MAAJABU YA AKIBA

Image
MAAJABU YA AKIBA Akiba (saving) ni kiasi cha fedha au rasilimali ambacho kimewekwa kwa matumizi ya baadaye, hata sasa kingeweza kutumika lakini umuhimu wake kwa kutumika baadaye ni mkubwa kuliko matumizi yake ya sasa. Hata katika biblia ``Mwanzo 41:35-36`` kama umewahi soma utaona Farao baada ya kutafsiriwa ndoto yake na kufahamu kuwa, imempasa kuweka akiba alilifanya hilo kwa uharaka ili kuhakikisha linaendelea vizuri ndio akamweka Yusufu kama msimamizi wa hili. Farao aliona kabisa kuwa nidhamu yake ya kujiwekea akiba haipo sawa hivo alihitaji msaidizi wa kumsaidia kama yeye alivyokuwa ndivyo tulivyo baadhi yetu siku za leo hatuwezi kujiwekea akiba ya vile tulivyo navyo. yaani huwa tunapenda kusema kesho itajisumbukia yenyewe,  Hata hivyo tangu zamani hata leo mataifa mbalimbali yamekuwa yakijiwekea akiba kwa manufaa na matumizi ya baadaye. Ukiangalia nabii Samweli alikuwa akijiwekea akiba na aliitoa pale Sauli alipomtembelea wakaila ile akiba ya chakula. Ni muhimu kujiw...

KWELI TATU KUHUSU NDOTO YAKO.

 

KWELI TATU KUHUSU NDOTO YAKO.

Kama unakumbuka shule ya msingi kwenye somo la Kiswahili, tulijifunza kuhusu utata katika maneno pamoja na sentensi. Maneno tata ni maneno ambayo yana maana zaidi ya moja. 

Hata neno ndoto lina utata, kwani lina maana zaidi ya moja. Au ngoja nikuulize kwa mfano mtu akisema ”ndoto nzuri” kwa haraharaka utamwelewaje? 

Bila shaka huyu mtu anaweza akawa amelenga, aidha ndoto zile mtu anaota hasa akiwa katika usingizi au ndoto kwa maana ya maono. Ni mesema maono ili  tu unipate kwa haraka kwani maneno haya yanarandana sana kimaana. Ingawaje maneno haya yanatofautiana. Sijui umenipata sasa!

Kwa ujumla ndoto ni taswira au mtazamo wa mbele  ambao mtu anatamani kuufikia (tazama picha hapo juu). Na mtazamo huu unaweza kuwa ni halisi au sio halisi, wa wazi au siyo wa wazi, kujulikana au usio julikana n.k. 

Kwa ufupi ni matamanio ambayo mtu anataka kuwa/kuyafikia. Ukweli ni kwamba matamanio na shauku hii kila mtu huwa anayo, pengine ya kuwa mwandishi bora wa vitabu, mtangazaji, Mc mashuhuri, shauku ya kusaidia watu, kushauri watu na mengine kibao.

Shauku hii humfanya mtu ajisikie kuwa na deni au mzigo wa kukifanya kitu ambacho anakitazamia. Lakini ajabu ni kwamba pamoja na watu kuwa na ndoto kubwa sana za kuwa watu wakubwa na wenye kugusa maisha ya watu duniani, lakini hawawi kama wanavyotaka , matokeo yake wanaondoka tu hapa duniani bila kufanya lolote juu ya ndoto zao. Badala yake wanakwenda kuyanufaisha makaburi. wewe usiwe mmoja wao.

Kunasababu nyingi zinazowafanya watu kuondoka duniani bila kutimiza na kufikia kile walicho jipangia kufanya.

Gusa maandishi haya ya bluu kujifunza sababu hizo .

Pamoja na hayo yote kuna mambo matatu muhimu kuyafahamu kuhusu ndoto yako. Utakapo yafahamu mambo haya hautaghairisha tena kuifanyia kazi ndoto yako.

Badala yake yatakupa hamasa ya fanyia kazi ndoto yako mchana na usiku. Mambo haya pia yamezungumzwa na wandishi mbalimbali kama vile Godius Rweyongeza katika kitabu chake cha jinsi ya kutimiza ndoto yako.

Yafahamu sasa mambo haya ili uweze kusonga mbele zaidi.

1.   NDOTO YAKO SIYO YAKO PEKE YAKO, UMEPEWA KWA DHAMANA YA WATU WENGINE.

Napenda moto (kaulimbiu) ya chuo kikuu Mzumbe kwa namna ulivyo wekwa moto huu umeandikwa kwamba “TUJIFUNZE KWA MAENDELEO YA WATU”.   Siusifii moto huu au chuo kikuu Mzumbe lah! Bali nachotaka nikueleze kwamba moto huu umebeba uhalisia fulani hasa linapo kuja suala zima la ndoto yako.  

