MAAJABU YA AKIBA

KATA TAMAA KUKATA TAMAA (GIVE UP TO GIVE UP)!
Kukata tamaa; Ni fikira zinazo mfanya mtu kukosa tumaini la kusonga mbele au kuendelea kufanya kile alicho jipangia kufanya, ili, kutimiza malengo yake. Fikira hizi humfanya mtu afikirie kuwa, changamoto alizo nazo ni kubwa kuliko uwezo alionao wa kukabiliana nazo. Ni hulka ya kila binadamu kupitia nyakati kama hizi za kukata tamaa. Hakuna binadamu asiye pitia kipindi hichi kwa baadhi ya nyakati.
Nyakati kama furaha, huzuni, kukataliwa, kujichukia, kufeli, kudhalilika, kuheshimika, kudharaurika, kuwa maarufu, kupendwa, kuchukiwa, kutaka msaada, kutoa msaada, kukosea, kusamehewa n.k. Ni sehemu ya maisha ya kila binadamu kwa baadhi ya nyakati. Nyakati kama hizi ndizo huleta radha ya maisha. Vinginevyo maisha yangekosa radha kabisa. Na watu kwa kushindwa kulitambua hili wamejikuta wakikata tamaa na kushindwa kuendelea tena kwa yale waliyo jiwekea.
Zipo sababu zinazo wafanya watu wengi kukata tamaa na
kushindwa kusonga mbele katika kufanikisha mipango yao waliyo jiwekea ambazo ni;
1.
CHANGAMOTO
WANAZOKUTANA NAZO;
Pamoja
na kwamba changamoto ni sehemu ya maisha, watu wengi wanashindwa kukubaliana na
jambo hili. Ndiyo maana wamekuwa wakikata tamaa kila wanapo kutana na
changamoto. Jifunze hili na tambua kuwa changamoto zinapo kuja kwako, zinakuja na
somo au fundisho fulani kwako. Lijue funzo hilo ili uweze kufaidika na kila
changamoto unayo kutana nayo. Afu by the way, kukata tamaa ni dhambi ujue!
Thomas Packet Mfanya biashara maarufu nchini mareka. Alifanya kazi kwa kujituma hadi kufikia umri wa miaka 50 alikuwa Bilionea tayari. Siku moja mfanya kazi wake mmoja alikutwa amekufa ofisini kwake. Uchunguzi ulifanyika na iligundulika kuwa yeye ndiye aliye fanya mauaji hayo. Kesi ikafika mahakamani, alitumia takribani pesa zake zote bila mafanikio hadi kufilisika. Hivyo mahakama ikaamru Thomas afungwe kifungo cha maisha kwa kosa la mauaji hayo.
Maisha
ya Thom hayakuwa si mazuri hata kidogo. Kutokana na changamoto hizo hakuona thamani ya kuishi tena. Alikosa maana
ya kuishi kwake na hivyo alikata tamaa na kuamua kujiua kwa kunywa vidonge 35
vya usingizi.
Thom
alisema alipokuwa karibu na kukata roho, alisikia sauti ikimwijia na kumwambia mambo
mawili ambayo ni,
a) Maisha
yako ni wajibu wako wewe mwenyewe 100%, hivyo unauwezo wa kuyajenga au
kuyabomoa.
b) Mali na fedha ambazo ulizipata hukuja nazo. Kuna mambo ulifanya na kuzipata, hata sasa unaweza kufanya mambo hayo na ukapata tena zaidi ya mwanzo. Huna sababu ya kukata tamaa.
Kuanzia hapo Thom hakuwa na tabia ya kutaka kukata tamaa tena. Aliamua kwenda kufanya kazi kwa bidii na maarifa na baada ya Muda kupita alirudi tena katika utajiri wake na alikuwa mtu tajiri zaidi ya alivyokuwa awali.
Kuna
mambo mengi sana ya kujifunza kutoka kwa huyu jamaa, yaani, pamoja na umri kwenda, kupoteza
mali na utajiri wote aliokuwa nao, kusingiziwa kesi ya mauaji, kukataliwa na
watu, magonjwa na mengine mengi. Changamoto hizi kwakweli hata wewe msomaji
zingekupata sijui ingekuwaje...
