halafu unaanza kujiuliza:

“Mimi niko wapi?” mara unasema mimi si chochote.

Mdogo mdogo, unajikuta unapima thamani yako kwa vipimo vya watu wengine. Hapo ndipo tatizo linapo anzia.

Lakini ukweli ni huu; 

๐Ÿ‘‰ kila mtu ana safari yake, kila mtu anasababu yake. Ambayo yaweza kuwa nitofauti kabisa na wengine.

Kuna anayekimbia haraka kwa sababu alianza mapema.

Kuna anayepanda polepole kwa sababu anajenga msingi imara.

Kuna anayeficha mapambano yake nyuma ya picha nzuri.

Usilinganishe mwanzo wako na mwisho wa mtu mwingine.

Si unajua maisha ni kama kitabu, ukurasa wako wa kwanza una weza kuwa ni wa mwisho kwa mwingine. Kila mtu anakitabu chake na kurasa zake.

Maisha yako hayakuitwa KUIGA watu wengine, bali kuishi KUSUDI lako.

Vipaji vyako ni vya kipekee.

Uwezo wako ni wakipekee.

Wakati wako ni wa kipekee.

Safari yako ina maana yake.

Badala ya kuangalia wengine wamefika wapi, jiulize:

๐Ÿ‘‰ Leo nimekua kiasi gani kuliko jana?

๐Ÿ‘‰ Nimejifunza nini leo?

๐Ÿ‘‰ Ninakaribia kiasi gani ndoto yangu?

Kumbuka;

Wakati unajilinganisha, unapoteza amani.

Kujlinganisha ni mwizi wa muda.

Mara tu unapojilinganisha unapoteza NGUVU, THAMANI YAKO NA UWEZO WAKO WA KUFIKRI.

Lakini ukiacha kujilinganisha, kimya kimya utaanzq  kujithamini, unapata nguvu, furaha, amani, kujiamini, kutumia uwezo wako na mengine kibao yafananayo na hayo.


Hivyo basi;

Tambua wewe ni nani, UDHAIFU na UIMARA  wako ni upi. Wekeza sana kwenye UIMARA wako.

Kisha pambana mdogo mdogo #MAISHA yanajengwa na kuandaliwa siku moja na wee utafika huko.

Baini, uko wapi unataka nini na unaenda wapi?. Heshimu hatua zako unazopiga kidogo kidogo.

Heshimu mwendo wako.

Heshimu historia yako.

Kwa sababu wewe sio wao.

Na wewe haukuitwa kuwa wao.

Wewe uliitwa kuwa wewe halisi. Yes wewe Orginal.๐Ÿ’™๐Ÿ”ฅ

Kama umejifunza kitu tuandikie kwa comment.

Kujifunza zaidi bonyeza hapa

Migongo Elias 

Add Value Network 

#knowledgeispower 

#seeyounextlevel

Popular posts from this blog

UKIJUA HILI KUHUSU WATU UTAFANIKIWA SANA.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 27.

UCHAMBUZI WA KINA HATIMA YA KIMUNGU SEHEMU YA 29