Sikia rafiki, ndoto yako ni yako lakini umepewa ndoto hiyo kwa dhamana ya kuwatumikia watu wengine.( Tafadhali soma tena uelewe).

Ndiyo maana utakuja kugundua kuwa kila mtu anachofanya kuhusu ndoto yake kinagusa aina fulani ya watu katika jamii.

 Kuna watu wanandoto kubwa na wanatazamia kuzifikia na kuzifanyia kazi, mfano kuwa kiongozi mkubwa, kusaidia watu wengine, kuwa mwalimu, kuwa mchungaji, kuwa askali, kuwa mkulima , mwanasheria, mwimbaji n.k lakini hawataki kuanza kufanyia kazi ndoto zao. 

Utakuta mtu anauwezo mkubwa sana wa kushauri au wa kuimba lakini ana sema hakuna haja ya kuimba kwani uwezo huo anao ndani na anaweza kuimba au kufanya muda wowote akitaka.

Rafiki, tambua kuwa ndoto ni kwaajili yako mwenyewe na watu wengine. Mfano chukulia kwa mwandishi wa vitabu anaandika vitabu labda kuajili ya kumbukumbu na  kujisomea mwenyewe lakini utakuta vitabu hivyo vinasomwa na kuwanufaisha maelfu ya watu ulimwenguni. 

Hivi Robert Kyosaki alikuwa anajua kuwa nitakuja kusoma vitabu vyake? Angalia hata alie tengeneza mitandao ya kijamii na simu pengine alikuwa na lengo la kufanya mawasiliano na kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwaajili yake. 

Lakini wanufaika wengi ni watu wengine ambao haikuwa ndoto yako kabisa, hata kwa mfanya biashara anafanya kwa lengo la kupata pesa lakini hapo hapo anawasaidia wengine kupata mahitaji yao ya msingi, waimbaji hivyo hivyo nyimbo zao zinawaburudisha wao na watu wengine tena utakuta wengine ndiyo wananufaika sana kuliko hata mwanye wimbo.

Nasema kwamba ndoto yako ipo ndani yako kwa dhamana tu hivyo inahitajika kuwafikia wenye nayo, nao ni watu waliokuzunguka nikiwemo na mimi hapa. Fanya kwaajili ya watu. Kwani watu hawa wanakudai huo wimbo wako, wanakudai hicho kitabu chako, wanakudai huo ushauri wako, wanakudai hayo maarifa yako. Fanyia kazi kabla hujaenda kuyanufaisha makaburi asee.

 

2.   KADIRI UNAVYOCHELEWA KUTIMIZA NDOTO YAKO, NDIVYO UNAVYO WAZIBIA NAFASI WATU WENGINE KUTIMIZA NDOTO ZAO PIA.

Steven Paul Jobs Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Apple. Alikuwa na lengo la kutengeneza kompyuta na simu hadi ifiki wakati kila mtu awe ana miliki kompyuta.

Vipi kuhusu akina Larry Page na Sergy Brin Waanzilishi wa Google ambayo tunaitumia sote hivi leo. Nakupa mifano hii michache ili uone namna ambavyo watu hawa kutimiza kwa malengo yao tu kulivyo saidia na kurahisisha maisha ya watu wengi. 

Kutimiza ndoto zao wamesaidia watu wengi kutimiza ndoto zao. Mfano mimi leo natumia compyuta, intanet na google kutimiza ndoto yangu hata watu wengine pia wanatumia hivi vitu kutimiza ndoto zao. Hivyo unapofanyia kazi ndoto yako na kuitimiza unafungua milango na fursa ya wengine kutimiza ndoto zao pia. 

Sikia ndugu, kuna watu hawatafanyia kazi ndoto zao hadi pale utakapo timiza ndoto yako kwanza. Kuna watu wana subiri ufungue hiyo kampuni ili uwaajili, wakati huu wewe huna hata habari, unasaka na kulilia kuajiliwa kumbe umebeba ajira za watu looh! 

Afu sema tu hujui kufanikiwa kwako ni mwanzo wa hatua ya mtu mwingine katika kutimiza ndoto yake. Amka anza kufanyia kazi ndoto yako unawachelewesha watu wengine kupata ajira, kupata maarifa na hata kutimiza ndoto zao ujue!. 

3.   KADIRI UNAVYO WASAIDIA WATU KUPATA KILE WANACHO KITAKA NDIVYO UTAKAVYOPATA UNACHO KITAKA TENA UTAPATA ZAIDI.

Hivi ulishawahi kujiuliza kwanini watu maarufu au wakubwa duniani wanalipwa sana kuliko watu wa kawaida? Hawa watu wanakuwa wamesaidia idadi kubwa sana ya watu katika jamii, taifa na dunia kwa ujumla yaani, wamegusa maisha ya watu wengi sana kuliko kawaida.

Hata wafanya biashara waliofanikiwa wanakuwa wamesaidia watu wengi sana kupata bidhaa zao. Hapo ndipo watu wanarudisha fadhira kwa kuwalipa fedha ndipo wanajikuta wanafanikiwa sana. 