Lakini tunaona kwa Bwana Packet ilikuwa tofauti kabisa, alipata Nguvu na kuendelea mbele tena, kubwa zaidi akapata kile alicho kitaka tena alipata zaidi. Hivi packet angekata tamaa ingekuwaje? Nadhani asingetimiza ndoto yake kabisa. Hivyo usikubali kukata tamaa kizembe pambania ndoto yako. Tambua changamoto ni sehemu tu ya maisha na haziji kukuumiza wala kukukomoa bali zinakuja kukupa somo jifunze usonge mbele.
kujifunza zaidi namna ya kukabiliana na tatizo lolote bonyeza hapa
2.
MANENO
HASI WALIYOWAHI KUAMBIWA;
Wapo
watu wengi sana wamerudi nyuma na kukata tamaa kutokana na maneno waliyo wahi
kuambiwa. Maneno haya mara nyingi huwa ni Maneno hasi na yanakatisha tamaa
kwelikweli. Nunaweza ukawa umeambiwa na watu wako wa karibu sana. Mfano waalimu, ndugu, mwenza
wako, majirana n.k.
Na
watu hawa wanaweza wakawa walisha fanya jambo hilo na wakashindwa, hivyo kila ukitaka kujaribu
kufanya wanamwambia haiwezekani. Mara nyingi lengo lao huwa wanataka kukusaidia
ili usipate hasara kama wao walivyo pata hasara. Hapa kumbuka kabla hujapokea
ushauri wa namna hii usikubali kwa maana kila mtu anauwezo tofauti na wengine lakini pia, “watu hatufanani na hatuwezi kufanana”.
Lakini
wapo watu ambao wao huwa wameshindwa katika eneo hilo na hawataki mtu mwingine
afanikiwe kwani atawadhalilisha. Hivyo kila utakapo jaribu watakwambia
haiwezekani yaani, hawataki washindwe peke yao, watakwambia maneno hasi ili na wewe ukate tamaa.
Watu wengine ni wale watu wenye wivu wa kijinga ambao wanawaonea wenzao gere, katika kusonga
mbele, hawataki wengine wafanikiwe kama wao walivyofanikiwa watawakatisha tamaa
sana.
Kuwa
makini na wakatisha tamaa wa namna yeyote ile, iwe ni
wazazi, waalimu, rafiki, majirani n.k. Kataa kukata tamaa hadi mkatisha tamaa akate
tamaa. Kataa kisha jiamini mwenyewe, jitamkie maneno chanya na kataa maneno hasi
kwenye maisha yako. Hivi unafahamu kuwa kila neno moja hasi
ukitamkiwa linahitaji maneno 17 chanya ili kuliondoa?
3. HITILAFU
YA MIILI AU MAUMBILE YAO;
Nakosa
namna nzuri ya kuiweka pointi hii, lakini nina uhakika utanipata vizuri tu. Kuna
watu kutokana na maumbile yao, hitilafu walizo nazo aidha ni kwa kuzaliwa au
kwa kupata ukubwani katika maisha yao. Kitu hiki kimekuwa ni kikwazo kikubwa na
kisingizio lukuki cha watu wengi hata kukata tamaa katika kutimiza malengo yao.
Haben
pamoja na kuwa na ndoto kubwa ya kuwa mwanasheria. Lakini akiiangalia familia
yake hamna wa kumtegemea wadogo zake ndiyo hivyo tena. Kuna wakati ulifika hadi akakata
tamaa kama binadamu lakini, baada ya kutafakari sana kuhusu ndoto yake hakujali tena juu ya hali aliyokuwa
nayo. Aliamua kupambana na hakutaka kuonewa huruma na mtu na aliamua kupambana ili kutimiza ndoto yake ya kuwa mwanasheria. Alifanikiwa kuwa mwanasheria wa kwanza
wa aina hiyo kuhitimu katika chuo kikuu cha Havard nchini Marekani. Na alitimiza
lengo lake la kuwa mwanasheria.