Hivi kuna mtu haifahamu juice ya mo Tanzania hii? Je vipi kuhusu Azam? Watu hawa wamewasambazia watu wengi sana bidhaa zao ndiyo maana watu wako tayari kuwalipa kwa kazi zao. 

Hapo naomba nieleweke kuwa kumsaidia mtu siyo lazima umpe pesa. Msaada siyo pesa tu kama wengine wanavyo fahamu bali unaweza kutumia ndoto yako pia kuwasaidia watu, muda wako, ushauri wako, n.k wala si pesa pekee kama ulivyo mtazamo wa watu wengi.

Je wewe kuhusu ndoto yako umewasaidia watu wangapi hadi sasa? Huo ushauri wako umewashauri watu wa ngapi hadi sasa? Hiyo biashara yako umewafikia watu wangapi hadi sasa? Huo ualimu umewafundisha watu wa ngapi hadi sasa?

Kumbuka kwamba kadiri unavyo wasaidia watu wengine kupata kile wanachokitaka na wewe utapata unachokitaka tena utapta Zaidi. 

Fanyia kazi ndoto yako, saidia watu wengi zaidi kupitia ndoto yako. Hakika utapata kile unataka. 

Moja ya lengo la ndoto ni kukupa furaha ya maisha na kadiri unavyo zidi kutimiza ndoto yako ndivyo unavyokuwa na furaha katika maisha yako

Chukulia wewe ni Mwalimu, kadiri unavyofundisha watu wengi na wanaelewa na kurudisha ripoti kuwa umewasaidia. Utajikuta unaishi maisha ya furaha  na bado watu wale watakulipa. Lakini pia hao watu utakuwa umewasaidia kutatua changamoto zao.

Hivyo usiwe mchoyo wa ndoto yako kwa watu wengine.

Rafiki tambua kuwa ndoto yako unayo kwa dhamana tu, kadiri unavyotimiza ndoto yako ndivyo unavyo toa nafasi kwa watu wengine kutimiza ndoto zao pia. Hata hivyo kadri unavyocuelewa kutimiza ndoto yako ndivyo unvyowachelewesha wengine. Kadri unavyo wasaidia watu kupata kile wanachotaka ndivyo unavyopata unachotaka tena unapata zaidi.

 

rafiki! ni matumaini yangu kuwa umejifunza kitu. kitakusaidia kutimiza na kuipambania ndoto yako. na kama unachangamoto katika hili pengine namna gani ya kutambua ndoto yako wasiliana na mimi moja kwa moja kupitia mawasiliano hapo chini naamini utasaidika.

 GeT tO ThE nExT lEvEl!

Makala hii imeandaliwa na kuandikwa na MIGONGO ELIAS Mshauri & Mwalimu Wa Saikolojia, Uchumi maendeleo binafsi na Maisha. Mwanzilishi na Mwendeshaji wa Mtandao wa addvaluenetwork. Karibu sana ujiongezee thamani yako. 

Kwa mawasiliano;

Whatsapp & Sim >>+255767653697 /+255783327456

Email>> eliasmigongo120@gmail.com.

Facebook>> MIGONGO ELIAS.

Facebook page>> Add Value Network

Pinterest>>eliasmigongo.

Kama umejifunza kitu, niachie maoni yako nitafurahi kujifunza pamoja nawe .

 

Comments (7)

Loading... Logging you in...
  • Logged in as
Daaah rafiki umetoa madini kuntu sana...barikiwa aisee nimejifunza zaidiii... kumbe ndoto yangu ni dhamana tu ndani yangu! Looh kumbe kuna watu wananisubiria kutimiza ndoto zao... daaah umenikumbusha maemo usemao.. get rise, the world is waiting for you... wooow hakika nimejifunza kaka
1 reply · active 102 weeks ago
woow ,ahsante sana rafiki nimejifunza pia kuwa get rise, the world is waiting for you
Amina, ubarikiwe sana kwa makala nzuri mwalimu wangu.
1 reply · active 77 weeks ago
Ahsante nashukuru sana rafiki
Janeth Mollel's avatar

Janeth Mollel · 50 weeks ago

Kazi yako njema sanaaa Elias.
Be blessed 🙏🙏🙏♥️
1 reply · active 50 weeks ago
Migongo Elias's avatar

Migongo Elias · 50 weeks ago

Ahsante nashukuru sana rafiki
Amani yapundaa's avatar

Amani yapundaa · 50 weeks ago

Extra mind add extra ideas to other minds👍🏿👍🏿

Post a new comment

Comments by

Popular posts from this blog

NJIA 7 ZA KUOSHA UBONGO WAKO.

VITU 9 MUHIMU KWA MTU YEYOTE KUJIFUNZA KWENYE MAHAFALI.

SIRI ILIYOPO NYUMA YA TABASAMU.