Usije
kukata tamaa kwa sababu ya maumbile na mwonekano wa mwili wako. Pambania Ndoto zako, uzitimize. Halafu, kukata tamaa hakutatui
tatizo ujue!
Daah! Naandika huku nikisikitika sana, wakati mwingine Mungu mwacheni aitwe Mungu tu jamani, hivi haya si ni maajabu kabisa asee! yaani, mtu hana miguu wala mikono eti anahangaika kumtia moyo mtu ambaye ana mikono na miguu yote, ambaye pengine tu alisumbuliwa na mafua, miguu kuwaka moto, kichomi, njaa, kukataliwa na wazazi, kuumwa, kufeli mtihani, kukosa mtaji n.k.
Katika hili nimejifunza kuwa, nguvu ana uwezo wa mtu upo ndani yake, yaani, mtu halisi ni yule wa ndani na siyo hii miili na maumbile yetu ya nje. Haya ni sawa na nyumba tu ya utu wetu wa ndani. Sababu tumeona watu wenye mionekano isiyo waruhusu kuendelea lakini, hawakutaka kukata tamaa na kuwa omba omba kama wengine wanavyofanya. Sikatai kuombaomba lakini, hili nalo la kukata tamaa tuliangalie kwa jicho la tatu.Vinginevyo, tuache masihara na kama ulifikiria kukata tamaa fikiri tena.
4. KUSHINDWA MARA KWA MARA;
Mtu
kama Thomas Edson karibuni kila mtu anaelewa habari zake ambaye hadi sasa
tunanufaika na ugunduzi wake wa taa (bulb). Gwiji huyu alifanya majaribio ya
kutengeneza taa mara 999 bila, kukata tamaa na raundi ya 1000 alifanikiwa
kutengeneza taa ambazo tunatumia hadi leo hii.
Mtu
huyu alichukulia kushindwa kwa faida na si kulalamika na kukata tamaa kama baadhi ya watu
wa sasa.
Mtu
mmoja akauliza nishindwe mara ngapi ili nikate tamaa? Hivi mtu kama huyu wewe
ungemjibuje? Rafiki! Ukiona umeshindwa siku moja acha utani endelea kufanya
kazi, mara kumi acha utani endelea kufanya kazi, wiki moja acha utani endelea
kufanya kazi, mwaka mmoja acha utani na sema endelea kufanya kazi hadi
kieleweke. Haijalishi utashindwa mara ngapi, rudi kapambane hadi kieleweke labda
kama siyo ndoto yako na hauipendi kabisa. Vinginevyo acha utani piga kazi.
Rafiki! ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu.
na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya
kuondokana na adha hii wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo
chini naamini utasaidika.
GeT tO ThE nExT lEvEl!
Makala hii imeandaliwa na kuandikwa
na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi na
Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluetz. Karibu sana ujiongezee thamani yako.
Kwa
mawasiliano;
Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456
Email>> eliasmigongo120@gmail.com.
Facebook>> MIGONGO ELIAS.
LinkedIn>>Migongoe.
Pinterest>>eliasmigongo.
Kama umejifunza kitu,niachie
maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe
Sort by: Date Rating Last Activity
Comments by IntenseDebate
Posting anonymously.
Daniel · 103 weeks ago
Migongo 9p · 103 weeks ago
Vivian Gwimevir · 103 weeks ago
Gloria · 103 weeks ago
Migongo · 103 weeks ago
Migongo · 102 weeks ago
.
Ayusto Busanda · 103 weeks ago
Migongo · 103 weeks ago
Ngwala · 97 weeks ago
Migongo · 97 weeks ago
Jacob · 97 weeks ago
Migongo · 97 weeks ago
Jaredy Naftali · 92 weeks ago
Elias Migongo · 92 weeks ago
Lailat Kashushu · 90 weeks ago
Elias Migongo · 90 weeks ago
Cheyo · 88 weeks ago
Migongo · 88 weeks ago